UNAMKUMBUKA ABETI MASEKINI?
Jina lake kamili alikuwa akitwa
Elisabeth Finant alizaliwa Novemba 09, 1954 katika mji wa Kisangani,
Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Abeti alitokea katia familia tajiri yenye watoto wanane.
Baba yake mzazi mzee Jean Fionant, alikuwa Chotara wa mchanganyioko wa Ukongomani na Ubelgiji.
Mwaka 1961, Masekini alipatwa na pigo baada ya Baba yake
kauawa kikatili mjini Mbujimayi kutokana matatizo ya Kisiasa.
Mzee Finant alikua mwanachama wa cha MLC, kilichokuwa
kikiongozwa na hayati Emery Patrice Lumumba.
Lumumba alikuwa Waziri Mkuu wa zamani nchini DRC Kongo ambae
pia anaelezwa kuwa ndie Shujaa wa Uhuru wa nchi hiyo.
Hali hiyo ikampelekea mama yake Abeti Masekini kuchukua
uamuzi wa kuhamia katika jiji la Kinshasa ili apate kujihifadhi akiwa na
Wanawe.
Walipofika Kinshasa, mama yake alimchukua Abeti Masekini karejesha
darasani kwenye Shule iliokuwa ikijulikana kwa Jina la ‘Lycee Ycee Sacre Ceur.
Kwa sasa inaitwa ‘Bosongani’.
Baada ya kumaliza shule ya sekondari, Masekini akaajiriwa kama Katibu kwenye Ofisi
ya Waziri wa Utamaduni.
Kwa mshangao wandugu zake na Familia kuona Abeti Masekini
akiamua kujiuzuru kwenye kazi aliokua nayo. Akaelekeza mawazo yake kwenye fani ya muziki, ndipo wakati akajipachika jina
la ‘Betty’.
Mwaka 1971 chini ya usimamizi wa mwanamuziki ‘Gerard Madiata’, palitokea mashindano ya
kumtafuta mwanamuziki chipukizi. ‘Betty’akaamua kushiriki kwenye mashindano
hayo, ambayo kwa bahati mbaya hajafaulu.
Changamoto ya kupenda muziki ndipo ilipoongezeka huku akiwa
mdogo akichipukia mwenye umri wa miaka 17 wakati huo.
Ili apate kuruhusiwa kutumbuiza katika unenguaji kwa jina
lake mwenyewe, ilibidi ajiongezee miaka
mitatu zaidi, akawa anasema yeye ni mkubwa
wa miaka 20.
Abeti akisaidiwa na kaka yake ‘Jean Abumba’ ambae alikuwa mpiga
gitaa mashuhuri, akawa kila siku anafanya onesho kwenye vilabu vidogodogo
Jijini Kinshansa.
Abeti Masekini alikutana na Gerard Akueson, aliyekuwa raia
wa nchi ya Togo katika jiji la Kinshasa
mwaka 1971. Hapo ndipo fani yake ya muziki ilipoanza rasmi.
Gerard Akueson ndiye akawa meneja wake mkuu tangia mwaka
1972. Abeti na Akueson wakaanzisha mahusiano ya kimapenzi na ilipotimu mwaka1989,
wakakufunga ndoa jijini Paris nchini Ufaransa.
Walibahatika kupata watoto wanne, wa kike 3 na mvulana mmoja.
Mumewa huyo alimshauri waongozane kwa kuhamia kwenye nchi za
Afrika ya Magharibi, ambako walitumaini kupata mafaanikio zaidi.
Wikiwa hukowalijikuta akiwa na Mashabiki wengi sana kwenye nchi
za Benin, Conte D’ivoire, Togo, Niger, Nigeria, Guinea na Ghana.
Baada ya miaka kadhaa akiwa kwenye nchi hizo, Abeti Masikini
aliaamua kurudi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Aliporejea mapokezi
hayakuwa mazuri kwa kuwa watu wengi walikua hawamfahamu kabisa.
Kilicho mponza zaidi ni kwa kipindi chote hicho, alikua
hajaweka hata na album japo moja sokoni.
Licha ya kutofahamika kwake, aliamua kufanya onesho kubwa katikati
ya jiji la Kinshasa kwenye ukumbi wa CINE Palldium ambako aliambulia watu 12
pekee ndio walio jitokeza kumuangalia.
Tukio hilo halikumdhoofisha moyo Abeti, aliendelea kufanya
kazi kwa bidii ili malengo yake yakamilike.
Kaanza kufanya mazoezi ya kuboresha Sauti yake,
Baada ya kufanya mazoezi makubwa ya kuboresha sauti yake, mwaka
1973 alitoka na album yake ya kwanza ‘Pierre Cardin’ ikiwa na nyimbo kadhaa
zikiwemo Mutoto wangu, Bibile,
Aziza, Miwela na Safariet Papy
yaka.
Album hiyo haikupokelewa vilivyo na wakazi wa jiji la Kinsahasa.
Machoni mwao walimchukulia Abeti kama mgeni.
Walimlaumu kwa tabia yake ya kupenda kuimba baadhi ya nyimbo
zake kwa lugha ya Kiswahili.
Nguli huyo Abeti Masekini akapatwa na wazo la kuunda kundi
lake akalipa jina la ‘Les Redoutables’.
Kundi hilo lilikuwa na wanenguaji wake machachari walio
julikana kama ‘Les Tigresses’, ambalo lilifanya watu wengi waanze kuvutiwa
naye.
Maonesho yake katika jiji la Kinshasa yakawa gumzo mitaani.
Kazi lizokuwa akizifanya meneja wake, zikazaa matunda mema.
Alifanikiwa kupata mkataba uliompeleka kwenda kufanya onesho
katika ukumbimaarufu wa Olympia uliopo katika jiji la Paris, ncini Ufaransa.
Mwaka1973 akiwa njiani kuelekea Paris kwenye onesho hilo,
alitua katika jiji la Dalkar nchini Senegal. Huko alifanya onesho ambalo pia
rais wa nchi hiyo wakati huo Leopald Seadar Senghor alihudhuria.
Pesa zilizopatikana katika onesho hilo alizotoa kama msaada wake
kwa watu walioathiriwa kwa ukame wa ardhi.
Alipotuwa katika jiji la Paris Februari 02, 1973
aliporomosha onesho kabambe lilowavutia hasa mashabiki wakizungu kwenye ukumbi
wa Olympia.
Abeti Maseki alifanikiwa kufanya onesho jingine Juni 06,
1974 kwenye ukumbi wa Carnegie, uliopo
katika jiji ma New York nchini Marekani.
Umaarufu wake ulizidi kuja juu zaidi hususani pale alipopewa
fursa ya kutumbuiza kwa pamoja katika jukwaa moja na nguli wa muziki duniani.
Jukwaa hilo lilipambwa na wanamuziki akina James Brown, Miriam Makeba, Tabu Ley
na Franco Luambo Makiadi, kabla ya pambano la masumbwi la kihistoria kati ya Mohammed
Alli ‘Clay’ na George Foreman jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Albam yake ya pili alifyatua mwaka 1975 ikiwa na jina la ‘La
Voix Du Zaire’.
Nyimbo zilizokuwa zimesheheni katika albam hiyo ni Likayabo,Yamba
yamba, Kiliki, Bamba, Nalikupenda na Ngoyaye.
Mwaka huo huo Abeti alipokea mualiko kutoka kwa ‘Bruno Coquatrix’ ambae ndie aliyekuwa mmiliki wa ukumbi wa Olympia
ya jijini Paris. Akaenda kwa mara nyingine tena kufanya maonesho kwa Siku mbili
mfululizo.
Ndipo hapo akapachikwa jina bandia la ‘Tiger mwenye kucha za
dhahabu’
Mwaka uliofuatia wa 1976, ulikuwa mbaya ki maslahi kwa Abeti
Masekini.Alimpata mpinzani wa uhakika katika muziki aliyejulikana kwa majina ya
Mpongo Love, aliyekuja juu kuliko yeye. Mpongo akaongoza Hit Parade kwenye radio
ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( Zaire) wakati huo.
Wimbo wake ‘Pas Possible’ ulimafanya kuwa ni mwenye kupendwa
mno na mashabiki.
Pamoja na yote mwaka 1977, wanamuziki hao Abeti na Mpongo
walifanya kitu ambacho hakikutarajiwa na wengi. Walifanya onesho kubwa kwa
pamoja kwenye ukumbi wa ‘Cine Palldium’ katika jiji la Kinshasa na kuacha simulizi
kubwa.
Kila mmoja wao kaimba kiaina yake, wakaweka misingi mizuri ya kupendana kwa wanamuziki wa
kike wa kizazi kijacho.
Historia ya Abeti Masekini itaendelea kukumbukwa daima kwa kuwa
yeye ni darasa tosha,
Wanamuziki wengi maarufu wamepitia kwenye bendi yae
wakiwamo akina Mbilia Bel, aliyenengua
toka 1976 hadi1981, Lokua Kanza aliyekuwa
mpiga gitaa mwaka 1980- hadi 1981, Abby Surya aliyekuwa mnenguaji mwaka 1984 hadi
1986 na Malage De Lugendo aliyekuwa
mwimbaji. Wengine walikuwa wanenguaji Joëlle Esso, Tshala Muana mwaka 1978
hadi 1979, Yondo Sister mwaka 1986 na Lambio Lambio ‘Komba Bellow’ kwan
upande wa kinanda.
Abeti Masekini ni mmoja kati ya wanamuziki wa kike barani
Afrika, waliofanikiwa kujiwekea jina Kimataifa. Alidhihirisha uwezo wa kipaji
chake na kufahamika nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo muziki umetawalia na Wanaume.
Abeti pia alikuwa mstari wa mbele kupigania haki ya
Wanawake.
Kwa miujiza ya mungu Abeti alifariki dunia Septemba
09, 1994 akiwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa.Tarehe hiyo inafanana na
ile aliyozaliwa ya Novemba 09, 1954.
Ni mwaka wa 21 tangu atutoke mwana muziki huyo, mungu ailaze
pahala pema peponi, Amina.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment