KANDA BONGO MAN ALIVYOTESA AFRIKA MASHARIKI.
KANDA BONGOMAN NI MWANAMUZIKI AMBAYE KAMWE HATASAHAULIKA NA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI HUSUSANI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM NCHINI TANZANIA.
WASIFU WA BONGOMAN UNAELEZA KUWA ALIZALIWA MWAKA WA 1955 KATIKA KIJIJI CHA INONGO, KILICHOPO NJE KIDOGO YA MJI WA KINSHASA HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.
ALIWEZA KUJIPATIA UMAARUFU MKUBWA KATIKA MUZIKI WA SOUKOUS AKITUNGA, KUIMBA NA KUCHEZA KATIKA MTINDO WA KWASA KWASA.
KANDA BONGOMAN ALIKUWA MWIMBAJI WA BENDI YA ORCHESTRA BELLE MAMBO MWAKA WA 1973.
KANDA ALIANZA MUZIKI RASMI BAADA YA KUHAMIA KATIKA JIJI LA PARIS NCHINI UFARANSA MWAKA 1979.
MUZIKI WAKE ULIANZA KUINGIZA VIPENGELE VYA MUZIKI WA ZOUK (ASILI YAKE NI KIFARANSA KATIKA WEST INDIES).
ALBAMU ZAKE ZA KWANZA "IYOLE" ILIYOTOKA MWAKA 1981 NA "DJESSY" MWAKA 1982 ZILIVUMA VILIVYO KWA WAPENZI NA MASHABIKI WA MUZIKI WAKATI HUO.
BONGOMAN ALIWAHI KUSHIRIKI KATIKA MAONESHO YA WOMAD YALIYOFANYIKA NCHINI UINGEREZA MWAKA 1983, AMBAKO ALIFANIKIWA ‘KUWAKUNA’ MASHABIKI WALIOHUDHURIA.
MWAKA 1989, BONGO MAN ALIACHIA ALBUM YAKE YA KWANZA YA KWASA KWASA, ILIYOSAMBAZWA NA WAMAREKANI ILIYOUNGANISHA ZILE ALIZITOA ZA “LELA LELA" NA "SAI"
ALIENDELEA KUTANUA WIGO WA MUZIKI KWA KUPIGA MUZIKI WA ZING ZONG, AKIWAKUMBUKA WANAMUZIKI WAWILI NDUGU AMBAO NI MAREHEMU SOKI VANGU NA SOKI DIAZENZA ALIOKUWA AKIPIGA NAO MUZIKI KATIKA BENDI YA ORCHESTRA BELLA BELLA MWAKA 1991.
BONGOMAN ALIFYATUA ALBUM YAKE YA TATU YA SOUKOUS CENTRAL PARK, ILIYOSAMBAZWA NCHINI MAREKANI MWAKA 1993. BAADAE AKAPATWA NA ARI YA KUCHEZA MUZIKI ‘LIVE ‘
AKIWA NA ALBUM YAKE HIYO MWAKA 1998, ALIALIKWA NCHINI AFRKA YA KUSINI AMBAKO ALIPATA UZOEFU MKUBWA TOKA MUZIKI WA NCHI HIYO.
MIAKA HIYO YA 1990, KANDA ALIWEZA KUZIKONGA NYOYO ZA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI WA KENYA NA TANZANIA.
AKIWA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM MIAKA YA 1990, ALIWEZA KUJAZA WATU KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA KILIMANJARO.KIINGILIO KILIKUWA KIKUBWA CHA SHILINGI LAKI MOJA KWA MTU MMOJA.
TIKETI ZILIMALIZIKA HUKU WAPENZI NA MASHABIKI WAKIOMBA ZIKACHAPWE NYINGINE. LAKINI HAIKUWEZEKANA KUTOKANA NA UWEZO MDOGO WA UKUMBI KUMUDU KUBEBA IDADI KUBWA YA WATU.
REKODI YA KIINGILIO KIKUBWA KAMA HICHO HADI LEO HAIJAVUNJWA NA BENDI NYINGINE YEYOTE YA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI.
BAADA YA KUONDOKA NCHINI, ‘ALIZALISHA’ BONGOMAN MWINGINE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM ALIJULIKANA KWA JINA LA SHAABAN KADET.
ALIPEWA JINA BANDIA LA ‘BONGOMAN WA TANZANIA’, KWA UWEZO WAKE MKUBWA WA KUIGA MINDOKO YA KANDA BONGOMAN.
MSANII HUYU KUTOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO, NI MIONGONI MWA WASANII WALIOJITENGENEZEA UMAARUFU MKUBWA KATIKA MIONDOKO YA SOUKOUS BARANI AFRIKA.
LICHA YA UWEZO WAKE MKUBWA KATIKA UIMBAJI NA UTUNZI, UMAARUFU WAKE ULIJENGWA ZAIDI NA MUONEKANO WAKE WA KIMAVAZI SAMBAMBA NA UCHEZAJI.
KUPENDELEA KWAKE KUPENDA KOFIA ZA PAMA, KULICHANGIA KOFIA HIZO KUPACHIKWA JINA KANDA BONGOMAN.
BONGOMAN PAMOJA NA WANAMUZIKI WAKE, PIA YEYE NI MBUNIFU MAHUSUSI WA NGUO.YAELEZWA KUWA BAADHI YA NGUO ZAKE HUZIBUNI NA KUZISHONA MWENYEWE.
NI YEYE ALIYEREMBESHA SOUKOUS KWA KUHIMIZA UTUMIAJI WA GITA BAADA YA KILA MSTARI NA HATA WAKATI MWINGINE KATIKA MWANZO WA WIMBO.
KAMA WENGI WA WANAMUZIKI SOUKOUS NA RUMBA KUTOKA AFRIKA WALIOKUWA MBELE YAKE, KANDA BONGOMAN PIA ALIKUWA NA KUNDI LA WANAMUZIKI ALILOIMBA NALO.
WENGI WA WANAMUZIKI WA KUNDI HILO, BAADAE WALIHAMA NA KUANZA KUIMBA BINAFSI.
MFANO WA KARIBU NI MPIGAJI MAARUFU WA GITAA LA SOLO DIBLO DIBALA ALIYEJULIKANA KAMA "MACHINE GUN", ALIKUWA SEHEMU MUHIMU KATIKA KUNDI LA BONGOMAN KATIKA ALBAMU KADHAA ZIKIWEMO ZA "KWASA KWASA" NA "AMOUR FOU".
KANDA ALIWAHI KUZURU NCHI ZA ULAYA NA MAREKANI. JULAI 2005 ALIIMBA KATIKA ONESHO LA AFRIKA KATIKA CORNWALL.
KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA KENYA, ALIWASHANGAZA WAKAZI WA WAISHIO KATIKA ENEO LA MUMIAS MAGHARIBI MWA NCHI YA KENYA, ALIPOFIKA KATIKA KITUO KIMOJAWAPO CHA KUJAZIA MAFUTA.
KANDA BONGOMAN KUANZA KUHUDUMIA WATEJA WALIOFIKA NA VYOMBO VYAO VYA USAFIRI, IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 TANGU NCHI YA KENYA ILIPOPATA UHURU WAKE KUTOKA MIKONONI MWA WAKOLONI.
MTANDAO MMOJA NCHINI KENYA ULIANDIKWA KWAMBA BONGOMAN ALIWASHANGAZA WATEJA WENGI WALIOFIKA KUJAZA MAFUTA KATIKA KITUO HICHO, KUTOKANA NA UMAARUFU MKUBWA ALIOJIZOLEWA NA KUPENDWA NA WATU WARIKA MBALIMBALI.
MSANII HUYO ALIPATA NAFASI YA KUFUNGUKA KUHUSIANA NA TUKIO HILO KWA KUSEMA KWAMBA ALIKUWA NCHINI KENYA KWA ZIARA YA KIMUZIKI KATIKA MIJI YA BUNGOMA, KISUMU NA MIJI MBALIMBALI NCHINI HUMO.
AKIWA NCHINI HUMO KANDA ALIAMUA KUINGIA MTAANI KUSIKILIZA CHANGAMOTO MBALIMBALI WANAZOPATA MASHABIKI WAKE.
NYIMBO NYINGI ZA MKALI HUYO ALIZOTAMBA NAZO ZILIKUWA ZA IYOLE YA MWAKA1981, DJESSY YA1982, AMOUR FOU 1984, MALINGA YA 1986, LELA LELA MWAKA 1987, SAI NA LIZA ZA 1988, KWASSA KWASSA MWAKA 1989, NA ISAMBE NA INDE MONIE ZA 1990.
ZINZIGINE ZILIKUWA ZA ZING ZONG YA 1991, SANGO YA 1992, SOUKOUS KATIKA CENTRAL PARK MWAKA 1993 NA TAMU ALIYOFYATUA MWAKA 1995.
ALIACHIA VIBAO VINGINE VYA KARIBU AFRIKA KUSINI YA MWAKA 1995, FRANCOPHONIX YA1999, BALOBI 2002 NA SWALATI YA MWAKA 2003.
KANDA BONGOMAN ANA KIPAJI CHA KUWEZA KULITAWALA JUKWAA HUKU MASHABIKI WOTE HUFURAHIA BURUDANI KAMAMBE TOKA KWA NYOTA HUYO HASA KUPITIA MTINDO WAKE MAARUFU WA KWASAKWASA.
SAUTI YAKE NYORORO INAYOBEBA MASHAIRI MARIDHAWA KATIKA LUGHA YA KILINGALA NA KIFARANSA, ILIMFANYA KANDA BONGOMAN KUWA MIONGONI MWA WATUMBUIZAJI MACHACHARI BARANI AFRIKA.
KATIKA KUUELEZEA WASIFU WAKE, YAELEZWA KWAMBA ALPOKUWA MWANAFUNZI ALIPANDWA NA MZUKA KATIKA MUZIKI NA KUMFANYA NYOTA HUYO ‘AKUKACHA SHULE’.
AKIWA NA UMRI WA MIAKA 18, TAYARI KANDA ALISHAAMUA KUACHANA NA MASOMO NA KUJIUNGA NA BENDI ZA MTAANI ILI KUTIMIZA NDOTO YAKE YA KUWA MWANAMUZIKI.
ALIFANYA HIVYO ILI KUINGIA KWENYE TASNIA HIYO YA MUZIKI AMBAYO ALIAMINI ILIKUWA IMO NDANI YA MOYO WAKE.
PAMOJA NA KUWA BONGOMAN ALIFAHAMIKA ZAIDI MWANZONI MWA MIAKA YA 1980, ALIVUTIWA ZAIDI NA UTUNZI NA UIMBAJI WA MWANAMUZIKI TABU LEY.
AKAJARIBU KILA NJIA ILI SIKU MOJA NAYE AWE NA JINA KUBWA KWENYE RAMANI YA MUZIKI JAMBO AMBALO LILIFANIKIWA.
ALIAMUA KUJITOA NA KUANZA KUFANYA KAZI ZAKE KAMA MWANAMUZIKI WA KUJITEGEMEA AKIAMINI KUWA IPO ANGELIFANIKIWA KUFIKIA MALENGO YAKE.
HAIKUMCHUKUA MUDA MREFU KWANI MWAKA 1981, ALIWEZA KUKAMILISHA ALBAMU YAKE YA KWANZA ILIYOITWA 'IYOLE' AMBAYO ALIREKODI KWA KUMSHIRIKISHA MCHARAZA GITAA MAHIRI DIBLO DIBALA.
HUO NDIYO UKAWA MWANZO WA MWANAMUZIKI HUYU KUJITENGENEZEA UMAARUFU MKUBWA HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO NA BARA ZIMA LA AFRIKA KWA UJUMLA.
KANDA BONGOMAN HIVI SASA YAELEZWA KUWA AMEACHANA NA MASWALA MAZIMA YA MUZIKI, ANAFANYA SHUGHULI ZAKE ZINGINE.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment