YVONNE CHAKA CHAKA.
YVONNE CHA CHAKA
ALIKUWA MSANII WA MUZIKI YA KATIKA MIAKA YA 1980 NA KWA JUHUDI
ZAKE HISASA NI MTANGAZAJI NA MWENDESHA KIPINDI KATIKA KITUO CHA NEW
MILLENNIUM,CHAKA CHAKA NI MBURUDISHAJI MAARUFU WA AFRIKA KUSINI NA AFRIKA KWA
UJUMLA.
CHAKA CHAKA KWA MARA YA KWANZA ALITIKISA KATIKA MUZIKI
WA AFRIKA KUSINI AKIWA KIJANA MNAMO MWAKA 1984 KWA WIMBO WA “I’M IN LOVE WITH A
DJ”. MUZIKI WA DISKO ULIOTENGENEZWA NA SELLO ‘CHICCO’ TWALA AMBAO ULITENGENEZWA
KWA MUZIKI WA ASILI YA MBAGANGA KUTOKA MJINI MWA AFRIKA KUSINI,LAKINI UKIWA NA
MASHAIRI YA KIINGEREZA. MTINDO HUO ULIWEZA KUJULIKANA KAMA ‘BUBBLEGUM’ NA
YVONNE CHAKA CHAKA SAMBAMBA NA BRENDA FASSI WALIBAKI WAKITAMBA KWA MIAKA HIYO
YA 1980.
SAUTI YAKE NZURI ILIJIDHIHIRISHA KATIKA ALBAMU YA
UMQOMBOTHI MWAKA 1988 KATIKA WIMBO ULIOKUWA NA JINA LILELILE LA “I’M LOVE WITH
A DJ”.ALBAMU HII AMBAYO ILIKUWA INASIFIA POMBE YA KIAFRIKA INAYOTOKANA NA MTAMA
ILIKUWA KATIKA MTINDO WA POP,INGAWA ILIFUATA KWA KARIBU DESTURI ZA MBAGANGA NA
SINGALONG KATIKA KIITIKIO. AMBAPO ILIWEZA KUWAVUTIA WATU WA AFRIKA KUSINI NA
AFRIKA KWA UJUMLA.
MWISHONI MWA MIAKA YA 1980 ALBAMU YA UMQOMBOTHI YA
YVONNE CHAKA CHAKA ILIPENDWA NA WATU WENGI. ALIFANYA ZIARA KATIKA AFRIKA KWA
KUFANYA MATAMASHA KATIKA VIWANJA VYA NIGERIA,KENYA NA ZAIRE.NJE YA AFRIKA
KUSINI. CHAKA CHAKA ALIKUWA NI MSANII WA MUZIKI WA AFRIKA NZIMA NA ANAENDELEA
KUFURAHIA HADI LEO.
ALITAMBULIKA KAMA “MALKIA WA AFRIKA” KUTOKA NA
KUTEMBELEA BARA LA AFRIKA NA UVAAJI WAKE WA KILEMBA KICHWANI.
KWENYE MIAKA YA 1990 ALIENDELEA KUFANYA ZIARA NA KUUZA
ALBAMU KATIKA KILA NCHI ZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA. IKUMBUKWE KUWA ALIWAHI
KUTUMBUIZA KATIKA KUNDI LA VIONGOZI WA
NCHI ZA AFRIKA PAMOJA NA TUKIO LA KIHISTORIA LA KUZALIWA KWA NCHI YA AFRIKA
KUSINI.
YVONNE NI MLEZI WA MRADI WA ‘GIVING AND SHARING’ AMBAO
UNAHUSU UNAJISHUGHULISHA NA KUSAIDIA MASKINI WENYE UHITAJI,PIA INAJIHUSISHA
UKUSANYAJI WA MAPATO ILI KUPAMBANA NA GONJWA LA UKIMWI,MFANO NI KITUO CHA
ORLANDO CHILDREN’S HOME.
ALIACHIA ALBAMU YA ‘YVONNE AND FRIENDS’ MWISHONI MWA
MWAKA 2000 AMBAYO ILISHIRIKISHA WASANII WA KIGENI KAMA VILE TSEPO TSHOLA AMBAYE
ALIKUWA SANKOMOTA.
MWAKA 2002 ALIFANYA KAZI YA KUWA MTANGAZAJI KATIKA
RADIO NA TELEVISHENI, HII ILPELEKEA KUHAMA KUTOKA KUWA ‘MALKIA WA AFRIKA’ MPAKA
KUWA MFANYABIASHARA MAARUFU, MBURUDISHAJI NA MUELIMISHAJI.
YVONNE CHAKA CHAKA AMEOLEWA NA MWANAFIZIKIA KUTOKA
SOWETO NA NI MAMA WA WATOTO WANNE.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment