ALLY CHOKI ‘MZEE WA FARASI’ MCHACHALIKAJI
ALLY CHOKI BAADHI YA
WATU HUMUITA “MZEE WA FARASI” AU “MZEE WA KIJIKO”, NI MWANAMUZIKI ANAYETAMBA
MIONGONI MWA WANAMUZIKI WA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI.
ANA VIPAJI VINGI
VILIVYOJENGEKA KICHWANI MWAKE VIKIWEMO VYA KUTUNGA, KUIMBA PAMOJA NA UONGOZI.
HISTORIA YAKE KATIKA
MUZIKI CHOKI ILIIELEZA KWAMBA ALIANZA MUZIKI RASMI MWAKA 1988, ALIPOJIUNGA
KATIKA BENDI YA LOLA AFRICA. BAADAE AKAJIUNGA NA BENDI YA MWENGE JAZZ ILIYOKUWA
CHINI YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ).
HAKUDUMU KWA
KIPINDI KWANI BAADA YA MIEZI SITA ALIHAMIA KATIKA BENDI YA BANTU GROUP
ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA ‘KOMANDOO’ HAMZA KALALA.
“MWAKA 1990 NIKIWA
BANTU NA HAMZA KALALA AKIWA KIONGOZI TULITOA ALBAMU YA BABA JANE. MWAKA 1991
NILITOKA BANTU, NIKAJIUNGA NA LEGHO STARS CHINI YA TSHIMANGA KALALA ASOSA...”
ALISEMA ALLY CHOKI
SAFARI YA KUSAKA
MAFANIKIO ILIKUWA IKISABABISHA KWENDA HUKU NA KULE AMBAPO HUKO LEGHO STARS,
NAKO HAKUDUMU SANA AKAAMUA KURUDI KATIKA BENDI YA BANTU GROUP.
CHOKI ALIKUWA MITHIRI
YA KUNGURU KWANI HUKO NAKO HAKUKAA SANA, AKAENDA KUJIUNGA NA BENDI
YA BENDI YA MK BEAT ‘TUKUNYEMA’ ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA SHEM IBRAHIM KARENGA.
MWAKA 1992 ALIHAMIA
KATIKA BENDI YA WASHIRIKA STARS ‘WATUNJATANJATA’ AMBAKO WALITOA ALBAMU
ILIYOPEWA JINA LA GUBU LA WIFI. PALE WALIKUWA NA MWIMBAJI MAHIRI ADAM BAKARI
‘SAUTI YA ZEGE’, MPAPASAJI KINANDA ABDUL SALVADO ‘FATHER KIDEVU’ NA WENGINE
WENGI.
KATIKA HARAKATI ZA KUSAKA MAISHA ALLY CHOKI ALIAMUA KUVUKA MPAKA WA NCHI NAKUINGIA KATIKA JIJI LA NAIROBI, NCHINI KENYA MWAKA 1994.
AKIWA KATIKA JIJI HILO
ALIUNGANA NA WANAMUZIKI WENGINE AKIWEMO MUUMINI MWINJUMA, AMBPO WAKAANZISHA
BENDI YAO IKIITWA EXTRA KIMWA MWAKA 1998.
CHOKI ILIPOTIMU
MWAKA MWAKA 1999, ALIAMUA KUREJEA NCHINI BAADA YA KUPATA TAARIFA
KUWA MAMA YAKE MZAZI KUWA ALIKUWA MGONJWA.
AKIWA HAPA NCHINI
ALIAMUA KUJIUNGA KATIKA BENDI YA THE AFRICAN STARS ‘TWANGA PEPETA’ CHINI
YA UONGOZI WA MKURUGENZI ASHA BARAKA. ALIKUBALI KUJIUNGA NA BENDI HIYO
BAADA YA KUPOKEA USHAURI KWA MWANAMUZIKI MWENZAKE ROBERT HEGGA ‘CATERPILLAR’
AMBAYE WALIKUWA WOTE NAIROBI.
MWAKA 2000 WALITOA
ALBAMU IITWAYO JIRANI ILIKUWA NA NYIMBO NYINGI LAKINI JIRANI ULIKUWA UTUNZI
WAKE YEYE CHOKI.
KAMA KUNA KITU AMBACHO HAWEZI KUKISAHAU WAKATI AKIWA TWANGA, NI PALE WANAMUZIKI WENGI WALIHAMA BENDI HIYO NA KWENDA KUJIUNGA NA BENDI NYINGINE YA CHUCHU SOUND. WENGINE WAKATIMKIA KATIKA BENDI YA MCHINGA SOUND, AKIWEMO ADOLF MBINGA MPIGA SOLO.
BUSARA ZAKE AKAZITUMIA
KWA KUMFUATA MPIGA SOLO MWINGINE MIRAJI SHAKASHIA ‘SHAKA ZULU’.
SHAKASHIA NAYE
HAKUDUMU KWA KIPINDI KIREFU AKATIMKA NDIPO NAFASI YAKE ILISHIKWA NA KASSIM
RASHID ‘KIZUNGA’ ALIYEKUJA KUPIGA GITAA LA RHYTHM.
BAADAE ALIPEWA CHEO
KUWA KIONGOZI WA BENDI NA NDIPO WALIPOTENGENEZA ALBAMU YA FAINALI UZEENI.
ALBAMU HIYO ILIFUATIWA NA ILE YA ‘UKUBWA JIWE’ HATIMAE ‘CHUKI BINAFSI’.
ALLY CHOKI ALIKUWA NA
KILA SABABU ZA KUJIVUNIA AKIWA HAPO TWANGA, KWA KUWA ALIKUWA AKIONGOZA
KWA KUTUNGA NYIMBO NYINGI ZILIZOVUMA.
BAADA YA KUJIPIMA
UWEZO WAKE, AKANZISHA BENDI YAKE YA EXTRA BONGO MWAKA 2003. BENDI HIYO
ILIKUSANYA WANAMUZIKI WENGI MAHIRI HAPA NCHINI NA KUWEZA KUWA TISHIO KWA BENDI
ZINGINE HUSUSAN KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM.
LAKINI KAMA WASEMAVYO
WASWAHILI “PENYE RIZIKI HAPAKOSI FITINA” NDIVYO ILIVYOTOKEA KWA ALLY CHOKI
AMBAPO FITINA IKATENGENEZWA NA WANAMUZIKI WAKE WAKANUNULIWA AKABAKI PASIPO
‘MWEUPE’
KUTOKANA NA HALI HIYO,
ALILAZIMIKA KUIACHA BENDI YAKE NA KWENDA KUJIUNGA KATIKA BENDI YA MCHINGA. HUKO
NAKO HAKUDUMU KWA KIPINDI KIREFU, AKAREJEA TENA TWANGA PEPETA.
BAADAE TENA AKAJIUNGA
NA KUNDI ZIMA LA TANZANIA ONE THEATER LILILOKUWA LIKIONGOZWA NA KAPTENI MSTAAFU
JOHN KOMBA. AKIWA NI MMOJA WA VIONGOZI WA TOT, CHOKI ALIFANIKIWA KUIPANDISHA
CHATI BENDI HIYO BAADA YA KUWALETA WANAMUZIKI TOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA
KONGO.
ALIDUMU NA BENDI HIYO
YA TOT HADI MKATABA WAKE ULIPOKWISHA, AKAAMUA KUIFUFUA TEA BENDI YAKE YA EXTRA
BONGO MWAKA 2009.
ALLY CHOKI
AKIZUNGUMZIA KISA CHA SABABU ZA KUSHUKA KWA KIWANGO CHA MUZIKI WA DANSI, CHOKI
ALIKANUSHA KAULI HIYO.
ALISEMA KWAMBA MUZIKI
WA DANSI HAUJASHUKA KIWANGO ISIPOKUWA VYOMBO VYA HABARI VIMEUPA KISOGO KWA
KUANGALIA ZAIDI MUZIKI WA BONGO FLEVA LICHA YA WAO KUNTOA NYIMBO NZURI NA HATA
VIDEO NZURI.
“UONGOZI WA BENDI ZA
MUZIKI NI MGUMU UKILINGANISHA NA MWANAMUZIKI WA BONGO FLEVA AMBAPO KIONGOZI
HANA WANAMUZIKI WENGI. HATA HIVYO NAAMINI NI WAKATI NA KUNA MUDA UTAFIKA MUZIKI
HUU UTAKUWA JUU…” ALISEMA ALLY CHOKI.
CHOKI AKITHAMINI
MCHANGO MKUBWA WA WANAMUZIKI WALIOMTANGULIA, ALIMUELEZEA MAREHEMU MUHIDIN
MAALIM GURUMO KUWA ALIKUWA MWALIMU NA MTU ANAYESIKILIZA USHAURI.
ALISEMA KWAMBA YEYE
BINAFSI NILIFANYA NAYE KAZI NYINGI ZIKIWAPO ZILI WAIZOTOA ALBAMU YENYE NYIMBO
ZAKE TATU NA ZA GURUMO TATU.
“ALBUM HIYO ILIFANYA
VIZURI SANA NA TULIPATA FEDHA NYINGI MPAKA KILA NINAPOKUTANA NAYE AKAWA ANASEMA
NAKUSHUKURU SANA KIJANA….” ALISEMA MZEE WA FARASI.
AKIELEZEA SIRI YA
MAFANIKIO YAKE , CHOKI ALIELEZA KUWA YANATOKANA NA YEYE KUFANYA JUHUDI,
KUTOKUTA SIGARA WALA KUNYWA POMBE ALIYOANCHANA NAYO 1994.
AIDHA AMESEMA KWAMBA
ANAMILIKI NYUMBA, GARI, MKE NA WATOTO SITA.
IKUMBUKWE KABLA YA KUONDOKA THE
AFRICAN STAR, ALIKWARUZANA MA MKURUGENZI WA ASET ASHA BARAKA. KATIKA
PURUKUSHANI HIZO CHOKI ALIFIKA MBALI KWA KUTOA KIAPO KIBAYA DHIDI YA
MKURUGENIZI WAKE. BARAKA MSILWA.
KWANZA KITENDO CHA ASET KUMPELEKA
MAHAKAMANI KUMDAI GARI, PILI ASET KUKATAA KURUDISHA PESA ZA MIRAJI SHAKASHIA NA
TATU NI ASET KUTOTHAMINI MICHANGO YA WASANII WALIOIZALISHIA PESA NYINGI.
CHOKI ANSEMA KITENDO CHA ASET
KUMPELEKA MAHAKAMANI KUMDAI GARI AMBALO WALIMPA MWENYEWE KILIMKERA SANA
HUU, CHOKI HIVI
KARIBUNI AMEREJEA KWA KISHINDO KWENYE BENDI YAKE YA ZAMANI YA AFRICAN STAR
ENTERTAINMENT (TWANGA PEPETA)
ALITANGANZWA MBELE YA
WAANDISHI WA HABARI NA MKURUGENZI WA ASET, ASHA BARAKA ALIYEKUWA AMEFUATANA NA
KATIBU WA BENDI, LUIZA MBUTU.
No comments:
Post a Comment