JOSEPH
KABASELE ALIYETAMBA KWENYE MUZIKI WA DANSI
MUZIKI
WA DANSI UNA HISTORIA NDEFU PIA UNA WAPENZI WENGI HAPA TANZANIA NA AFRIKA KWA
UJUMLA.
PASIPO KUWATAJA BAADHI YA MAGWIJI UTAKUWA HUJAKAMILISHA HISTORIA NA
MAELEZO YA MUZIKI UPASWAVYO KUSIMULIA.
JOSEPH
KABASELA TSHAMA ‘GRAND KALLE’ NI MIONGONI MWA HAO ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI HUO HAPA
AFRIKA.
HUYO NDIYE ALIYESAIDIA MUELEKEO WA MUZIKI WA KISASA HUKO JAMHURI YA
KIDEMOKRASIA YA KONGO.
KABASELE
'GRAND KALLE' NDIYE ALIYEKUWA MUANZILISHI NA KIONGOZI WA BENDI YA AFRICAN JAZZ.
BENDI
HIYO ILITOA WANAMUZIKI MAHIRI AKIWAMO MPIGA GITAA MAHIRI, DK. NICO KASANDA.
AIDHA ILISHEHENI NGULI WENGINE AKINA TABU LEY ALIYEKUWA MTYUNZI NAMWIMBAJI WA
BENDI HIYO. MPULIZAJI WA SAXOPHONE ‘MDOMO WA BATA’ MAARUFU MANU DIBANGO.
JOSEPH
KABASELE ALIKUWA AKIITWA BABA WA MTINDO WA RUMBA PIA KINARA WA MUZIKI WA
KIAFRIKA NA MIONGONI MWA WAIMBAJI NA WATUNZI WAKUBWA KATIKA BARA HILI LA AFRIKA
YA WATU WEUSI WANAOZUNGUMZA KIFARANSA.
ALIZALIWA KONGO - MATADI KATIKA FAMILIA MAARUFU ILIYOMJUMUISHA
JOSEPH MALULA AMBAYE ALITOKEA KUWA ASKOFU WA KANISA KATOLIKI.
KABASELE
ALIONDOKEA KUWA MIONGONI MWA WATU WA ZAMA HIZO WALIOELIMIKA. ALIMALIZA ELIMU YA
SEKONDARI NA AKAAJIRIWA KAZI YA MPIGA MASHINE (TYPIST) KWENYE KAMPUNI ZA
BIASHARA KATIKA JIJI LA LEOPOLDVILLE (KINSHASA).
MUZIKI
ULIKUWA KAMA WITO WAKE NA AKAGUNDUA MWANYA WA KUUFUATILIA NA KWENYE MWAKA 1950
AKAWEPO KATIKA STUDIO MPYA ILIYOJULIKANA KWA JINA LA OPIKA.
KATIKA
STUDIO HIYO, ALIUNGANA NA WANAMUZIKI WA MUDA AMBAO WALIYEJULIKANA KWA
JINA LA JIMMY ‘ZACHARIE ELENGA’ AMBAYE ALIKUWA NDIYE NYOTA WA WAKATI HUO.
PIA
WALIKUWEPO WAPIGA MAGITA MASHUHURI GEORGES DOULA NA ALBERT YAMBA YAMBA. BENDI
HIYO HAIKUBAGUA WAPIGAJI WACHANGA AMBAO KAMA ALIVYOKUWA KWAKE YEYE, MWENYEWE
WALIONA MUZIKI NDIO UFUNGUO WA MAFANIKIO BAADAYE WAKIWA NJE YA MIHANGAIKO YA
KAZI NA PIA BAADA YA MAONEVU YA UKOLONI.
MSETO
WA HUO KABASELE, DOULA NA YAMBA YAMBA, ULIIGWA NA BENDI NYINGINE
ILIYOJULIKANA KWA JINA LA OTC BAADA YA KUFANYA ‘PROMOSHENI’ YA FILAMU KWA
AJILI YA RADIO STESHENI YA HAPO KINSHASA AMBAYO ILIKUWA IKITUMIA HERUFI HIZO –
OTC.
KABASELE
ALIWEZA KUBUNI MTINDO WAKE BAADA YA KUHAMASIKA NA KUMUONA MUIMBAJI MACHACHARI
‘TINO ROSI’ AMBAYE SAUTI YAKE YA KUGHANI NA YENYE MVUTO KWENYE NYIMBO ZAKE,
ILIKUWA KIVUTIO KIKUBWA KWA WAKAZI WA MJI WA KINSHASA.
‘GRAND
KALLE’ NYIMBO ZAKE ZA MWANZONI ZILIZO ZILIKUWA MITHIRI YA MOTO MKALI WA
KUOTE MBALI. ILIKUWA KAZI MARIDADI ILIYOTOKANA NA MJUMUIKO WA WANAMUZIKI VIJANA
WA OPIKA, HUSUSANI MPIGA GITAA DK. NICO KASANDA NA MCHEZA GITAA LA KATI
(RHYTHM), KAKA YAKE NICO, CHARLES ‘DECHAUD’ MWAMBA.
WIMBO
PARAFIFI ULIOFYATULIWA MWAKA 1952, ULIKUWA NA MAUDHUI YAKE YA KUMSIFIA
MTANGAZAJI WA RADIO ALIYEKUWA KONGO BRAZZAVILLE.
UTUNZI
WA KABASELE ULIOWEZA KUTIA FORA PAMOJA NA ULE ‘KALE KATO’ WA MWAKA 1952,
ULIHADITHIA JUU YA PENZI LA KABASELE KWA KIMWANA MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA
LA ‘KATHERINE’.
WIMBO
HUO ULIKUWA WA KWANZA WA KIKONGO KUCHEZWA KWA ALA YA ‘SAXOPHONE’, IKIMTUMIA
MPULIAJI WA KUAZIMA ‘FUD CANDRIX’.
KATIKA
KIPINDI CHA KWENYE MIAKA YA 1953 HADI 1955 BENDI MPYA ILIYOWAJUMUISHA JOSEPH
KABASELE, DK. NICO KASANDA NA DECHAUD ILIIBUKA KUTOKA KUWA WANAMUZIKI WA MUDA
WA STUDIO YA OPIKA WAKAJIITA AFRICAN JAZZ, WAKIAZIMA JINA HILO AMBALO HALIKUSHABIHIYANA
NA MTINDO WA MUZIKI WA KIMAREKANI WA ‘JAZZ’ KAMA JINA LILIVYO.
AFRICAN
JAZZ ILIPIGA MUZIKI WA NYIMBO ZAKILATINI NA BENDI ILICHANGIA KWA KIASI KIKUBWA
KUKUA KWA RUMBA LA KIKONGO LILILOIBUKA KIPINDI HICHO.
KABASELE
AKAJULIKANA KAMA ILIYEJULIKANA KAMA ‘LE GRAND KALLE’, UMAARUFU WAKE UKAWA HAUNA
MFANO.
WAIMBAJI
WENGINE KADHAA WALIANZA KUMUIGA STAILI ZAKE KIASI KWAMBA WATU WAKAANZA
KUZUNGUMZIA KUANZISHWA KWA SHULE (MCHAPUO) WA KABASELE AU WA AFRICAN JAZZ.
AIDHA
BAADHI YA NYOTA WENGINE ALIOKUWA NAO KATIKA AFRICAN JAZZ WALIKUWEPO WAIMBAJI
JOSEPH MULAMBA MUJOS, BOMBENGA NA MPIGA GITA TINO BAROZA AMBAPO BENDI HIYO YA
AFRICAN JAZZ ILIWEZA KUWEKA FURSA NZURI KUWA NI UWANJA WA MAFUNZO KWA
WANAMUZIKI VIJANA WA KIZAZI KILICHOFUATIA KONGO.
HADI
KUFIKIA MWAKA 1960 AFRICAN JAZZ ILIKUWA BENDI YA JUU NCHINI HUMO NA KUWEZA
KUFYATUA MAELFU KADHAA YA SANTURI ZILIZOTOLEWA KATIKA NEMBO YA ‘DECCA’ NA
KUWEZA KUWAPATA MASHABIKI WENGI KATIKA KUMBI MBALI MBALI.
JOSEPH
KABASELE ALIKUWA KARIBU SANA NA KUNDI LA ROCK MAMBO, HIYO ILILETA MUUNGANO
MZURI NA KUNDI LAKE LA AFRICAN JAZZ.
ALISHIRIKIANA
NAO NA KUWEZA KUTOA VIBAO VYENYE VIWANGO VIZURI HASA ALIPOKUWA AMESHIRIKIANA NA
JEAN SERGE ESSOUS, NINO MALAPET, ROSSIGNOL NA PANDI.
ILIPOTIMU
MWEZI JANUARI 1960, KABASELE NA KUNDI LAKE LA AFRICAN JAZZ PAMOJA NA WAJUMBE
WAWAKILISHI WA ILIYOKUWA ‘BELGIAN CONGO’ WALIFANYA KITU CHA KIHISTORIA AMBACHO
NI KONGOMANO LA UTAMBULISHO LA KISISASA HUKO BRUSSELS.
MIONGONI
MWA TUNGO ZAKE ALIZOZIFANYA KATIKA KONGOMANO HILO LA KISIASA LA MWAKA HUO, NI
UTUNZI WAKE ULIOJULIKANA KAMA ‘INDEPENDENCE CHA CHA’ NA ULE WA ‘LE TABLE RONDE’
AMBAO KWA PAMOJA ULITAMBULIKA KAMA WIMBO WA KITAIFA KUFIKIA UHURU.
UTUNZI
MWINGINE WA KABASELE ‘BILOMBE BA GAGNE’ (WENYE MAANA WENYE KUJIAMINI
WAMESHINDA).
WIMBO HUO ULIELEZEA MAISHA YA MADHILA CHINI YA UTAWALA WA
WABELGIJI KIPINDI AMABAPO UHURU ULIBADILIKA NA KUELEKEA KWENYE VURUGU.
KABASELE
ALITOA KIBAO KINGINE ‘TOYOKANA TOLIMBISANA NA KONGO’ (WENYE MAANA TUELEWANE NA
TUSAMEHE YALIYOPITA) UKIHIMIZA KUUNGANA WAKONGOMANI.
MWAKA
1960 KABASELE ALIREKODI KIBAO KILICHOJULIKANA ‘OKUKA LOKOLE’ AMBACHO NI
KWA HESHIMA YA MWANAMUZIKI ‘LOUIS ARMSTRONG’ (SATCHMO) AMBAYE ALITEMBELEA KONGO
KWA ZIARA ILIYODHAMINIWA NA SERIKALI YA AMERIKA.
MWAKA
1961 KUNDI LA AFRICAN JAZZ LIKIONGOZWA NA JOSEPH KABASELE LILIFANYA ZIARA NDEFU
KATIKA NCHI ZA AFRIKA MAGHARIBI NA KUSAMBAZA MTINDO WAO ILIOKUWA UMECHANGANYA
MAHADHI YA KIAFRIKA.
KWA
WASIKILIZAJI WA CHANA, NIGERIA, IVORY COAST, SIERRA LEONE NA GUINEA ILILETA
ATHARI KUBWA KWA WANAMUZIKI WA HUKO. KWA MFANO BENDI YA BEMBEYA JAZZ YA NCHINI
GUINEA, ILIWEZA KUFAIDIKA KWA ZIARA HIYO YA KABASELE YA MWAKA 1961 NA KUWEZA
KUZALIWA MUZIKI MCHANGANYIKO WA AFRIKA MAGHARIBI NA LATIN AMERIKA KWA
KUPATIKANA MITINDO YA HIGH-LIFE, JUJU NA AFRO-BEAT.
KABASELE
BAADAYE ALIIBUKA NA KUWA KIONGOZI MKALI, TABIA AMBAYO ILIPELEKEA WANAMUZIKI
WOTE KUHAMA KATIKA BENDI YA AFRICAN JAZZ MWAKA 1963.
ALIJIUNGA
NGUVU NA KUSHIRIKIANA NA MWIMBAJI JEAN BOMBENGA. BOMBENGA ALIKUWA MWANAFUNZI
WAKE ALIYEKUWA KATIKA BENDI YA VOX AFRICA.
KUNDI
HILO LA VOX AFRICA MARA NYINGINE LILITAMBULIKA KAMA AFRICAN JAZZ.
HATA HIVYO
HALIKUFANIKIWA KUFIKIA KIWANGO CHA ILIYOKUWA AFRICAN JAZZ HALISI.
BAADA
YA KUNDI HILO KUFANYA KUREKODI KWAO PAMOJA NA MAONESHO KUWA MACHACHE, LILIKUFA
MWAKA 1969.
BAADAYE
KABASELE AKAFANYA SAFARI YA KWENDA ULAYA KUREKODI AKIWA NA KUNDI LA WANAMUZIKI
WALIKUWEPO STUDIO NA KULIPA JINA ‘AFRICAN TEAM’.
KUNDI
HILO LILIKUWA NA WANAMUZIKI, WAPULIZAJI WA SXOPHONE, MKAMERUNI MANU DIBANGO NA
JEAN SERGE ESSOUS TOKA KONGO BRAZZAVILLE.
ALIKUWEPO PIA MPIGA FLUTI MCUBA DON
GONZALO AMBAO KWA PAMOJA WALICHEZA MIONDOKO YA AFRO-LATIN JAZZ.
MWANZONI
MWA MIAKA YA 1970, KABASELE AKAWA RAISI WA CHAMA CHA HAKI MILIKI CHA KONGO
KINSHASA (SONEKA).
AIDHA
ALIONEKANA JUKWAANI MARA CHACHE SANA KUTOKANA NA MARADHI YA ‘HYPERTENSION’
SUGU(SHINIKIZO LA DAMU) AMBAYO YALIMUANDAMA SANA.
ALIWAHI
KWENDA PARIS MARA MBILI KWA MATIBABU AMAKO ALIKUWA AKIPATA NAFUU YA MUDA.
MWAKA
1980 KABASELE ALITUNIKIWA NISHANI YA ‘MWALIMU MKUU’ WA MUZIKI WA ZAIRE NA UMOJA
WA WANAMUZIKI – UMUZA.
LAKINI
KWA MAPENZI YA MUNGU, MIAKA MITATU BAADAYE FEBRUARY 11, 1983 KABASELE
AKAFARIKI DUNIA AKIWA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.
KABASELE
ANAKUWA MMOJA WA WANAMUZIKI WAKUBWA WA KARNE YA ISHIRINI. ALIKUWA NA SAUTI
PAMOJA NA STAILI KIGEZO, AMBAYO WAIMBAJI WOTE WA KONGO WANGEWEZA KUPIMWA KWA
HIYO. BENDI YAKE YA AFRICAN JAZZ ILIKUWA NI MFANO KWA KILA KUNDI LA BENDI ZA
WAKONGO WALIOFUATIA.
MCHANGO WAKE KATIKA MUENDELEZO WA RUMBA LA KONGO
ULIWAFANYA WAKONGO WOTE KUMWITA ‘BABA WA MUZIKI WA KONGO’.
MUNGU
AIPUMZISHE ROHO YAKE PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment