ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' KIFO KIOLIKATIZA NDOTO ZAKE.
KILA MWANADAMU HUJIPANGIA MAMBO YAKE AKITARAJI KUIKAMILISHA
ANAYOYAFIKIRIA KUYAFANYA. LAKINI JUHUDI ZOTE HIZO HUWEZA KUPANGULIWA KWA UWEZO
WAKE MUNGU, KWA NJIA MOJA AMA NYINGINE.
MWANAMUZIKI MAHIRI ABUU SEMHANDO NI MMOJA WAPO AMBAYE
ALIWEKA FIKRA ZAKE ZOTE KATIKA KUYAENDESHA MAISHA YAKE NA FAMILIA KUPITIA
MUZIKI.
FIKRA HIZO ZILIKATISHWA GHAFLA BAADA YA KUPATA AJALI
ILIYOPELEKEA KUPOOTEZA MAISHA DESEMBA 18, 2010.
SEMHANDO KATIKA MAISHA YAKE ALICHANGIA MAFANIKIO MENGI
KATIKA BENDI YA AFRICAN STAR ENTERTAINMENT TANZANIA (ASET), KWA ASILIMIA KUBWA
KUTOKANA NA KUJITOA KWA KILA HALI.
ALIKUWA MMOJA KATI YA VIONGOZI WA ASET AKIWA ANA WADHIFA
WA KATIBU WA BENDI. ALIDUMU KWA KIPINDI KIREFU KATIKA BENDI HIYO YA TWANGA
PEPETA TOKA ALIPOJIUNGA MWAKA 1998, AKITOKEA BENDI YA DIAMOND SOUND WANA ‘KIBINDA
NKOI’.
KWA MUJIBU WA MKURUGENZI WA ASET ASHA BARAKA ALIMUELEZEA
ABUU KUWA ALIITUMIKIA TWANGA KAMA MALI YAKE BINAFSI. ALISEMA KUWA KIFO CHA
SEMHANDO KILIMTIA SIMANZI YEYE BINAFSI, WANAMUZ\IKI WENZAKE PAMOJA NA WAPENZI WOTE
WA TWANGA PEPETA NDANI NA NJE YA NCHI.
ALITAMKA KUWA ABUU ALIKUWA NI CHACHU YA MAFANIKIO YA
ALBAMU ZOTE 10 AMBAZO WAMEZITOA KUTOKANA NA KUSHIRIKI KATIKA KUANDAA MUZIKI NA
KUSIMAMIA NIDHAMU YA BENDI.
KIFO CHA ABUU SEMHANDO KATIKA FAMILIA YAKE KILIMGUSA
SANA BINTI YAKE SHARIFA, AMBAYE SIKU AMBAYO ALIKUWA ANATAKIWA KUFUNGISHWA NDOA
NA BABA YAKE NDIYO MAUTI YALIPOMKUTA NA KUFANYA SHEREHE HIZO KUGEUKA MSIBA.
WASIFU WA NGULI HUYO UNAELEZA KUWA JINA LAKE KAMILI
LILILKUWA ABUU ALLY SEMHANDO MAARUFU ‘LOKASSA’ AU ‘BABA DIANA’
ALIKUWA MCHARAZAJI MAHIRI WA DRUM WAKATI HUOHUO ALIKUWA
NDIYE MENEJA WA BENDI YA AFRICAN STARS ‘TWANGA PEPETA’.
ABUU ALLY SEMHANDO ‘LOKASSA’ ALIZALIWA MWAKA 1953 KIJIJI
CHA KIBANDA WILAYA YA MUHEZA MKOANI TANGA.
ALIANZA SHUGHULI ZA MUZIKI MWANZONI MWA MIAKA 1970 AKIWA
KATIKA BENDI YA TANGA INTERNATIONAL, BAADAE ALIKWENDA KUWA MMOJA KATI YA
WAASISI WA BENDI ZA TANZA MUZIKA NA ORCHESTRA TOMATOMA KABLA YA KUTUA SAFARI
SOUND ORCHESTRA (OSS)
SEMHANDO NA HAMZA KALALA NI MIONGONI MWA WANAMUZIKI
WAANZILISHI WA BENDI YA SUPER MATIMILA NA NDIO WALIOWAKARIBISHA WANAMUZIKI RAIA
WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO MOSESE FANFAN NA RAMADHA MTORO ONGALA ‘DK.
REMMY’
BAADAE ALIJIUNGA NA BENDI YA VIJANA JAZZ ‘PAMBA MOTO’, INAYOMILIKIWA
NA JUMUIA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM AMBAKOKWA UWEZO WAKE WA KUONGOZA
ALIKABIDHIWA NAFASI YA KUWA KATIBU WA BENDI.
ABUU ALISHIRIKI KUPIGA DRUMS KWA KIWANGO KIKUBWA KATIKA
NYIMBO NYINGI AMBAZO ZILIILETEA MAFANIKO YA BENDI HIYO.
AKIWA KATIKA BENDI HIYO MWIMBAJI MAARUFU TOKA JAMHURI YA
KIDEMOKRASIA YA KONGO KASALOO KYANGA, ALIMPACHIKA JINA BANDIA LA ‘LOKASSA’.
LICHA YA KUWA MPIGA DRUMS, SEMBANDO ALIKUWA NI
MWANAMUZIKI MWENYE KIPAJI KIKUBWA CHA UONGOZI WA BENDI (MUSIC BAND MANAGEMENT).
ALIKUWA AKISHIRIKI KATIKA KUANDAA MUZIKI ILI KUHAKIKISHA BENDI YOYOTE
ALIYOPITIA INAPATA MAFANIKIO. JAMBO HILO LILIMJENGEA UMAARUFU KATIKA KILA BENDI
ALIYOPIGIA.
HISTORIA INAONYESHA KUWA KILA BENDI ALIZOWAHI KUPITIA
AKIWA KIONGOZI, MARA BAADA YEYE KUONDOKA, ZILIYUMBA NA ZINGINE KUTOKOMEA KABISA
KATIKA MEDANI YA MUZIKI WA DANSI.
LAKINI SI MATIMILA PEKEE YAKE HATA ALIPOKUWA NA VIJANA
JAZZ ‘SAGA RHUMBA’ AMBAKO ALIKUWA KATIBU CHINI YA UONGOZI WA HEMED MANETI,
ALIKUWA MMOJA WANAMUZIKI WALIOSHIRIKI KATIKA KUILETEA MAFANIKIO KWA MIAKA YOTE
HIYO KABLA YA KUJIONDOA. YAELEZWA KUWA ABUU PIA ALIKUWA MUASISI WA ‘VIJANA
DAY’.
KATIKA BENDI HIYO YA VIJANA ALISHIRIKI KWA KIWANGO
KIKUBWA KUTENGENEZA NYIMBO AKIWA NA WAIMBAJI KINA HEMED MANETI, SAIDI HAMIS
‘MISUKOSUKO’, FRED BENJAMIN, COSMAS TOBIAS CHIDUMULE NA KIDA WAZIRI.
AIDHA WAPIGA VYOMBO WAKATI HUO WALIKUWA AKINA KURWA WA
MILONGE, HAMZA KALALA, HASSAN DALALI, AGGREY NDUMBALO NA DISFA SEMHANDO (MDOGO
WAKE), ALIYEKUWA AKILIUNGURUMISHA GITAA ZITO LA BESI. ALIKUWEPO PIA MPIGA GITA
LA SOLO SHABANI YOHANA ‘WANTED’ NA WENGINE WENGI.
AKIWA NA WANAMUZIKI HAO AMBAO NI BAADHI TU YA KUNDI
ALILOKUWA NALO, WALISHIRIKI KUTENGENEZA NYIMBO KALI KAMA ‘BUJUMBURA’, ‘MARY
MARIA’, ‘TAMBIKO LA PAMBAMOTO’, ‘MUNDINDE’, ‘ALI HASSAN MWINYI APEWE KURA ZA
NDIYO’, ‘WIFI ZANGU WANANINYANYASA’, STELLA, ‘PENZI HALIGAWANYIKI’ NA NYINGINE
NYINGI NZURI KUPINDUKIA.
NYIMBO HIZO ZILITIKISA ANGA YA MUZIKI CHINI YA UONGOZI
SHUPAVU WA HEMED MANETI ALIYEKUWA KIONGOZI, HAMZA KALALA ALIKUWA NI KIONGOZI
MSAIDIZI NA ABUU SEMHANDO MWENYEWE
ALIYEKUWA KATIBU.
KATIKA KUDHIHIRIKISHA UWEZO ALIOKUWA NAO ALIPOJING’ATUA
VIJANA JAZZ, NDIPO JINAMIZI NA ANGUKO LA BENDI HIYO LILIPOANZA KUINYEMELEA.
TANGU HAPO BENDI HIYO HAIJAFANYA VYEMA KATIKA MEDANI YA MUZIKI NCHINI.
BAADHI YA WANAMUZIKI ALIOFANYA NAO KAZI WALIMZUNGUMZIA
MAREHEMU SEMHANDO AKIWEMO JOHN KITIME
AMBAYE ALISEMA KUWA ATAENDELEA KUMKUMBUKA ABUU SEMHANDO KWA UCHESHI WAKE, NA
VILEVILE ALIMPOKEA NA KUMTAFUTIA MALAZI JIJINI MWAKA 1989, WAKATI ANAJIUNGA NA
VIJANA JAZZ AKITOKEA TUNCUT ALMASI YA IRINGA.
KWA UPANDE WAKE MKUNG’UTAJI WA GITAA LA SOLO ALDOF
MBINGA AMBAYE NAYE ALISEMA TASNIA YA MUZIKI WA DANSI IMEPOTEZA JEMEDARI AMBAYE
ALIKUWA HAYUMBI KATIKA MISIMAMO YAKE JAMBO AMBALO LILIILETEA MAFANIKIO VIJANA
JAZZ AKIWA KATIBU NA ASET.
MBINGA ALIFANYA KAZI NA SEMHANDO KWA KUTENGENEZA ALBAMU
YA KWANZA YA TWANGA PEPETA YA ‘KISA MPEMBA’ NA ‘JIRANI’.
WENGINE WALIOMZUNGUMZIA MAREHEMU NI WAZIRI ALLY AMBAYE
NI MWANAMUZIKI WA BENDI THE KILIMANJARO ‘WANA NJENJE’ AKIMTAJA SEMHANDO KAMA
NGUZO ILIYOKATIKA GHAFLA WAKATI WATU WAKIHITAJI HUDUMA NA UKONGWE WAKE KATIKA
MUZIKI.
USHUHUDA MWINGINE ULITOLEWA ISIHAKA KIBENE, AMBAYE
ALISEMA, TWANGA PEPETA IMEPOTEZA MPIGANAJI NA MTAWALA MAHIRI KUTOKANA NA KUWA
KIUNGO KATIKA KUFANYA MAJUKUMU YA KILA SIKU YA BENDI. “HUYU JAMAA NI RAFIKI
YANGU SANA AMBAYE NILIWAHI KUFANYA NAYE KAZI KIWANDA CHA UCHAPAJI CHA PRINTPAK
MIAKA YA 1970, NA HATA ALIPOANZA SHUGHULI ZA MUZIKI TULIENDELEA KUWA
MARAFIKI..." ALISEMA KIBENE.
ABUU ALLY SEMHANDO AMEACHA MKE NA WATOTO 10 NA KABURI
LAKE LIPO KIJIJI CHA KIBANDA WILAYA YA MUHEZA ALIPOZALIWA.
MUNGU AILAZE ROHOYO YAKE PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.
No comments:
Post a Comment