UNAMKUMBUKA
FRANKLIN BOUKAKA?
Ule usemi
usemao kuwa “Maji hufuata mkondo” unajionesha wazi kwa mwanamuziki Frankin
Boukaka aliyerithi mikoba ya baba yake.
Alikuwa
ni mtoto wa Aubin Boukaka aliyekuwa mwanamuziki wa kundi la ‘The Gaiety’ wakati
mkewe Yvonne Ntsatouabaka alikuwa mshereheshaji
(MC) maarufu kwenye misiba na pia
alikuwa mwanamuziki muimbaji.
Mara
baada ya kuzaliwa Oktoba 10, 1940, alipewa jina la François Boukaka baadae akajulikana
kama Franklin.
Alikuwa mtoto wa kwanza katika familia ya
watoto wanane wavulana watatu na wasichana watano.
Franklin Boukaka alijongezea umaarufu
zaidi nchini mwake pale alipojiunga na wenzie waliotaka kuipindua serikali ya
Kongo Brazzaville wakati huo ikiwa chini ya uongozi wa rais Marien Ngouabi.
Elimu
yake alipata katika shule mbalimbali nchini kwake Kongo Brazzaville.
Franklin alianza kujishighulisha na mambo
ya muziki 1955 katika kundi lililojiita Sexy Jazz.
Kundi hilo lilikuwa likiongozwa
na Miguel Samba, baadae akaanzisha kundi la Negro Band.
Hatimae
katika safari yake ya muziki akaungana na wakali wengine kama Edo Clary Lutula, Jeannot Bombenga, Tabu Ley
,Mutshipile "Casino", André Kambite " Damoiseau ",
Papa Bouanga, Charles Kibongue katika lile kundi maarufu la African Jazz, sauti
ya Franklin imo katika nyimbo kama Mwana
mawa , Catalina cha cha na Marie José zilizotungwa na Tabu Ley.
Mwaka
1959 kundi la African Jazz lilimeguka baada ya wanamuziki wengine walipohamia katika
jiji la Brussels nchini Ubelgiji wakifuatana na wanasiasa wa Kongo kwenye
mazungumzo ya awali ya uhuru wa Kongo.
Wanamuziki
waliobaki akiwemo Jeannot Bombenga, ila
Tabu Ley wakajiunga na kuanzisha kundi jingine lililotingisha nchi lililoitwa
Vox Africa.
Waimbaji wakati huo wakiwa ni akina Franklin Boukaka na Jeannot
Bombenga.
Baada ya
hapo Franklin akaaliacha kundi hilo na kurudi kwao Brazzaville ambako mwaka 1962,
akawa mmoja wa wanamuziki wa bendi ya Cercul Jazz.
Bendi hiyo ilianza miaka ya 1950,
ikiwa chini ya Chama cha vijana kilichokuwa kikipata ufadhili wa serikali ya
Ufaransa.
Chama hicho kiliitwa Cercule Culturel de Bacongo.
Hatimae
Boukaka alikuja kuwa kiongozi wa chama hicho na kikawa na umaarufu wa mkubwa.
Wimbo wa bendi hiyo ‘Pont Sur le Congo’ (Daraja juu ya Mto Congo), ulikuwa una hamasisha
kuunganika kwa Kongo Leopoldville (Kinshasa) na
Kongo Brazzaville baada ya nchi hizo kupata uhuru.
Kufikia hatua hiyo wimbo huo ukapata
umaarufu kuliko nyimbo zote za bendi hiyo.
Baadae Franklin akiwa na gitaa lake kavu
akaanzisha kikundi ambacho kilikuwa na wapiga marimba wawili akaweza kufanya
ziara kadhaa hata nje ya nchi yake na kundi hilo.
Mwaka 1970 Boukaka aliweza kurekodi nyimbo 12 zilizopangwa
vyombo na Manu Dibango. Nyimbo za Nakoki na Le Bucheron ndipo zilipopatikana.
Baada ya hapo Franklin alijiunga na wenziwe waliotaka kuipindua serikali ya Kongo
Brazzaville, wakati huo ikiwa chini ya uongozi wa rais Marien Ngouabi.
Jaribio
hilo lililofanyika tarehe 22 February 1972 lilishindwa na siku chache baadae
kifo cha Boukaka kilitangazwa.
Mungu ailaze roho yake pahala pema pepeni,
Amina.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment