KUTANA NA MAWNAMKE JASIRI ASHA BARAKA.
Na: Kiyungi Moshy.
January
20, 2013
Asha
Baraka ni mwanamke wa mfano wa kuingwa kwa ujasiri mkubwa, asiyesita kujaribu
na hatimaye kufanikiwa.
Mama huyu
ana vipaji lukuki ambavyo kwa kauli yake anasema vingine bado hajavionyesha.
Baadhi ya
vipaji vyake hivyo vilianza kujitokeza akiwa katika shule ya Sekondari ya
Tabora Girls alipokuwa katika mchezo mpira wa Pete na kikapu, iliyomfikisha
kuchaguliwa timu ya shule.
Kwa
uhodari wake katika michezo hiyo Asha baadaye alichaguliwa kuwa mmoja kati ya
wanafunzi waliounda timu ya UMISETA mkoani Tabora.
Akiieleza
historia ya maisha yake, Asha amesema
alizaliwa katika kijiji cha Mwandiga, kilichopo katika Wilaya Kigoma Vijijini ,
Mkoani Kigoma.
Masomo
yake ya msingi aliyapata katika shule mbili tofauti. Darasa la kwanza hadi la
tatu alisoma katika Shule ya msingi Kipampa iliyopo Ujiji, mjini Kigoma.
Baba yake
Mzee Ramadhani Baraka alikuwa Daktari hivyo alihamishwa kwenda kufanya kazi katika
hospitali nyingine ya Nguruka, mkoani humo.
Asha alilazimika
kuandamana na wazazi wake kwenda Nguruka, akiwemo mama yake mzazi, maliyemtaja
kwa jina maarufu la Mama Ali Baraka.
Alisoma
katika shule ya msingi Nguruka darasa la nne hadi alipofanya mtihani wa kumaliza
elimu ya msingi.
Asha Baraka
alikuwa ‘Kichwa’ kweli kweli darasani, alifaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa
kwenda kusoma katika Sekondari ya vipaji maalumu ya Tabora Girls, iliyopo mkoani
Tabora.
Akiwa
shuleni hapo alicheza mpira wa pete na kikapu hatimaye alichaguliwa kuwakilisha
mkoa wa Tabora, akiwa katika timu ya
mpira wa Pete.
Licha ya
kucheza mchezo wa Pete na kikapu, Asha
Baraka alikuwa mwanariadha mashuhuri akikimbia mbio za mita 100, na kuwa kati ya mwanamichezo bora shuleni
hapo.
Alipomaliza
masomo ya Sekondari mwanzoni mwa miaka ya 1980, aliajirawa katika Shirika la
Bima la Taifa (NIC) la jijini Dar es Salaam katika Idara ya mauzo na masoko.
Asha
Baraka ni mama mwenye familiya ya mume na watoto wawili wa kiume. Anawataja kwa majina kuwa ni Mope mwenye umri
wa miaka 18, ambaye ansema amefuata
nyayo zake za uhezaji wa mpira wa kikapu
Alichaguliwa katika timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18. Mwingine ni Imani mwenye umri wa miaka 14, ambaye ni mwanafunzi katika shule ya Sekondari ya Bearden Paul, iliyopo Wilaya ya Bagamoyo.
Asha
licha ya majukumu yake ya kazi, pia alikuwa akijishughulisha kibiashara kwa kuongoza
kundi la vijana waisopungua 45, katika bendi ya African Stars ‘ Twanga Pepeta’
Nikukumbushe
kwamba enzi za miaka ya nyuma kulikuwa
na mipango mzuri ambapo mashirika mengi ya umma yalikuwa na timu za mpira wa
miguu,wavu, kikapu, pete hadi bendi za
muziki wa dansi.
Shirika
la Bima la Taifa lilikuwa mojawapo ambalo lilikuwa natimu ya mpira wa pete
halakadharika ilikuwa na bendi ya Bima Lee Orchestra.
Alicheza
mpira wa pete na kikapu katika timu ya Bima pia lichaguliwa katika timu ya wilaya hadi ya mkoa wa Dar es Salaam.
Kipaji kigine
cha mwana mama huyo ni kile cha kuchaguliwa katika timu ya ya taifa ya riadha,
akikimbia mbio za mita 100, kabla ya kuchujwa wakiwa kambini jijini Arusha.
“ Siwezi
kumshau Juma Ikangaa ambaye aliniletea viatu mahsusi kwa ajili ya kukimbilia (Sparks) toa Japan. Kabla ya hapo, nilikuwa
ninakimbia nikiwa na viatu vya raba” anasema Asha Baraka.
Anatolea
mfano wa mwanariadha wa zamani ambaye aliyepata mafanikio makubwa licha ya kutokuwa
na zana, Mwinga Mwanjala. Mwanjala alishinda mashindano ya kitaifa ikikimbia
bila viatu ‘Pekupeku’
Asha anatanabaisha
kwamba hata kuchaguliwa kwake kukimbiza mwenge wa Olympic haukufanyika kwa upendeleo,
anasema yeye ni mwanariadha wa siku nyingi mwenye rekodi kitaifa.
Kama nilivyokueleza
hapo awali kuwa Asha ana vipaji vingi mno, alionyesha maajabu baada ya kuendesha
gari akiwa na umri mdogo wa miaka 14, wakati huo alikuwa kidato cha pili hapo
Tabora Girls.
Anaeleza
kwamba hata alipoanza kazi Shirika la Bima, watu wengi wakiwemo wafanyakazi wenzake,
walikuwa wakimshangaa kumuona binti mdogo
wakati huo akiendesha ‘mkoko’
kuja kazini.
Mama Asha
kupitia uzoefu wake wa muda mrefu wa kuendesha magari, aliwahi kupatwa na
shauku ya kushindana katika mbio za magari hapa Tanzania. Asha alikosa gari maalumu
la mashindano hayo, licha ya kufanya mazoezi makali kupitia maeneo mbalimbali hadi
Chalinze.
“
Nilikuwa napenda sana kuendesha magari, nilifanya mazoezi ya
kushindana nikapitia maeneo mengi hadi Chalinze. Anajisifu Asha Baraka.
Analisema
kwamba Pamoja na kukosa gari, alijichomeka katika katika gari la wasindikizaji na kuweza
kuzunguka toka mwanzo wa safari hadi mwisho wa mashindano hayo.
Ujasiri
wa mama Asha ulionekana mwaka 2010, baada ya kuacha kazi yake nzuri katika Shirika
la Bima la Taifa (NIC) na kuamua
kujikita katika Biashara na Siasa.
Shirika
la Bima la Taifa mwaka 2000, liliwataka waajiriwa wote kuomba kazi upya. Japo yeye alikuwa nje ya mji
kikazi wakati huo, lakini aliporejea hakutaka kuendelea na kazi, hivyo akaamua kutoandika barua ya maombi ya kazi hatimaye akacha kazi rasmi 2010.
Asha baada ya kuacha kazi Shirika la Bima la Taifa
(NIC) aliamua kujikita katika Biashara na Siasa.
Kwa
upande Siasa, Asha Baraka hivi sasa ni mjume wa National Executive Committee (NEC)
kupitia wilaya mpya ya Uvinza, iliyopo mkoani Kigoma.
Anajuvunia
kuwa karibu na wanamuziki wake wa African Stars, wana ‘Twanga Pepeta’ kwa kuwa anapata muda wa kuzungumza na kuelewa
matatizo yanayoikabiri bendi sanjari kujua mafanikio.
Historia
inaeleza kwamba kabla ya kuwa kampuni African Stars Entertainment Tanzania
(ASET), kulikuwa na bendi ya African
Stars iliyoanza mnamo tarehe 01 July 1994, katika Hoteli ya Bahari
Beach jijini Dar es
Salaam. Baadaye bendi za M.K.Group, M.K. Beat na M.K. Sound zikaanzishwa na Alli Baraka, aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Zambia (Zambia Airways) baadaye akawachia uongozi Msilwa Baraka, aliyekuwa kwa Mwenyekiti na Asha Baraka akawa Mkurugenzi Mtendaji.
Kampuni
ya African Stars Entertaiment Tanzania (ASET) iliyoasisiwa mwaka 2000 na yeye kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo.
Anasema
ASET ni mithiri ya Chuo ambacho kinatengeneza vipaji kwa vijana kisha kuwaruhusu kwenda popote wanapohitajika pasipo mashrti.
“Tuna Academy ya kuendeleza vipaji vya vijana, inayoitwa
Twanga Pepeta Acade Asha ni Mkurugenzi wa kampuni ya African
Stars Entertainment Tanzania (ASET) ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2000 jijini
Dar es Salaam.
my. Vijana
hao hupewa nafasi ya kupiga muziki siku za Jumamosi pale Mango Garden,
kabla ya African Stars wana ‘Twanga
Pepeta’ kupanda jukwaani” Anasema
mkurugenzi huyo wa ASET.
Akiyaelezea mafanikio
katika kampuni yake ya ASET, Asha
anasema ni makubwa sana
licha ya kwa kuwa wana Academy na pia ina wanamuziki wa kuingia na kutoka
wapatao 45. Vilevile wamekwisha tunukiwa tuzo kibao zikiwemo za BBC, BASATA,
ile Mascut huko Arabuni ambako
kulifanyika festival. ASET imekuwa mstari
wa mbele kuisaidia jamii katika matatizo mbalimbali ya kijamii.Mojawapo ni lile la Asha kuandaa onyesho maalumu la muziki ambalo pesa zilizopatika hapo, alizikabidhi kwa mwanamuziki mkongwe Maalim Gurumo ambaye hali yake ya kiafya bado ni tete.
Mwaka 2000 wakati wa shindano la Tanzania Musical Awards, The African Stars Band ilifanikiwa kuwa bendi bora ya mwaka kwa mwaka 2000/2002 na wimbo wa Kisa cha Mpemba ukawa ndiyo mwibo bora namba mbili.
Asha Baraka alimalizia kwa kuwataka wanasanii wa tasnia zote kuzingatia upendo na nidhamu ambayo kwake yeye anaona kuwa ndiyo nguzo kuu kwa mafanikio ya msanii.
Mwisho.
Mwanadishi wa makala hii anapatikana kwa:
0713331200, 0784331200, 0767331200 na 0773331200
m_kiyungi@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment