Monday, October 31, 2011

IHUNGO HILLS IN WEST LAKE REGION

The former Students at IHUNGO Secondary School in West Lake Region (Now Kagera) Mr. Kiyungi and Mr. Kabaraza relaxing at Ihungo hills in 1970's. Kiyungi to date  is a Senior Journalist and  Mr.Kabaraza is a Major with JWTZ.

FAMILIA YA MZEE KIYUNGI .

PICHA YA PAMOJA YA FAMILIA  NYUMBANI KWA MZEE KWA KIYUNGI YOMBO DOVYO TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM 2007.

Thursday, October 27, 2011

VITA KAWAWA NA WANA HABARI MAARUFU.



 
MBUNGE WA NAMTUMBO VITA KAWAWA (KATIKATI) AKIWA NA WAANDISHI WA HABARI MAARUFU KIYUNGI  KIYUNGI (KUSHOTO) NA MUHIDI ISSA MICHUZI NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA 2008.

MBUNGE WA ISIMANI WILLIAM LUKUVI NA KIYUNGI KIYUNGI



MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI WILLIAM LUKUVI AKIBADILISHANA MAWAZO NA MWANDISHI WA HABARI KIYUNGI  KIYUNGI (KUSHOTO) NJE YA VIIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA  JANUARI 2004

MBUNGE WA VUNJO JAMES MBATIA AKIMREKEBISHA TAI KIYUNGI WA KIYUNGI

MBUNGE WA VUNJO(NCCR - MAGEUZI) JAMES MBATIA AKIMREKEBISHIA TAI KIYUNGI  KIYUNGI  NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA 1998.

WAZIRI KATIKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS EWDARD LOWASSA NA WANAHABARI


 
WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS EDWARD LOWASSA(KATIKATI) AKIWA NA WANAHABARI KIYUNGI WA KIYUNGI (KUSHOTO) ABOUBAKAR LIONGO (ITV/RADIO ONE) NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA 1997.

RAIS BENJAMIN MKAPA CHAMWINO DODOMA

RAIS WA AWAMU YA TATU BENJAMIN WILLIAM MKAPA AKISALIMIANA NA WANAHABARI WAANDAMIZI TOKA IDARA YA HABARI (MAELEZO) RAPHAEL HOKORORO NA KIYUNGI  KIYUNGI IKULU NDOGO YA CHAMWINO MJINI DODOMA MWAKA 2002)

WAZIRI MKUU EDWARD LOWASSA AKISALIMIANA NA MWANAHABARI KIYUNGI KIYUNGI KWENYE VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA

WAZIRI  MKUU EDWARD LOWASSA AKISALIMIANA KWA FURAHA NA MWANAHABARI MKONGWE KIYUNGI  KIYUNGI (KUSHOTO) NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA AUGUST 2007.

KWAHERI BABA WA TAIFA MWL. NYERERE IKULU

BAADHI YA VIONGOZI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MWL. NYERERE SIKU  YA KUMUAGA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA KUSTAAFU MWAKA 1985.
KUSHOTO NI DAVID WAKATI(RTD),NYUMA YA MWL. NI MZEE SAILEN(AVI), GERVACE MSILO (DAILY NEWS, ADINAN MIHANJI (SHIHATA) NA KIYUNGI  KIYUNGI (MAELEZO)

BABA WA TAIFA MWL.NYERERE NA KIYUNGI -BUTIMA

BABA WA TAIFA MWL. NYERERE AKIWA NA KIYUNGI KIYUNGI SHAMBANI KWA BABA WA TAIFA  KIJIJINI BUTIAMA.. KIYUNGI ALIKUWA MMOJA KATI YA WANAHABARI WACHACHE WALIOMSIINDIKIZA MWL. NYERERE KURUDI KIJINI KWAKE BUTIAMA MKOANI MARA MWAKA 1985.PIA ALIPATA BAHATI YA KWENDA KUMZIKA KIJIJINI HAPO BAADA YA KUFARIKI AKIWA KATIKA HOSPITALI YA ST. THOMAS HUKO LONDON..

WAPIGA PICHA WAKUU WAKIMUAGA BABA WA TAIFA IKULU

BAADHI YA WAPIGA PICHA WAKUU TOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI NCHINI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BABA WA TAIFA MWL. NYERERE WAKATI WA KUMUAGA BAADA YA KUSTAAFU URAIS IKULU JIJINI DAR ES SALAAM 1985.WALIOSIMAMA TOKA KUSHOTO MAX MADEBE(MFANYAKAZI),SAM MMBANDO(SHIHATA),VINCENT URIO, (DAILY NEWS),JOHN MAKWAIA (MAELEZO), MZEE SILEN(AVI), JUMA DIHULE(SHIHATA), ADINAN MIHANJI (SHIHATA)NA  KIYUNGI  KIYUNGI (MAELEZO). WALIOCHUCHUMAA WAPILI TOKA KUSHOTO,CHARLES KAGONJI (MAELEZO),GERVACE MSILO (DAILY NEWS), MWANAKOMBO JUMAA (MAELEZO), KHATIBU ALLY (UHURU) NA RAPHAEL HOKORORO (MAELEZO).

Friday, October 14, 2011

KUMBUKUMBU YA FRANCO LWANZO MAKIADI

François Luambo Luanzo Makiadi  alizaliwa 6 July 1938, katika kijiji cha Soni Bata magharibi mwa jimbo la Bas Zaire huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wakati bado mchanga wazazi wake walihamia jiji la Leopodville ambalo sasa linaitwa Kinshasa. Baba yake aliitwa Joseph Emongo alikuwa mfanyakazi wa shirika la reli wakati huo mama yake alikuwa akiuza maandazi sokoni. Alipofikia umri wa miaka saba alitengeza gitaa lake akawa analipiga kwenye genge la mama yake ili kuita wateja.. Mwanamuziki maarufu Paul Ebengo Dewayon ndie aliyegundua kipaji cha mtoto huyu na kuanza kumfundisha rasmi namna ya kupiga gitaa. Mwaka 1950 akiwa na umri mdogo wa miaka 12 alichukuliwa rasmi kama mwanamuziki wa bendi ya Watam iliyokuwa inaongozwa na Dewayon. Kipaji chake kiliwashangaza wengi hasa kwa vile alikuwa akionekana umbo lake kubwa kama gitaa analolipiga lakini akiwa analipiga kwa umakini mkubwa. Akiwa na miaka 15 alirekodi nyimbo yake ya kwanza Bolingo na ngai na Beatrice (Mapenzi yangu kwa Beatrice). Wimbo huu aliutunga alipojiunga na bendi iliyokuwa inamilikiwa na Studio za Loningisa. Kiongozi wa bendi hiyo Henri Bowane ndie aliyeanza kufupisha jina la mwanamuziki huyu na kumuita Franco, jina alilokuja kujulikana nalo maisha yake yote. Mwaka 1955 alianzisha bendi akishirikiana na Jean Serge Essous bendi ilizinduliwa katika ukumbi wa OK Bar, hatimae bendi ilichukua jina la OK Jazz kwa heshima ya bar ambapo ilizinduliwa.Katika muda mfupi ikiwa na mwimbaji Vicky Longomba(Baba yake Lovy Longomba) walianza kuwa bendi pinzani ya bendi kongwe ya African Jazz iliyokuwa inaongozwa na Grand Kalle. Mwaka 1958 Essous na Franco kuwa kiongozi na mtunzi mkuu wa kikundi alichokuja kukijenga kwa kuanzia watu 6 hadi kufikia  watu 30 kwenye mwaka 1980. Franco mwenyewe alikuwa anasema OK Jazz iliweza kutoa album 150 katika miaka 30 ya bendi hiyo.Mwaka 1958 Franco alifungwa kwa mara ya kwanza kwa kosa la uendeshaji mbaya wa gari siku ya kutoka kwake jela ilikuwa kama shujaa katoka vitani. 1960 Vicky Longomba aliacha bendi. Lakini wakati huo Kongo ilikuwa kwenye vuguvugu za kutafuta uhuru na nchi ilikuwa si shwari Franco akahamia Ubelgiji. Baada ya Mobutu Sese Seko kushika nchi na kukawa na amani  katika nchi iliyoitwa sasa Zaire franco alirudi 1966. Akashiriki katika Tamasha la Sanaa Za Afrika lililofanyika Kinshasa 1966 na Franco akawa kipenzi cha serikali ya Mobutu. 
Franco hakuwa tu mwanamuziki mzuri bali pia aliendesha vizuri sana biashara zake za kurekodi na kampuni alizozianzisha wakati huo. Alikuwa na lebo kama (Surboum OK Jazz, Epanza Makita, Boma Bango and Éditions Populaires). Katika miaka ya 70 muziki wa Kongo ulishika kasi sana Afrika na Franco akiongoza jahazi kwa nyimbo kama Infidelité Mado,  na akaendeleza kupiga mitindo mbalimbali kama Bolelo na muziki uliotokana na ngoma za asili toka Kongo zikichanganywa na mapigo kutoka Cuba na kuanza upigaji wa gitaa uliokuja itwa Sebene.
 Mwaka 1970 Franco alimpoteza mdogo wake ambaye nae alikuwa mpiga gitaa mashuhuri Bavon Marie-Marie Siongo ambaye alifariki katika ajali ya gari baada ya kuwa akiendesha gari kwa hasira baada ya ugomvi na kaka yake wakigombea msichana ambaye nae alipata kilema kutokana na ajali hiyo. Lilikuwa pigo kubwa kwa Franco kwa miezi kadhaa aliaacha hata kupiga muziki. Baada ya hapo OK Jazz ilibadili jina na sasa kuitwa TP OK Jazz na mwaka 1973 kutoa kibao kingine kilichotikisa Afrika ,AZDA.  Wimbo huu kwanza ulirekodiwa kama tangazo kwa ajili ya  kampuni ya Volkswagen VW. Mahusiano yake na Mobutu yalikuwa na mawimbi mara wakipatana mara wakikosana kutokana na Franco kuwa anatumia nyimbo zake kukosoa serikali ya Mobutu. 1970 Franco alikuwa ni Rais wa wanamuziki wa Kongo na pia kuajiliwa na kampuni ya kugawa mirabaha ya wanamuziki. Aliendelea kutajirika kwa kuweza hata kunua ardhi nchini Ufaransa, Ubergiji na Kongo, na kuwa na nightclub 4 kubwa kuliko zote Kinshasa kwa wakati huo na kufanya club ya
 Kuwa ndio makao makuu yake. Hapo ilijengwa studio kubwa, office na apartment za kuishi kadhaa. Mwaka 1978 alitiwa mbaroni  tena baada ya kugundulika kuwa alikuwa anasambaza nyimbo zenye matusi ambazo hakuzipitisha katika  kamati ya kuchunguza mashahiri kama ilivyokuwa kawaida wakati ule. Kufikia kipindi hiki TPOK Jazz  ilikuwa kubwa kiasi iliweza kumeguka kuwa mbili moja ikifanya kazi Afrika wakati nyingine ikiwa inafanya maonyesho Ulaya. !983 Franco alifanya maonyesho kadhaa Marekani lakini hayakufanikiwa haijajulikana mpaka leo sababu za kushindikana huko. Katikati ya miaka ya 70 Franco alibadili dini na kuwa Muislam na kupewa jina la Abubakkar Siddiki, japo hakuonekana kufuata taratibu zozote za Kiislamu na akaendelea kuitwa Franco. 1980, Franco alitajwa kama ndie Grand Master wa muziki wa Kongo na serikali yake, ghafla na nyimbo zake nyingi zikaanza kuwa zinasifia utawala ulikuweko madarakani. 1985 Franco alitoa wimbo ambao uliuza kuliko nyimbo zake zote
, Mario,  ambao ulikuwa ni hadithi ya mwanaume kijana  ambae alikuwa anategemea akina mama watu wazima wamlee. !987 zilianza habari kuwa Franco anaumwa sana, na kwa mwaka ule alitoa wimbo mmoja Attention Na SIDA (Jihadhari na UKIMWI), wimbo huu ukaanzisha maneno kuwa pengine Franco kasha upata ugonjwa huu. Franco akawa taratibu anakosekana kwenye shughuli za bendi nayo ikaanza kumeguka kutokana na kutokuwa na uongozi thabiti. Franco tena akarudi kwenye dini yake ya awali ya Roman Catholic. Tarehe 12 Oktoba 1989, Franco alifariki katika hospitali moja Ubelgiji. Mwili wake ukarudishwa Kongo, sanduku likiwa limefunikwa bendera ya Taifa lake na kupitishwa katika mitaa ya Kinshasa na kuagwa na maelfu ya wapenzi wake. Serikali ikatangaza siku 4 za maombolezo ambapo redio ya serikali ilipiga nyimbo za Franco tu. Franco alizikwa tarehe17 Oktoba 1989. Alifariki akiwa na miaka 51. Mumgu amlaze pema peponi

Women Jazz Band, bendi ya akina mama 1966

Kijakazi Mbegu kwenye solo gitaa
Mwaka 1965 kundi jipya la muziki la aina yake lilianzishwa Tanzania. Lilikuwa ni bendi ya akina mama watupu. Akina mama hawa, wengine wakiwa wafanya kazi wa Government Press walijichagua na kuanza kuhudhuria mafunzo ya muziki chini ya yule mwanamuziki mahiri Mzee Mayagilo aliyekuwa kiongozi wa shughuli za muziki katika Jeshi la Polisi. Akina mama hawa wakawa chini ya kitengo cha Polisi Jazz Band, wakaanza kufanya mazoezi ya nguvu. Bendi hiyo ya akina mama ilikuwa chini ya TANU Youth League. Wakati wakianza shughuli hii walikuwa hawana ujuzi wowote wa muziki. Kutokana na jitihada waliyofanya taratibu wakaanza kufanya maonyesho yao hasa kwenye hafla za serikali na Chama tawala wakati huo.
Tarehe 31 Mei 1966 Women Jazz band iliingia katika studio za RTD na kurekodi nyimbo sita.
1. Tumsifu Mheshimiwa
2. Leo Tunafuraha
3.Mwalimu Kasema
4.Women Jazz
5.Sifa nyingi tuwasifu viongozi
6.TANU yajenge nchi. 
Washiriki katika bendi hiyo walikuwa;
1.Mary Kilima- Mwimbaji
2.Juanita Mwegoha-Mwimbaji
3.Siwema Salum- Mwimbaji
4.Rukia Hassan- Mwimbaji
5. Kijakazi Mbegu- Solo Guitar
6.Mwanjaa Ramadhan-Bass Guitar
7.Chano Mohammed-Rhythm Guitar
8.Tatu Ally-Alto Sax
9.Mina Tumaini-Tenor Sax
10. Anna Stewart-Alto Sax
11. Rukia Mbaraka-Tenor Sax
12.Lea Samweli-Bongos
13. Josephine James-Drums
14. Zainab Mbwana-Maracass
15. Tale Mgongo-Timing.
Women Jazz ilipata umaarufu kiasi cha kuanza kufanya safari nje ya Tanzania, na kuweza kufanya maonyesho Nairobi na Mombasa, baada ya kutembelea miji kadhaa hapa nchini. Wakati wa matayarisho ya kwenda China kundi lilisambaratika. Kikubwa kilichosababisha hili ilikuwa ni wanamuziki kuona hawapati chochote kutokana na mapato yaliyotokana na muziki.

Tancut Almasi Orchestra na Kashasha

Kuanzia album ya kwanza ya Tancut Almasi Orchestra , bendi iliendelea kutoa vibao vilivyoweza kudumu katika kumbukumbu za wote waliovizisikia kuanzia enzi hizo, album ya kwanza ilikuwa na nyimbo kama vile, Nimemkaribisha nyoka(Kasaloo Kyanga), Kashasha(Kyanga Songa), Tutasele (Kasaloo), Mtaulage(John Kitime), Big Four(Utunzi wa wimbo huu ulileta utata kwani ulianza kwa ugomvi kwa Mamado Kanjanika kudai kuwa aliutunga yeye wakati akina Kasaloo na Kyanga wakidai wameutunga wao. Lakini hatimae akina Kasaloo waliacha ugomvi huo na Mamado hutajwa kama mtunzi wa wimbo huu. Hebu angalia mambo yalivyokuwa wakati Kashasha likipigwa. Niko hapo na miwani kubwa nikiungurumisha rhythm guitar

Eddy Sheggy akikuletea Shakaza 'live'

Jambo ambalo naliona wazi ni kuwa Watanzania wanapenda sana nyimbo za dansi zinazotokana na nyimbo zenye asili ya makabila ya hapa Tanzania. Nikikumbuka nyimbo kama  Mtaulage, Malaine, Nyongise, ambazo ni kazi yangu mwenyewe nikiwa Tancut na Vijana Jazz, kila Munu ave na kwao ya Les Mwenge, Boko wa Kilimanjaro Band, Shakaza ya Bantu  na nyingi nyingine zote zilichukua nafasi ya juu katika anga za muziki wakati wake, na hata sasa. Pengine lingekuwa somo kwa wanamuziki wa Tanzania na kuliangalia hili katika tungo zao. Hebu tumkumbuke Eddy Sheggy hapa akiwa na Bantu, akiimba na ndugu zaki Francis na Christian

Maoni ya mdau

The Legendary Safari Trippers, Marijani wa pili kulia kati ya waliosimama, wa kwanza ni Uvuruge mtunzi wa wimbo Georgina



Nyumbani tulikuwa na video cassette VHS aliyorekodiwa Marehemu Doza(Marijan Rajabu) na Orchestra Dar International kwenye show yao moja kule Buguruni Casanova Bar ( Kama sikosei) kwa Mwalimu Msuya. Ngoja nitawauliza waungwana nijue iko wapi.

Marehemu Doza si tu alikuwa muimbaji, mtunzi na mpiga guitar bali pia alikuwa anajua kuusoma muziki. Nadhani nadharia ya muziki alijifunza shuleni Olympio na Tambaza kwa sababu wakati ule muziki ulikuwa bado unafundishwa shuleni. Muziki lilikuwa somo linalofundishwa shule ya Tambaza hadi miaka ya '90 sijui kwa sasa.

Nikisikiliza tungo za Safari Trippers huwa nasikia muziki uliotungungwa kitaalam haswa kuanzia kwenye ghani/melody, midundo/rhythm, vikolombwezo/harmon hadi tenzi/lyrics. Safari Trippers iliundwa na na baaadhi ya wanamuziki waliokuwa "wataalam wa muziki" wakiwemo David Mussa, Mohamed Ibun, Musiba, Marehemu Doza na Marehemu Cris kazinduki. Nakumbuka Marehemu Cris alikuwa anafanyakazi Wizara ya Elimu na alikuwa wakati mwingine anajam na Mzee Kibira (Baba yao kina Onesmo Kibira) wakipiga muziki kwenye sherehe mbali mbali pale Wizarani. Mzee Kibira alikuwa anapiga Trombone. Naomba mnisahihishe kama nimekosea.

Kwa kumalizia: Moja ya Disadvantage ya kukosa televisheni Tanzania ni kukosa hifadhi ya mambo mengi katika mfumo wa filamu.

Mkuu, tafadhali wasiliana na Televisheni Zanzibar uone kama kuna uwezekano wa kupata clips za muziki. Nakumbuka kuna ile show ya Marquis du Zaire waliyokuwa wanaionyesha katika sherehe za kuzaliwa CCM mwaka 1977. Pia unaweza kuwasiliana na Audio-Visual Institute Kijitonyama walikuwa wana materials za muziki kibao. Chuo cha Sanaa Bagamoyo walikuwa wanarekodi sana matukio wakati wa Tamasha nina hakika kutakuwa na clips nyingi tu za bendi mbali mbali zilizokuwa zinatumbuiza katika ufunguzi na maonyesho mengine wakati wa Tamasha. Mtu mwingine ambaye anaweza kuwa na materials ni Mohamed Kissoky na ni Prof. Martin Mhando nina hakika haya majungu kuu hayakosi ukoko.

Nakutakia kila la heri na mafanikio katika jitihada zako.

Mdau Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.

Monday, October 3, 2011

BIRTH DAY YA KING DAVY


 MZEE KIYUNGI AKIWA NA KIJUKUU CHAKE  NJE  YA OFISI ZA BOMBA FM JIJINI MBEYA.
MZEE KIYUNGI AKICHAGUA MUNYU KATIKA SHEREHE YA FREDY HERBERT 
(MFALME DAUD)
Mzee Kiyungi akiwa katika sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Bwana Frey Herbert "Mfalme Daud" kwenye viwanja vya ofisi  ya Bomba fm jijini Mbeya hivi karibuni.

ISENGA TABORA.

Vijana wa zamani ambao kwa sasa ni wazee toka kushoto ni Mzee Bakari Kawego,Mzee Mashaka Mapalala Mankupu na Mzee Kiyungi wakiwa katika picha ya pamoja mjini Tabora mwaka 2008.Wazee hawa walizaliwa mwaka mmoja kwenye miaka ya 1950's lakini wakakutana na kukumbushana mengi hususan walivyokuwa wakuchezea magari ya mabua, kuogelea mabwawani, kuwinda ndege kwa manati na kuchuma na kupopoa matunda ya porini. Wallah ilikuwa siku ya furaha sana baada ya kupotezana toka mwaka 1968 katika kijiji chao walikozaliwa cha Isenga Tarafa ya Ilolanguru Wilaya ya Tabora Vijijini wakati huo(sasa ni Uyui) Mkoani Tabora.

BOMBA FM Radio Staff

WATANGAZAJI BOMBA FM Redio WAKIWA NA FAMILIA ZAO WAKIMPA SHAVU MWENZAO IMMA "BOY" MWENYE TSHIRT(104)AMBAYE ALIKUWA DJ BORA KATIKA SHINDANO LA MA DJ JIJINI MBEYA 2011. 
MZEE KIYUNGI AKIMSHANGILIA IMMA "BOY" WA BOMBA FM Radio,WAKATI ALIPOKUWA AKI"SCRATCH"DJ MACHINE WAKATI WA SHINDANO LA DJ BORA JIJINI MBEYA. KUSHOTO MTANGAZAJI WA REDIO HIYO LIZZY ROMMY.(Picha:Mroki Mroki) 

POZI LA NGUVU

BI..FATUMA KATANGA KATIKA  MAPOZI YA SHEREHE YA MJUKUU WAKE ,JIJINI  DAR ES SALAAM MWAKA 2010.

MFANO WA KUIGWA.

"WANANDOA WA MAFANO WA KUIGWA" MAZA HAUSI AKIMSUKA MTEJA, FAZA HAUSI NAYE AKIMYOA MTOTO KIJIONGEZEA KIPATO NDANI YA FAMILIA YAO.HUKO MWANZA ROAD MJINI TABORA HIVI KARIBUNI.

MWALIMU TAUSI KIYUNGI

MWALIMU TAUSI KIYUNGI AMEJAA VITUKO KWELI KWELI. MUONE ETI SASA ANAWAJIBIKA IPASAVYO KUANDAA MSOSI NYUMBANI KWA BABA YAKE ,JIJINI  DAR ES SALAAM 2010.

TICHA KIYUNGI

HAYA MAPYA TENA. MWALIMU TAUSI  KIYUNGI,AKIFANYA MASIHARA HUKU, PICHA YA INAYOONEKANA NYUMA YAKE  IKIMSUTA. ILIKUWA JIJINI DAR ES SALAAM 2010.

FAMILIA.

MAREHU MAMA YETU MKUBWA BI.ASHURA KAZI AKIWA NA DADA ZANGU BI.TABU OMAR MABARA(kushoto) NA BI. FATUMA KATANGA, ENZI ZA UHAI WAKE KIJIJINI ILOLANGURU 2010.

FATUMA KATANGA

DADA YANGU MPENDWA BI FATUMA KATANGA, AKIINGIA NYUMBANI KWAKE BAADA YA KULITUMIKIA TAIFA

AMANI NGONYANI

BWANA AMANI NGONYANI, AKITABASAMU BAADA YA KUTOKA MASJID HUKO BUZZA JIJINI DAR ES SALAAM 2010.

TICHA TAUSI KIYUNGI

TICHA TAUSI KIYUNGI KATIKA MAPOZI KABLA YA MTOKO..

MAFOTOGRAFA

HAWA NI WAZEE WA MAKAMERA WAKATI WA NEEMA ZA IIP MEDIA(GUARDIAN NA ITV) JIJINI DAR.2002. TOKA KUSHOTO NI Mr. MMBAGA, Mr.MPOCHI, Mr.MICHUZI, Mr.KIYUNGI, Mr.KALIMANZILA, Mr.DIHULE NA MR.MWANGASA.

Nyerere/Madiba

 
Baba wa Taifa hayati Mwalimu KJ Nyerere akijibu maswali ya waandishi wa habari. Kushoto ni Nelson Mandela (Mzee Madiba)