JABARI LA MUZIKI MARIJANI RAJABU
APRILI 15,2014.
MARIJANI
RAJABU KWELI HATUNAYE TENA HAPA DUNIANI LAKINI KAMWE WADAU NA
WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI HAWATAMSAHAU.
ALIKUWA MMOJA MIONGONI MWA WANAMUZIKI WALIOTOA MCHANGO
MKUBWA WA MAENDELEO YA NCHI KUPITIA TUNGO ZA NYIMBO ZAKE MARIDHAWA ZILIZOKUWA ZIKIENDANA NA WAKATI.
MARIJANI MWEZI MACHI 23, 2014, ALITIMIZA MIAKA 18 TOKA
KIFO CHAKE. NGULI HUYO ALIFARIKI MACHI 23, 1995 NA KUZIKWA SIKU ILIYOFUATIA YA
MACHI 24, 2013 KATIKA MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM.
MARIJANI ALIZALIWA TAREHE MARCHI 03, 1955 KARIAKOO,
JIJINI DAR ES SALAAM. KWA MAPENZI YAKE MUNGU, AKAMCHUKUA AKIWA NA UMRI MDOGO WA
MIAKA 40 TU.
ALIKUWA AKITUNGA NA KUIMBA NYIMBO ZILIZOKUWA ZIMEJAA
MAUDHUI MEMA KWA JAMII, IKIZINGATIWA KWAMBA TAKRIBAN NYIMBO ZAKE ZOTE ZILIKUWA
NI VISA VYA KWELI.
NGULI HUYO ALIKUWA NI MITHIRI YA ‘MTAMBO’ WA KUREKEBISHA
TABIA YA MTU YEYOTE ALIYEFANYA MAMBO KINYUME CHA MAADILI PASIPO KUJALI CHEO,
URAFIKI, UDUGU HATA UKARIBU.
UBORA WA MASHAIRI KATIKA NYIMBO HIZO, NI KATI YA SABABU
ZA KUENDELEA KUPENDWA NA WAPENZI WA MUZIKI HAPA NCHINI HADI KUFIKIA KUITWA
‘JABARI LA MUZIKI’
KILA KUMBI ZA STAREHE UTAKAZOINGIA HAPA NCHINI, NYIMBO
ZAKE HAZIKOSI KUSIKIKA ZIKIRINDIMA. HALI KADHALIKA BENDI ZETU ZA MUZIKI WA
DANSI ZILIZOSALIA NAZO HAZIWEZI KUMALIZA ONESHO PASIPO KUPIGA ANGALAU WIMBO
MMOJA WA NGULI HUYO.
WASIFU WA MARIJAN RAJABU UNAELEZA KWAMBA MAMA YAKE
ALIKUWA MAMA WA NYUMBANI WAKATI BABA YAKE ALIKUWA NA SHUGHULI ZA UCHAPISHAJI.
MAISHA YAKE YA UTOTO YALIKUWA YA KAWAIDA ILA ALIKUWA
AKIPENDA SANA UIMBAJI WA TABU LEY, MWIMBAJI TOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA
CONGO NA MWIMBAJI TOKA NCHINI GUINEA, SORRY KANDIA. PIA ALIKUWA AKICHEZA MPIRA
WA MIGUU.
ALILELEWA KATIKA MISINGI YA DINI YA KIISLAM KWA HIVYO
ALIHUDHURIA MAFUNZO YA DINI UTOTONI KAMA INAVYOTAKIWA.
ALIPOKARIBIA UMRI
WA MIAKA 18, NURU YAKE YA KATIKA MUZIKI ILIANZA KUNG’ARA, BAADAYE ALIJIUNGA NA
BENDI YA STC JAZZ, IKIWA CHINI YA MPIGA GITAA MAARUFU WAKATI HUO RAPHAEL
SABUNI. KABLA YA HAPO, BENDI HIYO
ILIKUWA UNAJULIKANA KAMA THE JETS.
AKIWA KATIKA BENDI HIYO MARIJANI ALIWEZA KUTOKA NJE YA
TANZANIA KWA MARA YA KWANZA AMBAPO ALIKWENDA NAIROBI NCHINI KENYA.
KATIKA SAFARI HIYO ALIAMBATANA NA BENDI KWA MADHUMUNI YA
KWENDA KUREKODI NYIMBO ZILIZOTOKA KATIKA NEMBO
YA PHILLIPS.
AKIWA NA BENDI HIYO YA STC, UONGOZI WA SHULE YA
SEKONDARI YAKE YA TAMBAZA ULILETA MALALAMIKO KWA UONGOZI WA STC ILIYOKUWA
IKIMILIKI BENDI HIYO JAMBO AMPALO STC IKALAZIMIKA KUMUENGUA.
MWAKA 1972 MARIJANI ALIHAMIA BENDI YA SAFARI TRIPPERS,
ILYOKUWA INAUNDWA NA VIJANA WENZAKE NA HAIKUWA IKIMILIKIWA NA CHOMBO CHA UMMA.
JAMBO PEKEE MARIJANI ALIONEKANA KWAMBA ALIKUWA
‘AMEBANWA’ HUKO STC KATIKA FURSA YA KUNG’ARA KATIKA UIMBAJI, UBORA WAKATI HUO
ALIFINGUKA HASWA NA KUWEZA KUINYANYUA SAFARI TRIPPERS KUWA MOJA YA BENDI
MAARUFU HAPA NCHINI.
ALIWAKUTA VIJANA WENZAKE AKINA DAVID MUSSA ALIYEKUWA
AKIPIGA GITA LA SOLO NA KUIMBA. DAVI HIVI SASA NI MLOKOLE AMEACHANA NA MAMBO YA
MUZIKI ANAISHI KARIBU NA KLABU YA TTC CHANG’OMBE.
WENGINE WALIKUWA ALLI RAJABU (MWIMBAJI), CHRISTIAN
KAZINDUKI ALIYEKUWA AKILIUNGURUMISHA GITA ZITO LA BESI, JOSEPH BERNARD KWA
UPANDE WA SAXOPHONE NA JEFF AMBAO HADI
SASA WANAPIGA KATIKA BENDI YA MLIMANI PARK WALIOJIUNGA NAYO MWAKA 1978.
WALIWEZA KUTOA VIBAO VILIVYOPENDWA MFULULIZO PIA
WALIZUNGUKA NCHI NZIMA. VIBAO KAMA ROSA NENDA SHULE, MATILDA, BABA NYERERE
MLEZI, MKUKI MOYONI, KUMEKUCHA AMBAO ULIPENDWA NA RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM
(RTD) NA KUFANYWA KUWA KIAMSHO CHA KIPINDI CHA KUMEKUCHAKILICHOKUWA KIKIRUSHWA
KILA CHA ALFAJIRI.
SAFARI TRIPPERS
ILIKUWA KATIKA USHINDANI NA BENDI NYINGINE ZA VIJANA NA HASA AFRO 70, ILIWEZA
KUUZA ZAIDI YA NAKALA 10,000 ZA SANTURI NA HIVYO KUWEZESHA BENDI KUNUNUA VYOMBO
VYAKE VIZURI AINA YA RANGERS VILIVYOKUWA MAARUFU WAKATI HUO, IKIWA NA MAKAO
YAKE MAKUU ENEO LA CHANG’OMBE UHINDINI, TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM.
‘JABALI LA MUZIKI’ MARIJANI ALIHUSUDU KWA KIASI KIKUBWA
UIMBAJI WA ALIYEKUWA KIONGOZI WA EMPIRE BAKUBA KABASELE YAMPANYA ‘ PEPE KALE’
HATA BAADHI YA NYIMBO ZAKE ZILIKUWA AKIZIGHANI, ZIKISHABIHIANA NA LADHA YA
UIMBAJI WA PEPE KALE.
‘LAKUVUNDA HALINA UBANI’ MSEMO HUU ULIJIONESHA WAZI PALE
MAELEWANO MABAYA KATI YA WANAHISA WANNE WA BENDI HIYO, YALIYOPELEKEA
KUSAMBARATIKA LICHA YA BENDI HIYO AMBAYO ILIKUWA IKO JUU KIMUZIKI WAKATI HUO
MWAKA 1978.
MARIJANI AKIAMBATANA NA WENZAKE KAZINDUKI ‘PACHA’ WAKE KATIKA KUIMBA HATA KUSHABIHIANA MAJINA,
ALLY RAJABU, BENARD NA JEFF WAKAJIUNGA
NA BENDI MPYA YA DAR INTERNATIONAL ILIYOKUWA ILIYOONGOZWA NA MPIGAJI GITA LA
SOLO ABEL BARTAZAR ALIYEAMBATANA NA GWIJI MWINGINE MUHIDINI GURUMO.
WAKIUNGANA NA WANAMUZIKI
WENGINE, MAHIRI WALISHIKAMANA KUUNDA KIKOSI ‘MOTO’ AMBACHO BAADA YA KUPAKUA ‘VIBAO’ VYAKE VYA KWANZA
UKIWEMO WA ‘MARGARET’ WALITIKISA ANGA YA MUZIKI HAPA NCHINI.
KATIKA BENDI HIYO YA DAR INTERNATIONAL WALIKUTA WANAMUZIKI
WAZURI NAO WAKAONGEZA NGUVU NA KUIFANYA
BENDI HIYO KUPATA UMAARUFU WA HALI YA JUU KWA VIBAO VYAKE KAMA ZUWENA NA
MWANAMEKA, AMBAVYO VILITAMBA KATIKA VIPINDI KADHAA VYA SALAMU VYA RADIO
TANZANIA DAR ES SALAAM (RTD) WAKATI HUO.
HALI YA WAKATI ULE, BENDI ILIREKODI VIBAO VYAO RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM (RTD) NA
KUAMBULIA SHILINGI 2,500 TU.
YAELEZWA KWAMBA NYIMBO ZAO TISA ZILIUZWA KWA KAMPUNI YA
POLYGRAM BILA YA RIDHAA YAO.
KATI YA MWAKA 1979 NA 1986 BENDI ILIPIGA MUZIKI KARIBU
KILA WILAYA HAPA NCHINI KWA MINAJIRI YA
KUTOA ELIMU SANJARI NA KUWABURUDISHA WANANCHI WAKIPIGA KATIKA MTINDO WAO WA
SUPER BOMBOKA.
MARA NYINGI ILIPOKUWA HAPA DAR ES SALAAM, KAMA
ILIVYOKUWA SAFARI TRIPPERS, MAKAO YAKE MAKUU YALIKUWA KATIKA HOTELI YA PRINCESS
MNAZI MMOJA, SUPER BOMBOKA LILISAKATWA KILA WIKI, KATIKA UKUMBI WA SUPER FANAKA
BUGURUNI.
‘MBIO ZA SAKAFUNI
HUISHI UKINGONI’ UCHAKAVU WA VYOMBO
HATIMAE MWAKA HUO 1986, UKAMALIZA MBIO NDEFU ZA BENDI HII.
MARIJANI RAJABU ‘JABARI LA MUZIKI’ ALIKUWA MMOJA KATI YA
WANAMUZIKI 57 WALIOUNDA KUNDI LA WASANII LIKIJULIKANA KAMA TANZANIA ALL STARS,
MWAKA 1987.
KUNDI HILO LILITIA FORA MKWA WIMBO WAKE WA ‘FAGIO LA
CHUMA’ WIMBO HUO ULIKUWA NI KUITIKIA
KAULIMBIU YA RAIS WA AWAMU YA PILI ALI HASSAN MWINYI, JUU YA UWAJIBIKAJI.
KUNDI HILO LILIREKODI VIBAO VINGINE VINNE AMBAVYO SI
RAHISI KWA BENDI ZILIZOPO SASA KUFIKIA UBORA WAKE KIMUZIKI.
KUNA WAKATI DAR INTERNATIONAL ILISIMAMA KIMUZIKI,
MARIJANI ALISHIRIKI KUPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA
(JWTZ) YA MWENGE JAZZ AMBAKO ALIPIGA MUZIKI
KWA MUDA MFUPI.
MARIJANI ALIPIGA HODI KATIKA JIJI LA ARUSHA NA KUJIUNGA
NA BENDI YA KURUGENZI JAZZ AMBAKO HUKO ALIDUMU MWAKA MMOJA PEKEE NA KUREJEA DAR
ES SALAAM.
MFANYABIAHARA MMOJA WA JIJINI DAR ES SAAM ALIYEJULIKANA
KWA JINA ROGER MALILA,ALIMCHUKUWA MARIJANI KWA AJILI YA KUANZISHA BENDI YA
ORCHESTRA BENE BENE. BENDI HIYO WAKATI HUO ILITAMBA NA MTINDO WAKE WA ‘MAHEPE’
MWANZONI MWA MIAKA YA 1990.
MARIJANI KWA MARA NYINGINE TENA BAHATI HAIUKUWA UPANDE
WAKE, KWANI BENDI HIYO HAIKUDUMU KWA KIPINDI KIREFU KUFUATIA UKOSEFU WA VYOMBO
VYA MUZIKI. HATIMAYE MAMBO YAKAENDA KOMBO TOFAUTI NA WALIVYOTARAJIA.
BAADA KUHANGAIKA KWA MUDA MREFU HUKU NA KULE MARIJANI ‘JABARI LA MUZIKI’
ALIAMUA KUTHUBUTU KWA KUANZISHA KUNDI LAKE LA MUZIKI LIKIITWA AFRICULTURE.
LAKINI NAYO HAIKUDUMU NAYO IKAFA ‘KIFO CHA MENDE.’
MAISHA YA MWANADAMU NI KITENDAWILI KILICHOJAA MAJARIBU
MENGI.
INAELEZWA KWAMBA KUFIKIA MWAKA 1992, HALI YA MAISHA YA
MARIJANI ILIKUWA NGUMU KUPITA KIASI. ALIFIKIA KUENDESHA MAISHA YAKE KWA KUUZA
KANDA ZA NYIMBO ZAKE. ALIJENGA KIBANDA NJE YA NYUMBA YAKE, MAENEO YA KARIAKOO,
JIJINI DAR ES SALAAM.
PAMOJA NA NYIMBO NYINGI, ZA KUIMBIA CHAMA TAWALA NA
SERIKALI, NA HATA TUNGO YAKE MWANAMEKA KUTUMIWA KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA
NNE, MARIJANI RAJABU HADI SEPTEMBA 09, 2012
NDIPO RAIS DK. JAKAYA KIKWETE ALIPOMTUNUKIA TUZO YA HESHIMA YA MUUNGANO
KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU
IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.
WASANII WENGINE WALIOTUNUKIWA SIKU HIYO NI PAMOJA NA
KIONGOZI WA ZAMANI WA MSONDO NGOMA, MUHIDINI GURUMO, MWIMBAJI WA MKONGWE WA TAARABU, FATUMA BINT BARAKA, MSANII WA
MAIGIZO YA FILAMU, FUNDI SAID ‘MZEE KIPARA’ NA MWANARIADHA MKONGWE JOHN STEVEN
AKWARI.
HAPANA SHAKA UTAKUWA UNAZIKUMBUKA NYIMBO ZA NGULI HUYU
ALIZOTUNGA NA ZINGINE KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUIMBA KAMA VILE MASUDI, HABARI
YAKO, SAUTI YAKO NYORORO, BABA ANNA, KITINDA MIMBA, SALAMA NAKUITA, NAMSAKA
MBAYA WANGU, ZUWENA NA NDOA YA MATESO.
MARIJANI RAJABU HAKUISHIA HAPO KWANI ALITOKA NA NYIMBO
ZANGINE ZA TABU NI HALI YA DUNIA, NDOA YA MATESO, NAMSAKA MBAYA WANGU, MAMA
WATOTO, TAMAA MBELE NA BABA WATOTO AMBAZO ZILIGUSA HISIA ZA WAPENZI WA MUZIKI NA WALE WAKAWAIDA WALIOKUWA
WAKISIKILIZA REDIO.
NYIMBO WA ‘UKE WENZA UNA MAMBO’, ULIOFYATUA, NDOA NYINGI
ZA MITARA ZILIJIREKEBISHA KITABIA.
WIMBO WA GEORGINA ULIKUWA WIMBO ULIOTIA FORA MIONGIONI
MWA NYIMBO BORA HAPA NCHINI.
MTUNZI WA WIMBO HUO WA GEORGINA ALIKUWA WANAMUZIKI
MKUNG’UTAJI GITA LA RHYTHM MAHIRI NCHINI JUMANNE UVURUGE, UKAIMBWA KWA UMAHIRI
MKUBWA KWA SAUTI YENYE HISIA KALI NA MARIJANI RAJABU.
MARIJANI ALITHUBUTU KUKEMEA TABIA MBOVU YA NDUGU YAKE WA
KARIBU KUPITIA WIMBO WA ‘CHAKUBANGA’.
WIMBO HUO ULIKUWA NI KISA CHA KWELI AMBACHO NDUGU YAKE HUYO BAADA YA
KUTOKA ULAYA, AKAJIITA JOHN SMITH BADALA YA JINA LAKE HALISI LA CHAKUBANGA.
KUPATA LADHA HALISI YA WIMBO HUO, SEHEMU FUPI YA GHANI
ZAKE KATIKA KIBAO CHA CHAKUBANGA NI KAMA IFUATAVYO:
“LEO KIJANA NINASEMA EEH! HAYO MAMBO YAKO UNAYOFANYA
EEH, MWISHO WAKE BWANA, MAMBO YATAKUWA MABAYA, WALA USIDANGAYIKE NA CHEO
ULICHOPATA, KUDHARAU WAZAZI KUHADAIKA NA DUNIA, MWANA VIBAYA EEH, VIBAYA MWANA
VIBAYAA.
“FIKIRI KWANZA ULIKOTOKAA, USIJIFANYE HUNA BABA WALA
MAMA WALIO KULEA, KWA TAABU NYINGI NA MASHAKA , WAKAKUSOMESHA UKAHITIMU
MAFUNZO, MBONA UNAWANYANYASA NA MATUSI KUWATUKANAAA, MWANA VIBAYAA, VIBAYA
MWANA VIBAYAA. MAMBO YA AJABU ULIYOFANYA EEH, ULIPOCHAGULIWA KWENDA NG’AMBOO
ULIPORUDU BWANA, NA JINA UMEBADILISHA, JINA LAKO CHAKUBANGA, UNAJIITA JOHN
SMITH, NA MWENDO UMEBADILI BEGA MOJA UMELISHUSHA…”
NYIMBO ZA NGULI
HUYU ZITAENDELEA KUSIKIKA VIZAZI NA VIZAZI KWAKUWA ZIMEBEBA UJUMBE MZITO KWA JAMII
YEYOTE ILE.
JE, TUNAMUENZIJE MARIJANI RAJABU? USHAURI WANGU KWA VIJANA WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA
KUFUATA NA KUYAENDELEZA YOTE MAZURI YA WATANGULIZI WAO KAMA AKINA MARIJANI,
GURUMO, MBARAKA MWINSHEHE NA WENGINE WENGI.
MUNGU AIWEKE ROHO YAKE PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment