MZEE WA FARASI ALLY CHOKI.
Ally Choki ni mwanamuziki anayetamba miongoni
mwa wanamuziki wa muziki wa dansi hapa nchini.
Ana talanta vingi zilizojengeka kichwani mwake zikiwemo za kutunga, kuimba pamoja na uongozi.
Historia yake katika muziki Choki iliieleza
kwamba alianza muziki rasmi mwaka 1988 nilipojiunga na bendi ya Lola Africa.
Baadae
akajiunga na bendi ya Mwenge Jazz iliyokuwa chini ya Jeshi la Wananchi
Tanzania(JWTZ).
Hakudumu kwa kipindi kirefu baada ya miezi sita alihamia katika
bendi ya Bantu Group iliyokuwa ikiongozwa na ‘Komandoo’ Hamza Kalala.
“Mwaka 1990 nikiwa Bantu na Hamza Kalala akiwa
kiongozi tulitoa albamu ya Baba Jane. Mwaka 1991 nilitoka Bantu, nikajiunga na
Legho Stars chini ya Tshimanga Kalala Asosa...” alisema Ally Choki
Safari ya kusaka mafanikio ilikuwa
ikisababisha kwenda huku na kule. Alijikuta yuko katika bendi ya Legho Stars. Hata hivyo huko nako hakudumu sana
akaamua kurudi katika bendi ya Bantu group.
Choki alikuwa mithiri ya 'Kunguru' kwani huko Bantu group nako hakukaa sana, akaenda kujiunga
na bendi ya Bendi ya MK Beat ‘Tukunyema’,
iliyokuwa ikiongozwa na Shem Ibrahim Karenga.
Mwaka 1992 alihamia katika bendi ya Washirika
Stars ‘Watunjatanjata’ ambako walitoa albamu iliyopewa jina la Gubu la Wifi.
Huko aliwakuta mwimbaji mwingine mahiri akiwemo Adam Bakari ‘Sauti ya Zege’, mpapasaji Kinanda
Abdul Salvado ‘Father Kidevu’ na wengine wengi.
Katika harakati za kusaka maisha Choki aliamua kuvuka mpaka wa nchi nakuingia katika jiji la Nairobi, nchini Kenya mwaka 1994.
Akiwa katika jiji hilo aliungana na wanamuziki
wengine akiwemo Muumini Mwinjuma, ambako huko wakaanzisha bendi yao ikiitwa 'Extra
Kimwa' mwaka 1998.
Choki ilipotimu mwaka mwaka 1999, aliamua kurejea nchini baada ya kupata taarifa kuwa mama yake mzazi
kuwa alikuwa mgonjwa.
Akiwa hapa nchini aliamua kujiunga katika bendi
ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’
chini ya uongozi wa mkurugenzi Asha Baraka.
Alikubali kujiunga na
bendi hiyo baada ya kupokea ushauri kwa
mwanamuziki mwenzake Robert Hegga ‘Caterpillar’ ambaye walikuwa wote Nairobi.
Mwaka 2000 walitoa albamu iitwayo 'Jirani',
iliyokuwa na nyimbo nyingi lakini hiyo ulikuwa ni utunzi wake yeye Choki.
Kama kuna kitu ambacho hawezi kukisahau wakati akiwa Twanga, ni pale wanamuziki
wengi waliihama bendi hiyo na kwenda kujiunga na bendi nyingine ya Chuchu Sound.
Baadhi yao wakatimkia katika bendi ya Mchinga Sound, akiwemo Adolf Mbinga aliyekuwa gitaa la mpiga
solo.
Busara zake akazitumia kwa kumfuata mpiga solo
mwingine Miraji Shakashia ‘Shaka Zulu’.
Shakashia naye hakudumu kwa kipindi kirefu
akatimka ndipo nafasi yake ilishikwa na Kassim Rashid ‘Kizunga’ aliyekuja
kupiga gitaa la rhythm.
Baadaye alipewa cheo kuwa kiongozi wa bendi na
ndipo walipotengeneza albamu ya Fainali uzeeni. Albamu hiyo ilifuatiwa na ile
ya ‘Ukubwa Jiwe’ hatimae ‘Chuki Binafsi’.
Ally Choki alikuwa na kila sababu za kujivunia akiwa hapo Twanga, kwa kuwa
alikuwa akiongoza kwa kutunga nyimbo nyingi zilizovuma.
Baada ya kujipima uwezo wake, akanzisha bendi
yake ya Extra Bongo mwaka 2003. Bendi hiyo ilikusanya wanamuziki wengi mahiri
hapa nchini na kuweza kuwa tishio kwa bendi zingine hususan katika jiji la Dar
es Salaam.
Lakini kama wasemavyo waswahili “Penye riziki
hapakosi fitina” ndivyo ilivyotokea kwa Ally Choki ambapo fitina
ikatengenezwa na wanamuziki wake
wakanunuliwa akabaki ‘mweupe’ pasipo na mwanamuziki.
Kutokana na hali hiyo, alilazimika kuiacha
bendi yake na kwenda kujiunga katika bendi ya Mchinga.
Huko nako hakudumu kwa
kipindi kirefu, akarejea tena Twanga Pepeta. Baadae tena akajiunga na kundi
zima la Tanzania One Theater, lililokuwa likiongozwa na Kapteni mstaafu John
Komba.
Akiwa ni mmoja wa viongozi wa TOT, Choki alifanikiwa kuipandisha chati
bendi hiyo baada ya kuwaleta wanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Alidumu na bendi hiyo ya TOT hadi mkataba
wake ulipokwisha, akaamua kuifufua tea
bendi yake ya Extra Bongo mwaka 2009.
Ally Choki akizungumzia kisa cha sababu za
kushuka kwa kiwango cha muziki wa dansi, Choki alikanusha kauli hiy.
Alisema kwamba muziki wa dansi haujashuka
kiwango isipokuwa vyombo vya habari vimeupa kisogo kwa kuangalia zaidi muziki
wa Bongo Fleva licha ya wao kuntoa nyimbo nzuri na hata video nzuri.
“Uongozi wa bendi za muziki ni mgumu
ukilinganisha na mwanamuziki wa Bongo Fleva ambapo kiongozi hana wanamuziki
wengi. Hata hivyo naamini ni wakati na kuna muda utafika muziki huu utakuwa
juu…” alisema Ally Choki.
Choki akithamini mchango mkubwa wa wanamuziki
waliomtangulia, alimuelezea marehemu Muhidin Maalim Gurumo kuwa alikuwa mwalimu
na mtu anayesikiliza ushauri.
Alisema kwamba yeye binafsi nilifanya naye
kazi nyingi zikiwapo zili waizotoa albamu yenye nyimbo zake tatu na za Gurumo
tatu.
“Album hiyo ilifanya vizuri sana na tulipata
fedha nyingi mpaka kila ninapokutana naye akawa anasema nakushukuru sana
kijana….” Alisema Ally Choki.
Akielezea siri ya mafanikio yake , Choki
alieleza kuwa yanatokana na yeye kufanya juhudi, kutokunywa pombe aliyoanchana
nayo mwaka 1994.
Aidha amesema kwamba havuti sigara, amefanikiwa kujenga
nyumba,kununua gari aidha ni baba wa familiya ya mke na watoto sita.
Ikumbukwe kabla ya
kuondoka The African Star, Choki alikwaruzana na mkurugenzi wa ASET Asha
Baraka. Katika purukushani hizo alifika
mbali kwa kutoa kiapo kibaya dhidi ya Mkurugenzi wake Asha Baraka.
Choki akasema kitendo cha ASET kumpeleka mahakamani kumdai gari
ambalo walimpa mwenyewe kilimkera sana. Pia ASET kukataa kurudisha pesa za
Miraji Shakashia vilevile ASET kutothamini michango ya wasanii walioizalishia ASET
pesa nyingi.
Msomaji wa makala haya hauwezi kaumini kwamba Choki
hivi karibuni amerejea tena kwa kishindo kwenye bendi yake ya zamani ya African
Star Entertainment (Twanga Pepeta)
Alitanganzwa mbele ya waandishi wa habari na
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka aliyekuwa amefuatana na Katibu wa bendi, Luiza
Mbutu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment