KABEYA ‘NYOTA’ ILIYOZIMIKA GHAFLA.
NA
MOSHY KIYUNGI.
MARCH 2013.
KABEYA BADU ALIKUWA MWIMBAJI MAHIRI KATIKA BENDI YA LA
CAPITALE, ALIYEWAACHA WAPENZI NA
MASHABIKI WA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI, WAKIWA BADO WANAMHITAJI.
ALIAGA DUNIA TAREHE 06 MARCH, 2013 AKIWA KATIKA
HOSPITALI WA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA KWA MARADHI YA FIGO, AKIWA AMEFIKISHA
UMRI WA MIAKA 68.
MPAKA ALIPOFIKWA NA UMAUTI, ALIKUWA NI MWANAMUZIKI
MWENYE VIPAJI VYA KUTUNGA NA KUIMBA KATIKA BENDI YA LA CAPITALE ‘WAZEE SUGU’
INAYOONGOZWA NA MKONGWE KIKUMBI MWANZA MPANGO ‘KING KIKI’.
MSIMBA WA KABEYA ULIWATIA SIMANZI NA MAJONZI MAKUBWA
WAOMBOLEZAJI WALIOFIKA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUUAGA MWILI WAKE NA
KATIKA MAZISHI YALIYOFANYIKA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI MARCHI 07, 2013.
UMATI WA WATU WALIBUBUJIKWA MACHOZI MARA WALIPOONA MWILI WAKE UKISHUSHWA
KABURINI.
KABEYA BADU TOKA ALIPOANZA SAFARI YAKE KATIKA MUZIKI,
KAMWE HAKUWA MTU MWENYE SONI. ALIKUWA TAYARI KUIACHA BENDI NA KWENDA NYINGINE
WAKATI WOWOTE ULE, ILI MRADI MASLAHI YAWE MAZURI. BADU ALIPITIA BENDI NYINGI
AKIWA HUKO KWAO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO, NA HAPA TANZANIA, AMBAPO ALIPIGIA KATIKA BENDI SI CHINI YA TANO
TOFAUTI.
SI VYEMA KUMSIFIA MTU BAADA YA KUFA, LAKINI KWA KABEYA
NINALAZIMIKA KUFANYA HIVYO KWA KUWA MWISHONI MWA MWAKA JANA 2012, NILIBAHATIKA
KUPATA FURSA YA KUFANYA MAHOJIANO NAYE ILI KUJUA WASIFU WAKE.
NILIZUNGUMZA NA KABEYA BADU KWA TAKRIBANI SAA MBILI MFULULIZO,
AKINISIMULIA HISTORIA YA MAISHA YAKE KWA UJUMLA.
KABEYA ALIAZA KWA KUTAJA MAJINA YAKE
AKISEMA ANAITWA KABEYA CHIBANGU BADU. ALIZALIWA JANUARI 22, 1945 KATIKA
MJI WA LIKASI, HUKO JAMHURI YA
KIDEMOKRASIA YA CONGO.
ELIMU YA MSINGI ALIPATA KATIKA SHULE YA ECOLE OFFICIALLE LAIQUE DE KOLWEZI NA KUMALIZA
MWAKA 1959.
KABEYA ALISEMA MUZIKI ALIANZA TANGU AKIWA BADO MDOGO
NA ALIPOPATA UMRI WA KWENDA KANISANI, ALIJIUNGA KATIKA KWAYA AKIIMBA NYIMBO
INJILI.
AKIWA KANISANI HUMO, ALIJIFUNZA JINSI YA KUTENGENEZA
‘MELODY’ BAADAYE MWAKA 1963, AKAJIAMINI
KWAMBA ANAWEZA KUFANYA MUZIKI. ALIKWENDA KUJIUNGA NA BENDI YA MUZIKI WA DANSI
YA RICCO JAZZ, ILIYOKUWA KATIKA WILAYA
YA KOLWEZI.
AKIWA KOLWEZI,
KABEYA ALIJIUNGA NA CHUO CHA UFUNDI AMBAKO ALICHUKUA MASOMO YA USEREMALA
NA UASHI.
“TANGU NIKIWA
MDOGO, NILIPENDA SANA NYIMBO NA UIMBAJI WA TABU LEY ROCHEREAU NA KABASELE
YAMPANYA ‘PEPE KALE’ NIKATAMANI SIKU MOJA NIFIKIE HADHI YAO…” ANASEMA KABEYA.
FAMILIYA YAKE ILIJITAHIDI KUMPA MOYO ILI AWEZE KUFANYA
VIZURI KATIKA MUZIKI, HIVYO ILIMSHAURI KABEYA KUJIFUNZA LUGHA YA KIFARANSA
AMBAYO INAZUNGUMZWA NCHINI MWAO.
KABEYA ALIKUBALIANA NA
USHAURI HUO NA ALINGIA KATIKA CHUO KILICHOKUWA KIKIMILIKIWA NA DHEHEBU
LA DINI YA PROTESTANT HUKO KANANGA, JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.
KIU CHA KABEYA KILIPOZWA PALE ALIPOPOKEA CHETI BAADA
YA KUFUZU SOMO HILO LA KIFARANSA.
HARAKATI ZA KABEYA BADU ZA KUTAFUTA MAISHA
ZILIMFIKISHA KUFANYA KAZI KATIKA GAZETI MOJA LA LEALITY CONGOLESE LA MJINI KANANGA, KWENYE KITENGO CHA USAMBAZAJI
MWAKA 1967.
“BAADA YA MIAKA MIWILI KUPITA, MMILIKI WA GAZETI HILO
ALIKAMATWA BAADA YA GAZETI HILO KUANDIKA HABARI ZILIZO MUUDHI RAIS WA WAKATI
HUO MOBUTU SESESEKO, HATIMA YAKE GAZETI LIKAFUNGIWA, TUKAKOSA KAZI….” ANAELEZA
KABEYA BADU.
‘KUVUNJIKA KWA KOLEO SI MWISHO WA UJENZI’ MSEMO HUU
ALIUFANYIA KAZI KABEYA AMBAYE MWAKA HUO HUO ALIANZA SAFARI YAKE YA MUZIKI
KIKAMILIFU. AKAJIUNGA KATIKA BENDI YA LUPE
JAZZ, BAADAYE AKAENDA KATIKA BENDI NYINGINE YA AMIDE SUCCESS.
KABEYA HAKUISHIA HAPO KWANI ALIONDOKA TENA NA KWENDA
KUJIUNGA NA BENDI YA SANTA FEE BAADAYE AKAJIUNGA KATIKA BENDI YA LUPINA
NATIONALE, AMBAKO ALIKUTANA NA KASONGO MPINDA ‘CLAYTON’ HUKO KANANGA.
UTULIVU KATIKA BENDI KWAKE HAUKUWEPO KABISA, KWANI ALIONDOKA TENA NA KWENDA KUJIUNGA
KATIKA BENDI YA LUPE REVOLUTION, ILIYOKUWA YA VIJANA KAMA YEYE.
JINA NA SIFA ZA UIMBAJI WAKE ZIKAZAGAA NDIPO
ALIPOCHUKULIWA NA OMER BABA GASTON
KATIKA BENDI YAKE YA BABA NATIONALE MWEZI SEPTEMBA 1968.
BAADAYE MWAKA 1970, KABEYA ALISHAWISHIKA KWENDA
KUTAFUTA AJIRA KATIKA MJI WA KINSHASA. ALIBAHATIKA KUPATA AJIRA KATIKA BENDI
AMBAYO BAADAYE AKAGUNDUA KWAMBA ILIMPA
AHADI ZA UONGO ZA MASLAHI, NAYE AKAACHANA NAYO.
KATI YA MWAKA
1971 NA 1972 KABEYA BADU ALIPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YA FESTIVAL DU ZAIRE
KATIKA JIJI LA KINSHASA, JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.
KABEYA ALIRUDI LIKASI MWAKA HUOHUO WA 1972 NA KUJIUNGA
NA BENDI YA SAFARI NKOI BAADA YA KUITWA NA MWANAMUZIKI KIKUMBI MWANZA MPANGO
‘KING KIKI’. KATIKA BENDI HIYO PIA
ILIKUWA NA WANAMUZIKI WENGINE MAGWIJI NDALA KASHEBA NA BAZIANO BWETII.
KABEYA BADU NASEMA KWAMBA ALISOMA DARASA MOJA NA KIKUMBI MWANZA MPANGO ‘KING
KIKI’ KATIKA SHULE YA MSINGI YA SHULE YA
ECOLE OFFICIALLE LAIQUE DE
KOLWEZI, AMBAKO WALIMALIZA MASOMO YAO MWAKA 1959.
“TANGU TUKIWA VIJANA TULIKUWA TUKIELEWANA SANA NA
KIKI, NDIYO SABABU NIMEKUWA NAYE SAMBAMBA TUKIENDA SEHEMU MBALIMBALI HADI LEO
NINAYE…” ANSEMA KABEYA.
WALIPOKUWA KOLWEZI WAKIPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YA
SAFARI NKOI, WALIKUWA WAMEPANGA NYUMBA MOJA, WALICHANGIA BAJETI YA CHAKULA KWA
PAMOJA KILA MWISHO WA MWEZI.
MWAKA 1973 UONGOZI WA
SAFARI NKOI ULIANZA KUWAFANYIA ‘MTIMANYONGO’ WANAMUZIKI WAKE AKIWEMO
‘KING KIKI’ LAKINI KIKI ALIGUNDUA MAPEMA HALI HIYO, AKAMSHAWISHI
KABEYA MWAKA HUOHUO WA 1973, KUONDOKA NA KWENDA KUANZISHA BENDI YAO.
‘MWENYE BAHATI HABAHATISHI’ MSEMO HUO ULIJIONESHA
DHAHIRI KWANI KABLA HAWAJAAZISHA BENDI YAO, AKAJITOKEZA TAJIRI MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA
PARADIZO, AKIMTAKA KIKI KWENDA LUBUMBASHI KUANZISHA BENDI YAKE.
“KIKI HAKUNIACHA MWAKA 1974 TUKAENDA LUBUMBASHI KUUNDA
BENDI YA TAJIRI HUYO YA BUKA BUKA MABELE. NI UKIRITIMBA WA TAJIRI YETU,
ULISABABISHA BENDI HIYO KUFA BAADA YA MIEZI SITA…” ANAELEZEA MWANAMUZIKI HUYO.
KABEYA AKAONGEZA AKISEMA BAADA YA KUFA KWA BENDI YA
BUKA BUKA MABELE, KIKI MWAKA 1974 MWISHONI ALIAMUA KWENDA MJI MKUU WA CONGO DRC
WA KINSHASA LAKINI KABLA HAJAONDOKA, ALIWASHAWISHI YEYE NA WANAMUZIKI WENZAKE
WAREJEE SAFARI NKOI.
WALIKUBALI USHAURI HOU NAO WAKAREJEA NA
WAKAPOKELEWA NA UONGOZI WA SAFARI NKOI
KWA MARA NYINGINE TENA. KWA KIPINDI HICHO AKIWA SAFARI NKOI, KABEYA AKAWA NA
MAWASILIANO YA KARIBU NA KIKI AKIMSHAWISHI KURUDI SAFARI NKOI KWA HALI YA
UTULIVU KATIKA BENDI ILIKUWA NI IMEIMARIKA.
KING KIKI ALIREJEA LUBUMBASHI MWAKA 1976, AKITOKEA
KINSHASA PASIPO KUMAFAMAMISHA MTU
YEYOTE.
KABEYA ANASEMA “ TULIKUWA TUNAPIGA MUZIKI KATIKA
UKUMBI MMOJA WA RELE NIGHT CLUB MJINI
LUBUMBASHI, GHAFLA KIKI AKAPANDA
JUKWAANI NA KUSHIKA ‘MIC’ AKAANZA KUIMBA. SOTE TUKABUTWAIKA TUKAONA KAMA VILE ‘SHETANI’ ALIYETUA
KIMIUJIZA JUKWAANI”
MWAKA 1977
KIKUMBI MWANZA MPANGO ALIFUATWA NA
CHIBANGU KATAYI ‘ MZEE PAUL’ ALIYETOKEA MAQUIS DU ZAIRE ILIYOKUWA HAPA
NCHINI. KIKI ALIMUULIZA MZEE PAUL IWAPO
WANAMUZIKI WALIOPO MAQUIS DU ZAIRE WANAKIDHI
VIWANGO? MZEE PAUL ALIJIBU KWA
WASIWASI NA KUPENDEKEZA BORA KUCHUKUA
WANAMUZIKI HUKO DRC. KIKI ALIPENDEKEZA WANAMUZIKI WA KUONDOKA NAYE KUJA
TANZANIA AKIWEMO KANKU KELLY, MUTOMBO SOZY, ILUNGA BANZA
‘MCHAFU’ WAKIWA SAFARINI KUJA NCHINI WALIPITIA
MJI WA KAMINA AMBAKO WALIMPATA MNENGUAJI
MWANADADA NGALULA TSHIANDANDA
ALIYEKUWA AKINENGUA KATIKA BENDI YA SAKAYONSA YA MJINI HUMO.
KABEYA BADU ALIKUWA AKIWASILIANA NA KING KIKI NA AKAMUAHIDI KWAMBA ATAJITAHIDI
AJE TANZANIA.
AHADI YA KIKI KWA KABEYA IKATIMIA BAADA YA KUFIKA
MAQUIS DU ZAIRE. SAFU YA UIMBAJI IKAONEKANA KUPWAYA. ALIPENDEKEZA KUONGEZWA KWA
WANAMUZIKI ZAIDI ILI KUIMARISHA BENDI HIYO YA MAQUIS DU ZAIRE.
CHIBANGU KATAYI ‘ MZEE PAUL’ KWA MARA NYINGINE TENA AKATUMWA KWENDA
CONGO KUWALETA WANAMUZIKI
WALIOPENDEKEZWA NA KIKI.
“ TULICHUKULIWA MIMI
KABEYA BADU NA KALALA
MBWEBWE TUKIWA NI WATUNZI NA WAIMBAJI, MONGA KIYOMBO
ALIYEKUWA NA UWEZO WA KUPIGA GITA
LA RHYTHM NA SAXOPHONE. WENGINE
WALIOCHUKULIWA NI KINA NGOI MUBENGA KWA
UPANDE WA TARUMBETA NA KHATIBU ITEYI ITEYI ALIYEKUWA MPULIZJI WA SAXOPHONE TUKALETWA TANZANIA MWAKA 1978…” NATAMKA
KABEYA.
KABEYA ANASEMA MARA ALIPOTUA MAQUIS DU ZAIRE, ALITUNGA
NA KUIMBA NYIMBO NYINGI, BAADHI YAKE NI ‘NDOA YA KWANGU NA MAMA KAZI’,
‘PONDAMALI’, ‘KIBWE MUTOMBO’ NA ZINGINE ZA MUNTANDA MULI, LWEMBE NA MANENO,
AMBAZO HAZIKUWAHI KUREKODIWA.
KABEYA BADU ALIPIGA NA MAQUIS DU ZAIRE KWA MIAKA
MIWILI BAADAYE MWAKA 1980, ALICHOROPOKA NA KWENDA AKIJUNGA NA KING KIKI KATIKA
BENDI YA ORCHESTRA SAFARI SOUND (OSS) ILIYOKUWA IKIMILIKIWA NA MFANYABIASHARA
MAARUFU HUGO KISIMA.
AKIWA NA OSS KABEYA ALITUNGA NA KUIMBA NYIMBO ZA NANI
ATASHIKA JEMBE NA POLE NDUGU. ANAELEZA KUWA WIMBO WA ‘YUYU’ ULIPIGWA NA
KUREKODIWA KATIKA KIPINDI CHA KLABU RAHA LEO SHOW KILICHOKUWA KIKIRUSHWA NA
RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM. (RTD)
BADU ALIKUWA AKIHITAJIKA SANA KATIKA BENDI HIZO MBILI
PINZANI WAKATI HUO ZA MAQUIS NA OSS. HIVYO
AKAWA MITHIRI YA ‘MUIGIZAJI’ KWA
KUHAMAHAMA. ALIREJEA TENA MAQUIS KWA
KIPINDI KIFUPI KISHA MWAKA 1986 AKATAKIWA KUREJEA KWA MARA NYINGINE TENA KATIKA
BENDI YA ORCHESTRA SAFARI SOUND.
ALIPOREJEA OSS TAYARI BENDI ILIKUWA CHINI YA UONGOZI
WA NDALA KASHEBA NA HAICHUKUA MUDA MREFU AKATOKA NA WIMBO ULIOWAPAGAISHA
WAPENZI WA OSS WA ZIADA. WIMBO HUO ALIUIMBA PEKE YAKE KWA HISIA KALI AKIMLILIA
ZIADA, NA UKAMUONGEZEA SIFA KUBWA MIONGONI MWA WAIMBAJI WA MUZIKI WA DANSI HAPA
NCHINI.
ZINGINE ZILIKUWA ZA ‘ KURUTHUMU’, ‘SIMBA WALA WATU
WAMEVAMIA MJI’ MAMA MWITA, KAYANDA NA
NYINGINE NYINGI.
KABEYA BADU ANAMWELEZEA KIKUMBI MWANZA MPANGO ‘KING
KIKI’ KUWA NDIYE ANAYEJUA UMUHIMU WAKE NA HAPA ANASEMA… “ KIKI NDIYE ALIYEKUWA
AKIJUA UMUHIMU WANGU KATIKA MUZIKI TOKA MWANZO HADI AKANIPACHIKA JINA LA ‘ CHANGA CHA MKONYOYO’ IKIWA NA MAANA
YA SIRI ILIYOFICHIKA…” ALIPEWA JINA HILO BAADA YA KUFYATUA WIMBO WA CHANGA CHA
MKONYOYO’ ANAOULEZEA KUWA NI UJUMBE
MZITO JAPOKUWA WIMBO HUO HAUKUWAHI
KUREKODIWA.
ALIONDOKA OSS
NA KWENDA KUJIUNGA KWA MARA NYINGINE TENA NA MAQUIS DU ZAIRE MWAKA 1988, HAPO NAPO HAKADUMU AKACHUKULIWA
NA KWENDA KUJIUNGA NA BENDI YA TANCUT ALMASI ILIYOKUWA IKIPIGA MUZIKI WAKE
MJINI IRINGA.
‘MSAHAU KWAO MTUMWA’ KABEYA ALITAMANI KUREJEA KWAO
CONGO, NDIPO MWAKA 1990 AKAAMUA KURUDI KWAO LIKASI KATIKA JIMBO LA KATANGA.
KAMA NILIVYOKUJUZA MWANZONI KWAMBA KABEYA ALIKUWA
MTAFUTAJI WA MASLAHI MURUA, HIVYO
ALIREJEA TENA TANZANIA MWISHONI MWA
MWAKA 1998. MWAKA ULIOFUATIA WA 1999,
AKAPEWA KAZI YA KUANZISHA BENDI YA MAGOMA SOUND YA JIJINI DAR ES SALAAM.
MWAKA 2001 ALIJIUNGA KATIKA BENDI YA LA CAPITALE
INAYOONGOZWA NA KIKUMBI MWANZA MAPANGO ‘KING KIKI’ AU ‘BWANA MUKUBWA’ HADI
MAUTI YAKE YALIPOMFIKA JUMATANO ILIYOPITA YA TAREHE 06 MACHI, 2013.
KABEYA ALISEMA KWAMBA ANA MATARAJIO MAKUBWA ANAYOTAMANI KUFIKIA. “NINA MPANGO WA KUNUNUA VYOMBO VYANGU VYA
MUZIKI, PIA NATARAJIA KUREKODI NYIMBO ZAGU ZOTE NILIZOTUNGA NA KUZIIMBA,
NZIUZE MIMI MWENYEWE…” ANASEMA KABEYA
AKIWA MWINGI WA TABASAMU USONI.
NINASIKITIKA KWA KUSEMA KUWA KUMBE KAULI HIYO
IKIFUATIWA NA TABASAMU HILO, ILIKUWA LA
NDIYO MWISHO, TUKIAGANA NAYE!
KABEYA BADU ALINISISITIZA KWAMBA MARA TU MAKALA HII IKITOKA, NIMUALIFU ILI
AWAHI KUNUNUA GAZETI HILI, LAKINI MPANGAJI WA YOTE NI MUNGU.
KIONGOZI WA BENDI YA LA CAPITALE, KIKUMBI MWANZA
MPANGO KING KIKI’ ALIMUELEZEA KUWA PENGO LA KABEYA KAMWE
HALITAZIBIKA. “ KABEYA PENGO LAKE HALITAZIBIKA KAMWE AMETUACHIA UKIWA USIO NA KIFANI. ALIKUWA NI MTUNZI NA MWIMBAJI MZURI SI HIVYO TU PIA ALIKUWA
MSIKIVU, MTU WA KAZI TULISHAURIANA KUTENGENEZA ‘MELODY’NA KWA KWA USHIRIKIANO
HUO TULIKUWA TUKICHOKOZANA NA KUTOA VIBAO ‘MATATA’ SANA. TUMEMPOTEZA KABEYA…”
KWA MASIKITIKO NA MAJONZI ANASEMA KIKI.
KABEYA CHIBANGU
BADU, AMEACHA MJANE NA WATOTO WANANE KATI YAO WATANO NI WA KIKE.
WAPENZI NA WADAU WA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI, KAMWE HATAMSAHAU KABEYA BADU KWA JINSI
ALIVYOKUWA NA UWEZO WA KULISHAMBULIA
JUKWA KWA KUCHEZA NA KUPAZA SUTI YAKE ILIYOKUWA NYORORO WAKATI AKIIMBA.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE PAHALA PEMA
PEPONI, AMINA.
MWANDISHI WA MAKALA HII ANAPATIKANA KWA NAMBA HIZI:
0784331200, 0767331200 na 0713331200.
No comments:
Post a Comment