BOZI BOZIANA ‘MZEE BENZI’ ASIYECHUJA KIMUZIKI.
Bozi Boziana
‘mzee Benzi’ kama anavyojulikana na wengi ni mwanamuziki ni kiongozi wa
kundi Anti Choc toka Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo.
Licha ya umri wake kuwa mkubwa, awapo jukwaani huwezi
kuamini macho yako unapomuona akiimba na kucheza sambamba na wanenguaji wa
bendi hiyo.
Muziki wa nguli huyo huwa hauchuji kama ilivyo kwa wanamuziki
wengine.
Bozi amejizolea sifa lukuki kwa kuweza kuongoza kundi
hilo ambalo ni miongoni mwa bendi zinazokubalika huko Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo.
Sifa nyingine kubwa ya mwanamuziki huyo ni kwamba pamoja
na utunzi na uimbaji Bozi pia ni mkung’utaji mzuri wa gita, aliyepitia katika
bendi nyingi kupiga muziki katika mtindo wa soukous.
Imani iliyojengeka kwa baadhi ya wadau wa muziki ni
kwamba mwanamuziki bora ni yule anayekubalika kupiga muziki katika bendi yeyote
atakayokwenda.
Kama ni hivyo basi miongoni mwa hao ni Bozi Boziana
ambaye aliwahi kupitia bendi nyingi zikiwamo za Bamboula de Papa Noel, na Zaiko Langa
Langa. Zingine zilikuwa za Isifi Lokole,
Yoka Lokole,
Langa Langa Stars na Choc Stars.
Baada ya
kupata uzoefu wa muda mrefu katika muziki, alihamasika kuunda bendi yake,
akaweza kuanzisha bendi ya Orchestra Anti-Choc.
Wasifu wa mwanamuziki huyo unaeleza kuwa jina lake
kamili anaitwa Mbenzu Ngamboni Boskill.
Alizaliwa
mwaka 1952 huko Jamhuri ya Kidemkokrasia ya Kongo.
Alianza
muziki wa Afro-Pop
katika bendi ya Air Marine. Mafanikio yake katika muziki alianza kuyaona ilipotimu mwaka 1974,
alipojiunga na bendi ya Zaiko Langa Langa.
Hapo
Zaiko alishirikiana na waimbaji wengine mahiri
wakati huo, wakiongozwa na mkongwe Papa Wemba
na mwezake Evoloko Jocker.
Kabla
mwaka haujatimia, waimbaji Papa Wemba na
Evoloko waliondoka katika bendi hiyo ya Zaiko Langa Langa.
Kuondoka
kwao kulikuwa ni changamoto kwa Bozi Boziana ambaye naye aliamua kuwafuata na
wakanzisha bendi mpya ikaitwa Isifi Lokole.
Kukosekana
kwa uongozi madhubuti kulisababisha kutokukubaliana katika masuala mbalimbali
ya msingi, miongoni yakiwemo ya kimaslahi.
Mtafaruku
huo uliwafanya wanamuziki akina Papa Wemba, Boziana, Mavuela Somo na wengine
kuondoka bendi ya Isifi Lokole’ wakaunda bendi nyingine mpya iliyopewa jina la
Yoka Lokole.
Bozi baada ya kuona
kaachwa mithiri ya mkiwa, mwaka 1977 naye akaondoka Yoka Lokole licha ya bendi
hiyo kuwa maarufu kwa kipindi kifupi.
Kwa miezi michache Boziana alishirikiana na mwanamuziki Efonge Gina, ambaye
naye alikuwa katika bendi ya Zaiko Langa Langa.
Walirekodi nyimbo
kadhaa kama vile Selemani iliyotungwa
na Bozi na Libanko Ya Ngai utunzi wake Gina.
Produza
maarufu Kiamuangana Mateta
‘Verckys’ ambaye ni mkongwe wa muziki nchini huo mwaka 1981, aliibadilisha bendi ya Soukous Super group
na kuita Langa Langa
Stars.
Bendi hiyo alikuwa
imejaza wanamuziki waliokuwa na vipaji tofauti akina Evoloko Jocker, Dindo Yogo na
wnengine wengi. Bozi Biziana alialikwa
kujiunga vijana hao naye akaubali na kuicha
Zaiko Langa kwa mara ya pili.
Boziana alidumu kwa
miaka michache hapo Langa Langa Stars kabla ya kuondoka kwenda kujiunga na
bendi kubwa nchini humo Choc Stars
aliyokuwa chini Ben Nyamabo ambako
alipiga hadi mwezi Novemba 1985.
Akiwa na bendi hiyo ya
Choc Stars alirekodi baadhi ya nyimbo ambazo zilikuja kuwa maarufu za Sandu Kotti, Alena, Mbuta-Mutu
na Retrouvailles a Paris.
Bendi ya Choc Stars
ilikuwa na wanamuziki wengi wenye vipaji lukuki
akina Fifi Mofude, Djo Nolo, Koffi Alibaba, Wally Ngonda, Rigo Star,
mpiga gita la besi Ngouma Lokito.
Boziana aliwahi
kushinda zawadi ya Kora All-African kwa album yake kuwa bora toka nchi
za Afrika ya Kati.
Kwa wapenzi wa muziki hapa nchini watamkumbuka Bozi
jinsi alivyoteka wapenzi katika maonesho kadhaa aliyoyafanya hapa nchini kwa
ushirikiano walioonshea kati ya Bozi Boziana, Deesse Mukangi na Joly Detta
walivyokuwa wakilishambulia jukwaa kwka staili ya ‘Nzawisa’ katika nyimbo za
Tembe na Tembe, Palpitation na zingine nyingi zilifanya watu kuviacha viti vyao
kwenda kuwatuza.
Bozi Boziana ana sauti nzuri, yakupendeza akimba huku
akipokezana na timu yake ya wanadada wawili, Joly pamoja na Deesse.
Sifa nyingine za mwanamuziki huyu mzee Benzi ni kwamba
muziki wake hauna mwingiliano kati ya sauti ,gitaa na synthesizer katika nyimbo
zake zote. Mfano katika wimbo wa ‘Ngoyartong020’ tune tatu za mwanzo
Boziboziana amemshirkisha Jolly Detta na Deesse, na sehemu ya pili ya wimbo huo aliongeza
nguvu kwa kumuongeza waimbaji na wanenguaji
Scola Miel maarufu kwa jina ‘Nzawissa’ na Betty.
Bozi alifyatua vibao vingi
vilivyompa sifa nyingi ukiwemo wa La reine de Sabah, Lelo Makambo Lobi Makambo
Evelyne na Fleur de Lys ambazo alimshirikisha mwimbaji wa kike Joly Delta.
Boziana aliachia wimbo mwingine akimshirikisha Deesse na
Ba Bokilo.
Bozi Boziana na bendi yake bado anaendeleza muziki akiwa
na bendi yake na watanzania watakumbuka kwa mara ya mwisho alikuja hapa nchini
kwa mwaliko wa African Stars Entertainment Tanzania (ASET) iliyo chini ya
uongozi wa Mkurugenzi Asha Baraka.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment