MUZIKI WA DANSI ULIINGIJE HAPA NCHINI?
SWALI LILILOAINISHWA HAPO JUU, SINA HAKIKA WATU WENGI HUSUSANI WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI KAMA WANAWEZA
KULIJIBU LICHA YA KUUCHEZA MUZIKI HUO KWA MIAKA MINGI NYUMA.
NIMEFUATILIA NA KUYASOMA MAGAZETI, MAJARIDA NA MITANDAO
MBALIMBALI YA KIJAMII, NIMEBAHATISHA KUPATA HISTORIA HIYO.
YAELEZWA KWAMBA UKITAKA KUONGEA MUZIKI WA DANSI
ULIINGIAJE NCHINI, HUNA BUDI KUIJUA HISTORIA YA MJI WA TANGA.
HISTORIA FUPI YA MJI WA TANGA UNAELEZWA KUWA WAJERUMANI
WALIUSAMBARATISHA MJI HUO KWA MIZINGA KATI MWAKA 1888 NA 1889.
BAADA YA HAPO ULIJENGWA UPYA KWA KUFUATA MPANGILIO
ULIOSABABISHA TANGA KUWA NA MITAA MAARUFU KWA KUTUMIA NAMBA. HUKO TANGA MITAA
INAITWA BARABARA YA KWANZA YA PILI, TATU, NNE NA KUENDELEA.
WAJERUMANI WALIANZISHA SHULE YA KWANZA YA SERIKALI YA
TANGA 1892.
HAPOHAPO WAKANZISHA BENDI YA SHULE YA KWANZA. PAMOJA NA
KUWA WAJERUMANI HAWAKUTAWALA MUDA MREFU, LAKINI WAINGEREZA WALIPOSHIKA MADARAKA
WALIIENDELEZA SANA BENDI HIYO.
ILIKUWA IKIPIGA AINA MBALIMBALI ZA MUZIKI WA
KIGENI.
DANSI ILIANZA KWANZA KAMA KLABU AMBAPO WATU WALIALIKANA
KUJA KUCHEZA AINA MBALIMBALI ZA MUZIKI WA KIZUNGU.
MTINDO MAARUFU ULIOTUMIWA
WAKATI HUO UNAOJULIKANA KAMA BALLROOM DANCING.
AINA HIZI ZA KLABU ZILIANZIA MOMBASA
NCHINI KENYA NA KUINGIA NCHINI HUMU KUPITIA TANGA, KISHA KUPELEKWA DAR ES
SALAAM.
KLAB ILIYOKUWA MAARUFU MJINI TANGA ILIITWA TANGA YOUNG
COMRADES CLUB.
KLABU NYINGINE ILIANZISHWA IKAITWA NEW GENERATION CLUB AMBAYO
ILIANZISHA MATAWI MIJI MBALIMBALI.
KLABU HIZI NDIZO ZILIZOZAA BENDI ZA DANSI. INAONEKANA
DAR ES SALAAM NDIO ILIKUWA YA KWANZA KUWA NA BENDI YAKE AFRICAN ASSOCIATION
JAZZ.
BAADAE WANAMUZIKI WENGINE WALIIHAMA NA KUANZISHA BENDI YA DAR ES SALAAM
JAZZ ‘MAJINI WA BAHARI’ KATI YA MIAKA 1930 NA 1940.
MNAMO MWAKA 1950 KULIKUWA NA BENDI MAARUFU BAGAMOYO
ILIYOITWA LUCKY STAR JAZZ AMBAYO ILIKUWA NA URAFIKI NA DAR ES SALAAM JAZZ.
BAADA YA HAPO KULIANZA BENDI AMBAZO WANAMUZIKI NA
WANACHAMA WAKE WALIPATIKANA KUTOKANA NA MAENEO WANAKOTOKA.
KULIKUWEPO NA BENDI
YA ULANGA JAZZ YA WAPOGOLO, TOKA MKOANI MOROGORO, BENDI YA RUFIJI JAZZ
ILIYOANZISHWA NA WANDENGEREKO TOKA MKOA WA PWANI, WESTERN JAZZ ILIYOANZISHWA
KWANZA NA WANYAMWEZI TOKA TABORA.
BENDI ZOTE HIZI BAADAE ZILIKUJA KUWA NA WANACHAMA
MCHANGANYIKO BILA KUJALI UZAWA. PIA KULIKUWEKO NA BENDI YA SKOKIAN JAZZ,
AMBAYO ILIKUWA BENDI YA WATU MCHANGANYIKO.
MWAKA 1958
WANAMUZIKI KUTOKA KILWA WALIANZISHA BENDI IKAITWA KILWA JAZZ.
WANAMUZIKI WAKE
WALITOKA BENDI ILIYOITWA TANGANYIKA JAZZ.
ILIPOFIKA MWAKA 1966 BENDI ILIKUWA NA WANAMUZIKI
TAKRIBANI 26, 15 WAKIWA KILWA A NA 11 KILWA B. ZAMANI BENDI ZILIKUWA NA MTINDO
WA KUWA NA BENDI B AMBAYO NI YA VIJANA.
HATA PATRICK BALISDYA ALIWAHI KUWA DAR ES SALAAM JAZZ B.
KILWA JAZZ
ILIKUWA NA WANACHAMA KAMA 50 WENGINE WAKIWA VIONGOZI WA JUU SERIKALINI.
WALIOLIPA
ADA YA UANACHAMA NA HIVYO KUWEZA KUINGIA MADANSI YA BENDI BILA KULIPA.
WAKATI
HUO MAKAO MAKUU YA KILWA JAZZ LICHA YA WANAMUZIKI WAKE WAKITOKEA KILWA,
YALIKUWA KATIKA UKUMBI AMBAO KWA SASA UNAITWA KWA MADOBI MAENEO YA JANGWANI,
JIJINI DAR ES SALAAM.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment