RASHID PEMBE GWIJI LA SAX TANZANIA
RASHID PEMBE KATIKATI AKIWA NA WANAMUZIKI WENZAKE KATIKA JIJI LA STOCKHOLM NCHINI SWEDEN.
RASHIDI PEMBE AKIWA NA WANAMUZIKI WENZAKE
RASHIDI PEMBE(WAPILI KUSHOTO)AKIWA MELINI NA WANAMUZIKI WENZAKE,DEKULA KAHANGA(KATIKATI)STOCKHOLM NCHINI SWEDEN.
RASHIDI PEMBE AKIWA NA MDOGO WAKE NA MWENYEJIWAO HUKO ULAYA
HISTORIA YA MAISHA YA RASHIDI PEMBE.
RASHID PEMBE
NI MWANAMUZIKI MASHUHURI KWA UPULIZAJI WA SAXOPHONE HAPA NCHI NA NJE YA
MIPAKA YETU. ALIZALIWA MWAKA 1957.
WAZAZI WAKE
BI. FRIDA ABEL AMBAYE NI MAREHEMU, ALIKUWA MZALIWA WA KIJIJI CHA
MIHUGWE, WILAYA YA KISARAWE MKOANI PWANI.
BABA YAKE MZEE PEMBE RASHID PIA MAREHEMU ALIKUWA MZALIWA WA KIJIJI CHA KURUWI, TARAFA
YA MZENGA, WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI.
RASHIDI PEMBE ANAIELEZEA HISTORIA YAKE AKISEMA...
RASHIDI PEMBE ANAIELEZEA HISTORIA YAKE AKISEMA...
"MWAKA 1963
NILIANZA ELIMU YA MSINGI CHANZIGE PRIMARY SCHOOL HAPO KISARAWE, ILA KWA KUWA
MAMA ALIKUWA DAKTARI ALIHAMISHWA HUKU NA KULE
NASI NDIO
TULIKUWA TUKIISHI NA MAMA KWANI WALISHAACHANA NA BABA
MAMA
ALIPENDA SANA TU
SOME, ILA BABA HAKUWA NA MSISITIZO SANA WA SHULE, SIJUI KWA
KUWA ALIKUWA MBALI NA SISI MAANA HUDUMA ILIKUWA KWA MBINDE KIDOGO.
1966 MAMA
ALIHAMISHWA HOSPITALI YA KISARAWE NA KUPELEKWA VIKINDU HOSPITALI NASI TUKAHAMA SHULE
KWENDA KUSOMA HAPO VIKINDU -WILAYA HIYO YA
KISARAWE
NIKIWA DARASA LA 4.
1967
NILIINGIA MIDDLE SCHOOL HAPO VIKINDU DARASA LA 5 HAPO NDIO NILIKUTANA NA
MWANAMUZIKI JOSEPH BENARD TUKIWA DARASA MOJA NA DAWATI MOJA AMBAE
NI MPIGA
SAXAPHONE DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA.
JOSEPH AMBAE
SASA ANAITWA YUSUPH BENARD ALIKUWA NI MPIGA FILIMBI BINGWA PALE SHULENI, KIASI
AMBACHO NILIUMIA SANA, HADI NIKAMUOMBA ANIFUNDISHE NA ALINIFUNDISHA TUKAWA
TUNAPIGA WOTE FILIMBI KTK BENDI YETU YA SHULE.
1968 NIKIWA
DARASA LA 6 NILIUGUA MKONO ULIKUWA HAUKUNJUKI SIJUI ILIKUWA NI NINI MUHIMBILI
HOSPT WALIAMUA WAUVUNJE NIKAKATAA, WAKANIFUKUZA HOSPT
KAMA SITAKI
KUVUNJWA HALAFU UUNGWE TENA NA NITAKUWA KILEMA WA MKONO KUTOKUKUNJA TENA,
KWA MAPENZI
YA MUNGU MKONO ULIKUNJUKA SIKU HIYOHIYO JIONI YAKE, WAKATI MWAKA MZIMA ULINIUMA
, ULIVIMBA NA HAUKUWA UNAKUNJUKA.
KW HALI HIYO
NILIACHA SHULE MWAKA MZIMA.
MWAKA HUO WA
1968 MAMA ALIHAMISHWA KUPELEKWA SOTELE HOSPT NA BAADAE KUHAMISHWA TENA KWENDA
KISIJU HOSPT WILAYA HIYOHIYO YA KISARAWE NA NDIPO NILIPORUDI TOKA KWA BABA
NILIPOKUWA NAUGUA, NA KURUDI TENA KWA MAMA.
MAMA AKANIAMBIA
NIANZE DARASA LA 4 TENA KWA KUWA ILE SHULE ILKUWA MPYA HAIKUWA NA DARASA LA 5
WALA LA 6.
SIKUWA
NAPENDA SHULE KABISA, KWENDA SHULE ILIKUWA HADI KWA VIBOKO KILA SIKU
NILIPAMBANA NA MAMA NA NILIMSUMBUA SANA HADI KUMALIZA DARASA LA 7 MWAKA 1972
HAPO KISIJU PRIMARY SCHOOL.
MAMA
ALINIPELEKA KWA MJOMBA DAR ILI ANITAFUTIE KAZI, NA KWELI MJOMBA ALINITAFUTIA
KAZI KILIMANJARO TEXTILE KIWANDA KILICHOKUWA KINATENGENEZA
KHANGA NA
VITENGE HAPO GONGOLAMBOTO .
1973
NILIANZA KAZI, NILIPOKUWA KAZINI TUKIWA NA MAVITAMBAA KUZIBA PUA NA WENGI
KUUGUA TB KUTOKANA NA PAMBA TUNAZOSINDIKA KWENYE MASHINE
NIKAONA
VIJANA WENZANGU VIJANA WADOGO, WAKIWA WAMESHIKA MAFAILI NA KUZUNGUKA HUKU NA
KULE, WENGINE WAKIWA OFISINI ,NIKAWA NATAMANI KWA NINI NISIPATEKAZI KAMA WALE?
IKABIDI NIULIZE MBONA WALE WANA KAZI NZURI? NDIO KUAMBIWA WALE WAMESOMA FORM 4
WALE, NDIO KUSHTUKA KUWA KUMBE NDIO MAANA MAMA ALINIAMBIA NISOME NIKAANZA KUJUA
FAIDA YA KUSOMA NA KUMWAMBIA MAMA NATAKA KUACHA KAZI NIKASOME KITU AMBACHO
KWANZA ALICHEKA
SANA HALAFU
AKANIULIZA UMEONA ? ULINISUMBUA HUTAKI SHULE SASA UMEONA NINI? NIKAMUELEZA
NDIPO ALIPOMUOMBA KAKA ANITAFUTIE SHULE NIKAPELEKWA SHULE YA BAGAMOYO TECHNICAL
SECONDARY SCHOOL 1973 HADI 1978 SHULE ILIKUWA INAMILIKIWA NA UMOJA WA WAZAZI
TAPA WAKATI HUO.
SASA NIKIWA
MDOGO NILIPENDA SANA NGOMA ILIKUWA MDUNDIKO UKIPITA MAMA UPESI HUWAAMBIA DADA
ZANGU WANITAFUTE WANIKAMATE BILA HIVYO NAWEZA KWENDA NAO NA NISIJUE MWISHO WAPI
NILIKUWA NAPOTEA HADI WATAFUTE NGOMA HIYO ILIPOENDA NDIO WATANIKUTA HUKO? NA
SIKUWA NA UJANJA WA KURUDI WATANIKUTA HAPOHAPO KWENYE MDUNDIKO.
WAKATI NIPO
KAZINI, NILIPENDA SANA BENDI YA SAFARI TRIPERS YA MAREH MARIJANI RAJABU PALE
PRINCES BAR MNAZI MMOJA. MI NILIKUWA NAJUA MUZIKI MTU ANAJUA TU KAMA KIPAJIN
KAZALIWA NACHO MTU SIKUJUA KAMA HADI UJIFUNZE, SASA PALE NILIMKUTA ABDALLAH
GAMA AKIWA ANAPIGA GUITAR NA ALIKUWA MDOGO SANA NDIPO NIKAJIULIZA KWA NINI HUYU
MDOGO ANAJUA NA NI MDOGO HIVI? NDIPO NILIAMUA NIJIFUNZE GITA.
NIKAWA NA
GUITAR SHULE KITU AMBACHO KAKA ANENISOMESHA ALIKASIRIKA AKNIAMBIA NILIUZE
NIKAKATAA AKAAMUA KUNIFUKUZA KWAKE, NA NIKAAMUA KWENDA KWA DADA NAE SHEMEJI
AKASEMA HAWEZI KUWA NA WATU LUKUKI PALE HOME KWAKE NIKAAMUA KUONDOKA, NA KUWA
NALALA SOKONI KARIAKOO PALE NJE NDIPO SHIDA YA MAISHA ILIANZA NILITAMANI KUFA
LAKINI SIKUUZA GUITAR. NILIKUBALI YOTE, NIKABEBA MIZIGO YA ABIRIA WANAOTOKA
MBEYA NA MIKOA MBALIMBALI PALE
MANZESE HADI
NIKATEUKA SHINGO JAMANI MAISHA NI KIBOKO LAKINI NILIMUAMINI SANA MUNGU NA
KUMUOMBA KWA YALE MATESO NILIPATA HADI NILIMALIZA SHULE
BABA AKIWA
ANALIPA ADA YA SHULE KAKA ALIKATAA KABISA KUNISOMESHA TENA.
BAADA YA
MATOKEO NILICHAGULIWA KWENDA KUSOMEA UALIMU WA UFUNDI MRUTUNGURU -SIJUI NI
MUSOMA AU WAPI NIKAKATAA, KWA NILISOMA KWA TAABU NAE BABA AKASEMA NDIO MAANA
KAKA YAKO, KAKUFUKUZA WE HUTAKI KUSOMA UNATAKA KUPIGA MAGITAA KUANZIA LEO
SITAKUSAIDIA KWA LOLOTE NIKAKUBALI NILAENDELE A JIONI KULALA SOKONI KARIAKOO HADI RAFIKI YANGU
MAREHEMU JOHN SEMLAMBA ALINIKUTA NAAMKA PALE AKAMUA KUNICHUKUA NA KUKAA KWAKE
KWA KUWA NILIMUELEZA KILA KITU.
1979
NILIENDA JKT NILIJUA KUTOKANA NA CHETI CHANGU CHA UFUNDI MASON (UASHI) GRADE
1 KINGENIPA KAZI KUMBE KULE IKAWA
KUJITOLEA NIKATOROKA KARIBU NAMBA ZA JESHI ZITOKE, WAKATI HUO JESHI LA POLISI
WALIKUWA WANATAKA MAFUNDI TOKA SHULENI NA CHETI CHANGU NIKACHUKLIWA MOJA KWA
MOJA NA POLISI. NIKAWA NAFANYA KAZI POLICE MAIN STORE PALE KILWA ROAD NA KUANZA
MAISHA.
PALE NDIO
NILIPOKUTANA NA TX MOSHI WILLIAM, MZEE KASSIM MAPILI AMBAE
AKAAMUA KUNIENDELEZA KUPIGA GITA NA WALIAMUA WANICHUKUE ILI NIKAJIENDELEZE PALE
POLICE BAND NA NILIKUBALI KUOMBA KUBADILISHA SECTION TOKA KIKOSI CHA UFUNDI NA
KUINGIA BENDI YA POLISI.
KWA KUWA
NILIKUWA KAMA MWANAFUNZI WA KUENDELEZWA MAREHEMU MZEE MAYAGILO ALIAMUA ANIPE SAX NIACHE GITA KWA SABABU KUNA MPIGA SAX MZEE
ABDUL MWALUGEMBE ALIKUWA ANASTAAFU HIVYO NILIINGIZWA SHULE YA PALE NA KUANZA KUSOMA
NOTA NA KUANZA KUJIFUNZA SAXOPHONE MWAKA 1981.
MWAKA 1985
NILICHAGULIWA KWENDA COPLO COARSE ZANZIBAR NA NIKAFANIKIWA KUTUNIKIWA CHEO
CHA COPLO. SIKUWA NAPENDA SANA KUWA POLISI
ILA NASHUKURU JESHI LA HILO LIMENIFIKISHA
HAPA NILIPO HASA KWA MASOMO YA MUZIKI AMBAYO YAMENIFANYA KUWA HAPA LEO"
MWEZI APRILI
1987 ALIAMUA KUJIUNGA NA BENDI YA VIJANA
JAZZ AMBAKO ALIPIGA MUZIKI HADI MWAKA 2005 ALIPOAMUA KUACHA . AKAUNGA NA
MWANAMUZIKI TOKA DRC SAMBA MAPANGALA KATIKA ZIARA ZAKE ZA AFRIKA HADI MWAKA
2006 ALIPOMUOMBA SAMBA MAPANGALA AMUACHE
KWA KUWA WANAMUZIKI NDIO WALIOKUWA WAMEANZISHA BENDI HIYO MARK AMBAYO HADI HIVI
SASA YUPO NAYO.
WALIIUNDA KWA AJILI YA KUPIGA MUZIKI KATIKA MAHOTELINI KWA KUWA ALIONA MIAKA
TAKRIBANI 26 ALIYOITUMIA KUPIGA MUZIKI
HAYAJAKUWA NA MAISHA BORA.
WAKAANZA
KUPIGA KWENYE MAHOTEL YOTE HAPOYA JIJI LA DAR ES SALAAM HADI WALIPOPATA MKATABA HUO AMBAO ULIWAPELEKA
NCHI NYINGI ZA ULAYA ZIKIWEMO ZA UJERUMANI, MISRI,UFARANSA NA WAKAENDA
NCHINI SWEDEN KUPIGA MUZIKI KATIKA MELI YA KITALII KATIKA JIJI LA
STOCKHOLM KWA MKATABA.
ALIPOULIZWA
JUU YA MAFANIKIA ALIYOYAPATA PAMOJA NA
CHANGAMOTO ZLIZOKUMBANA NAZO. PEMBE
ALISEMA …
“MAISHA YA
MUZIKI NI MAGUMU SANA HASA KUTOKANA NA MPANGILIO WA HAKI ZA MUZIKI NA
WANAMUZIKI WA AFRIKA NI TATIZO KUBWA AMBALO UDHIBITI HAKUNA KITU AMBACHO NI
KIGUMU KWA MAISHA YETU”
MWISHO.
No comments:
Post a Comment