MAKOMA TROUPES
TUNAPOTAJA WAIMBAJI WA INJILI AMBAO
WAMEWAHI KUTAMBA KATIKA KATIKA TASNIA HIYO NI PAMOJA NA KUNDI LA MAKOMA.
KUNDI HILO LILILOKUWA LIKIWAKILISHWA
NA NDUGU SITA KAKA WAKIWA WATATU NA DADA WATATU PAMOJA NA RAFIKI WA FAMILIA YAO
LILIWEZA KUITIKISA DUNIA HASA KWA WAPENZI WA MUZIKI WA INJILI NA HATA WALE
WANAOSIKILIZA NYIMBO ZA KIDUNIA KWA NYIMBO ZAO.
HISTORIA YA KUNDI HILO LINALOVUTIA
AMBALO LINAIMBA KWA KUTUMIA MTINDO WA RUMBA, POP NA R & B HUKU WAIMBAJI
WAKE WAKITOKEA KINSHASA,JAMHURI YA DEMOKRASIA YA KONGO NA KUHAMIA UHOLANZI
LIMESHAFANYA KAZI KARIBU NCHI NYINGI ZA AFRIKA.
WAIMBAJI WANALOUNDA KUNDI HILO NI NATHALIE MAKOMA
ALIYEJITOA MWAKA 2004, ANNIE MAKOMA, PENGANI MAKOMA, TUTALA MAKOMA, DUMA
MAKOMA, MARTIN MAKOMA NA RAFIKI YAO PATRICK BADINE.
WAKIIMBA KWA KUTUMIA LUGHA YA
LINGALA NA KIINGEREZA LAKINI PIA WANATUMIA KIFARANSA,KIRENO NA KIJERUMANI
WAMEWEZA KUJIHAKIKISHIA KUENDELEA KUBAKI KATIKA TASNIA HIYO KILA WANAPOFYATUA
ALBAMU.
KUNDI HILO LILIPATA PIGO MWAKA 2004
BAADA YA MWIMBAJI WAO NYOTA WA KUNDI HILO LILILOJIPATIA UMAARUFU BARANI AFRIKA
NA KWINGINEKO DUNIANI, NATHALIE MAKOMA AMBAYE AMEJIFUNGUA MTOTO WAKE WA KWANZA
AITWAYE GIOVANNI CLAUDIO II, MWAKA HUU NA MUMEWE, JC ATAMBOTO, AMBAYE PIA
ANAJIHUSISHA NA MAMBO YA MUZIKI KULIKACHA KUNDI HILO.
NATHALIE BAADA YA KULIKACHA KUNDI
HILO NA KUAMUA KUIMBA MUZIKI WA KIDUNIA AKIWA NJE YA KANISA KUTOKANA NA KILE
ALICHODAI KUTAKA KUFANYA KAZI NYINGINE, HUKU WAJUZI WA MAMBO WAKIDAIWA KUWA NI
UGOMVI BAINA YAKE NA KAKA YAKE MKUBWA AMBAO AMEKUWA AKIUZUNGUMZA SANA KWENYE
VYOMBO VYA HABARI HADI KUFIKIA MASHABIKI KUMTAKA BINTI HUYO AMBAYE ALIKUWA NI
MWANZILISHAJI NA ANAYETEGEMEWA NA KUNDI HILO KWA TAKRIBANI NYIMBO ZOTE ZA KUNDI
HILO, KUACHA KUFANYA HIVYO KWANI HATA IWEJE YULE NI KAKA YAKE PIA WANATAKIWA
KUZUNGUMZA MASUALA YAO KIFAMILIA NA SIO KUANIKA KWA KILA MTU.
MWIMBAJI HUYO AMBAYE ALISHIKA NAFASI
YA PILI KATIKA SHINDANO LA KUTAFUTA MWIMBAJI MAARUFU LILILOITWA NETHERLANDS
IDOL MWAKA 2008 NA KUPEWA JINA LA TINA TURNER.
NATHALIE MAKOMA ALIYEANZA KUIMBA
MWAKA 1993 KATIKA BENDI YAO ILIJULIKANA KAMA "NOUVEAU TESTAMENT"
KABLA KUJIUNGA NA MAKOMA.
NATHALIE ALIPOFIKISHA MIAKA 14
ALIHAMIA UHOLANZI NA KUPATA ELIMU YA KULITAWALA JUKWAA KATIKA CHUO CHA
ROCKACADEMIE HUKO TILBURG.
BAADA YA KUNDI LA MAKOMA KUZUNGUKA
DUNIANI NA KUPATA MAFANIKIO NATHALIE ALIACHA SHULE RASMI NA KUZUNGUKA
AKITANGAZA NJILI KWA NJIA YA UIMBAJI.
MASHABIKI WA KUNDI LA MAKOMA
WAMEKUWA WAKIMUOMBEA MWIMBAJI HUYO ILI ARUDI KUMTUMIKIA MUNGU PIA KURUDISHA
MAHUSIANO NA NDUGU ZAKE AMBAO PIA WALIKOSA HATA KUHUDHURIA SHEREHE ZA
UVALISHWAJI PETE YA UCHUMBA AMBAYO ILIGUBIKWA NA UTATA BAADA YA KUONEKANA KWA
VITUKO VINGI VILIVYOTOKEA HADI HARUSI NA KUSABABISHA MASWALI MENGI KAMA ILIKUWA
NDOA YA KWELI ALIYOKUWA AKIIFANYA MWIMBAJI HUYO AMBAYE PIA AMESHIRIKISHWA NA
PAPA WEMBA KATIKA MOJA YA NYIMBO ZAKE MKONGWE NCHINI CONGO.
NATHALIE MAKOMA ALIZALIWA FEBRUARI
24, MWAKA 1982 HUKO LIBREVILLE ZAMANI GABON AKIWA KAMA MHOLANZI NA WAZAZI WAO
WAKITOKEA DRC.
NATHALIE MWIMBAJI MWENYE SAUTI
NZITO, YENYE MVUTO MWENYE AIBU UKIZUNGUMZA NAE LAKINI AKIWA JUKWAANI NI MTU
MWINGINE ASIYE NA AIBU WALA WOGA WA CHOCHOTE.
WANAMUZIKI HAO AMBAO WALISHAWAHI
KUPATA TUZO YA KORA WAKISHINDA KUNDI BORA LA MUZIKI LA AFRIKA MWAKA 2002 NA
KUNDI BORA LA KUSINI MWA UKANDA WA PASIFIKI MWAKA 2005.
KUNDI LA MAKOMA LINA ALBAMU SABA
KIBINDONI JAPO ALBAMU YAO YA KWANZA ILIYOTOKA MWAKA 1999 YA NZAMBE NA BOMOYI
(JESUS FOR LIFE) NDIYO ILIYOWAPA UMAARUFU NA KUKAMATA TASNIA YA MUZIKI WA
INJILI IKITAMBA KWA NYIMBO KAMA NAPESI, BUTU NA MOYI, MWINDA, MOTO OYO,
NATAMBOLI NA NZAMBE NA BOMOYI.
MWAKA 2000 KUNDI HILO LILIFYATUA
ALBAMU NYINGINE ILIYOPEWA JINA LA KUNDI HILO AMBAYO ILIKUWA NA NYIMBO 14
IKIWEMO BABY COME,I'M SO EXCITED,MY LOVE IS TRUE ,SWEETER NA NYINGINEZO.
HARAKATI ZA KUNDI HILO HAZIKUISHIA
HAPO KWANI MWAKA 2002 WALITOA ALBAMU YAO NYINGINE MOKONZI NA BAKONZI IKIWA NA
MAANA MFALME WA WAFALME IKIBEBA NYIMBO ZILIZOIMBWA KWA KILINGALA KAMA VILE
MOKONZI NA BAKONZI, NASENGI,BANA, NALELI,NZAMBE NA NGAI NA TOLINGANA.
MWAKA 2005 ALBAMU YA NA NZAMBE TE,
BOMOYI TE IKIMAANISHA BILA YESU HAKUNA MAISHA WAKICHANGANYA LINGALA NA
KIINGEREZA ILITAMBA NA KUWAFANYA KUENDELEA KUWA JUU KATIKA MUZIKI HUKO NCHINI
UHOLANZI WAKIIMBA BILA NDUGU YAO NATHALIE.
NA ALBAMU YAO YA TANO YA MY SWEET
LORD WALIOFANYA KAMA KUNDI NA KUMSHIRIKISHA NATHALIE KAMA MWIMBAJI
ANAYEJITEGEMEA.
ALBAMU YA EVOLUTION WALIYOITOA MWAKA
HUU IKIWA NA NYIMBO KUMI, ALBAMU HIYO INA NYIMBO KAMA VILE EVOLUTION, ALINGI BISO,
YO OZALI, NDEKO, MOKONZI, SE YE, MABOKO LIKOLO, MOKILI, SOSOLA NA NGUYA NA
YE.
ALBAMU HIYO AMBAYO NI YA KWANZA
TANGU WAUNGANE TENA MWAKA JANA NA KUAMUA KUITENGENEZA KUNA NYIMBO KAMA SOSOLA,
YO OZALI NA NYIMBO NYINGINE ZIKIWA ZINAFANYA VIZURI KWENYE VITUO VYA RADIO
NCHINI KWAO WALIKOZALIWA KONGO PAMOJA NA NCHINI NYINGINE DUNIANI BILA KUSAHAU
AFRIKA YA MASHARIKI.
No comments:
Post a Comment