Na Moshy Kiyungi.
SHEM IBRAHIM KARENGA ni mmoja
kati ya wanamuziki wachache wenye uwezo wa kucharaza gita huku akiimba kwa
wakati mmoja. Shem alitamba sana
miaka ya 1970 akiwa na bendi ya Tabora
Jazz wana Segere Matata.
Alizaliwa mwaka 1950 eneo la
Bangwe mkoani Kigoma na kupata elimu yake katika shule ya msingi Kihezya kati
ya mwaka 1957 na 1964.
Alianza kujifunza muziki
akiwa mwanafunzi katika shule ya wamissionari na huko ndiko fani hiyo ilianza kuchipua
hatimaye mwaka huo huo wa 1964 akajiunga
na bendi ya Lake Tanganyika Jazz iliyokuwa na maskani yake mjini Kigoma.
Alipoingia Lake Tanganyika
Jazz alijifunza Ala
za muziki za drums, Kinanda na gita la rhythm, Solo. Besi gita pamoja akiimba.
Alidumu katika bendi hiyo kwa kipindi cha miaka
minane na mwaka 1972 Shem Kalenga aliitwa katika bendi ya Tabora Jazz ambako
aliingia kwa kishindo na nyimbo zake alizozitunga akiwa na Lake Jazz
na kuanza kuzipiga katika bendi yake mpya.
Nyimbo hizo zilikuwa Dada Asha
na Remmy ambazo zilimpa umaarufu na kujulikana kwa haraka na kuwa simulizi katika
kila pembe za mji huo wa Tabora.
Shem alipata ushindani mkubwa
baada ya kuwakuta wakali wengine wa kupiga gita akina Kassimu Kaluwona, Athuman
Tembo pamoja na Salumu Luzila na Issa
Ramadhan ‘Baba Isaya’ lakini alijitutumua
na kuwa mmoja kati ya wapiga solo gita
bora la katika bendi hiyo.
Mwaka wa 1983 Shem Kalenga
aliicha bendi hiyo kwa sababu zake mwenyewe na kuachana na mambo ya muziki kwa
muda.Lakini baada ya kuondoka yeye bendi hiyo haikudumu tena na ikapotea katika
ramani ya muziki.
Aliondoka Tabora mwaka 1990
baada ya kuitwa na mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam Baraka Msilwa ambaye alimuomba ajiunge
katika bendi yake ya M.K. Beat iliyokuwa ikipiga katika mtindo wa ‘Tunkunyema’
Bendi hiyo ilikuwa ndugu na ile ya M.K. Group.
Ndani ya M.K.Beat Shem
Kalenga aliwakuta vijana machachari akina
Maliki Star, Bwani Fanfan, Sisco Lunanga
na Fungo Shomari. Kwa mshikamano waliokuwa nao waliweza kuiinua Bendi hiyo vilivyo na kuwa
tishio kwa bendi zingine za jijini Dar
es Salaam.
Bendi hiyo ilisambaratika
mwaka 1995 na mwaka uliofuatia alianzisha bendi yake ya Tabora Jazz Star ambayo
ina wanamuziki sita na huburudisha katika kumbi mbalimbali za jijini Dar es
Salaam hadi sasa.
Anasema miaka ya hivi karibuni
biashara huria ziliporuhusiwa, Studio nyingi binafsi zilifunguliwa lakini hazina
manufaa kwao kufuatia kiwango cha pesa zinazotozwa na Studio hizo kuwa kubwa mno kiasi cha wao kushindwa kumudu
kulipia.
Kalenga anatoa wito kwa
Serikali aidha kwa wafadhili kuwaona kwa
jicho la huruma wanamuziki hao wazamani kuwawezasha kwa vile bado wanao uwezo mkubwa wa kupiga
muziki na kutoa elimu kwa jamii pamoja burudani kwa wapenzi kama zamani.
Anajutia umaskini na ufinyu
wa fikra uliowakumba wanamuziki wa dansi wa zamani umewafanya kushindwa
kujitutumua na kwamba wanchosubiri ni kudra za mwenye mungu, serikali,
wafadhili au yeyote atakayeguswa kutaka
kuwakwamua wakongwe hao kwa kuwapatia
vyombo vya muziki.
Shem Kalenga anakumbuka miaka
ya nyuma jinsi Serikali ilivyokuwa ikiwasaidia kurekodi nyimbo zao bure katika
Studio za Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), ambapo gharama yao
ilikuwa ni nauli ya kwenda Dar na kurejea Tabora.
Anaendelea kuifagilia Studio RTD
enzi hizo ilivyokuwa ikichuja nyimbo zao
tofauti na sasa ambapo Studio nyingi zinarekodi pasipo kuzichuja
matokeo yake baadhi ya nyimbo zinazosikika katika vituo vya redio hazina
maadili mema kwa jamii.
Mzee mzima Kalenga ambaye
sifa zake zimezagaa kila kona Afrika ya Mashariki na Kati anawaasa vijana wa
muziki wa kizazi kipya kujifunza kupiga Ala
za muziki badala ya kutembea na CD mkononi.
PICHA ZAIDI.
PICHA ZAIDI.
MTUNZI NA MWIMBAJI WA SOUKOUS STARS, MAYAULA MAYONI, AKIMPONGEZA SHEM KARENGA{kushoto} KWA UHODARI WA KULIKUNG'UTA SOLO,JIJINI DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment