JOHN BOKELO MKONGWE WA MUZIKI KONGO.
JINA LA JEAN 'JOHNNY' BOKELO ISENGE LILIVUMA MNAMO MIAKA
YA 1950 NA 1960.
ALIZALIWA MIAKA YA 1930 MWISHONI KATIKA KITONGOJI CHA
KONGO BELGE, NJE KIDOGO NA MJI WA KINSAHASA HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA
KONGO.
JOHN ALIKUWA NI MDOGO WA MWANAMUZIKI MAARUFU NCHINI
HUMO, PAUL 'DEWAYON' ISENGO.
DEWAYON ALIKUWA NA KUNDI LAKE LA WANAMUZIKI LILILOKUWA
LIKIITWA WATAM.
BOKELO AKIWA NA UMRI WA MIAKA 12, ALIANZA KUPIGA GITA
MNAMO MWAKA 1950.
BAADAE AKAPIGA MUZIKI KATIKA BENDI ZA KAKA YAKE ZA
CONGA JAZZ NA ORCHESTRA COBANTU. AKIWA KATIKA BENDI
HIZO, BOKELO ALIWEZA KUCHOTA UJUZI MKUBWA KIASI KWAMBA MWAKA 1958, ALIAMUA
KUUNDA KUNDI LAKE LIKAITWA ORCHESTRA
CONGA SUCCESS.
KAKA DEWAYON NAE PIA ALIJIUNGA KATIKA KUNDI HILO MWAKA
1960.
NYIMBO ZA BENDI HIYO ZILILENGA MAHSUSI KWENYE MAPENZI NA
VIFO.
BOKELO NA KAKA YAKE DEWAYON WALIGAWANYIKA TENA MWAKA
1962, AMBAPO BOKELO ALIENDELEA KUIONGZA BENDI YAKE YA CONGA SUCCESS.
HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO MTINDO WA MUZIKI
ULIOKUWA UKIPIGWA NA NGULI HAO BOKELO, DEWAYON NA FRANCO MAKIADI ZIMEBAKIA KAMA
ALAMA YA MUZIKI NCHINI HUMU.
NYIMBO NYINGI ZA JOHN BOKELO ZILIKUWA NA MIRINDIMO
INAYORANDANA NA ILE YA FRANCO.
MWAKA 1968 JOHNNY BOKELO ALIBADILISHA JINA LA BENDI YAKE
YA CONGA SUCCESS, IKAIITWA “CONGA 68" VILE VILE AKABUNI NEMBO YAKE.
GARY STEWART ALIWAHI KUSIMULIA JINSI WANAMUZIKI WA BENDI
HIYO WALIPOTISHIA KUIANCHA BENDI KWA KUTOLIPWA CHOCHOTE.
NYIMBO NYINGI WAKATI HUO ZILIREKODIWA LEBO ILIYOTOLEWA
NCHINI UFARANSA IKIWA LEBO YA KIAFRIKA.
MNAMO MIAKA YA 1972 HADI 1974, BOKELO ISENGO ALIKUWA
AKIFANYA KAZI YA KUREKODI MIZIKI KATIKA STUDI YAKE YA KUREKODI.
MNAMO MIAKA YA KATIKATI MWA MIKA YA 1970, VITENDEA KAZI
KATIKA KUREKODI NYIMBO, ULIKUWA MBAYA.
BOKELO ISENGO ALIKUWA MMOJA WA WATAYARISHAJI
WALIOATHIRIKA. ALIAMUA KUVUKA MIPAKA HADI KATIKA JIJ LA NAIROBI NCHINI KENYA
AKIWA NA TAPE KWENDA KUREKODI.
JOHN BOKELO ISENGE ALIFARIKI DUNIA MWAKA 1995.
MUNGU ALAZE ROHO YAKE PAHALA PEPONI, AMINA.
MUNGU AIWEKE ROHO YAKE PAHALA PEMA PEPONO, AMINA.
No comments:
Post a Comment