WAMKUMBUKA MKONGWE JIMMY MONIMAMBO?
Wapenzi wa muziki wa dansi hapa nchini wanatakumbuka
wimbo wa Sisili ulioimbwa kwa umahiri mkubwa na bendi ya Orchestra Shika Shika.
Ilikuwa ikiongozwa na mwanamuziki Jimmy ikiwa na makao makuu yake katika jiji la Nairobi,
nchini Kenya.
Shika Shika ilikuwa ikichuwana vikali na bendi zingine kubwa
zikiwemo za Super Mazembe, Les Mangelepa, Baba Gaston, Les Wanyika na nyingine
nyingi.
Akiwa na bendi hiyo ya Shika Shika walitoa album yao ya
kwanza mwaka 1982, iliyotikisa jiji la Nairobi na mbili zaidi alizitoa mwaka
uliofuatia.
Katika safu ya waimbaji alikuwepo Lovy Longomba ambae
alitunga wimbo wa Tika Nalela, ulioibeba kwa kaisi kikubwa Shika Shika na yingine zikiwemo za "Sisili," "Amba," na
"Inyo"
Wasifu wa Jimmy Monimambo anaeleza kuwa alizaliwa katika
jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Wazazi wake wake walikuwa raia wa Angola, waliokuwa miongoni mwa raia
walioikimbia nchi yao ya Angola na kwenda kuishi nchini Kongo wakitafuta kazi.
Monimambo pia alifahamika kwa majina ya Jimmy Monimambo
Mfumu Ntoto “Mfalme wa dunia”, aliyewahi kupiga muziki katika bendi ya Ochestra
Maquis du Zaire, ilikuwa na makao yake makuu katika ukumbiwa wa White House ,
maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Baadae akajiunga katika bendi ya Orchestra Shika Shika, pia alikwenda kujiunga katika
bendi za Special Liwanza, Boma Liwanza,
na Viva Makale iliyokuwa ikiongozwa na Kalombo Mwanza George.
Baadhi ya wanamuziki waliounda Shika Shika walikuwa
Jimmy Monimambo Vicky Longomba "Lovy"
na Moreno Batamba, aliyekuwa mwimbaji mwenye sauti nzito yenye mvuto. Wengine
walikuwa ni pamoja na Bwami Walumona na
Kasongo Kanema.
Wengi wa wanamuziki hao kabla ya kujiunga katika bendi
ya Orchestra Shika Shika walikuwa katika bendi ya Baba Gaston Nationale,
iliyokuwa ikiongozwa na Baba Gaston
Ilunga wa Ilunga.
Safu hiyo ilinogeshwa zaidi na wanamuziki akina Lawi
Somona, Sammy Mansita, mpiga gitaa Mwalimu Siama Matuzungidi, na aliyekuwa mcharanga drums Lava Machine.
Hao kwa pamoja walitoka katika bendi ya Virunga
iliyokuwa ikiongozwa na Samba Mapangala.
Safari ya mwanamuziki Monimambo ilimfikisha kuungana na Lovy
Longomba kurekodi nyimbo katika studio iliyokuwa ikimilikiwa na bendi za
Orchestra Mos Mos na Orchestra Pole Pole.
Safu ya wanamziki waliiuda bendi ya Shika Shika ilikuwa
ni waimbaji Jimmy Monimambo, Dago Mayombe na Lovy Longomba wakati kwa upande wa
wapiga magitaa walikuwepo Siama Matuzungidi, aliyekuwa akiliungurumisha gitaa
zito la besi, aliwahi kupigia katika beni ya Cavacha katika jiji la Kinshasa
mnamo miaka ya 1970.
Chery Matumona,Tabu Frantal, Manitcho na kwenye besi
alikuwa Silu Waba Nsilu.
Mpiga gitaa Chery Matumona ambae baadae aliiacha bendi hiyo mwaka 1981,
akaenda nchini Uganda na baadae Zambia. Hivi sasa anaishi nchini Canada.
Bendi yake Cavacha iliundwa na waimbaji Dona Mobeti na Mopero wa Maloba. Mopero baadae
aliicha bendi hiyo na kwenda kuunda kundi lake akalipa jina la Orchestra
Cavacha de Mopero, ambayo nayo iliingia katika migogoro.
Hatimae nguli wa muziki huo huko DRC Franco Luambo
Makiadi, aliingilia kati na kumshawishi Mopero kubuni jina jipya.
Binti ailiyekuwa akiitwa Vicky Shama Shama alikuwa na
mahusiano ya kimapenzi na Mopero wa Maloba, ambae aliamua jia la binti huyo
liwe jina la bendi hiyo ikaitwa Orchestra Shama Shama.
Shama Shama iliundwa ikiwa na wanachama toka bendi ya Cavacha,
ambayo hata Mopero Wa Maloba alikuwa mwimbaji katika bendi hiyo.
Bendi hiyo ya Shama Shama, alikuja kugawanyika muda
mfupi kabla ya safari yao ya kwenda nchini U Uganda.
Hapo ndipo busara za Mopero zilionekana baada ya
kusajili wanamuziki wengine wapya aliokwenda na Uganda.
Ule usemi kuwa “La kuvunda halina ubani” ulijionesha
wazi pale bendi hiyo ikiwa nchini Uganda ikasambaratika tena.
Mwanamuziki KoKo Zigo alimshawishi Jimmy Monimambo
kuondoka nchini Uganda, wakaunda bendi ya Orchestra Kombe Kombe mwaka 1978
wakiwa na na mwimbaji Koko Zigo. Walifika nchini Kenya wakiwa na bendi hiyo
mpya ya Orchestra Kombe Kombe, lakini waliingia mkataba wa kupiga muziki katika
ukumbi uliopo Garden Square katika jiji la Nairobi wakiwa wamebadilisha jina la
bendi kuwa Orchestra Viva Makale.
Bendi hiyo ilikuwa na wanamuziki mahiri waliokuwa
wakitoa burudani maridadi kwa wapenzi wake. Baadhi ya wanamuziki hao ni pamoja
na George Kalombo Mwanza aliyekuwa kipuliza saxophone na kuimba, Buami Walumona na Chery Matumona walikuwa akicharaza gitaa
la solo, Siama Matuzungidi, alikuwa akisimama kwa upande wa gitaa la kati la rhythm
pamija na Tabu Frantal akiliungurumisha gitaa.
Wengine walikuwa akina Thomy Kabea Lomboto aliyekuwa
akiliungurumisha gitaa zito la besi, Coco Zigo, Moreno Batamba, Jimmy
Monimambo, Tambwe Mandola wakiwa waimbaji.
Tarumbeta ilikuwa ilipulizwa na Tshamusoke na drums
zilicharangwa na Lava Machine.
Jimmy Monimambo alikisha tangulia mbela za haki mungu
ailaze roho yake pahala pema peponi, amina.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment