BELLA BELLA
ILIYOTIKISA VIGOGO WA MUZIKI DRC.
Miaka
ya nyuma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kulikuwa na ushindani mkubwa
katika muziki.
Walikuwapo wanamuziki wakubwa kama Franco Luambo Makaidi, Tabu
Ley, Mpongo Love, Joseph Kabasele ‘Grand Kalle’, na wengine wengi waliokuwa
wakitamba katika muziki wa dansi.
Katika
makala haya yanawaeelezea ndugu wawili Maxime Soki Vangu na Emile Dianzenza ambao
kwa pamoja walaimua kuunda bendi yao ya Orchestra Bella Bella ililojulikana pia
kwa majina ya Frères Soki & l’Orchestre Bella Bella iliyoanzishwa mwaka
1969.
Bendi
hiyo ilileta chamgamoto kubwa kwa vigogo hao katika muziki, wakajikuta wakikwaa
vikwazo vya kunyang’ayana wapenzi wa dansi toka kwa vijana hao.
Orchestra
Bella Bella iliwajumuisha wanamuziki wengine akina Nyboma Mandido, Pepe Kalle,
Shaba Kahamba na wengine wengi, waliofanya bendi hiyo kama jukwaa la kuanzia
umaarufu.
Waliongozwa
na ndugu hao Maxime Soki Vangu na Emile Dianzenza, wakiwa na wapiga magitaa Johnny
Rodgers na Jean Bosco, Kahamba Uzalu maarufu kama Shaba Kahamba.
Wakati
huo Emile Soki alikuwa na miaka 16 tu hivyo kuwa kipenzi cha vijana wenzie
wakati huo.
Bendi
hiyo ilirekodi vibao vilivyotikisa Afrika ya Mashariki na kati na kama vile “Baboti
Bapekisi”, “Sylvie”, “Alexandrine”, “Mwasi ya moto”, “Luta”, “Lina”,
Mandendeli”, “Mbuta”, “Bipale ya pembeni” na “Sofele”.
Kama
wasemavyo waswahili kuwa “ngoma ikipigwa sana hupasuka” haya yalijiri baada ya
ugomvi kutokea mwaka 1972, kati ya wanamuziki, uliopelekea bendi ipate
mabadiliko makubwa.
Ile
semi isemayo “hasira za mkizi…” zikajionesha kwa Emile, ailiyekuwa nguzo katika
bendi ya Bella Bella, kuliacha kundi hilo na kwenda kuanzisha kundi la Bella
Mambo.
Mtunzi
na mwimbaji Kabasele Yampanya ‘Pepe Kalle’ akajiunga na kundi hilo kwa
miaka michache ili aweze kupata fedha za kununulia vyombo vyake mwenyewe.
Kujiunga
kwa Pepe Kalle kukafanya Bella Bella iendelee kushikilia chati kwa kwa kufyatua
vibao vya “Mbuta”, “Kamale”, “Kimbundi”, “Lipua Lipua” na “Sola”.
Kama
wasemavyo waswahili kuwa “ Ngoma ya watoto haikeshi”, mwaka 1973 Emile
Dianzenza aliicha bendi aliyoianzisha ya Bella Mambo na kurudi tena Orchesta
Bella Bella kwa kaka yake Soki Vangu.
Alipotua
kundini, wakatengeneza nembo ya kurekodia yenye majina ya “Allez-y frères Soki”
Kwa
kupitia nembo hiyo waliachia vibao viwili vilivyoandikwa “Dizzy
Mandjeku”, ambavyo ndivyo vilivyowaingizia fedha nyingi kuliko kazi nyingine
yoyote walizowahi kuzifanya kabla ya hapo.
Baada
ya vibao hivyo, vilifuatia vingine vya “Mwana yoka toil”, “Menga”, “De
base”, “Tikela ngai mobali”, “Pambindoni”, “Nganga”, “Houleux-houleux” na
“Zamba”.
Ukwasi
ulipowakolea walifikia kuanza kukodi vikundi vingine wakitaka kufanya maonesho
kwa niaba yao.
Mwaka
1977, wakati wakiwa kwenye maonesho huko Ulaya, Emile akaanza kupatwa na
maradhi yaliyosababisha kuchanganyikiwa.
Maradhi
hayo hayakumpa nafasi tena ya kucheza muziki, akalazimika kuacha bendi.
Maxime
alijitahidi kufufua upya bendi yao baada ya kupwaya kwa kiasi
kikubwa, lakini wale wanamuziki alioanza nao wengi walikuwa wamekwisha
ondoka.
Licha
ya wanamuziki nguli akina Kanda Bongoman na Diblo Dibala kujiunga, hata nao
walishindwa kuirudisha bendi katika uhai wa enzi zake.
Maji
yalipozidi unga, Maxime Soki Vangu hatimaye aliiacha bendi yake ya Bella Bella
na kuhamia nchini Ujerumani.
Maxime
Soki Vangu aliyezaliwa Agosti 08, 1947, aliishi nchini humo hadi mauti
yalipomfioka Mei 18, 1990 akiwa mjini Cologne.
Nduguye
Emile Soki Dianzenza aliyezaliwa Kinshasa, Dec. 14, 1954, alifariki dunia Mei
04, 1990 akiwa na umri mdogo wa miaka 36.
Orcherstra
Bella Bella haipo tena kwenye taswira ya muziki, lakini nyimbo zake bado
zinarindima.
Mungu
azilaze roho zao pahala pema peponi, amina.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment