Thursday, January 9, 2014

YVONNE CHAKA CHAKA



YVONNE CHAKA CHAKA.


YVONNE CHA CHAKA  ALIKUWA  MSANII WA  MUZIKI YA KATIKA MIAKA YA 1980 NA KWA JUHUDI ZAKE HISASA NI MTANGAZAJI NA MWENDESHA KIPINDI KATIKA KITUO CHA NEW MILLENNIUM,CHAKA CHAKA NI MBURUDISHAJI MAARUFU WA AFRIKA KUSINI NA AFRIKA KWA UJUMLA.

CHAKA CHAKA KWA MARA YA KWANZA ALITIKISA KATIKA MUZIKI WA AFRIKA KUSINI AKIWA KIJANA MNAMO MWAKA 1984 KWA WIMBO WA “I’M IN LOVE WITH A DJ”. MUZIKI WA DISKO ULIOTENGENEZWA NA SELLO ‘CHICCO’ TWALA AMBAO ULITENGENEZWA KWA MUZIKI WA ASILI YA MBAGANGA KUTOKA MJINI MWA AFRIKA KUSINI,LAKINI UKIWA NA MASHAIRI YA KIINGEREZA. MTINDO HUO ULIWEZA KUJULIKANA KAMA ‘BUBBLEGUM’ NA YVONNE CHAKA CHAKA SAMBAMBA NA BRENDA FASSI WALIBAKI WAKITAMBA KWA MIAKA HIYO YA 1980.

SAUTI YAKE NZURI ILIJIDHIHIRISHA KATIKA ALBAMU YA UMQOMBOTHI MWAKA 1988 KATIKA WIMBO ULIOKUWA NA JINA LILELILE LA “I’M LOVE WITH A DJ”.ALBAMU HII AMBAYO ILIKUWA INASIFIA POMBE YA KIAFRIKA INAYOTOKANA NA MTAMA ILIKUWA KATIKA MTINDO WA POP,INGAWA ILIFUATA KWA KARIBU DESTURI ZA MBAGANGA NA SINGALONG KATIKA KIITIKIO. AMBAPO ILIWEZA KUWAVUTIA WATU WA AFRIKA KUSINI NA AFRIKA KWA UJUMLA.

MWISHONI MWA MIAKA YA 1980 ALBAMU YA UMQOMBOTHI YA YVONNE CHAKA CHAKA ILIPENDWA NA WATU WENGI. ALIFANYA ZIARA KATIKA AFRIKA KWA KUFANYA MATAMASHA KATIKA VIWANJA VYA NIGERIA,KENYA NA ZAIRE.NJE YA AFRIKA KUSINI. CHAKA CHAKA ALIKUWA NI MSANII WA MUZIKI WA AFRIKA NZIMA NA ANAENDELEA KUFURAHIA HADI LEO.

ALITAMBULIKA KAMA “MALKIA WA AFRIKA” KUTOKA NA KUTEMBELEA BARA LA AFRIKA NA UVAAJI WAKE WA KILEMBA KICHWANI.

KWENYE MIAKA YA 1990 ALIENDELEA KUFANYA ZIARA NA KUUZA ALBAMU KATIKA KILA NCHI ZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA. IKUMBUKWE KUWA ALIWAHI KUTUMBUIZA KATIKA KUNDI LA VIONGOZI  WA NCHI ZA AFRIKA PAMOJA NA TUKIO LA KIHISTORIA LA KUZALIWA KWA NCHI YA AFRIKA KUSINI.

YVONNE NI MLEZI WA MRADI WA ‘GIVING AND SHARING’ AMBAO UNAHUSU UNAJISHUGHULISHA NA KUSAIDIA MASKINI WENYE UHITAJI,PIA INAJIHUSISHA UKUSANYAJI WA MAPATO ILI KUPAMBANA NA GONJWA LA UKIMWI,MFANO NI KITUO CHA ORLANDO CHILDREN’S HOME.


ALIACHIA ALBAMU YA ‘YVONNE AND FRIENDS’ MWISHONI MWA MWAKA 2000 AMBAYO ILISHIRIKISHA WASANII WA KIGENI KAMA VILE TSEPO TSHOLA AMBAYE ALIKUWA SANKOMOTA.

MWAKA 2002 ALIFANYA KAZI YA KUWA MTANGAZAJI KATIKA RADIO NA TELEVISHENI, HII ILPELEKEA KUHAMA KUTOKA KUWA ‘MALKIA WA AFRIKA’ MPAKA KUWA MFANYABIASHARA MAARUFU, MBURUDISHAJI NA MUELIMISHAJI.

YVONNE CHAKA CHAKA AMEOLEWA NA MWANAFIZIKIA KUTOKA SOWETO NA NI MAMA WA WATOTO WANNE.


MWISHO.


DEKULA KAHANGA 'Vumbi'


DEKULA  KAHANGA “VUMBI”

Mafanikio katika maisha ni lazima mtu kuwa na malengo, nia na dhamira ya dhati, kujiamini  na hatimaye kufanya maamuzi magumu. Maneno haya yametamkwa na mwanamuziki wa dansi Dekula Kahanga maarufu kwa jina la ‘vumbi’ambaye safari yake ya kwenda kupiga muziki huko Ulaya ilitokea katika bendi ya Maqius Original ya  hapa Tanzania.

Moja kati ya maamuzi magumu aliyoyafanywa mwanamuziki huyo lile la kondoka bendi hiyo iliyompa chati iliyokuwa ikipiga muziki wake katika ukumbi wa Lang’ata Kinondoni jijini Dar es Salaam na kutokomea hadi  Sweden bila kujua atakuwa mgeni wa nani huko ugenini.

Anaeleza kwamba hivi sasa hajutii maamuzi yake kwa vile tayari amepata mafanikio makubwa akiwa ni pamoja na kumiliki bendi yake iitwayo Dekula Band. Bendi hiyo hupiga  muziki kwa mkataba mara mbili kwa mwezi katika ukumbi wa Lala Vin, mjini Stockholm nchini Sweden.

Bendi hiyo ina  wanamuziki mahiri  wenye vipaji vingi toka nchi mbalimbali hapa duniani wakiwemo akina Luhembwe Mwanahita ‘Bobo Sukari’ (kuimba na Show), Sammy  Kasule (Injinia, kuimba, Bass,Drums na Keyboard), Joe Gerald Nnaddibanga(kuimba, Conga na Show),Christina Frank, na Marceline Kouakoua.

Wengine ni yeye Dekula Kahanga(Solo na rhythm), Arne Winald (Keyboard) kwa pamoja huufanya muziki wao kukubalika kimataifa hadi kupelekea kupata mialiko lukuki ndani na nje ya nchi ya Sweren zikiwemo za Ulaya, Asia, Marekani, Japan,  Falme za kiarabu na Afrika.

Anaelezea mafanikio mengine ni kutengeneza mahusiano mema kwa baadhi ya watu toka nchi mbalimbali wanazotembelea na sasa anaweza kuongea  kwa ufasaha lugha tano tofauti za Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Lingala na Kiswidish.

Dekula Kahanga ni  alizaliwa Aprili 02, 1962 katika kijiji cha Lumera, Wilaya ya Kivu  Kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni baba wa familia akiwa na mke na watoto watatu na yeye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto kadhaa wa mzee Aloyce Obeid Dekula aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la reli katika serikali iliyokuwa ikiongozwa na rais Mobutu Seseseko Kuku Ng’endu wa Zabanga.


Alipata elimu Sekondari hadi kidato cha nne karika miji Bukavu na  Uvira.
na kumaliza elimu hiyo mwaka 1979.
Mwaka uliofuatia wa 1980 safari yake katika muziki ilianza kwa kujiunga na bendi za Bavy National, na Grand Mike jazz, ambako alikutana na wanamuziki akina Kyanga Songa na Issa Nundu.

Akiwa Kivu, ‘Vumbi’ alikuwa msikilizaji mzuri wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo ilikuwa ikisikika vyema wakati huo na alizitamani nyimbo zilizokuwa zikiporomoshwa na bendi za Morogoro Jazz, Tabora Jazz, Cubzn Marimba, JUWATA Jazz, Mlimani Park na Orchestra Safari Sound.

Anamtaja John Luanda aliyekuwa akimiliki bendi ya Chamwino Jazz kuwa ndiye chanzo cha yeye kuingia hapa Tanzania baada ya kuwachukua toka Kongo yeye na wenzake akina Bwami Fanfan, Sisco Lunanga na Baposta ili  kujiunga katika bendi yake iliyokuwa ikipiga muziki Manzese maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam.

‘Mewenye bahati habahatishi’ ndivyo anavyosema mkung’utaji huyu wa gita la Solo Dekula Kahanga ‘Vumbi’ kwamba mwaka 1980 alikutana na mwanamuziki  Chimbwiza Nguza Mbangu ‘Viking’ katika Ofisi za Ubalozi wa Kongo hapa nchini.

 Nguza Viking  wakati huo alikuwa mpiga gita la Solo pia akiwa mmoja kati ya  wanahisa na viongozi wa bendi ya Orchestra Maquis du Zaire, hapo alimpa mwaliko yeye na wenzake kwenda kuburudisha kwenye ukumbi wa White House uliokuwa maeneo ya Ubungo Kibo jijini Dar es Salaam.

Dekula alikubali mwaliko huo kisha weekend moja walifika na kupewa nafasi ya kuburudisha kwa muda mfupi ambapo waliutumia vyema na kuweza kuzikonga nyoyo za wanamuziki wa bendi hiyo ya Maquis  na wapenzi wa muziki waliokuwa mamefurika wakishuhudia vijana hao.

Baada ya kuburudisha usiku huo hazikupita  siku nyingi Dekula akaitwa na uongozi wa bendi ya Maquis du Zaire akina Chibangu Katai (mzee Paul), Mutombo Lufungula (Audax) na Mbuya Makonga (Adios) wakimtaka aandike barua ya kuomba ajiunge na bendi yao kwa mkataba wa kazi isiyo na mshahara ili kuziba nafasi ya Nguza Vicking ambaye tayari alikuwa ameanza mgomo baridi.
Naye aliona kama ngekewa imemshukia kwa kuitwa katika bendi kubwa ya Maquis du Zaire. Hakufanya ajizi alikubali kaunndika barua na akajiunga na bendi hiyo.

Vumbi anakumbuka siku mmoja wakipiga muziki ukumbi wa Temeke Stereo, alimuona kwa mbali Nguza Vicking akiwa kajibanza pembeni mwa ukuta ukumbini humo akisikiliza nyuzi alivyokuwa akizicharaza.

Baada ya kumuona anasema aliingiwa na tashwishwi isiyo mfano na kujiona kama anamvunjia heshima Nguza na kuomba ampishe ili aje kushika nafasi yake. Lakini viongozi wake akiwemo Chibangu Katai (mzee Paul) na  Ilunga Lubaba, walimtaka aendelee kupiga gita hilo.

Dekula Kahanga anasema alimudu akizipiga nyimbo zote alizokuwa zikipigwa na Nguza zikiwemo za Makumbele, Ngalula, Seya, Malokelee, Karubandika, Dora mtoto wa Dodoma, Nimepigwa Ngwala na nyingine nyingi kiasi kwamba wapenzi wa muziki walishindwa kutofautisha upigaji wa gitaa la Solo kati yake na Nguza katika mitindo yao ya Bishe bishe, Kamanyola, Ogelea piga mbizi na Zembwela.

Aliendelea kulivurumisha gita hadi  mwisho wa onyesho na baada ya hapo kwa adabu zote alikwenda kumsalimia na Nguza pale alipokuwa kajibanza, naye hakusita kumsifia kwa kazi  nzuri.

Taharuki kati ya uongozi wa  Maquis du Zaire  na Nguza ziliendelea  kupamba moto hatimaye aliondoka rasmi bendi hiyo na akaanzisha bendi yake ya Orchestra Sambulumaa akiwa na wanamuziki wengine akiwemo mwanaye Papii Kocha.

Bendi hiyo  haikudumu kwa kipindi kirefu kufuatia matatizo yaliyomikumba familia yake akiwemo yeye na watoto wake wote wa kiume kwa kufunguliwa kesi ya ubakaji wa wanafunzi wa shule ya msingi maeneo ya Sinza jijini
Dar es Salaam.

Kesi hiyo ilichukua muda mrefu kusikilizwa hatimaye mahakama Kuu  aliwatia hatiani yeye  Nguza na mwanaye Papi Kocha na kuhukumiwa kutumikia kifungo  cha maisha gerezani.

Miaka ya 1989 na 1990 Dekula alikuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa Maquis Original. Maquis Original lilikuwa jina jipya lililo badilishwa toka Maquis du Zaire baada ya kuhamia katika ukumbi Lang’ata, Kinondoni.

Dekula alivutia wapenzi wake kwa upigaji wa gita  hasa pale wimbo wa Ngalula ulipokuwa ukipigwa huku  mwimbaji Tshimanga Kalala Assosa akimpandisha mori, akipaza sauti kwa kumuita Vumbiii,Vumbiii,Vumbiii kila mara kama kibwagizo cha  wimbo huo.

Vumbi anawakumbuka baadhi wanamuziki aliokuwanao katika bendi ya  Maquis du Zaire na Maquis Original kwa wakati huo  wakiwemo waimbaji akina Mbuya Makonga ‘Adios’ Mutombo Lufungula ‘Audax’ Mukubule Lulembo ‘Parashi’, Kiniki Kieto, Tshimanga Kalala Assosa, Issa Nundu, Kasalo Kyanga.

Wapiga gita la Solo walikuwemo akina Chimbwiza Nguza Mbangu”Nguza Vicking”, Ilunga Lubaba na Suleiman Mbwana ‘Cocks’.

 Anawataja wapigaji wa gita la  kati  walikuwepo akina Mulenga Kalonji ‘Vata’ Omari Makuka  na Steven Kaingilila Mauffi. Gita zito la besi lilikuwa likiungurumishwa na Ilunga Banza ‘Banza Mchafu’ na Mujjos wa Bayeke.

Wapuliza midomo ya Bata walikuwa Mafumu Billar  ‘Bombenga’ Majengo Bakari, Mukuna Roy ‘ Mukuna wa Mukuna’, Akulyake Suleiman ‘King Maluu’, Alex Kanyimbo na Khatibu Iteitei.

Wengine anawataja Kanku  Kelly Ilunga Bizoo, Mpoyo Kalenga, Kaumba Kalemba na Ngenda Kalonga kwa upande wa Trampet na Drums walikuwepo Mbuya Makonga ‘Adios’ na Matei Joseph.


 Pia hakumsahau Kiongozi  wa wacheza shoo, Nkulu Wabangoi na wapiga Tumba akina Siddy Morris na Pulukulu Wabandoki Motoo ambao wote kwa pamoja waliifanya Maquis kuwa tishio kwa bendi zingine hapa nchini.

Dekula anaeleza kwamba alipofika Stockholm alianza kuchacharika mitaani  akitafuta bendi ya kupiga. Kwa bahati nzuri mwaka 1993  akakutana na mwanamuzi toka Uganda aitwaye  Sammy Kasule nao kwa pamoja wakaamua kuanzisha bendi yao ikiitwa  Makonde Group.

Mapema mwaka 1999, Dekula Kahanga alifyatua Album iitwayo Bolingo Ekesemi iliyosheheni nyimbo za ‘Dunia kuna mambo’ na ‘Mpenzi Asha’

Dekula anajivunia kuwa mwanamuziki wa kwanza mwaafrika huko Sweden baada ya kufyatua Album  iitwayo DEKULA Sultan Qaboos, yenye nyimbo za Sultan Qaboos, Mon Amour, Babylon, Mayanga, Rozina, Mambo leo na Nostalgie  nyimbo ambazo hupigwa  katika vituo vingi vya redio duniani.

Usemi wa ‘Mtaka cha Uvunguni sharti ainame’ ulimpata Dekula pale alipotaka kupata  unafuu wa maisha nchini Sweden ambao ni lazima uwe raia wa nchi hiyo. Hivyo alilazimika kuomba uraia kwa kufuata taratibu zote.

Dekula alitoa mfano wa Shubiri kwamba ni chungu lakini ni dawa, hivyo alifikia  maamuzi mengine magumu zaidi ya kuukana uraia wa nchi yake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Hivi sasa yeye na wanamuziki wenzake wa bendi hiyo ni  raia halali wa nchi ya Sweden na wanaweza kusafiri kwenda nchi nyingi za Marekani Ulaya Asia na kwingineko pasipo kubughuziwa kwa kuomba VISA.

Mwanamuziki huyo ambaye kwa tabia ni mpole japo ni mcheshi, ametoa mwito kwa Vijana chipukizi  katika muziki kujifunza kupiga Ala ili wafikie viwango vya kuwa  wanamuziki na kuwaasa kaachana na anasa za dunia sisizo na maslahi kwao.

Vilevile amewaonya  kuondokana na ulevi wa  sifa toka kwa washabiki ambazo huwavimbisha vichwa na kusababisha kijisahau majukumu yaliyo mbele yao.

Dekula kwa kuona vijana wa kizazi hiki hawana munkari wa kujifunza kupiga Ala za muziki, ametoa ahadi kwamba atajitahidi  kwa kadri ya uwezo wake siku za usoni kuanzisha bendi hapa nchini itakayokuwa ikitumia Ala za muziki za kisasa ili vijana wa Tanzania wajifunze.

Mwisho.

KOMANDOO HAMZA KALALA ''Mzee wa madongo'



HAMZA KALALA ‘KOMANDO’

HAMZA KALALA NI MWANAMUZIKI MKONGWE KATIKA TASNIA YA MUZIKI HAPA NCHI. SIFA ZAKE ZILIANZA KUZAGAA WAKATI ALIPOANZA KULICHARAZA GITA LA SOLO KWA UMAHIRI MKUBWA.

ALIZALIWA MKOANI TANGA NA KUSOMA SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI HUMO. MARA BAADA YA KUZAILIWA ALIPEWA JINA LA NYUMBANI LA ‘KAPESULA’  BABA YAKE ALIKUWA MFANYAKAZI WA KATIKA SHIRIKA LA RELI KATIKA STESHENI YA MPANDA. BAADAE ALIHAMISHIWA MKOANI TANGA AMBAKO ALIBAHATIKA KUOA MKE WA KABILA LA KIZIGUA AMBAYE NDIYE MAMA WA KOMANDO KALALA. KWA MATIKI HIYO HAMZA KALALA NI CHOTARA WA KINYAMWEZI NA KIZIGUA.

KOMANDO HAMZA KALALA ALIANZA KUHAMASIKA KATIKA MAMBO YA MUZIKI MWAKA 1966 AKIWA SHULE YA MSINGI DARASA LA NNE WAKATI ALIPOKUWA AKIMSHUDIA BABA YAKE AKIIMBA NA KUCHEZA NGOMA YA KINYAMWEZI YA MANYANGA HUKO HUKO TANGA.
WAKATI HUO WAKATA MIKONGE WALIKUWA WAKIFANYA MASHINDANO YA NGOMA KATI YA WANYAMWEZI NA NGOMA ZA MAKABILA MENGINE WALIOKUWA KATIKA MASHAMBA TOFAUTI YA  MKONGE YA KIBARANGA YA AMBONI NA MENGINE MENGI LAKINI NGOMA  YA MANYANGA YA WANYAMWEZI NA ILE YA WAMAKONDE NDIZO ZILIZOKUWA ZIKITIA FORA  KATIKA MASHINDANO HAYO KILA MARA.

KALALA ANELEZA KWAMBA MJOMBA WAKE ALIKUWA NA GITA NYUMBANI HIVYO ALIKUWA AKIJARIBU KUSHIKA GITA KAMA ANAVYOSHIKA YEYE MJOMBA WAKE. KIPAJI CHAKE KILIANZA KIJITOKEZA BAADA YA KUONA KWAMBA HAIKUMSUMBUA SANA KUJUA KUCHANGANYA NYUZI ZA GITA.

KOMANDO ‘MZEE WA MADONGO’ MWAKA 1968 ALIANZA KUPIGA MUZIKI KATIKA BENDI NDOGO SANA HAPO TANGA IITWAYO KWANDURU JAZZ BAND. BENDI HIYO  ILIKUWA KATIKA MASHAMBA YA MKONGE NA BAADAYE AKAJIUNGA NA BENDI YA  AMBONI JAZZ.

HUKO HAKUKAA SANA NA ALIRUDI MJINI TANGA AMBAKO AKIWA NYUMBANI AKIFANYA MAZOEZI YA KUPIGA GITA,  AKAPITA MKONGOMAN  MMOJA ALIYEMTAJA KWA JINA MOJA LA CHIVOSHA AMBAYE ALIKUWA MWIMBAJI MZURI SANA  ALIMCHUKUA  NA KUANZA KUPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YAOM YA VILLA NEGRO SUCCSSES. MWAKA 1969 ALIACHANA NA BENDI HIYO NA KUELEKEA MKOA  WA MOROGORO AKIWA NA NIA YA KUJIU KATIKA BENDI YA MOROGORO JAZZ AU CUBAN MARIMBA. LAKINI ALIAMUA KWENDA KATIKA WA KILOSA AMBAKO ALIKUWA AKIJUWA KUWA ABELL BARATAZAR YUKO HUKO. LAKINI ALIPOFIKA ALIAMBIWA KUWA ALISHAREJEA DAR ES SALAAM. ALIPIGA MUZIKI HAPO MKILOSA  LAIKINI HAKUPAPENDA KWA KUWA HAPAKUWA NA USHINDANI WA BENDI. KOMANDOO AKAAMUA KURUDI KWAO TANGA NA KUKUTANA MWANAMUZIKI MWENZAKE AMBAPO WAKAPANGA SAFARI YA KWENDA MOROGORO. WALIFIKA KATIKA MJI HUO WAKIWA NA HALI MBAYA SANA KIFEDHA KALALA WAKATI HUO ALIKUWA AKIVUTA SIGARA HIVYO ALIJIKUTA AMEFIKA MJINI MOROGORO AKIWA NA SENTI KUMI NA TANO PEKEE MFUKONI MWAKE AMBAZO HAZITOSHI KULA  WALA CHOCHOTE KILA LAKINI MWENZAKE  HAUKWA MVUTAJI SIGARA ALIKUWA NA AKIBA YA SENTI HAMSINI ZILIZOWAZWEZESHA KUPATA CHAI NA WAKALALA STENDI YA BASI HADI ASUBUHI WAKAANZA KUZITAFUTA HIZO KLABU ZA BENDI ZA MOROGORO JAZZ NA CUBAN MARIMBA
BAHATI HAIKUWA UPANDE WAO KWANI WALIKUTA BENDI HIZO ZIKIWA SAFARI  MOROGORO JAZZ ALIKUWA IMEENDA ZANZIBAR WAKATI CUBAN MARIMBA ALIKUWA SONGEA.
HAMZA KALALA ANAMTAJA MPIGA GITA LA SOLO WA CUBAN MARIMBA WAZIRI NYANGE ALIYEWAPOKEA WAKATI WAKISUBIRI BENDI HIZO ZIREJEE. MSEMO WA KUFA KUFAANA ULIJITOKEZA BAADA YA WANAMUZIKI WA MOROGORO JAZZ KUPATWA NA MATATIZO HIVYO ALIPOFANYIWA USAILI ILIKUWA KWAKE NI RAHISI KUCHUKULIWA KATIKA BENDI HIYO BAADA YA KUFANYIWA USAILI WAM KUPIGA GITA KATIKA WIMBO WA ‘ SINA PESA MIYE’
CUBAN MARIMBA ALIPOREJEA IKIONGOZWA NA JUMA KILAZA AMBAYE ALIKUWA MSHIRIKA MWASISI MWENZA  PIA NDIYE ALIYEKUWA  MWENYEJI WAO WAZIRI NYANGE, HIVYO ALICHUKULIWA NA CUBAN MARIMBA  NA ALIPOFIKA HAPO ALIKUTA  BENDI IKIPIGA KATIKA MTINDO WA SUBI SUBI.  AKIWA NA CUBAN ALIPATA SAFARI YA KWANZA YA KWENDA TANGA KUPIGA MUZIKI.
SIKU MOJA USIKU ALIKUJA KATIBU WA CHAMA WA WILAYA YA BAGAMOYO  MZEE MWITA ALIYETUMWA NA MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO WAKTI HUO
MOSSES NNAYE KWENDA BAGAMOYO KUENDESHA BENDI YA VIJANA YA TYL.
WAZIRI NYANGE ALIKUWA NA FAMILIYA YAKE PALE MOROGORO HIVYOM IKIMUWIA VIGUMU KWENDA BAGAMOYO LAKINI AKAMPA PANDE HAMZA KALALA KWENDA BAGAMOYO. KAZI KUBWA YA BENDI HIYO KILA JUMAMOSI WALIKUWA WAKIENDA RUVU KUWABURUDISHA WAPIGANIA UHURU WA FRELIMO NA ZAMBIA.
MWAKA 1970 AKASIKIA BENDI YA VIJANA JAZZ ANAANZISHWA. ALIFUATWA NA WANAMUZIKI ANAOWATAJA KWA MAJINA YA NDALA FASUTINE AMBAYE BAADAYE ALIONDOKA NCHINI KWA MATATIZO YA KUCHANGANYA KAZI NA UASHERATI.
NDALA ALIKANYWA NA WAZEE WA BAGAMOYO KUACHA UASHERATI LAKINI HAKUSIKIA. HAMZA ANAELEZEA KISA CHA KUKUTA PAKA ZAIDI YA 30 KWENYE MAKAZI YAO YALIYOKUWA GHOROFANI,WALIKUWA WAKILIA KWA SAUTI KAMA MAGITA.NDALA FAUSTINE AKAINGIA NDANI AKACHUKUA MKIA WA TAA , KALALA AKAMKANYA ASIWACHAPE PAKA HAO LAKINI YEYE ALIENDELEA KUWACHAPA LAKINI HAWAKUONDOKA HADI SA 11 ALFAJIRI NDIPO WALIPOONDOKA TARATIBU. SAUTI ZA PAKA HAO ZILIPOTOWEKA NDALA NAYE AKAANZA KUIMBA NYIMBO  AKIMTAJA MPENZI WAKE ALIYEKUWA AKIKANYWA ASIMCHUKUE. WAZEE WA BENDI HIYO AKIWEMO MASUDI NA MZEE DOLA ALIYEKUWA AKIKUSANYA USHURU SOKONI BAGAMOYO AMABO WALKUWA WAZEE BENDI WAKAMSAIDIA NA ALIPOPONA AKAONDOKA BAGAMOYO.
MWAKA HUO WA 1970 ALIPOKWENDA VIJANA JAZZ ALIKUTA KUNA VYOMBO VYA MUZIKI LAKINI HAPAKUWA NA MPANGO WA KUANZISHA BENDI.
HAMZA KALALA AKAFIKIRIA JINSI YA KUISHI MJINI DAR ES SALAAM NDIPO AKAMFUATA JOHN ONDOLO CHAHA ALIYEKUWA AFISA UHUSIANO WAKATI HUO. MZEE ONDOLO AKAMUELEAZA KWAMBA VYOMBO HIVYO VIMEFUNGIWA BAADA YA KUVUNJWA KWA BENDI YA GREEN JAZZ BAND NA  BARAZA KUU LA UMOJA WA VIJANA  NA KWAMBA HIVI SASA HAPANA MPANGO WA KUANZISHA BENDI.TENA. ONDORO AKAMUULIZA ANAPIGA CHOMBO GANI AKAMWELEZA KUWA ANAOIGA GITA. MZEE JOHN ONDORO AKAMWAMBIA AENDE AKAMSIKILIZA NIKAPIGA NYIMBO ZAKE KAMA USAILI BAADAYE AKARIDHIKA NA KUWAPA PESA YA CHAKULA. ALIPELEKWA KWENDA KINONDONI MAGO GARDEN NA KUANZA KUFANYA MAZOEZI YA KUPIGA MUZIKI.
WALONGEZEKA WANAMUZIKI WENGINE WAKIWA  KATIKA KAMBI KAMA YA JESHI.
RAMADHAN MTORO  DRUMS, ABDALLAH KWESA HASSAN HOKORORO NA IKATOKEZEA BAHATI YA MTENDE KUOTA JANGWANI BAADA YA BENDI HIYO KUJIPATIA UMAARUFU BILA KUJALI KKIPATO.
KATIBU MKUU WA CHAMA MICHAEL BARUTI KUPITA NA KUWAKUTA WAKIPIGA MUZIKI AKAWAPENDA SANA. MIAKA KUMI YA UHURU MZEE  JOHN ONDORO ALIENDA KWENYE SHIRIKA LA MAZAO WAKATI HUO AMBAKO ALIWAAMBIA KWAMBA WANA BENDI AMBAYO ITAKUWA IKIBURUDISHA KWENYE BANDA LAO. WALIKUBALIANA NA AKALIPWA SHILINGI ELFU KUMI NA MOJA. WALIFANAYA KAZI NA SHIRIKA HILO HADI MAADHIMISHP YA MIAKA KUMI YA UHURU  YALIPOKWISHA  NDIPO WAKAAMBIWA KUWA WATAKUWA WAKILIPWA POSHO YA SHILINGI HAMSINI KWA MWEZI. TUKAENDELEA  KUPIGA MUZIKI HADIM KILIPOFIKIA KIFO CHA RAIS WA KWANZA WA  ZANZIBAR  BENDI AMANI KARUME MWAKA 1972 WAKATENGENEZA WIMBO AMBAO ULIPENDWA NA WAZEE. AKAJA MZEE ANDREW SHIJA AKASHANGAA KUWAONA WAKIZAGAA NJE YA OFISI AKAAMRISHA WAPELEKWE JKT WAKAFUNZWE NIDHAMU. TUKAPELKWA KAMBI YA JKT RUVU WAKIWA NA HASSAN DALALI NA DK. CHARLES KIMEI. BAADAYE WALIPELEKWA MPAKANI MWA TANZANIA NA UGANDA VITANI AMBAVYO HATA HIVYO HAVIKUPUGANWA. WALIPOREJEA WAKATUNGA WIMBO UNAHUSU KIFO CHA MAREHEMU ABEID AMANI KARUME NA MGENI WA HESHIMA SIKU HIYO ALIKUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS NA WAZIRI MKUU RASHID MFAUME KAWAWA NA MAKAMU WA RAIS WA KENYA DANIEL ARAP MOI. MZEE KAWAWA AKAFURAHISHWA NA MUZIKI WALIUPOROMOSHA SIKU HIYO NA NDIPO ALIPOWAULIZA HAWA VIJANA WANATOKA WAPI. AKATOA MAELEKEZO YA KUANZISHWA BENDI YA VIJANA JAZZ.
BAADA YA KUANZISHWA MWISHO WA MWEZI ULIPOFIKA WALIANZA KULIPWA POSHO ZAO KATIKA OFOSI YA LUMUMBA ZA SHILINGI 150 TOKA SHILINGI 50 ZA AWALI.  KWA WAKATI HUO SHILINGI 150 ZILIKUWA NI NYINGI SANA  KWA MATUMIZI YA KAWAIDA. MWAKA 1974/75 WAKATOKA NA WIMBO HEMEDI MANETI AKIWA AMEKWISHA INGIA AKITOKEA MOROGORO  AKATUNGA WIMBO KURUKA UKUTA UTUNZI WA MANETI.
KALALA AKATUNGA WIMBO WA MAGDALENA NIPENI POLE.
WAKENYA WALIUSIKIA WIMBO HUO NA KUUPENDA SANA WIMBO HUO. AKAJA MKENYA ALIYEJULKANA KAMA OLUOCHI KANINDO AKAWAOMBA KWENDA KENYA KUREKONDI NYIMBO ZAO KWENYE KAMPUNI YAKE HUKO NAIROBI. WAKAPATA OFA YA KUREKODI KILA MWAKA ZAIDI YA MARA MBILI.
1977 KALALA AKAJIUNGA NA UDA JAZZ IKARUS KUMBAKUMBA. AKIWA NA UDA JAZZ KUNA SIKU ALIKUTANA NA MZEE MMOJA AMBROS MBURA ALIYEKUWA MMILIKI WA BENDI YA SUPER MATIMILA AKAMWAMBIA AENDE KILIMANAJARO HOTEL AKIWA NA HEMEDI MANETI  AJILI YA MAZUNGUMZO.
WALIPATANA KUONDOKA KWENDA SONGEA KWA NDEGE KUFUATIA BARABARA YA HUKO KUWA MBAYA. ALIWAKODIA NDEGE LAKINI MANETI HAKUWEZA KWENDA KWANI  HADI NDEGE INAPAA  ALIKUWA HAJAFIKA UWANJA WA NDEGE.
MKATABA WAKE NA MZEE AMBROSE ULIKUWA MZURI LAKINI AKACHUKUA MKATABA WA MIAKA MIWILI HADI 1979 AKAMALIZA MKATABA WAKE.
1979 WAKATI WAAJESHI WA JWTZ WANAREJEA TOKA VITANI UGANDA AKATENGENEZA WIMBO UITWAO MCHAKAMCHAKA. BAADAYE AKARUDI DAR NA AKAHITAJIKA TENA NA BENDI YA UDA NDIPO AKAJIUNGA NAO KWA MARA NYINGINE TENA NA KUBUNI MTINDO WA BAYAKANTA.
MWAKA 1981 MATIMILA AKAHAMIA DAR NA MZEE AMBROSE AKAMAKA ARUDI KWENYE BENDI YAKE.
MASLAHI YAKAMSHAWISHI KUONDOKA UDA NA KUJIUNGA NA MATIMILA HADI MWKA 1981.AKISHIRIKIANA NA DK. REMMY ONGALA. MWISHONI MWA MWAKA HUOHUO ALIFUATWA NA KAPTENI MCHUNGA AKIFUATANA NA HEMEDI MANETI WAKIMTAKA AFIKE OFISI YA UMOJA WA VIJANA.
AKAAMBIWA MPIGA SOLO WA BENDI HIYO HASSAN DAALALI KAONDOKA HIVYO WAKAMTAKA ASHIKE NAFASI YAKE NA KUWA KIONGOZI WA BENDI YA VIJANA.  MWAKA 1982 AKAIUNGA RASMI VIJANA AKATOKA NA WIMBO WA MAISHA YA AMBA. MIAKA YA 1985 HADI 1988  VIJANA JAZZ WAKATOKA NA MITINDO YA TAKATUKA, HEKAHEKA  NA PAMBAMOTO
 WIMBO WA SIFA ZA STELLA ALIUTUNGA WIMBO  HUO IKIWA NI NJIA YA KUMSHAWISHI BINTI HUYO AMBAYE WAKATI HUOA LIKUWA MWANAFUNZI WA CHUO MJINI MOROGORO NA NYUMBANI KWAO AMBAKO NI KWA MBUNGE WA BARIADI MASHARIKI, MHESHIMIWA JOHN CHEYO ‘ MZEE MAPESA’ AMBAYE NYUMBA YAKE ILIKUWA NA GETI KALI. STELLA ALIVUTIKA NA KUWA MPENZI WAKE HADI KUFUNGANAYE NDOA NA KUPATA WATOTO WAWILI AMBAO NAO WAMEFUATA NYAYO ZA BABA YAO AKIWEMO TOTO KALALA NA KALALA JOURNIOR. KOMANDO KALALA ANA WATOTO WENGINE WAWILI WA KIKE FATUMA AMBAYE NI MKE WA MTU NA FATUMA NI MWANFUNZI WA CHUO.




1988 AKAJIUNGA NA BENDI YA WASHIRIKA JAZZ ‘ WATUNJATANJATA’ KWA MWAKA MMOJA TU IKIWA NI NJIA YA KUTAFUTA JINSI YA KUJITEGEMEA MWENYEWE.MANDELA MWANA WA AFRIKA, NIMEKUSAMEHE  LAKINI SITOKUSHAU, JULLIE WIMBO ULIOTUNGWANA MADARAKA MORRIS NA NYINGINE NYINGI.
BAADAYE AKAANZISHA BENDI YA BANTU GROUP AMBAKO ALIWASHIRIKISHA WAPIGA MAGITA WAKIWEMO AKINA MANGELE SANGE UPANDE WA SOLO, ALLI ADINANI, RASHID KALALA BESI/SOLO. WENGINE NI BATI PETER NA MICHAEL LILOKO UPANDE WA DRUMS ALLI CHOKI NA MUUMIN MWINJUMA WAKIWA NI WAIMBAJI.MUSEMBOWA MINYUNGU NA ALLA MASHOOM KWA UPANDE WA TUMBA.
 BABA JENI NA SUVUYA WA NIMBA, NALILA MASUMANDA NA KASIMBAGU, NGOZI YA KITI MOTO.
 BABA YAKE MZEE KALALA ALIINGIA NCHINI AKIWA NA DADA ZAKE WAWILI WAKITOKEA DRC NA KUFIKIA KATIKA KIJIJI CHA IPWAGA HUKO INYONGA  AMBAKO ALIISHI NA KUWA MAARUFU NA KISHA KUFANYWA KUWA MTEMI. UFIKAPO INYONGWA FAMILIYA YA KALALA NI MAARUFU SANA HADI LEO.,
BANTU GROUP BADO IPO NAYE YUPO KWENYE MICHAKATO YAKINIFU YA KUANDAA VIBAO VIKALI VITAVYOTIKISA MASIKIO YA WAPENZI WA MUZIKI HAPA NCHINI.
KUHAKIKISHA WELEDI WAKE UIFAIDISHE FAMILIYA YAKE NA JAMII KWA UJUMLA.
USHAURI KWA WANAMUZIKI WA KIZAI KIPYA WAPIGE MUZIKI  LIVE. KISA KWA NINI BENDI HUFA BAADA YA KIONGOZI MKUBWA KUFARIKI
UOGOZI NI KIPAJI ANACHOKITOA MUNGU PEKEE SI KILA MTU ANAWEZA KUONGOZA.

MWISHO.