BURIANI MUTOMBO LUFUNGULA NYOTA YA MAQUIS.
JINA LA MWANAMUZIKI MUTOMBO LUFUNGULA ‘AUDAX’ SIYO NGENI KWA WALE WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI ULIOKUWA UKIPOROMOSHWA NA BENDI ZA MAQUIS DU ZAIRE NA MAQUIS ORIGINAL.
MAREHEMU AUDAX ALIKUWA MMOJA KATI YA
VIONGOZI NA WANAHISA WA BENDI YA MAQUIS
DU ZAIRE NA KAMPUINI YAO ORCHETSRA
MAQUIS COMPAY (OMACO).
BAADA YA KUUGUA KWA KIPINDI KIREFU, HATIMAE AUDAX ALIFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA ALHAMISI YA APRILI 23, 2015 AKIWA NYUMBANI KWAKE KIMARA MICHUNGWANI JIJINI DAR ES SALAAM.
KABLA YA KUFIKWA NA MAUTI HAYO, MUTOMBO ALIKUWA AKISUMBULIWA NA UGONJWA WA KIHARUSI TANGU MWAKA 2005 YALIYOPELEKEA KUPOOZA UPANDE MMOJA WA MWILI.
ALIKUWA AKIUGUZWA NA WANAWE KATIKA KIPINDI CHOTE HICHO IKIZINGATIWA KWAMBA MKEWE, ALIKWISHA TANGULIA MBELE ZAHAKJI HATA KABLA YA YEYE KUPATWA NA MARADHI HAYO.
MARADHI HAYO YALIMFANYA ASHINDWE KUENDELEA NA SHUGHULI ZA MUZIKI.
AUDAX ALIWAHI KUFANYA MAHOJIANO NA MTANGAZAJI WA TBC ‘MANJU WA MUZIKI’ MASOUD MASOUD, AKAELEZEA HALI YAKE ILIVYO MBAYA KIMAISHA.
HAKUWA NA MSAADA WOWOTE TOKA KWA WATU ALIOKUWA AKIWATAJIA. ALISEMA NI WACHACHE SANA WALIOJARIBU KWENDA KUMJULIA HALI NYUMBANI KWAKE.
BAADA YA KIFO, MAADALIZI YA MAZIKO YAKAFANYWA NA ILIPOTIMU SIKU YA JUMAPILI YA APRILI 26, 2015, IBADA YA KUUUGA MWILI WAKE ZILIFANYWA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA KABLA YA MWILI WAKE KUWEKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE KATIKA MAKABURI YA KINONDONI, JIJINI DAR ES SALAAM.
UMATI MKUBWA ULIKUSANYIKA KATIKA MAZISHI HAYO MIONGONI MWAO WAKIWA WANAMUZIKI ALIOWAHI KUFANYA NAYE KAZI.
‘AUDAX’ ATAKUMBUKWA KWA WAKAZI WENGI WA MAGOMENI MAPIPA, MTAA WA MIKUMI AMBAKO ALIISHI KWA KIPINDI KIREFU KABLA YA KUJENGA MAKAZI YAKE HUKO KIMARA MICHUNGWANI.
AMEIGA DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA INAYOKARIBIA 70, ALIZALIWA MWAKA 1945 HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.
LUFUNGULA AUDAX ALIKUWA MMOJA WA WANAMUZIKI WA KUNDI LA BENDI YA MAQUIS DU ZAIRE. BENDI HIYO ILITOKEA KATIKA MJI WA KAMINA, JIMBO LA SHABA, HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.
AWALI KUNDI HILO LILIANZA KWA KUITWA SUPER TEO, KISHA KUBADILI JINA NA KUITWA ROCKEN SUCCESS NA BAADAYE SUPER GABBY.
BENDI HIYO ILIINGIA NCHINI TANZANIA MWAKA 1972, IKIWA NA JINA LA MAQUIS DU ZAIRE. KUNDI HILI LA AWALI LIKUWA NA WANAMUZIKI TISA.
MUTOMBO ALIKUWA MFANO WA KUINGWA NA WANAMUZIKI WENGINE WA BENDI HIYO KWA JINSI ALIVYOKLUWA AKIJITOA KWA UWEZO WAKE WOTE KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE IPASAVYO.
ALIKUWA MTUNZI NA MWIMBAJI ALIYEMUDU VYEMA KULISHAMBULIA JUKWAA LA MAQUIS SAMBAMBA NA WAIMBAJI WENZAKE AKINA MBUYA MAKONGO ‘ADIOS’, MUKUMBULE LOLEMBO ‘PARASHI’, TSHIMANGA KALALA ASSOSA NA ABOUBAKAR KASONGO MPINDA.
HATA KULE MAQUIS ORIGINAL, MUTOMBO ALISHIRIKIANA VYEMA NA WAIMBAJI WENZAKE AKINA MUKUMBULE LOLEMBO PARASHI’, TSIMANGA KALALA ASSOSA, ISSA NUNDU, FREDITO ‘BUTAMU NA BOBO ‘SUKARI’
MPENDWA MSOMAJI WA MAKALA HAYA ITAKUWA NI VIZURI UIJUE HISTORIA FUPI YA BENDI YA MAQUIS DU ZAIRE.
BENDI HIYO INAANZIA MWAKA 1960 KWA WALIOKUWA VIJANA WA WAKATI HUO KATIKA MJI WA KAMINA HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO (ZAIRE), WALIOUNGANA NA KUUNDA BENDI YAO WAKAIITA SUPER THEO.
BENDI HIYO ILITOA BURUDANI TOSHA KWA
WAPENZI WA MUZIKI WA KAMINA NA VITONGOJI VINAVYOUZUNGUKA MJI HUO,
BAADAYE WAKAIBADILISHA JINA KUWA SUPER GABBY.
KUNDI LA HILO LILIINGIA NCHINI TANZANIA MWAKA 1972 LIKIWA NA JINA LA ORCHESTRA MAQUIS DU ZAIRE.
MAQUIS
DU ZAIRE WALIPOINGIA NCHINI, KUWA WALIPIGA KATIKA KUMBI NYINGI HUSUSANI MIKUMI
NA WHITE HOUSE PALE UBUNGO, JIJINI DAR ES SALAAM.
BENDI HIYO BAADAE
ILIFUNGUA KAMPUNI ILIYOITWA ORCHESTRE MAQUIS COMPANY (OMACO ) IKIONGOZWA NA
WANAHISA AKINA CHINYAMA CHIAZA ‘CHICHI’, CHIBANGU KATAYI ‘MZEE PAUL’, CHIMBWIZA
MBANGU NGUZA ‘NGUZA VICKING’, MBUYA MAKONGA ‘ADIOS’ PAMOJA NA YEYE MUTOMBO
LUFUNGULA ‘AUDAX’
KIFO CHA LUFUNGULA KIMEGEUZA
HISTORIA YA WANAMUZIKI WAANZILISHI WA BENDI HIYO. KATIKA ORODHA YA HAPO JUU, NI
MWANAMUZIKI CHIMBWIZA MBANGU NGUZA ‘VICKING’ NDIYE ALIYE HAI, LICHA YA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MAISHA
JELA.
BENDI
HIYO ILIWEZA KUKONGA NYOYO ZA WAPENZI NA MASHABIKI WA MUZIKI WA DANSI WAKITUMIA
MITINDO MINGI ILIYOKUWA IKIBADILIKA KILA MARA KUFUATIA UBUNIFU WA WANAMUZIKI
HAO.
WALIPOTUA WKAANZA KWA MBEWEMBWE NYINGI WAKITUMIA MTINDO WA ‘CHAKULA CHAKULA KAPOMBE’ UKAJA MTINDO WA ZEMBWELA UKAFUTIWA NA ‘KAMANYOLA BILA JASHO’.
MZEE MWEMA MUDJANGA ‘MZEE CHEKECHA’ ALIKUWA KIVUTIO KIKUBWA UKUMBINI LICHA YA KAZI YAKE YA KUPULIZA TARUMBETA, ALIWEZA KUWAINUA VITINI WAPENZI KWENDA KUCHEZA, AKITUMIA VIBWAGIZO VYA “CHEKECHAA CHEKEEEE…. CHEKECHAAA” “TUSANGALAA”, “AIMA IMAA”, ‘BISHE BISHEE”, “SAA… SANIFUU”, “CHEZA KAMANYOLAA” “CHEZA KWA MARINGO”, “ CHEZA UKIJIDAI” NA MENGINE MENGI.
MTINDO WA OGELEA PIGA MBIZI ULITIA FORA KWA
MASHABIKI AMBAO WALICHEZA MITHIRI WATU WAMO BAHARINI, BWAWANI, MTONI AMA ZIWANI
WAKIONESHA JINSI YA KUOGELEA’.
ALICHIA KIBAO KINGINE KILICHOSHIKA CHATI CHA ‘KISEMBENGO’ WAKATI HUO BENDI HIYO IKIWA NA JINA LA MAQUIS ORIGINAL.
MSOMAJI WA MAKALA HAYA NAKUOMBA NIKUKUMBUSHE BAADHI YA
WANAMUZIKI WA ENZI ZA BENDI YA MAQUIS DU ZAIRE.
ALIKUWEPO MWAMAMA TABIA
MWANJELWA, ALIYEKUWA MWIMBAJI PEKEE WA KIKE WAKATI HUO. ALIIMBA PEKE YAKE KWA
HISIA KALI WIMBO ULIOHUSU ‘KIFO’.
ALIIMBA HIVI. “MWISHO WA MAISHA NI KIFOOO... KWELI MAISHA NI
SAFARI NDEFU.... AMBAYO HAINA MWISHOOOO.... MWISHO WAKE NI KIFOOO.....DUNIA
HAINA MWISHOOO….. MWISHO WAKE NI KIFOOO....”
ULIKUWA
NI WIMBO WENYE MANENO YA KUTAHADHARIFA JUU KIFO, JAPO WATU HAWAKUTILIA
MAANANI, ILA WALIKUSAKATA RUMBA PASIPO HOFU.
MAQUIS
DU ZAIRE WAKATI HUO ILIKUWA IKIONGOZWA NA
CHINYAMA CHIAZA ‘CHICHI’ AKISAIDIANA NA CHIMBWIZA NGUZA MBANGU
‘VICKING’.
KULIKUWA
NA MPULIZAJI TARUMBETA, MWEMA MUJANGA ‘MZEE CHEKECHA’. CHEKECHA NDIE ALIYEKUWA
‘MFOKAJI’ MAARUFU WA BENDI HIYO. NA
NKULU WABANGOI, ALIYEKUWA KIONGOZI WA WANENGUAJI.
WENGINE WALIKUWA KANKU
NKASHAMA KELLY, NGOI MUBENGA,ILUNGA NGOI, KAUMBA KALEMBA, NGENDA KALONGA, MAFUMU BILALI NA
KHATIBU ITEI ITEI. PALIKUWEPO NA WAPIGA GITA LA SOLO AKINA ILUNGA LUBABA NA
DEKULA VUMBI KAHANGA ‘VUMBI’. ILUNGA KALONDJI, MUJOS WA BAYEKE PIA NI MIONGONI
WA KIKOSI HICHO.
WALIPOKWENDA
KATIKA UKUMBI WA LANG’ATA, KINONDONI, MAQUIS ORIGINAL ILIONGEZA WANAMUZIKI
WATATU TOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO. WALIINGIA MPIGA GITA LA SOLO KIVUGUTU
MOTTO NA TCHATCHO, WATUNZI NA WAIMBAJI WALIKUWA BOBO
SUKARI’ NA FREDITTO ‘BUTAMU’.
WAKIWA
KATIKA UKUMBI HUO, WAKAANZISHA MITINDO YA ‘SENDEMA’ NA ‘WASHA WASHA’ .
MWISHO.
MUNGU
IWEKE ROHO YA MUTOMBO LUFUNGULA ‘AUDAX’ PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment