KOFFI OLOMIDE MCHUMI
ALIYEBOBEA KATIKA MUZIKI.
Ni watu wachache mno ambao
wanaweza kuamini kuwa unaweza kumkuta msomi mwenye digrii mbili akiamua kupanda
jukwaani na kunengua kama mwanamuziki, lakini
hali hii ipo tofauti kwa mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na mafanikio aliyonayo kimuziki pia ni msomi
aliyebobea katika maswala ya hisabati
Koffi Olomide alizaliwa siku
ya ijumaa Julai 13, 1956 katika mji wa Kisangani
uliopo kaskazini mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Olomide
ana asili wa nchi mbili za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sierra
Leone. Mama yake ni raia wa Congo akitokea katika kabila la Songye ambalo
linapatikana katika mkoa wa kasai wakati baba yake ni mwenye asili ya Sierra Leone.
Kwa
mujibu wa mila nautamaduni wa kabila la babu zake mama yake alimpa jina la ‘Koffi’
kutokana kuwa alizaliwa siku ya ijumaa alipokuwa bado ‘kinda’ koffi alipachikwa
jina bandia la ‘Antoine Makila Mabe' likiwa na maana ya 'Damu mbaya ya Antony'.
Antoine Koffi Olomide alikulia katika familia ya watu wenye uwezo wa kati na mahali ambapo elimu ilikuwa ikipewa kipaumbele
Olomide
pamoja na kupenda muziki tangu akiwa mtoto, ndoto zake kubwa zilikuwa awe
mchezaji wa mipra wa miguu.
Alipoanza kupevuka akiwa na
umri wa miaka 18, wakati huo akiwa
mwanafunzi kijana, alivutiwa sana
na usanii pamoja na muziki, ndipo alipoanza kutunga na kuimba nyimbo.
Kwa mujibu wa historia hiyo,
Koffi alikuwa ana akili sana darasani hali ambayo ilimfanya apate
wadhamini wa kumlipia kwenda kusoma mjini Bordeaux,
Ufaransa ambapo alipata Shahada yake ya kwanza ya Biashara na Uchumi.
mbali na shahada hiyo inaeleza pia ana shahada ya pili katika masuala ya hisabati kutoka chuo kikuu cha paris
akiwa likizo Koffi alirekodi nyimbo za 'Asso' na 'Princesse ya Senza' katika Studio za Veve
huko Kinshasha. Tokea hapo
akashirkiana na wasanii wengine nguli akiwemo
Papa Wemba na bendi ya Zaiko
Langa Langa. Koffi alitangazwa na
kuzawadiwa kama msanii bora wa Congo
mwaka 1978 mbali na shahada hiyo inaeleza pia ana shahada ya pili katika masuala ya hisabati kutoka chuo kikuu cha paris
Akiwa Paris alianza kujifunza kupiga gitaa na kuandika nyimbo na aliporudi drc alijiunga na bendi ya muziki ya muziki ya viva la musica ambayo ilikuwa ikiongozwa na papa wemba, baada ya kujiunga na bendi hiyo Koffi aliimarisha mtindo wa polepole wa soukous uliokuwa umeisha umaarufu
aliuita mtindo huo Teha Tcho na ulipata umaarufu njee ya kongo, akiwa katika bendi hiyo mwanzo alikuwa ni mtunzi wa nyimbo, mwandishi na baadaye kama muimbaji, na hata baadaye aliamua kujitenga na kundi hilo na kuanza kuimba kama mwanamuziki wa peke yake na hadi mwaka 1986 alipounda bendi yake aliyoipa jina la Quartier latin mwaka wakati huo huo Olomide alikuwa akivutiwa sana kundi la wanamuziki wa kassav. baada ya miaka 10 ya mafaniko yake, akatamani kuwa mwanamuziki wa kimataifa. ilichukua kipindi kirefu akisubiri kuwa mwanamuziki wa kimataifa hadi ilipofika mwaka 1988, wimbo wa 'henriquet' ukatokea kuwa mkali uliopelekea kupachikwa jina bandia la ‘Golden Star'.
Koffi olomide aliyafurahia
mafanikio zaidi baada ya kuandika wimbo
akiwa na binti yake pekee minou, ukiitwa
D'elle et Moi', miaka ya 1990.
koffi toka mwaka 1990 hadi 1994, alifurahia
kukua kwa mafaniko yake ambayo kwa
kipindi cha miaka chini ya minne, alifyatua zaidi ya album saba zikiwa chini ya
jina lake na kundi lake la 'quartier latin'.mwaka 1992 olomide alichaguliwa kuwa mwimbaji bora wa kiume na mshindi wa video bora katika shindano la african music awards mjini abidjan, ivory coast.
muziki wa koffi olomide unapendwa na mashabiki
wengi afrika hata ulaya, kufuatia tungo
zake kuwa ni zenye ujumbe mzito kwa jamii. yaelezwa kwamba ujuzi wa aina yake,
mpangilio mzuri wa muziki, ukichangiwa
na kuusomea muziki, kumempa umaarufu
mkubwa ndani na nje ya nchi yake ya jamhuri ya kidemokrasia ya congo(drc).
antoine koffi
olomide amefyatua albam yake kali inayotamba hivi
saaa ya abracadabra, iliyonguliwa na albam za
ngounda, efrakata, tcha tcho, haute de gamme – koweit na rive gauche.
katika kile kuonyesha umahiri wake katika muziki,
koffi alitoka na albam zingine nyingi
za pas de faux pas, live a bercy,
attentant, le rambo du zaire, ultimutum, golden star na noblesse oblige.
kama hizo hazitoshi, msomi huyo aliwapagaisha wapenzi wake wa muziki kwa kutoa albam zaidi za v12,loimore, monde arabic, riziki, papa plus,
zaiton na phamacien. wimbo huo wa
phamacien, sehemu kubwa ya uimbaji alitamba mwimbaji wake fally ipupa.
zingine zilikuwa
loi, Magie, Stila, Sexy pop, Rounge
A Levre, Etant Civil, Round Poit,
San suit, Respect 2,l Autre la, Miss Dess, Nolesse Oblige na Escola. wimbo wa Escola alimshirikisha
mwimbaji nguli papa wemba.
Mwaka 1998, Koffi akiwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa, alikimbiwa na wanamuziki takribani
wote, baada ya onesho kubwa lilofanyika katika ukumbi wa Olympia.
Bendi hiyo ilisambaratika na baadhi ya wanamuziki
wake wakaenda kuunda bendi yao
ya Orchestra ‘Quartier Latin Academia.
Faida ya kufanya
muziki ukiwa msomi ilijionyesha kwa Koffi Olomide ambaye ni mithiri ya chuo.
hakuteteleka kabisa baada ya tukio hilo
kwani haikuchukuwa kipindi kirefu akaibua tena vijana wengine wenye vipaji toka sehemu mbalimbali nchini humo. Olomide
ana sifa kubwa ya kutokuchukuwa wanamuziki toka bendi kubwa. yeye huibua vipaji vya vijana wadogo hadi
wanafikia kuwa wanamuziki wa kukubalika.
Amewafundisha
wanamuziki wengi chipukizi ambapo wengine wameamua kujitegemea na kusimama
wenyewe katika kazi za muziki na wengine bado wapo na bendi hiyo hiyo
Baadhi ya wanamuziki ambao ameshawatoa ni Fele Mudogo, Motana Kamenga, ambaye alitimka kwenda kujiunga bendi ya big star ya general defao. Wengine ni pamoja na Bruno Mpela, Soleil Wanga, Sam Tshintu, Suzuki 4 by4, Ferre Gola na Fally Ipupa. Ipupa hivi sasa ni kati ya wanamuziki mwenye jina kubwa na kuheshimika duniani anakula ‘maisha’ murua nchini marekani, akiwa ubavuni mwa kundi la g unit na lile la mwanamuziki 50 cent.
Baadhi ya wanamuziki ambao ameshawatoa ni Fele Mudogo, Motana Kamenga, ambaye alitimka kwenda kujiunga bendi ya big star ya general defao. Wengine ni pamoja na Bruno Mpela, Soleil Wanga, Sam Tshintu, Suzuki 4 by4, Ferre Gola na Fally Ipupa. Ipupa hivi sasa ni kati ya wanamuziki mwenye jina kubwa na kuheshimika duniani anakula ‘maisha’ murua nchini marekani, akiwa ubavuni mwa kundi la g unit na lile la mwanamuziki 50 cent.
Hata hivyo katika
siku za hivi karibuni suzuki amekuwa akionekana mara kwa mara katika maonyesho
ya quartier latin sambamba na mwanamuziki wa kike mwenye sauti ya kumtoa nyoka
pangoni Cindy le Coeur
Koffi aliwahi kushiriki katika projekti ya muziki wa africando, pia aliwahi kushinda zawadi nne za kora huko afrika ya kusini. vilevile alikuwa msanii bora katika nchi za afrika ya kati mwaka 2002.
Koffi aliwahi kushiriki katika projekti ya muziki wa africando, pia aliwahi kushinda zawadi nne za kora huko afrika ya kusini. vilevile alikuwa msanii bora katika nchi za afrika ya kati mwaka 2002.
Olomide aliwahi
kufika hapa nchini mwezi Desemba 2012 aambapo alimwaga burudani kamambe zilizokonga nyoyo za
watanzania walihudhuria onyesho lake lililofanyika katika viwanja vya Leaders, Kinondoni
jijini Dar es salaam, Desemba 14,
2012.
Koffi Olomide
ni baba wa familiya ya mke na watoto saba.
Mungu mwingi wa rehma iwapo atamfikisha Julai 13,
2013 Koffi Antonie Olomide atatimiza
miaka 57 ya kuzaliwa kwake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment