BOZI BOZIANA NA ANTI-CHOC
Aprill 15,2014.
Bozi Boziana au ‘Mzee Benzi’ kama anavyojulikana na wengi ni mwanamuziki
anayeongoza kundi zima la Anti Choc toka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Jina lake kamili anaitwa Mbenzu Ngamboni Boskill ambaye alizaliwa mwaka 1952 huko Jamhuri ya Kidemkokrasia ya
Kongo.
Pamoja na utunzi na uimbaji Bozi pia ni mkung’utaji mzuri wa gita
aliyepiga katika bendi nyingi kubwa nchini mwao zinazopiga katika mtindo wa
soukous.
Bendi alizowahi kupigia ni pamoja na
Bamboula de Papa Noel, Minzoto Sangela, Zaiko Langa
Langa, Isifi Lokole, Yoka Lokole,
Langa Langa Stars na Choc Stars.
Baadaye akaunda
bendi yake Orchestra Anti-Choc.
Mzee Benzi
aliazia muziki wa Afro-Pop katika bendi ya
Air Marine lakini alianza kuyaona
mafanikio ya kazi zake ilipotimu mwaka 1974 alipojiunga na bendi ya Zaiko Langa Langa.
Zaiko LangaLanga ilikuwa na waimbaji
mashuhuri wakati huo wakiongozwa
na mkongwe Papa Wemba
na mwezake Evoloko Jocker.
Lakini
haikuzidi mwaka , Papa Wemba na Evoloko waliondoka Zaiko Langa Langa na Bozi
Boziana aliwafuata kwenda kuanzisha
bendi mpya ikaitwa Isifi Lokole.
Kutokukubaliana
katika maswala mbalimbali ya msingi kulimfanya wanamuziki Papa Wemba, Boziana, Mavuela Somo na wengine kuondoka bendi ya
Isifi Lokole na wakaunda bendi mpya iliyopewa jina la Yoka Lokole.
Yoka Lokole
ilipata mafanikio makubwa mwaka
1976 lakini mwinshoni mwa mwaka huohuo
Papa Wemba aliicha bendi hiyo na akaenda kuanzisha bendi ya Viva la Musica.
Bozi Boziana
naye mwaka 1977 akaondoka Yoka Lokole licha ya bendi hiyo kuwa maarufu kwa
kipindi kifupi.
Kwa miezi
michache Boziana alishirikiana na
mwanamuziki Efonge Gina, ambaye naye alikuwa katika
bendi ya Zaiko Langa Langa. Walirekodi nyimbo kadhaa kama vile Selemani iliyotungwa na Bozi na Libanko
Ya Ngai utunzi wake Gina.
Produza Verckys Kiamuangana mwaka
1981 aliibadilisha bendi ya Soukous super group
na kuita Langa Langa Stars
ikiwa imesheheni vipaji vya wanamuziki kaiwemo Evoloko Jocker, Dindo Yogo
na wnengine wengi. Bozi Biziana aliakwa kujiunga vijana hao naye
akaubali na kuicha Zaiko Langa kwa mara
ya pili.
Langa Langa Stars ilidumu kwa miaka michache
iliyofuatia kabla na Boziana naye akaondoka kwenda kujiunga na bendi kubwa
nchini humo Choc Stars aliyokuwa chini Ben Nyamabo ambako alipiga hadi mwezi
Novemba 1985.
Akiwa na bendi
hiyo ya Choc Stars Boziana alirekodi baadhi ya nyimbo ambazo zilikuja kuwa
maarufu za Sandu Kotti, Alena, Mbuta-Mutu na Retrouvailles
a Paris.
Anti –Choc
ilikuwa na wanamuziki wengi wenye vipaji lukuki wakiwemo akina Fifi Mofude, Djo Nolo, Koffi Alibaba, Wally Ngonda, Rigo Star,
Ngouma Lokito, Deesse Mukangi, Marthe Lamugenia, Ngimbi Yespe na Maoussi Solange.
Mpiga gita wa
kwanza katika bendi hiyo alikuwa Matou Samuel ambaye kwa sasa anaimba muziki wa Injili na nafasi yake ilishikwa na Dodoly ambaye kabla
ya kujiunga humo alitokea katika bendi ya mwanamuziki Lita Bembo
ya Orchestre Stukas.
Dodoly
alipachikwa jina bandia la ‘The sewing machine’
kwa umahiri wake wa kutumia vidole vyake kucharaza nyuzi kwa kasi kubwa.
Tokea miaka ya
1980 Boziana aliendelea katika bendi
yake ya Anti-Choc ikiwa ni pamoja na kurekodi nyimbo akishirikiana na wanamuziki wengine mahiri.
Boziana aliwahi
kushinda zawadi ya Kora All-African kwa album yake kuwa bora toka nchi
za Afrika ya Kati.
Kwa
wapenzi wa muziki hapa nchini watamkumbuka Bozi jinsi alivyoteka wapenzi katika
maonesho kadhaa aliyoyafanya hapa nchini kwa ushirikiano walioonshea kati ya
Bozi Boziana, Deesse Mukangi na Joly Detta walivyokuwa wakilishambulia jukwaa
kwka staili ya ‘Nzawisa’ katika nyimbo za Tembe na Tembe, Palpitation na
zingine nyingi zilifanya watu kuviacha viti vyao kwenda kuwatuza.
Bozi Boziana ana sauti nzuri, yakupendeza akimba huku
akipokezana na timu yake ya wanadada wawili, Joly pamoja na Deesse.
Sifa nyingine za mwanamuziki huyu mzee Benzi ni kwamba
muziki wake hauna mwingiliano kati ya sauti ,gitaa na synthesizer katika nyimbo
zake zote. Mfano katika wimbo wa ‘Ngoyartong020’ tune tatu za mwanzo
Boziboziana amemshirkisha Jolly Detta na Deesse, na sehemu ya pili ya wimbo huo aliongeza
nguvu kwa kumuongeza waimbaji na wanenguaji
Scola Miel maarufu kwa jina ‘Nzawissa’ na Betty. Bozi alifyatua vibao
vingi vilivyompa sifa nyingi ukiwemo wa La reine de Sabah, Lelo Makambo Lobi
Makambo Evelyne na Fleur de Lys ambazo alimshirikisha mwimbaji wa kike Joly
Delta.
Boziana aliachia wimbo mwingine akimshirikisha Deesse na
Ba Bokilo.
Bozi Boziana na bendi yake bado anaendeleza muziki akiwa
na bendi yake na watanzania watakumbuka kwa mara ya mwisho alikuja hapa nchini
kwa mwaliko wa African Stars Entertainment Tanzania (ASET) iliyo chini ya
uongozi wa Mkurugenzi Asha Baraka.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment