MJUE "JIM REEVES" ALIYETAMBA
KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI
Hapana shaka watu wazima wenye umri wa mkubwa kama wangu, ukitamka
jina la Jim Reeves, unakuwa umewakuna vilivyo.
Alikuwa ni mwanamuziki wa Kimarekani aliyejikita katika
miondoko ya muziki wa ‘Country’ na muziki wa kawaida kama mtunzi haklikadhalika uimbaji.
Reeves aliweza kuweka rekodi ya muziki wake ukupanda
chati toka miaka ya 1950 hadi ya 1980.
Muziki wake ukawa maarufu na kujulikana kama mwanamuziki wa midundo ya
‘Nashville’ (ambayo ni mchanganyiko wa muziki wa zamani wa country na ule wa
kisasa).
Wasifu wa nguli huyo unaonesha kuwa jina lake halisi alikuwa ikiitwa
James Travis aka “Jim” Reeves aliyezaliwa Agosti 20,
1923 Reeves amezaliwa katika kitongoji cha Galloways huko Texas, nchini
Marekani.
Alitambulika kama ‘Muungwana Jim’ na nyimbo zake ziliendelea kupanda chati kwa
miaka kadhaa hata baada ya kifo chake.
Reeve alikuwa akitoka katika jamii ya watu waliokuwa nje
ya mji karibu na Carthage. Alifariki Julai 31, 1964 akiwa na umri mdogo wa miaka
40 katika ajali ya ndege binafsi.
Yeye alikuwa mwanachama wa muziki wa ‘Country’ na pia
ule wa Texas Country Halls of Fame.
Jim alifanikiwa kupata nafasi ya kusomamsomo ya juu ‘Scholarship’
ambapo alijisaljili kusomea masuala ya kuhutubia na maigizo.
Baada ya miezi
sita katika masomo hayo, aliachana nayo akaamua kwenda kufanya kazi katika yadi
ya kutengeneza Meli huko Houston.
Licha ya kuwa na weledi katika muziki Reeves pia alikuwa
mwanariadha aliyewahi kuchezea ligi za Semi-Professional kabla hajaingia
mkataba na St. Louis Cardinals, timu ya shamba. Mwaka 1944 alicheza kama
right-handed Pitcher.
Aidha alicheza ligi ndogo kwa miaka mitatu kabla
hajaumia na kupata maumivu katika misuli iliyohitimisha juhudi zake za kuendelea
na michezo.
Reeves alianzia kufanya kazi kama mtangazaji wa radio.
Kila wimbo umalizikapo kuupiga radioni, yeye akawa anaimba wimbo huo.
Mwishoni mwa miaka ya 1940, aliingia mikataba na baadhi
ya Makampuni madogo ya kurekodi, huko Texas lakini hakupata mafanikio.
Muziki wa Magharibi ulimfanya kuhamasika sana hususani
alipokuwa akiwasikia wanamuziki kama Jimmie Rodgers na Moon Mullicann.
Waimbaji wengine maarufu wakati huo aliokuwa akiwatamani
ni akina Bing Crosby, Eddy Arnold na Frank Sinatra.
Mapenzi hayo makubwa katika
muziki yalimpelekea kuwa mwanachama wa bendi ya Moon Mulican.
Jim aliweza kufanya mitindo ya mwanzoni za bendi ya
Mullican, nyimbo zake kama ‘Each Beat of My Heart’ na ‘My Heart’s Like a
Welcome Mat’ mnamo miaka ya 1940 mwishoni na mwanzoni 1950.
Reeves aliweza kuimba nyimbo za ‘Mexican Joe’ ambazo zilishika
namba moja mwaka 1953.
Kutoka mwaka 1955 mpaka kuendelea mwaka 1969 Reeves
nyimbo zake ziliendelea kushika ‘ukanda’ hata baada ya yeye kufariki.
Nyimbo zake za kwanza za ‘Country’ zilizompa mafanikio
zilikuwa ni pamoja na ‘I Love You’ alouimba akishirikiana na Ginny Wright, na ‘Mexican
Joe’ ‘Bimbo’.
Nyimbo nyingine zilizotolewa na Fabor Records na Abbott Records ilitoa albam yake ya kwanza Novemba, 1955
iliyojulikana ‘Jim Reeves Sings’.
Mapema mwaka 1955, Reeves alisaini mkataba wa miaka 10
na Kampuni ya RCA Victor chini ya Steve Sholes, ambaye alitoa rekodi za kwanza
za Reeves akitumia Kampuni ya RCA na pia akaingia mkataba na Elvis Presley na
kampuni hiyo hiyo mwaka huo huo.
Alipokuwa akirekodi mwanzoni akiwa na Kampuni ya RCA, Reeves bado alikuwa anaimba
kwa staili ya sauti ya juu ambapo ilionekana ndio kipimo cha nyimbo za
‘Country’ Wanamuziki wa Magharibi kwa wakati huo.
Baadaye Jim alianza kupunguza sauti yake wakati akiimba
na kutumia ‘Pitch’ ya chini akiimba huku midomo yake ikikaribia kugusa kipaza
sauti, ingawaje waliokuwa wanamrekodi (RCA) walikuwa wanailalamikia hali hiyo.
Mwaka 1957 kwa maelekezo ya ‘Produysa’ wake Chet Arkins
alitumia mtindo huo katika toleo la wimbo wa maonesho wa ‘Penzi lililopotea’
uliokusudiwa uimbwe na mwimbaji wa kike.
Katika kipindi chote miaka yote ya 1950 na hadi 1960
mwanzoni, Jim Reeves aliachia nyimbo zake kali zizoshika ‘chati’ za ‘Anna
Marie’ na ‘Blue Boy’ No. 2 za mwaka 1958.
Alifyatua kibao
kingine cha ‘Billy Bayo’ mwaka 1959 na ‘He will have to go’ wa mwaka 1960., ‘Adious
Amigo’ (namba mbili, 1962), ‘Welcome to my World’ (namba mbili, 1964) na ‘I
guess I’m crazy’ (namba moja kwa wiki saba, 1964).
Jim Reeves pia
alikuwa na kikosi na idara ya nyimbo za dini katika jukwaa lake.
Wimbo wake, ‘Danny Boy’ akijitambulisha kwamba wazazi
wake wametokea Irish. Wimbo ‘But You Love Me Daddy’ ukirekodiwa wakati mmoja
akiwepo ‘Steve’ mtoto wa miaka minane wa mpiga gitaa la besi, Bob Moore,
ulikuwa katika ishirini bora huko Ulaya miaka kumi Baadaye.
Rekodi zake mara nyingi zilikuwa na utamanifu wa
kipekee, kama ‘I Love you Because’ (ulishika namba 5) na ‘I won’t forget You’
(namba 3) zilikuwa katika chati huko UK kwa wiki 39 na 25 mfululizo.
Reeves alikuwa amesaidia sana kuanzisha staili mpya ya
muziki wa ‘Country’ akitumia ‘violin’ na ‘mpangilio wa kupendeza wa background
ikijulikana kama ‘Nashville’ sound.
Alipata umaarufu kama muimbaji wa kiume mwenye sauti ya kupendeza na nzito
kiasi, yenye madaha.
Nyimbo kama ‘Adios Amigo’ ‘Welcome to My World’ na ‘Am I
Losing You’ zinaonyesha hili.
Nyimbo zake za Chrismas zikijirudia rudia na
kupendwa sana hasa zikiwa ni pamoja na ‘Chrismas’ ‘Blue Chrismas’ na ‘An Old
Chrismas Card’.
Hali kadhalika Jim Reeves amekuwa hodari kwa kuukweza na
kuzipa maarufu nyimbo nyingi za ‘Injili’ kama ‘We Thank Thee’ ‘Take My Hand,
Precious Lord’ ‘Across The Bridge’ ‘Where We’ll Never Grow Old’ na nyingine
nyingi.
Reeves aliibua mafanikio makubwa kwa utunzi wa Joe
Allison, ‘He’ll have to Go’.
Kwa kweli kulikuwa na mafanikio makubwa kwa muziki
huu wa kawaida na wa ‘Country’ ambapo ulimpatia ‘Platinum Record’ ambayo
ilitolewa mwishoni mwa mwaka 1959 na ilifanikiwa kuwa namba moja katika gazeti la ‘Billboard’.
Katika nyimbo za ‘Country’ ambazo zili ‘hit’ kuanzia 08/February, 1960 na kuendelea kwenye
chati kwa wiki 14 mfululizo hii moja wapo.
Mwana historia wa muziki wa Country, Bill Malone
alionesha kwamba ni katika namna nyingi Reeves aliendeleza utamu na ubora
katika muziki wa ‘Country’ kimpangilio
na ‘melodi’ safi na ujumbe unaogusa
mioyo ya watu.
Kwa nyongeza, Malone alimsifia Reeves kwa staili yake ya
kuimba ambayo anaishusha chini sauti yake, inakuwa kama ya kubembeleza na ndio
maana watu wengi wanatamka kwamba Jim Reeves ni muimbaji mwenye sauti ya mguso.
July 31, 1964, Reeves na mshirika mwenzake wa kibiashara, Meneja Dean Manuel
waliondoka Batesville, Arkansas kupitia Nashville wakitumia ndege ya injini
moja akiwa Reeves anaendesha.
Wawili hao walikuwa wamepata ‘dili’ ya kununua shamba huko
Deadwood Texas, Kaskazini mwa Galloway ambayo ni sehemu aliyozaliwa Reeves.
Wakati wanapaa juu kwa ndege akiwa na Brentwood, Tennessee, walikutana na dhoruba
ya upepo mkali na mvua kubwa.
Katika uchunguzi ilionekana ndege hiyo ndogo
ilinaswa katika dhoruba na Reeves alipata mstuko ikaanguka na wao wakafariki.
Mjane wa marehemu, Mary Reeves alianzisha uvumi kwamba Reeves alikuwa
akiendesha juu chini na aliongeza spidi ili kukwepa dhoruba.
Hata hivyo kulingana na Larry Jordan, maelezo ya mjane
wake kwamba Reeves alikuwa anaendesha chini juu si sahihi.
Kutokana na watu walioiona ajali hiyo jinsi ndege
ilivyoanguka na maelezo yaliyomo kwenye
tape iliyorekodi mwenendo wa ndege.
Pia maelezo ya ripoti ya ajali, kwamba Reeves
alikata kushoto katika jitihada zake za kuipata Franklin road ili afike uwanja
wa ndege aweze kutua.
Katika jitihada yake hiyo akazidi kuelekea kule kwenye mvua kubwa.
Katika kuhangaika ili akakipate kiwanja ili kutua, spidi ya ndege ikawa ipo chini hivyo
akaikwaza ndege.
Reeves alitegemea zaidi hisia zake katika kumuongoza na
hakutumia maarifa aliyofundishwa chuoni
kuikabili hali kama hiyo.
Baada ya masaa 42 mabaki ya ndege yalionekana ikiwa mbele, yaani usoni pamoja na injini vimejikita
ardhini. Reeves na mwenzake walikutwa
tayari wamekwisha fariki.
Jim Reeves alizikwa katika kipande cha ardhi maalum
ubavuni mwa ‘Highway 79’ Texas.
Licha ya kufariki Jim Reeves bado umaarufu wake haukupotea, kwa hakika mauzo ya
kazi zake yameongezeka baada ya kufariki.
Mjane wake, Mary Reeves (70) alifariki katika siku ya
‘Veteran’ Tarehe Novemba 11, 1999, iliripotiwa kuwa amekufa akiwa peke yake katika
nyumba ya kuuguza wagonjwa.
Hata hivyo mazishi yake yalipangwa kwa watu wachache tu
wa karibu ikiwa hii ni agizo la aliyekuwa mumewe wa pili Tery Davis.
Tangu kipindi cha kifo cha Jim Reeves kulipotokea, Mary alipatwa
na matatizo ya kuugua kabla hayajamzidia.
Alikuwa ni kiungo muhimu katika kuuweka
muziki wa Reeves na kumbukumbu zake alizifanya kuwa hai.
Kutokana na Mary Reeves Davis kushindwa kutokana na
ugonjwa kuzisimamia mali za Jim Reeves ziliuzwa kwa ‘United Show of America’
mwaka 1997 kwa thamani ya Dola za
Kimarekani milioni 7.3
Jim Reeves aliwekwa kwenye kundi la mwimbaji Nyota wa Kiume
ambaye ametokeza katika midundo ya ‘Nashville Sound’.
Sauti yake laini ya kidume yenye madaha imeendelea
kusikika hadi wakati leo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment