ANGELIQUE KIDJO ASHINDA TUZO YA GRAMMY
Mwanamuziki
wa nchi ya Benin Angelique Kidjo ameshinda tuzo ya Grammy pamoja na
wanaharakati watatu kutoka barani Afrika, wametuzwa tuzo ya haki za kibinaadamu
mwaka 2016 kwa kusimamia haki na shirika la Amnesty International.
Wengine
walioshinda ni pamoja na Yen a Marre wa Senegal, Le Bali Citoyen kutoka Burkina
Faso na Lucha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katibu
Mkuu wa Amnesty International Salil Shetty alitangaza katika taarifa yake
kwamba wote wameonyesha ujasiri, shirika hilo la haki za kibinaadamu kwamba wanapigania
haki za kibinaadamu kwa kutumia vipaji vyao kuwashiwishi wengine.
Kidjo
pia anajulikana kwa kampeni yake kwa uhuru wa kujieleza pamoja na vita dhidi ya
ukeketaji.
Mwanamuziki
huyo amejiunga na orodha ya watu maarufu ambao wameshinda tuzo ya ubalozi wa
watu walio na dhamira ya kubadilisha uovu katika jamii, akiwemo rais wa kwanza
Afrika kusini Nelson Mandela na msanii wa China Ai Weiwei.
Msomaji wa makala haya itakuwa vyema kuufahamu wasifu wa
mwanamama huyo Angelique Kidjo.
Yeye ni mwanamuziki mashuhuri aliyejizolea sifa
lukuki katika umahiri wa kutunga na kuimba nyimbo zenye maudhui yanayokubalika
katika jamii.
Anafahamika sana kwa mtindo wake wa kuchanganya miondoko
mbalimbali ya kimuziki ya Afro pop, Afro beat, reggae, muziki wa dunia, Jazz,
muziki wa injili na Latin.
Kidjo katika usifu wake unaeleza kuwa ni mtu mzima kwa
umri ambae Julai 14, 2016 atatimiza miaka 56 tangu azaliwe Julai 14, 1960 katika
mji wa Ouidah huko Jamhuri ya Benin, Afrika ya Magharibi.
Kwa wale wanaojuwa Jiografia vizuri watabaini kuwa nchi
hiyo zamani ilikuwa ikiitwa Dahomey.
Hadi sasa anaendeleza talanta zake za utunzi na uimbaji
wa muziki wa Afropop, Afrobeat, Reggae, muziki wa dunia, Jazz, muziki wa Injili
na Latini.
Wakati akiwa na umri wa miaka sita, Kidjo alianza
kijihusisha na kikundi cha Kibisa kilichokuwa kinamilikiwa na mama yake mzazi. Mama
huyo ndiye akawa anampa kipaumbele sana katika muziki na kucheza pia.
Lakini kuendelea kwa machafuko ya kisiasa nchini Benin,
kulipelekea Kidjo kukimbilia katika jiji la Paris nchini Ufaransa, mnamo miaka
ya 1982.
Mwaka huo huo ndipo mkongwe huyo alipoianza kazi ya muziki mpaka hivi sasa bado anaendeleza
talanta yake.
Alianza kama mwimbaji wa bendi za vichochoroni kabla ya
kuanzisha bendi yake mwenyewe, na mwishoni mwa miaka ya 1980.
Kidjo akatokea kuwa mmoja kati waimbaji maarufu wa
jukwaani huko Paris na amewahi kushinda mara tano tuzo ya Grammy kama mtunzi na
mwimbaji bora.
Aidha Angelique pia talanta ya ubunifu mzuri wa ‘sini’
za video.
Kidjo ni mama wa familiya ya mume ambaye pia ni
mwanamuziki na mtayarishaji aitwae Jean Hebrail.
Wamebahatika kupata mtoto mmoja aitwae Naïma,
aliyezaliwa mwaka 1993.
Kama walivyo wanamuziki wengi wenye mafanikio mazuri,
Kidjo kwa sasa anaishi New York, huko Marekani akifanya shughuli za muziki na
zinginezo.
Nguli huyo amekuwa balozi wa kujitolea wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la UNICEF tangu 2002.
Kidjo katika juhudi zake za maendeleo zilipelekea
kuanzisha mfuko uitwao Batonga Foundation. Mfuko ambao una lengo kubwa la kutoa
elimu ya juu ya sekondari kwa wasichana kwa madhumuni ya kuwapa mwongozo wa
maisha katika kuibadilisha Afrika.
Batonga Foundation pia unakubali ufadhili wa wanafunzi,
kujenga shule za sekondari, kuongeza uhandikishaji zaidi, kuboresha viwango vya
ufundishaji, na kukimu uenezaji wa shule.
Adha mfuko huo husaidia mipango
endelevu katika elimu, kutafuta njia ya mbadala ya elimu na kiuwakilisha katika
jumuiya kuwa kama ndio kutambua thamani ya elimu kwa wasichana.
Angelique Kidjo aliwahi kutamba kwa wimbo uliomuongezea
umaarufu ni wa ‘Agollo’.
Katika video ya wimbo huo anaonekana akitamba jukwaani
huku akiwa kanyoa kiparakichwani.
Mwanamama huyo amekwisha fyatua albamu nyingi zikiwemo
za ‘Parakou’ aliitoa mwaka 1990, ‘Longozo’ ya 1991, ‘Aye’ ilitoka mwaka 1994 , ‘Fifa’
ya mwaka 1996 na ‘Oremi’ ya mwaka 1998.
Alipiga nyimbo mchanganyiko zikiwemo za Black Ivory Soul
ya mwaka 2002, Oyaya ya mwaka 2004 na Djin Djini ya 2007.
Aidha Kidjo aliwahi urekodi nyimbo nyingi tu kwa ajili
ya filamu mbalimbali.
Amekwisha tunukiwa tuzo zikiwemo za Octave RFI na Prix
Afrique en Creation alizopokea mwaka 1992.
Kidjo pia aliwahi kurekodi nyimbo
nyingi kwa ajili ya filamu mbalimbali.
Alipata tuzo ya uimbaji bora wa kike mwaka 1995,
kwenye Kora Music Awards, mwimbaji bora
kike wa Afrika mwaka 1997 na tuzo ya Mobo ya mwaka 2002.
Grammy ilimtunuku tuzo kupitia kipengele cha nyimbo bora
ya Video ya mwaka 1995 na albamu bora ya Dunia kwa mwaka wa 1999, 2003 na 2005.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment