Sunday, November 1, 2015

MJUE "JIM REEVES" ALIYETAMBA KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI


MJUE "JIM REEVES" ALIYETAMBA KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI

Hapana shaka watu wazima wenye umri wa mkubwa kama wangu, ukitamka jina la Jim Reeves, unakuwa umewakuna vilivyo.

Alikuwa ni mwanamuziki wa Kimarekani aliyejikita katika miondoko ya muziki wa ‘Country’ na muziki wa kawaida kama  mtunzi haklikadhalika uimbaji.

Reeves aliweza kuweka rekodi ya muziki wake ukupanda chati toka miaka ya 1950 hadi ya 1980.   

Muziki wake ukawa maarufu na kujulikana kama mwanamuziki wa midundo ya ‘Nashville’ (ambayo ni mchanganyiko wa muziki wa zamani wa country na ule wa kisasa). 

Wasifu wa nguli huyo unaonesha kuwa  jina lake halisi alikuwa ikiitwa
James Travis aka “Jim” Reeves aliyezaliwa Agosti 20, 1923 Reeves amezaliwa katika kitongoji cha Galloways huko Texas, nchini Marekani.

Alitambulika kama ‘Muungwana Jim’ na nyimbo zake ziliendelea kupanda chati kwa miaka kadhaa hata baada ya kifo chake.
Reeve alikuwa akitoka katika jamii ya watu waliokuwa nje ya mji karibu na Carthage. Alifariki Julai 31, 1964 akiwa na umri mdogo wa miaka 40 katika ajali ya ndege binafsi.

Yeye alikuwa mwanachama wa muziki wa ‘Country’ na pia ule wa Texas Country Halls of Fame.

Jim alifanikiwa kupata nafasi ya kusomamsomo ya juu ‘Scholarship’ ambapo alijisaljili kusomea masuala ya kuhutubia na maigizo.

Baada ya miezi sita katika masomo hayo, aliachana nayo akaamua kwenda kufanya kazi katika yadi ya kutengeneza Meli huko Houston.

Licha ya kuwa na weledi katika muziki Reeves pia alikuwa mwanariadha aliyewahi kuchezea ligi za Semi-Professional kabla hajaingia mkataba na St. Louis Cardinals, timu ya shamba. Mwaka 1944 alicheza kama right-handed Pitcher. 

Aidha alicheza ligi ndogo kwa miaka mitatu kabla hajaumia na kupata maumivu katika misuli iliyohitimisha juhudi zake za kuendelea na michezo.
Reeves alianzia kufanya kazi kama mtangazaji wa radio. 

Kila wimbo umalizikapo kuupiga radioni, yeye akawa anaimba wimbo huo.

Mwishoni mwa miaka ya 1940, aliingia mikataba na baadhi ya Makampuni madogo ya kurekodi, huko Texas lakini hakupata mafanikio. 

Muziki wa Magharibi ulimfanya kuhamasika sana hususani alipokuwa akiwasikia wanamuziki kama Jimmie Rodgers na Moon Mullicann. 

Waimbaji wengine maarufu wakati huo aliokuwa akiwatamani ni akina Bing Crosby, Eddy Arnold na Frank Sinatra.

Mapenzi hayo makubwa katika muziki yalimpelekea kuwa mwanachama wa bendi ya Moon Mulican.

Jim aliweza kufanya mitindo ya mwanzoni za bendi ya Mullican, nyimbo zake kama ‘Each Beat of My Heart’ na ‘My Heart’s Like a Welcome Mat’ mnamo miaka ya 1940 mwishoni na mwanzoni 1950.
 
Reeves aliweza kuimba nyimbo za ‘Mexican Joe’ ambazo zilishika namba moja mwaka 1953.

Kutoka mwaka 1955 mpaka kuendelea mwaka 1969 Reeves nyimbo zake ziliendelea kushika ‘ukanda’ hata baada ya yeye kufariki.

Nyimbo zake za kwanza za ‘Country’ zilizompa mafanikio zilikuwa ni pamoja na ‘I Love You’ alouimba akishirikiana na Ginny Wright, na ‘Mexican Joe’ ‘Bimbo’.
 
Nyimbo nyingine zilizotolewa na Fabor Records na Abbott Records ilitoa albam yake ya kwanza Novemba, 1955 iliyojulikana ‘Jim Reeves Sings’. 

Mapema mwaka 1955, Reeves alisaini mkataba wa miaka 10 na Kampuni ya RCA Victor chini ya Steve Sholes, ambaye alitoa rekodi za kwanza za Reeves akitumia Kampuni ya RCA na pia akaingia mkataba na Elvis Presley na kampuni hiyo hiyo mwaka huo huo.

Alipokuwa akirekodi mwanzoni akiwa na  Kampuni ya RCA, Reeves bado alikuwa anaimba kwa staili ya sauti ya juu ambapo ilionekana ndio kipimo cha nyimbo za ‘Country’ Wanamuziki wa Magharibi kwa wakati huo. 

Baadaye Jim alianza kupunguza sauti yake wakati akiimba na kutumia ‘Pitch’ ya chini akiimba huku midomo yake ikikaribia kugusa kipaza sauti, ingawaje waliokuwa wanamrekodi (RCA) walikuwa wanailalamikia hali hiyo. 

Mwaka 1957 kwa maelekezo ya ‘Produysa’ wake Chet Arkins alitumia mtindo huo katika toleo la wimbo wa maonesho wa ‘Penzi lililopotea’ uliokusudiwa uimbwe na mwimbaji wa kike.

Katika kipindi chote miaka yote ya 1950 na hadi 1960 mwanzoni, Jim Reeves aliachia nyimbo zake kali zizoshika ‘chati’ za ‘Anna Marie’ na  ‘Blue Boy’ No. 2 za mwaka  1958.

 Alifyatua kibao kingine cha ‘Billy Bayo’ mwaka 1959 na  ‘He will have to go’ wa mwaka 1960., ‘Adious Amigo’ (namba mbili, 1962), ‘Welcome to my World’ (namba mbili, 1964) na ‘I guess I’m crazy’ (namba moja kwa wiki saba, 1964).
Jim Reeves  pia alikuwa na kikosi na idara ya nyimbo za dini katika jukwaa lake.
Wimbo wake, ‘Danny Boy’ akijitambulisha kwamba wazazi wake wametokea Irish. Wimbo ‘But You Love Me Daddy’ ukirekodiwa wakati mmoja akiwepo ‘Steve’ mtoto wa miaka minane wa mpiga gitaa la besi, Bob Moore, ulikuwa katika ishirini bora huko Ulaya miaka kumi Baadaye. 

Rekodi zake mara nyingi zilikuwa na utamanifu wa kipekee, kama ‘I Love you Because’ (ulishika namba 5) na ‘I won’t forget You’ (namba 3) zilikuwa katika chati huko UK kwa wiki 39 na 25 mfululizo.

Reeves alikuwa amesaidia sana kuanzisha staili mpya ya muziki wa ‘Country’ akitumia ‘violin’ na ‘mpangilio wa kupendeza wa background ikijulikana kama ‘Nashville’ sound.   

Alipata umaarufu kama muimbaji wa kiume mwenye sauti ya kupendeza na nzito kiasi, yenye madaha. 

Nyimbo kama ‘Adios Amigo’ ‘Welcome to My World’ na ‘Am I Losing You’ zinaonyesha hili. 

Nyimbo zake za Chrismas zikijirudia rudia na kupendwa sana hasa zikiwa ni pamoja na ‘Chrismas’ ‘Blue Chrismas’ na ‘An Old Chrismas Card’.
 
Hali kadhalika Jim Reeves amekuwa hodari kwa kuukweza na kuzipa maarufu nyimbo nyingi za ‘Injili’ kama ‘We Thank Thee’ ‘Take My Hand, Precious Lord’ ‘Across The Bridge’ ‘Where We’ll Never Grow Old’ na nyingine nyingi.

Reeves aliibua mafanikio makubwa kwa utunzi wa Joe Allison, ‘He’ll have to Go’. 

Kwa kweli kulikuwa na mafanikio makubwa kwa muziki huu wa kawaida na wa ‘Country’ ambapo ulimpatia ‘Platinum Record’ ambayo ilitolewa mwishoni mwa mwaka 1959 na ilifanikiwa  kuwa namba moja katika gazeti la ‘Billboard’. 

Katika nyimbo za ‘Country’ ambazo zili ‘hit’  kuanzia 08/February, 1960 na kuendelea kwenye chati kwa wiki 14 mfululizo hii moja wapo.

Mwana historia wa muziki wa Country, Bill Malone alionesha kwamba ni katika namna nyingi Reeves aliendeleza utamu na ubora katika   muziki wa ‘Country’ kimpangilio na ‘melodi’ safi na ujumbe unaogusa  mioyo ya watu. 

Kwa nyongeza, Malone alimsifia Reeves kwa staili yake ya kuimba ambayo anaishusha chini sauti yake, inakuwa kama ya kubembeleza na ndio maana watu wengi wanatamka kwamba Jim Reeves ni muimbaji mwenye sauti ya mguso.

July 31, 1964, Reeves na mshirika mwenzake wa kibiashara, Meneja Dean Manuel waliondoka Batesville, Arkansas kupitia Nashville wakitumia ndege ya injini moja akiwa Reeves anaendesha.

Wawili hao walikuwa wamepata ‘dili’ ya kununua shamba huko Deadwood Texas, Kaskazini mwa Galloway ambayo ni sehemu aliyozaliwa Reeves.

Wakati wanapaa juu kwa ndege akiwa na  Brentwood, Tennessee, walikutana na dhoruba ya upepo mkali na mvua kubwa.

Katika uchunguzi ilionekana ndege hiyo ndogo ilinaswa katika dhoruba na Reeves alipata mstuko ikaanguka na wao wakafariki. 

Mjane wa marehemu, Mary Reeves  alianzisha uvumi kwamba Reeves alikuwa akiendesha juu chini na aliongeza spidi ili kukwepa  dhoruba.

Hata hivyo kulingana na Larry Jordan, maelezo ya mjane wake kwamba Reeves alikuwa anaendesha chini juu si sahihi.
Kutokana na watu walioiona ajali hiyo jinsi ndege ilivyoanguka na  maelezo yaliyomo kwenye tape iliyorekodi mwenendo wa ndege.

Pia maelezo ya ripoti ya ajali, kwamba Reeves alikata kushoto katika jitihada zake za kuipata Franklin road ili afike uwanja wa ndege aweze kutua.  

Katika jitihada yake hiyo  akazidi kuelekea kule kwenye mvua kubwa.

Katika kuhangaika ili akakipate kiwanja ili kutua,  spidi ya ndege ikawa ipo chini hivyo akaikwaza ndege. 

Reeves alitegemea zaidi hisia zake katika kumuongoza na hakutumia maarifa  aliyofundishwa chuoni kuikabili hali kama hiyo. 

Baada ya masaa 42 mabaki ya ndege yalionekana ikiwa  mbele, yaani usoni pamoja na injini vimejikita ardhini.  Reeves na mwenzake walikutwa tayari wamekwisha fariki.

Jim Reeves alizikwa katika kipande cha ardhi maalum ubavuni mwa ‘Highway 79’ Texas.

Licha ya kufariki Jim Reeves bado umaarufu wake haukupotea, kwa hakika mauzo ya kazi zake yameongezeka baada ya kufariki.
  
Mjane wake, Mary Reeves (70) alifariki katika siku ya ‘Veteran’ Tarehe Novemba 11, 1999, iliripotiwa kuwa amekufa akiwa peke yake katika nyumba ya kuuguza wagonjwa. 

Hata hivyo mazishi yake yalipangwa kwa watu wachache tu wa karibu ikiwa hii ni agizo la aliyekuwa mumewe wa pili Tery Davis.

Tangu kipindi cha kifo cha Jim Reeves kulipotokea, Mary alipatwa na matatizo ya kuugua kabla hayajamzidia. 

Alikuwa ni kiungo muhimu katika kuuweka muziki wa Reeves na kumbukumbu zake alizifanya kuwa hai.

Kutokana na Mary Reeves Davis kushindwa kutokana na ugonjwa kuzisimamia mali za Jim Reeves ziliuzwa kwa ‘United Show of America’ mwaka 1997 kwa thamani  ya Dola za Kimarekani milioni 7.3
Jim Reeves aliwekwa kwenye kundi la mwimbaji Nyota wa Kiume ambaye ametokeza katika midundo ya ‘Nashville Sound’.
Sauti yake laini ya kidume yenye madaha imeendelea kusikika hadi wakati leo.

Mwisho.


Saturday, October 10, 2015

JE, UNAFAHAMU KAMA ILIKUWEPO BENDI YA WANAWAKE NCHINI?



JE, UNAFAHAMU KAMA ILIKUWEPO BENDI YA WANAWAKE NCHINI? 

Ule usemi kwamba “Wanawake wanaweza” inaelekea kwamba ulikuwepo tangu zamani. Mnamo miaka ya 1960, hapa nchini ilianzishwa bendi ya wanawake watupu ikiwa na jina la ‘ Women Jazz Band.
Bendi hiyo haikufahamika sana kwa kuwa haikudumu sana na pia nyimbo zake hakuendelea kupigwa katika vituo vya redio licha ya kuvirekodi katika redio ya taifa wakati huo ya Radio Tanzania Dar es Salaam(RTD).
Kama ilivyo kwa historia kwamba huwa haifutiki, inaeleza kuwa mwaka 1965, kundi jipya la aina yake lilianzishwa nchini humu lilikuwa ni bendi ya akina mama watupu. Bendi hiyo iliitwa Women Jazz.
Akina mama hao wengine walikuwa ni wafanyakazi wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali (Government Press), ambao walijichaguana wakaanza kuhudhuria mafunzo ya muziki chini ya yule mwanamuziki mahiri Mzee Mayagilo.
Mayagilo kipindi hicho alikuwa kiongozi wa kitengo cha muziki Brass band katika Jeshi la Polisi, waanza mazoezi kwa nguvu.

Bendi hiyo ilikuwa chini ya Umoja wa Vijana wa TANU (TANU Youth League) wakati ule. Sasa ni UVCCM.
Kina mamam hao walipokuwa wakianza shughuli hiyo walikuwa hawana ujuzi wowote wa katika muziki. Kutokana na jitihada zao wakajitengenezea utaratibu wa kuanza kufanya maonesho yao hasa kwenye hafla za serikali na Chama tawala cha TANU wakati huo.
Dhamira yao ilitimia Mei 31, 1966 ambapo bendi yao iliingia katika studio za RTD zilizopo jijini Dar es Salaam na kurekodi nyimbo zao sita.
Nyimbo hizo zilikuwa za Tumsifu mheshimiwa, Leo tunafuraha, Mwalimu kasema, Women Jazz, Sifa nyingi tuwasifu viongozi na TANU yajenge nchi.
Nathubutu kutamka kwamba nyimbo za akina mama hao hazifahamiki kwa kizazi hiki kwa kuwa hazisikika zikipigwa katika kituo cha redio chochote hata TBC taifa iliyo na maktaba kubwa ya muziki!
Ka mantiki hiyo basi itakuwa ni busura zikatumika kwa uongozi bora wa TBC Taifa, kuzikumbuka kupiga nyimbo hizo ili kuweka changamoto kwa kizazi hiki hususani kwa akina dada wanao chipukia kimuziki.
Women Jazz alikuwa ikiundwa na akina Mary Kilima, Juanita Mwegoha, Rukia Hassan na Siwema Salum ambao walikuwa waimbaji katika bendi hiyo.
Wengine ni Kijakazi Mbegu aliyekuwa akilicharaza gitaa la solo, Mwanjaa Ramadhani alikuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi na Chano Mohammed, aliyekuwa akipiga gitaa la kati la rhythm.
Kwa upande wa ‘mdomo wa bata’ walikuweapo Tatu Ally na Anna Stewart waliokuwa wakipuliza Alto Saxophone wakati Mina Tumaini na Rukia Mbaraka wakipuliza Tenor Saxophone.
Mama aliyejulikana kwa jina la Lea Samuel alikuwa akichangaya Bongos, wakati huohuo Josephine James alikuwa akidunda  drums.
Miaka hiyo kulikuwa na zana nyingi za muziki tofauti na miaka hii. Kulikuwepo na chombo kikiitwa Maracass kilichokuwa ambacho katika bendi hiyo kilichezwa na Zainabu Mbwana wakati kile cha Timing alikuwepo Tale Mgongo.
Kwa wale wasioijuwa ama kukumbuka historia ya chama cha TANU, kirefu chake ni Tanganyika African National Union. Hicho ndicho kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hicho na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar, vilipounda Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977.
Chama cha TANU kilianzishwa 7 Julai, 1954, kabla yake kulikuwepo na chama cha Tanganyika African Association (TAA).
TAA ilikuwa na mwelekeo wa kitamaduni zaidi ya siasa. Mwenyekiti wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Kambarage Nyerere.
TANU ilikuwa ikishinda kila uchaguzi chini ya utawala wa kikoloni ikawa chama cha kuongoza Tanganyika hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1961.
Katiba ya Taifa ya mwaka 1962 ilifanya TANU kuwa chama cha pekee nchini ikifuata mfano wa nchi za kijamaa zenye muundo wa siasa ya chama kimoja.
Bendi ya Women Jazz ilipata umaarufu kiasi cha kuanza kufanya safari nje ya Tanzania, na kuweza kufanya maonesho katika miji ya Nairobi na Mombasa, baada ya kutembelea miji kadhaa hapa nchini.
Baada ya waaamuziki wa bendi hiyo kujiona hawapati faida yeyote kutokana na mapato ya bendi yao, wakiwa katika maandalizi ya kufanya ziara ya kwenda nchini China, bendi hiyo ilisambaratika.
Hii chamngamoto kwa Wanawake wa hapa nchini kuiga mfano wa wenzao waliowatangulia wakathubutu, wakafanikiwa kuwa na bendi yao.

Mwisho.




BENDI YA MLIMANI PARK ILIVYOLITEKA JIJI LA DAR ES SALAAM



BENDI YA MLIMANI PARK ILIVYOLITEKA JIJI LA DAR ES SALAAM

KWA KAWAIDA HISTORIA YA JAMBO LOLOTE HUWA HAIFUTIKI. HISTORIA YA BENDI YA MLIMANI PARK ORCHESTRA INAELEZA KUWA MWANAMUZIKI MWANZILISHI WA BENDI HIYO ALIKUWA ABEL BARTAZAR ALIYEUNGANA NA WANAMUZIKI WANANE WALIOIHAMA BENDI YA DAR INTERNATIONAL WAKAENDA KUIJENGA VILIVYO MLIMANI PARK ORCHESTRA  MWAKA 1978.

WANAMUZIKI HAO NI PAMOJA NA ALIYEKUWA MTAALAMU WA KUPIGA ALA ZOTE ZA MUZIKI, MICHAEL ENOCK ‘KING’, JOSEPH BENARD, JOSEPH MULENGA, ABDALAH GAMA, COSMAS CHIDUMULE, MACHAKU SALUM NA HABIB JEFF. 

BENDI YA MLIMANI PARK ORCHESTRA ILIKUWA CHINI YA UONGOZI WA TANZANIA TRANSPORT AND TAX SERVICES (TTTS), IKIWA NA MASKANI YAKE PALE MLIMANI CLUB MITAA YA MWENGE JIJINI DAR ES SALAAM.

MLIMANI BAADAE MWAKA 1983, ILICHUKULIWA KUWA CHINI YA SHIRIKA LA MAENDELEO YA DAR ES SALAAM (DDC), BAADA YA  WALIOKUWA WAMILIKI TTTS  KUFILISIKA.

BENDI HIYO IKAANZA KUITWA KWA JINA LA DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA IKIWA CHINI YA WANAMUZIKI WAASISI, MUHIDIN MAALIM GURUMO, ABEL BALTAZAR, HASSAN REHANI BITCHUKA, AMBAO WALITOKEA JUWATA JAZZ BAND HUKU COSMAS THOBIAS CHIDUMULE, MICHAEL ENOCH ‘KING MICHAEL’ NA MPIGA GITAA LA SOLO MAHIRI, JOSEPH BATHOLEMEO MULENGA.

WANAMUZIKI HAO WALICHUKULIWA KATIKA BENDI YA DAR INTERNATIONAL.

ALIKUWA GWIJI MUHIDIN GURUMO ALIYEBUNI MTINDO WA SIKINDE NGOMA YA UKAE, ALIOUELEZEA KUWA NI MTINDO WA NGOMA ZA UTAMADUNI WA KABILA LAKE LA KIZARAMO.

MTINDO HUO HADI SASA NDIO UNAOTAMBA NA WAKATI MWINGINE HUTUMIWA NA WAPENZI KUITA SIKINDE KAMA JINA LA BENDI.

BENDI HIYO ‘ILIACHIA’ VIBAO VINGI VILIVYOTAMBA NA HADI LEO VINASIKIKA VIKIPIGWA NA BAADI YA VITUO VYA REDIO HAPA NCHINI.

BAADHI YA VIBAO HIVYO NI PAMOJA NA SAUDA, MV MAPENZI, NEEMA, USITUMIE PESA KAMA FIMBO, MUME WANGU JERRY, CLARA, HIBA NA MATATIZO YA NYUMBANI.

NYIMBO ZIGINE ZILIKUWA ZA MAJIRANI HUZIMA REDIO, NIDHAMU YA KAZI, KASSIM AMEFILISIKA,TALAKA YA HASIRA, HADIJA, BARUA TOKA KWA MAMA, CELINA, EDITHA NA FIKIRI NISAMEHE.

BENDI HIYO ILIKUWA NA WATUNZI WENGI MNO KIASI KWAMBA WALIWEZA KUTUNGA NA KUIMBA NYIMBO ZINGINE ZAIDI ZIKIQWEMO ZA POLE MKUU MWENZANGU, DIANA, PESA, HATA KAMA , BUBU ATAKA SEMA, MNANIONESHA NJIA YA KWETU, TANGAZIA MATAIFA YOTE, MTOTO AKILILIA WEMBE, NALALA KWA TABU NA DUNIANI KUNA MAMBO. 

ZINGINE ZAIDI NI KIU YA JIBU, DUA LA KUKU, NAWASHUKURU WAZAZI, PATA POTEA, NELSON MANDELA, UZURI WA MTU, MDOMO HUPONZA KICHWA, TAXI DRIVER, TUCHEZE SIKINDE, CONJESTA NA NYIMBO NIYNGINE NYINGI.


DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA ILIKUWA NA WANAMUZIKI WENGI WENYE VIPAJI TOFAUTI AKINA MICHAEL ENOCK, JOSEPH BENARD, JOSEPH MULENGA, ABDALAH GAMA, COSMAS CHIDUMULE, MACHAKU SALUM, HABIB JEFF NA MUHIDIN MAALIM GURUMO.

WENGINE WALIKUWA HASSAN REHANI BITCHUKA, ABEL BARTHAZAR, HENRY MKANYIA, FRESH JUMBE, HUSSEIN JUMBE, BENNO VILLA ANTHONY, TINO MASINGE 'ARAWA', HASSAN KUNYATA, FRANCIS (NASSIR) LUBUA, MAALIM HASSAN ‘KINYASI’, NA ABDALLAH GAMA.

SAFU HIYO ILIKUWA PIA NA MAX BUSHOKE, MUHARAMI SAID, KASSIM MPONDA, JULIUS MZERU, SAID CHIPELEMBE, ALLY JAMWAKA, MACHAKU SALUMNA  ALLY YAHAYA.

WENGINE WALIOENEZA SAFU HIYO NI PAMOJA NA SHABAN LENDI, JOSEPH BERNARD, JUMA HASSAN TOWN NA WENGINE WENGI. SHIRIKA LA MAENDELEO DAR ES SALAAM BAADE LIKAJITOA KUIFADILI BENDI HIYO JAPO ILIWAACHIA VYOMBO VYOTE VYA MUZIKI ILI WAWEZE KUJITEGEMEA. WAKABADILISHA JINA LA BENDI NA KUWA MLIMANI PARK ORCHESTRA. BENDI HIYO BADO INALITIKISA JIJI LA DAR ES SALAAM WAKIWA NA MAKAO YAO MAKUU KWENYE UKUMBI WA DDC KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM.

B

Thursday, October 8, 2015

UNAMKUMBUKA FRANKLIN BOUKAKA?



UNAMKUMBUKA FRANKLIN BOUKAKA?


Ule usemi usemao kuwa “Maji hufuata mkondo” unajionesha wazi kwa mwanamuziki Frankin Boukaka aliyerithi  mikoba ya baba yake.

Alikuwa ni mtoto wa Aubin Boukaka aliyekuwa mwanamuziki wa kundi la ‘The Gaiety’ wakati mkewe Yvonne Ntsatouabaka alikuwa  mshereheshaji (MC) maarufu  kwenye misiba na pia alikuwa mwanamuziki muimbaji.

Mara baada ya kuzaliwa Oktoba 10, 1940, alipewa jina la François Boukaka baadae akajulikana kama Franklin.

Alikuwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanane wavulana watatu na wasichana watano.

Franklin Boukaka alijongezea umaarufu zaidi nchini mwake pale alipojiunga na wenzie waliotaka kuipindua serikali ya Kongo Brazzaville wakati huo ikiwa chini ya uongozi wa rais Marien Ngouabi.

Elimu yake alipata katika shule mbalimbali nchini kwake Kongo Brazzaville. Franklin  alianza kujishighulisha na mambo ya muziki 1955 katika kundi lililojiita Sexy Jazz.

Kundi hilo lilikuwa likiongozwa na Miguel Samba, baadae akaanzisha kundi la Negro Band.

Hatimae katika safari yake ya muziki akaungana na wakali wengine kama  Edo Clary Lutula, Jeannot Bombenga, Tabu Ley ,Mutshipile "Casino", André Kambite " Damoiseau ",  Papa Bouanga, Charles Kibongue katika lile kundi maarufu la African Jazz, sauti ya Franklin imo katika nyimbo kama  Mwana mawa , Catalina cha cha na Marie José zilizotungwa na Tabu Ley.

Mwaka 1959 kundi la African Jazz lilimeguka baada ya wanamuziki wengine walipohamia katika jiji la Brussels nchini Ubelgiji wakifuatana na wanasiasa wa Kongo kwenye mazungumzo ya awali ya uhuru wa Kongo.

Wanamuziki waliobaki akiwemo Jeannot Bombenga,  ila Tabu Ley wakajiunga na kuanzisha kundi jingine lililotingisha nchi lililoitwa Vox Africa.

Waimbaji wakati huo wakiwa ni akina Franklin Boukaka na Jeannot Bombenga.

Baada ya hapo Franklin akaaliacha kundi hilo na kurudi kwao Brazzaville ambako  mwaka 1962, akawa mmoja wa wanamuziki wa bendi ya Cercul Jazz. 

Bendi hiyo ilianza miaka ya 1950, ikiwa chini ya Chama cha vijana kilichokuwa kikipata ufadhili wa serikali ya Ufaransa. 

Chama hicho kiliitwa Cercule Culturel de Bacongo. 
Hatimae Boukaka alikuja kuwa kiongozi wa chama hicho na kikawa na umaarufu wa mkubwa. Wimbo wa bendi hiyo ‘Pont Sur le Congo’ (Daraja juu ya Mto Congo), ulikuwa una hamasisha kuunganika kwa Kongo Leopoldville (Kinshasa) na  Kongo Brazzaville baada ya nchi hizo kupata uhuru.

Kufikia hatua hiyo wimbo huo ukapata umaarufu kuliko nyimbo zote za bendi hiyo.

Baadae Franklin akiwa na gitaa lake kavu akaanzisha kikundi ambacho kilikuwa na wapiga marimba wawili akaweza kufanya ziara kadhaa hata nje ya nchi yake na kundi hilo.

Mwaka 1970 Boukaka  aliweza kurekodi nyimbo 12 zilizopangwa vyombo na Manu Dibango. Nyimbo za Nakoki na Le Bucheron ndipo zilipopatikana. 

Baada ya hapo Franklin alijiunga na wenziwe waliotaka kuipindua serikali ya Kongo Brazzaville, wakati huo ikiwa chini ya uongozi wa rais Marien Ngouabi.

Jaribio hilo lililofanyika tarehe 22 February 1972 lilishindwa na siku chache baadae kifo cha Boukaka kilitangazwa.

Mungu ailaze roho yake pahala pema pepeni, Amina.

Mwisho.