HAMZA KALALA ‘KOMANDO’
HAMZA
KALALA NI MWANAMUZIKI MKONGWE KATIKA TASNIA YA MUZIKI HAPA NCHI. SIFA ZAKE
ZILIANZA KUZAGAA WAKATI ALIPOANZA KULICHARAZA GITA LA SOLO KWA UMAHIRI MKUBWA.
ALIZALIWA
MKOANI TANGA NA KUSOMA SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI HUMO. MARA BAADA YA
KUZAILIWA ALIPEWA JINA LA NYUMBANI LA ‘KAPESULA’ BABA YAKE ALIKUWA MFANYAKAZI WA KATIKA
SHIRIKA LA RELI KATIKA STESHENI YA MPANDA. BAADAE ALIHAMISHIWA MKOANI TANGA
AMBAKO ALIBAHATIKA KUOA MKE WA KABILA LA KIZIGUA AMBAYE NDIYE MAMA WA KOMANDO
KALALA. KWA MATIKI HIYO HAMZA KALALA NI CHOTARA WA KINYAMWEZI NA KIZIGUA.
KOMANDO
HAMZA KALALA ALIANZA KUHAMASIKA KATIKA MAMBO YA MUZIKI MWAKA 1966 AKIWA SHULE
YA MSINGI DARASA LA NNE WAKATI ALIPOKUWA AKIMSHUDIA BABA YAKE AKIIMBA NA KUCHEZA
NGOMA YA KINYAMWEZI YA MANYANGA HUKO HUKO TANGA.
WAKATI
HUO WAKATA MIKONGE WALIKUWA WAKIFANYA MASHINDANO YA NGOMA KATI YA WANYAMWEZI NA
NGOMA ZA MAKABILA MENGINE WALIOKUWA KATIKA MASHAMBA TOFAUTI YA MKONGE YA KIBARANGA YA AMBONI NA MENGINE
MENGI LAKINI NGOMA YA MANYANGA YA
WANYAMWEZI NA ILE YA WAMAKONDE NDIZO ZILIZOKUWA ZIKITIA FORA KATIKA MASHINDANO HAYO KILA MARA.
KALALA
ANELEZA KWAMBA MJOMBA WAKE ALIKUWA NA GITA NYUMBANI HIVYO ALIKUWA AKIJARIBU
KUSHIKA GITA KAMA ANAVYOSHIKA YEYE MJOMBA WAKE. KIPAJI CHAKE KILIANZA
KIJITOKEZA BAADA YA KUONA KWAMBA HAIKUMSUMBUA SANA KUJUA KUCHANGANYA NYUZI ZA GITA.
KOMANDO
‘MZEE WA MADONGO’ MWAKA 1968 ALIANZA KUPIGA MUZIKI KATIKA BENDI NDOGO SANA HAPO
TANGA IITWAYO KWANDURU JAZZ BAND. BENDI HIYO
ILIKUWA KATIKA MASHAMBA YA MKONGE NA BAADAYE AKAJIUNGA NA BENDI YA AMBONI JAZZ.
HUKO
HAKUKAA SANA NA ALIRUDI MJINI TANGA AMBAKO AKIWA NYUMBANI AKIFANYA MAZOEZI YA
KUPIGA GITA, AKAPITA MKONGOMAN MMOJA ALIYEMTAJA KWA JINA MOJA LA CHIVOSHA
AMBAYE ALIKUWA MWIMBAJI MZURI SANA
ALIMCHUKUA NA KUANZA KUPIGA
MUZIKI KATIKA BENDI YAOM YA VILLA NEGRO SUCCSSES. MWAKA 1969 ALIACHANA NA BENDI
HIYO NA KUELEKEA MKOA WA MOROGORO AKIWA
NA NIA YA KUJIU KATIKA BENDI YA MOROGORO JAZZ AU CUBAN MARIMBA. LAKINI ALIAMUA
KWENDA KATIKA WA KILOSA AMBAKO ALIKUWA AKIJUWA KUWA ABELL BARATAZAR YUKO HUKO.
LAKINI ALIPOFIKA ALIAMBIWA KUWA ALISHAREJEA DAR ES SALAAM. ALIPIGA MUZIKI HAPO
MKILOSA LAIKINI HAKUPAPENDA KWA KUWA
HAPAKUWA NA USHINDANI WA BENDI. KOMANDOO AKAAMUA KURUDI KWAO TANGA NA KUKUTANA
MWANAMUZIKI MWENZAKE AMBAPO WAKAPANGA SAFARI YA KWENDA MOROGORO. WALIFIKA
KATIKA MJI HUO WAKIWA NA HALI MBAYA SANA KIFEDHA KALALA WAKATI HUO ALIKUWA AKIVUTA
SIGARA HIVYO ALIJIKUTA AMEFIKA MJINI MOROGORO AKIWA NA SENTI KUMI NA TANO PEKEE
MFUKONI MWAKE AMBAZO HAZITOSHI KULA WALA
CHOCHOTE KILA LAKINI MWENZAKE HAUKWA
MVUTAJI SIGARA ALIKUWA NA AKIBA YA SENTI HAMSINI ZILIZOWAZWEZESHA KUPATA CHAI
NA WAKALALA STENDI YA BASI HADI ASUBUHI WAKAANZA KUZITAFUTA HIZO KLABU ZA BENDI
ZA MOROGORO JAZZ NA CUBAN MARIMBA
BAHATI
HAIKUWA UPANDE WAO KWANI WALIKUTA BENDI HIZO ZIKIWA SAFARI MOROGORO JAZZ ALIKUWA IMEENDA ZANZIBAR WAKATI
CUBAN MARIMBA ALIKUWA SONGEA.
HAMZA
KALALA ANAMTAJA MPIGA GITA LA SOLO WA CUBAN MARIMBA WAZIRI NYANGE ALIYEWAPOKEA
WAKATI WAKISUBIRI BENDI HIZO ZIREJEE. MSEMO WA KUFA KUFAANA ULIJITOKEZA BAADA
YA WANAMUZIKI WA MOROGORO JAZZ KUPATWA NA MATATIZO HIVYO ALIPOFANYIWA USAILI
ILIKUWA KWAKE NI RAHISI KUCHUKULIWA KATIKA BENDI HIYO BAADA YA KUFANYIWA USAILI
WAM KUPIGA GITA KATIKA WIMBO WA ‘ SINA PESA MIYE’
CUBAN
MARIMBA ALIPOREJEA IKIONGOZWA NA JUMA KILAZA AMBAYE ALIKUWA MSHIRIKA MWASISI
MWENZA PIA NDIYE ALIYEKUWA MWENYEJI WAO WAZIRI NYANGE, HIVYO ALICHUKULIWA
NA CUBAN MARIMBA NA ALIPOFIKA HAPO
ALIKUTA BENDI IKIPIGA KATIKA MTINDO WA
SUBI SUBI. AKIWA NA CUBAN ALIPATA SAFARI
YA KWANZA YA KWENDA TANGA KUPIGA MUZIKI.
SIKU
MOJA USIKU ALIKUJA KATIBU WA CHAMA WA WILAYA YA BAGAMOYO MZEE MWITA ALIYETUMWA NA MKUU WA WILAYA YA
BAGAMOYO WAKTI HUO
MOSSES
NNAYE KWENDA BAGAMOYO KUENDESHA BENDI YA VIJANA YA TYL.
WAZIRI
NYANGE ALIKUWA NA FAMILIYA YAKE PALE MOROGORO HIVYOM IKIMUWIA VIGUMU KWENDA
BAGAMOYO LAKINI AKAMPA PANDE HAMZA KALALA KWENDA BAGAMOYO. KAZI KUBWA YA BENDI
HIYO KILA JUMAMOSI WALIKUWA WAKIENDA RUVU KUWABURUDISHA WAPIGANIA UHURU WA
FRELIMO NA ZAMBIA.
MWAKA
1970 AKASIKIA BENDI YA VIJANA JAZZ ANAANZISHWA. ALIFUATWA NA WANAMUZIKI
ANAOWATAJA KWA MAJINA YA NDALA FASUTINE AMBAYE BAADAYE ALIONDOKA NCHINI KWA
MATATIZO YA KUCHANGANYA KAZI NA UASHERATI.
NDALA
ALIKANYWA NA WAZEE WA BAGAMOYO KUACHA UASHERATI LAKINI HAKUSIKIA. HAMZA ANAELEZEA
KISA CHA KUKUTA PAKA ZAIDI YA 30 KWENYE MAKAZI YAO YALIYOKUWA GHOROFANI,WALIKUWA
WAKILIA KWA SAUTI KAMA MAGITA.NDALA FAUSTINE AKAINGIA NDANI AKACHUKUA MKIA WA
TAA , KALALA AKAMKANYA ASIWACHAPE PAKA HAO LAKINI YEYE ALIENDELEA KUWACHAPA
LAKINI HAWAKUONDOKA HADI SA 11 ALFAJIRI NDIPO WALIPOONDOKA TARATIBU. SAUTI ZA
PAKA HAO ZILIPOTOWEKA NDALA NAYE AKAANZA KUIMBA NYIMBO AKIMTAJA MPENZI WAKE ALIYEKUWA AKIKANYWA
ASIMCHUKUE. WAZEE WA BENDI HIYO AKIWEMO MASUDI NA MZEE DOLA ALIYEKUWA
AKIKUSANYA USHURU SOKONI BAGAMOYO AMABO WALKUWA WAZEE BENDI WAKAMSAIDIA NA
ALIPOPONA AKAONDOKA BAGAMOYO.
MWAKA
HUO WA 1970 ALIPOKWENDA VIJANA JAZZ ALIKUTA KUNA VYOMBO VYA MUZIKI LAKINI
HAPAKUWA NA MPANGO WA KUANZISHA BENDI.
HAMZA
KALALA AKAFIKIRIA JINSI YA KUISHI MJINI DAR ES SALAAM NDIPO AKAMFUATA JOHN
ONDOLO CHAHA ALIYEKUWA AFISA UHUSIANO WAKATI HUO. MZEE ONDOLO AKAMUELEAZA
KWAMBA VYOMBO HIVYO VIMEFUNGIWA BAADA YA KUVUNJWA KWA BENDI YA GREEN JAZZ BAND
NA BARAZA KUU LA UMOJA WA VIJANA NA KWAMBA HIVI SASA HAPANA MPANGO WA
KUANZISHA BENDI.TENA. ONDORO AKAMUULIZA ANAPIGA CHOMBO GANI AKAMWELEZA KUWA
ANAOIGA GITA. MZEE JOHN ONDORO AKAMWAMBIA AENDE AKAMSIKILIZA NIKAPIGA NYIMBO
ZAKE KAMA USAILI BAADAYE AKARIDHIKA NA KUWAPA PESA YA CHAKULA. ALIPELEKWA
KWENDA KINONDONI MAGO GARDEN NA KUANZA KUFANYA MAZOEZI YA KUPIGA MUZIKI.
WALONGEZEKA
WANAMUZIKI WENGINE WAKIWA KATIKA KAMBI KAMA YA JESHI.
RAMADHAN
MTORO DRUMS, ABDALLAH KWESA HASSAN
HOKORORO NA IKATOKEZEA BAHATI YA MTENDE KUOTA JANGWANI BAADA YA BENDI HIYO
KUJIPATIA UMAARUFU BILA KUJALI KKIPATO.
KATIBU
MKUU WA CHAMA MICHAEL BARUTI KUPITA NA KUWAKUTA WAKIPIGA MUZIKI AKAWAPENDA SANA. MIAKA KUMI YA UHURU
MZEE JOHN ONDORO ALIENDA KWENYE SHIRIKA
LA MAZAO WAKATI HUO AMBAKO ALIWAAMBIA KWAMBA WANA BENDI AMBAYO ITAKUWA
IKIBURUDISHA KWENYE BANDA LAO. WALIKUBALIANA NA AKALIPWA SHILINGI ELFU KUMI NA
MOJA. WALIFANAYA KAZI NA SHIRIKA HILO
HADI MAADHIMISHP YA MIAKA KUMI YA UHURU
YALIPOKWISHA NDIPO WAKAAMBIWA
KUWA WATAKUWA WAKILIPWA POSHO YA SHILINGI HAMSINI KWA MWEZI. TUKAENDELEA KUPIGA MUZIKI HADIM KILIPOFIKIA KIFO CHA RAIS
WA KWANZA WA ZANZIBAR
BENDI AMANI KARUME MWAKA 1972 WAKATENGENEZA WIMBO AMBAO ULIPENDWA NA
WAZEE. AKAJA MZEE ANDREW SHIJA AKASHANGAA KUWAONA WAKIZAGAA NJE YA OFISI
AKAAMRISHA WAPELEKWE JKT WAKAFUNZWE NIDHAMU. TUKAPELKWA KAMBI YA JKT RUVU
WAKIWA NA HASSAN DALALI NA DK. CHARLES KIMEI. BAADAYE WALIPELEKWA MPAKANI MWA TANZANIA NA UGANDA VITANI AMBAVYO HATA HIVYO
HAVIKUPUGANWA. WALIPOREJEA WAKATUNGA WIMBO UNAHUSU KIFO CHA MAREHEMU ABEID
AMANI KARUME NA MGENI WA HESHIMA SIKU HIYO ALIKUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS NA
WAZIRI MKUU RASHID MFAUME KAWAWA NA MAKAMU WA RAIS WA KENYA DANIEL ARAP MOI.
MZEE KAWAWA AKAFURAHISHWA NA MUZIKI WALIUPOROMOSHA SIKU HIYO NA NDIPO
ALIPOWAULIZA HAWA VIJANA WANATOKA WAPI. AKATOA MAELEKEZO YA KUANZISHWA BENDI YA
VIJANA JAZZ.
BAADA
YA KUANZISHWA MWISHO WA MWEZI ULIPOFIKA WALIANZA KULIPWA POSHO ZAO KATIKA OFOSI
YA LUMUMBA ZA SHILINGI 150 TOKA SHILINGI 50 ZA AWALI. KWA WAKATI HUO SHILINGI 150 ZILIKUWA NI
NYINGI SANA KWA MATUMIZI YA KAWAIDA. MWAKA 1974/75
WAKATOKA NA WIMBO HEMEDI MANETI AKIWA AMEKWISHA INGIA AKITOKEA MOROGORO AKATUNGA WIMBO KURUKA UKUTA UTUNZI WA MANETI.
KALALA
AKATUNGA WIMBO WA MAGDALENA NIPENI POLE.
WAKENYA
WALIUSIKIA WIMBO HUO NA KUUPENDA SANA
WIMBO HUO. AKAJA MKENYA ALIYEJULKANA KAMA OLUOCHI KANINDO AKAWAOMBA KWENDA
KENYA KUREKONDI NYIMBO ZAO KWENYE KAMPUNI YAKE HUKO NAIROBI. WAKAPATA OFA YA
KUREKODI KILA MWAKA ZAIDI YA MARA MBILI.
1977
KALALA AKAJIUNGA NA UDA JAZZ IKARUS KUMBAKUMBA. AKIWA NA UDA JAZZ KUNA SIKU
ALIKUTANA NA MZEE MMOJA AMBROS MBURA ALIYEKUWA MMILIKI WA BENDI YA SUPER
MATIMILA AKAMWAMBIA AENDE KILIMANAJARO HOTEL AKIWA NA HEMEDI MANETI AJILI YA MAZUNGUMZO.
WALIPATANA
KUONDOKA KWENDA SONGEA KWA NDEGE KUFUATIA BARABARA YA HUKO KUWA MBAYA.
ALIWAKODIA NDEGE LAKINI MANETI HAKUWEZA KWENDA KWANI HADI NDEGE INAPAA ALIKUWA HAJAFIKA UWANJA WA NDEGE.
MKATABA
WAKE NA MZEE AMBROSE ULIKUWA MZURI LAKINI AKACHUKUA MKATABA WA MIAKA MIWILI HADI
1979 AKAMALIZA MKATABA WAKE.
1979
WAKATI WAAJESHI WA JWTZ WANAREJEA TOKA VITANI UGANDA AKATENGENEZA WIMBO UITWAO
MCHAKAMCHAKA. BAADAYE AKARUDI DAR NA AKAHITAJIKA TENA NA BENDI YA UDA NDIPO
AKAJIUNGA NAO KWA MARA NYINGINE TENA NA KUBUNI MTINDO WA BAYAKANTA.
MWAKA
1981 MATIMILA AKAHAMIA DAR NA MZEE AMBROSE AKAMAKA ARUDI KWENYE BENDI YAKE.
MASLAHI
YAKAMSHAWISHI KUONDOKA UDA NA KUJIUNGA NA MATIMILA HADI MWKA 1981.AKISHIRIKIANA
NA DK. REMMY ONGALA. MWISHONI MWA MWAKA HUOHUO ALIFUATWA NA KAPTENI MCHUNGA
AKIFUATANA NA HEMEDI MANETI WAKIMTAKA AFIKE OFISI YA UMOJA WA VIJANA.
AKAAMBIWA
MPIGA SOLO WA BENDI HIYO HASSAN DAALALI KAONDOKA HIVYO WAKAMTAKA ASHIKE NAFASI
YAKE NA KUWA KIONGOZI WA BENDI YA VIJANA.
MWAKA 1982 AKAIUNGA RASMI VIJANA AKATOKA NA WIMBO WA MAISHA YA AMBA.
MIAKA YA 1985 HADI 1988 VIJANA JAZZ
WAKATOKA NA MITINDO YA TAKATUKA, HEKAHEKA
NA PAMBAMOTO
WIMBO WA SIFA ZA STELLA ALIUTUNGA WIMBO HUO IKIWA NI NJIA YA KUMSHAWISHI BINTI HUYO
AMBAYE WAKATI HUOA LIKUWA MWANAFUNZI WA CHUO MJINI MOROGORO NA NYUMBANI KWAO
AMBAKO NI KWA MBUNGE WA BARIADI MASHARIKI, MHESHIMIWA JOHN CHEYO ‘ MZEE MAPESA’
AMBAYE NYUMBA YAKE ILIKUWA NA GETI KALI. STELLA ALIVUTIKA NA KUWA MPENZI WAKE
HADI KUFUNGANAYE NDOA NA KUPATA WATOTO WAWILI AMBAO NAO WAMEFUATA NYAYO ZA BABA
YAO AKIWEMO
TOTO KALALA NA KALALA JOURNIOR. KOMANDO KALALA ANA WATOTO WENGINE WAWILI WA
KIKE FATUMA AMBAYE NI MKE WA MTU NA FATUMA NI MWANFUNZI WA CHUO.
1988
AKAJIUNGA NA BENDI YA WASHIRIKA JAZZ ‘ WATUNJATANJATA’ KWA MWAKA MMOJA TU IKIWA
NI NJIA YA KUTAFUTA JINSI YA KUJITEGEMEA MWENYEWE.MANDELA MWANA WA AFRIKA,
NIMEKUSAMEHE LAKINI SITOKUSHAU, JULLIE
WIMBO ULIOTUNGWANA MADARAKA MORRIS NA NYINGINE NYINGI.
BAADAYE
AKAANZISHA BENDI YA BANTU GROUP AMBAKO ALIWASHIRIKISHA WAPIGA MAGITA WAKIWEMO
AKINA MANGELE SANGE UPANDE WA SOLO, ALLI ADINANI, RASHID KALALA BESI/SOLO.
WENGINE NI BATI PETER NA MICHAEL LILOKO UPANDE WA DRUMS ALLI CHOKI NA MUUMIN
MWINJUMA WAKIWA NI WAIMBAJI.MUSEMBOWA MINYUNGU NA ALLA MASHOOM KWA UPANDE WA
TUMBA.
BABA JENI NA SUVUYA WA NIMBA, NALILA MASUMANDA
NA KASIMBAGU, NGOZI YA KITI MOTO.
BABA YAKE MZEE KALALA ALIINGIA NCHINI AKIWA NA
DADA ZAKE WAWILI WAKITOKEA DRC NA KUFIKIA KATIKA KIJIJI CHA IPWAGA HUKO
INYONGA AMBAKO ALIISHI NA KUWA MAARUFU
NA KISHA KUFANYWA KUWA MTEMI. UFIKAPO INYONGWA FAMILIYA YA KALALA NI MAARUFU SANA HADI LEO.,
BANTU
GROUP BADO IPO NAYE YUPO KWENYE MICHAKATO YAKINIFU YA KUANDAA VIBAO VIKALI
VITAVYOTIKISA MASIKIO YA WAPENZI WA MUZIKI HAPA NCHINI.
KUHAKIKISHA
WELEDI WAKE UIFAIDISHE FAMILIYA YAKE NA JAMII KWA UJUMLA.
USHAURI
KWA WANAMUZIKI WA KIZAI KIPYA WAPIGE MUZIKI
LIVE. KISA KWA NINI BENDI HUFA BAADA YA KIONGOZI MKUBWA KUFARIKI
UOGOZI
NI KIPAJI ANACHOKITOA MUNGU PEKEE SI KILA MTU ANAWEZA KUONGOZA.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment