MORENO BATAMBA ALIVYOTAMBA
WIMBO WA ‘PILI MUSWAHILI’ ULIGONGA VICHWA VYA WAPENZI WA
MUZIKI WA DANSI AFRIKA MASHARIKI NA KATI MIAKA YA 1980 HADI 1990.
SAUTI NZITO YENYE MVUTO WA AINA YAKE KATIKA NYIMBO HIZO
ILIKUWA YA INAYOTAMBA KATIKA WIMBO HUO NI YA MORENO BATAMBA.
MAKALA YA LEO INAMZUNGUMZIA MWANAMUZIKI HUYU
ALIYEJIZOLEA SIFA KEMKEM KWA UTUNZI NA UIMBAJI WAKE USIOIGIKA.
WASIFU WA MORENO
UNAELEZA KUWA ALIZALIWA MWAKA 1955, KATIKA MJI WA KISANGANI, HUKO JAMHURI YA
KIDEMOKRASIA YA KONGO (DRC).
KAMA HISTORIA YA WANAMUZIKI WENGI KUACHA MASOMO NA
KUKIMBILA MUZIKI, HALI KADHALIKA MWANAMUZIKI HUYO NAE ALIINGIA KATIKA MKUMBO
HUO.
WAKANEMA NI MIONGONI MWA HAO YEYE ALIAMUA KUACHA SHULE
MWAKA 1971, AKAENDA KUJIUNGA KATIKA BENDI YA ORCHESTRA MAQUIS SASA BATA.
BAADA YA KUJIAMINI KWAMBA AMEKOMAA KIMUZIKI, ALIONDOKA
NCHINI MWAO NA AKAINGIA NCHINI UGANDA MWAKA 1974, AKAJIUNGA KATIKA BENDI YA
ORCHESTRA BANA NGENGE, ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA MWIMBAJI JOJO IKOMO.
AKIWA NCHINI HUMO ALIWAHI KUFANYA MAZUNGUMZO NA MMOJA WA
WANAMUZIKI WA BENDI YA ORCHESTRA VEVE, SAMBA MAPANGALA.
BENDI HIYO YA VEVE ALIKUWA NA ANAMUZIKI TOKA DRC
WALIOCHUKULIWA HUKO KWA AJILI YA KUFANYA MAONESHO KATIKA JIJI LA KAMPALA.
ORCHESTRA VEVE ILIKUWA TAYARI NI MAARUFU NCHINI HUMO,
WAKAIBEBA BENDI YA BANA NGENGE.
WAKIWA KATIKA JIJI LA KAMPALA BENDI YA BANA NGENGE
WALITOKA NA ALBAMU NYINGI.
BADHI YAKE NI KAMA MAYATU, ILIKUJA REKODIWA TENA KWA
JINA LA ‘MAYA TU’,
AZONGA, KOYOKA KOYOKA, OKEI KOLAKATE NIKA, NA BANGI
MAKAMBO NA MABAKU.
BANA NGENGE AU KWA JINA JINGINE ILIKUWA IKITWA BANA
MOJA, KATIKA MIAKA YA 1970 ILIONDOKA
KAMPALA WAKAENDA KATIKA JIJI LA NAIROBI NCHINI KENYA.
BAADHI YA WANAMUZIKI WALOIUNDA BENDI HIYO ILIKUWA NI
PAMOJA NA WATUNZI NA WAIMBAJI JOJO IKOMO, N'DALA MOBANGI, BEYA MADUMA, ROXY
TSHIMPAKA, FATAKI LOKASSA LOSI LOSI ‘MASUMBUKO YA DUNIYA’, MAKWANZI DUKI, KUKA
MWANA BITALA NA HASSAN OMARI.
WENGINE WALIKUWA AKIA NSILU BANSILU MANITCHO
ALIYEKUWA AKILIUNGURUMISHA GITAA LA BESI, MORO MAURICE NA LAWISON SOMANA WALIKUWA AKUPULIZA SAXOPHONE.
WALIKUWAPO OCHUDIS, MANDALI OTIS MUSA, ZENGELE SAIDA
ALIYEKUWA MPIGA GITAA. KWA UPANDE SAXOPHONE ALIKUWEPO N'TALU NKATU NA TUMBA
ZILIKUWA ZIKIDUNDWA NA MUKAPUTU KALEMBI.
MWAKA 1972 BENDI HIYO ILKIINGIA KATIKA MAPARAGANYIKO
ULIOSABABISHA WANAMUZIKI WENGI WAKAONDOKA.
IKUMBUKWE KWAMBA MTUNZI NA MWANAMUZIKI JOJO IKOMO,
ALIKUWA MMOJA WA WAANZILISHI WA BENDI YA ORCHESTRA BANA MOJA, AMBAPO AKIWA NA
BENDI HIYO MWAKA 1974.
MWANAMUZIKI FATAKI LOKASSA ALISAFIRI AKIWA NA BENDI YA
BANA NGENGE WAKAINGIA TANZANIA AMBAKO KWA BAHATI MBAYA MWAKA 1975, WANAMUZIKI
WA BENDI HIYO WAKAGAWANYIKA.
MGAWANYIKO HUO
ULIPELEKEA BENDI HIYO KUFA NA KUWAFANYA WANAMUZIKI MORENO BATAMBA NA
JOJO IKOMO WAKAENDA KUJIUNGA KATIKA BENDI YA LES NOIRS MWAKA 1976.
MWAKA 1978 FATAKI ALIREJEA TENA KATIKA JIJI LA NAIROBI
AMBAKO AKAJIUNGA KATIKA BENDI YA LES KINOIS, ILIYOJULIKANA BAADAE KWA JINA LA ORCHESTRA VIRUNGA.
WAKIWA KATIKA BENDI HIYO WALITOKA NA KIBAO CHA
"TSHIKU", AMBACHO HADI SASA HUSIKIKA KATIKA
BAADHI YA REDIO HAPA NCHINI.
WANAMUZIKI WENGINE WA BENDI HIYO WALIKUWA NI PAMOJA NA
MUKAPUTU KALEMBY KAJOS, WILLIAM TAMBWE LOKASSA, ALIYEKUWA AKILIUNGURUMISHA
GITAA ZITO LA BESI, MANKWAZI DUKI DIEUDOS NA
CHUZA KABASELLEH.
MWANAMUZIKI DIEUDOS MAKWANZI ALIONDOKA NCHI KENYA
AKAREJEA KWAO KONGO MAPEMA MIAKA YA 1980.
BENDI YA LES NOIRS ALIACHIA VIBAO VYA "MUNGU IKO
HELENA", “CHUZA NA LES NOIRS NA "SIKIYA SAUCE" KILICHOTUNGWA NA
DIEUDOS MAKWANZI.
WALIWAHI KUPIGA WIMBO WAKAIMBA KWA WAKIWASIFIA VIONGOZI
JOMMO KENYETTA WA KENYA NA MOBUTU SESESEKO WA KONGO (ZAIRE) WAKATI HUO.
BAADA YA KUACHIA WIMBO HUO, BENDI HIYO IKAONEKANA NI
BENDI YA KWANZA TOKA KONGO, KUNG’AA NCHINI KENYA KATIKATI MWA MIAKA YA 1970.
MORENO BATAMBA ALIWAHI KUISHI KATIKA JIJI LA DAR ES
SALAAM KATI YA MIAKA YA 1978 HADI 1980, AKITUNGA NA KUIMBA KATIKA BENDI YA
ORCHESTRA SAFARI SOUND (OSS), KABLA YA KURUDI TENA NAIROBI.
BENDI YA OSS
ILIKUWA IKIMILIKIWA NA MFANYABIASHARA MAARUFU WAKATI HUO HUGO KISIMA.
MWAKA WA 1980 MORENO ALIANZISHA BENDI YA ORCHESTRA MOJA
ONE, AKIWA SAFU YA WANAMUZIKI AKINA COCO
ZIGO MIKE, MPIGA GITAA SIAMA MATUZUNGIDI, MCHARANGA DRUM LAVA MACHINE NA
WENGINE WENGI WALIOTOKA KATIKA BENDI YA SHIKA SHIKA.
ORCHESTRA MOJA ONE ILFYATUA NYIMBO KALI
ZILIZOWASHIKA WAPENZI NA MASHABIKI WA
MUZIKI WA DANSI AFRIKA YA MASHARIKI.
NYIMBO HIZO ZILIKUWA ZA "PILI
MSWAHILI", "DUNIA NI DUARA”, " "MAPENZI YA SHINDA",
"MWANAMKE HATOSHEKI", UREMBO SI HOJA”
NA "ANGELA " ZILIZOREKODIWA MWAKA 1981 NA "UREMBO SI
HOJA.
KIBAO CHA "PILI MUSWAHILI" KILIKUWA MAHSUSI
KWA AJILI YA RAFIKI YAKE WA KIKE ALIYEJULIKANA KWA MAJINA YA PILI MIKENDO KASSIM.
PILI ALIKUWA MTANZANIA
WALIYEKUTANA NAYE ALIPOKUWA KATIKA BENDI YA ORCHESTRA LES NOIRS KATIKA MJI WA
MOMBASA MWAKA 1976.
MORENO KWA KIPINDI KIFUPI ALIJIUNGA KATIKA BENDI YA
ORCHESTRA VIRUNGA YA SAMBA MAPANGALA MWAKA 1983.
BENDI YA ORCHESTRA VIRUNGA, YAELEZWA KUWA ILIKUWA NI
BENDI ‘NYOTA’ ILIYOWEZA KUPIGA MUZIKI ‘LIVE’ KATIKA BAADHI YA KUMBI ZA JIJI
HILO.
ILIWASHIRIKISHA WANAMUZIKI WENGINE WAKIWEMO AKINA COCO ZIGO, FATAKI LOKASSA, DAGO MAYOMBE NA
BAADAE MORENO BATAMBA, OTTIS NA SAMBA
MAPANGALA.
WENGINE WALIKUWA NI MANITCHO NSILU, SAMMY MANSITA,
DJANGO NKULU MWILAMBWE, BEJOS, SIAMA MATUZUNGIDI KWA UPANDE WA UIMBAJI.
MPENZI MSOMAJI WA MAKALA HAYA UNAWEZA KUONA MAJINA YA
WANAMUZIKI HAO KUJIRUDIA KWA TAKRIBANI KILA BENDI.
HII NI KUTOKANA NA
KUHANGAIKA KWA WANAMUZIKI HAO AMBAPO KILA BENDI MPYA ILIPOANZISHWA WALIKUWA
WAKICHUKULIWA.
MORENO BATAMBA ALIKUWA AKIPENDELEA ZAIDI KUTUNGA NA
KUIMBA NYIMBO ZAKE KWA LUGHA YA KISWAHILI. NYIMBO ZAKE ZILIKUWA ZIKIGUSA HISIA
ZA JAMII ZOTE.
AIDHA ALIIMBA WIMBO WENYE MAHADHI YA TAARABU BAADA YA
KUIMBA WIMBO WA “VIDONGE SITAKI” AKIWA KATIKA KIKUNDI CH GOLDEN STAR MWAKA
1993.
KWA MAPENZI YA MUNGU NGULI HUYO MORENO BATAMBA ALIFARIKI MWAKA HUOHUO 1993,
AKIWA NA UMRI MDOGO WA MIAKA 38.
MUNGU AIWEKE ROHO YAKE PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment