MBILIA BELL
‘ALIKATAA KUOLEWA NA WAZIRI’
Na: Kiyungi
Moshy.
MBILIA BELL ni mwanamuziki alinyeonyesha
ujasiri kwa kukataa kuolewa na Waziri katika serikali ya nchi ya Gabon
huko Afrika ya Kati, aliyempa sharti la kuacha muziki ili
amuoe.
Bell ni mama aliyejaaliwa
kuwa sura, umbo lililojengeka lenye mvuto,
sauti nzuri ya uimbaji na hata uchezaji wake katika jukwaa.
Ni mwanamuziki mwenye sifa
adimu ambazo pengine yawezekana zisisifikiwe na mwanamke mwingine.
Sifa nyingine kubwa aliyonayo
mwama mama huyo ni kwa aliolewa na mwanamuziki nguli Tabu Ley na ndoa yao ya kifahari
iliyofungwa ndani ya ndege wakiwa hewani.
Jina lake halisi ni Marikirala Mboyo, ambaye kama walivyo watoto
wengine wa kiafrika wafikiapo umri wa miaka minane, hukaa na wazazi, Babu au nyanya zao na
kulazimishwa kusikiliza hadithi pia kuimba nyimbo za asili inayowazunguuka.
M’bilia alikuwa mmoja wa hao baada ya kuvutiwa na sauti ya babu
yake ambaye alikuwa bingwa wa kuimba, wakati Bibi yake alikuwa mchezaji wa ngoma
asiyeshindwa kijijini humo.
Marikirala M’bilia alizaliwa mwaka 1959 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 17 akiwa na mkongwe Abeti Massekini mwaka 1976.
Marikirala M’bilia alizaliwa mwaka 1959 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 17 akiwa na mkongwe Abeti Massekini mwaka 1976.
Akiielezea historia yake Bell anasema alianza kupenda muziki baada
ya kuangalia katika televisheni na kumuona mwanamuziki nyota toka nchi ya Togo, Bela Bello, ailiyekuwa akifanya onyesho
katika mji wa Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Anasema alivutiwa na kipaji cha mwanamuziki huyo na kutamani siku
moja aje kuwa kama Bello.
Ansema siku aliyosikia kwamba amefariki, alilia kwa siku kadhaa.
Baada ya siku saba kupita, akiangalia televisheni, alimuona mwanamuziki
mwingine AbÈti Massekini. Baadaye akaamua kumuandikia barua Abeti ya kuomba
kujiunga na bendi yake. Alishangazwa kuona Abeti alipomualika kujianga naye. Hapo ndipo historia katika muziki wake ilipoanzaia.
Alijifunza kuimba akiwa karibu na Abeti kwa kipindi cha miaka minne.
M’bilia baada ya kujiamini amefuzu, aliondoka kwa AbÈti na kwenda kuungana na Sam Mangwana, ambaye
aliwasiliana naye baada ya kumuona
katika televisheni akifanya vitu vyake. Lakini
huko nako hukukaa sana
kwani baada ya miaka miwili aliondoka na kujiunga na gwiji la muziki Afrika
Tabu Ley Rochereau mwaka
1981.
Bell alipatwa na mshituko siku aliyokutana na kiongozi wa bendi ya
Afrisa International Tabu Ley, akiwa na uso wa furaha katika mahojiano kwa njia
ya televisheni.
Ley alimwambia kwamba hana mabilioni ya kumpatia lakini kama wakifanya kazi pamoja hatajuta kamwe.
M’bilia alitumia mwanya huo akajiunga na bendi ya Afrisa Internationale
na ukizingatia sauti yake nyororo, uchezaji wake kupitia maungo yake
yaliyojengeka kipekee, kwa kipindi kifupi M’bilia akawa gumzo katika jiji la Kinshasa. Juhudi zake hizo
zilipelekea bendi hiyo kuongeza mapato kwa mauzo ya rekodi zao.
Yaelezwa kwamba M’bilia Bell na Tabu Ley Rochereau walifunga ndoa kabambe
ya kifahari wakiwa ndani ya ndege hewani. Katika maisha yao
ya ndoa walifanikiwa kupata mtoto mmoja
wa kike aitwaye Melodie Tabu, ambaye anasoma katika jiji la Paris na kufanya muziki na Baba yake.
M’bilia Bell anamuelezea Binti yake huyo kwamba anaongea kwa
ufasaha lugha ya kiingereza, na kwamba ni mwimbaji mzuri aliyefuata nyayo
za wazazi wake na tayari amemshirikisha katika
kuimba kwenye album yake mpya ya Belissimo.
Mwaka 1982 Bell alitoka na kibao
chake kiitwacho Mpeve ya Longo,
kikisimulia kisa cha mwanamke aliyetelekezwa na mumewe na kuachiwa watoto
awalee peke yake. Kibao ambacho kiligusa hisia na kuwa simulizi kila kona za
miji ya nchi hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(zamani Zaire).
M’bilia aliipenda nchi ya Kenya,
alipokuwa katika jiji la Nairobi
alilazimika kujifunza lugha ya Kiswahili na kuweza kuimba nyimbo kadhaa kwa lugha
hiyo.
Nyimbo zilizompatia chati M’bilia zalikuwa za Nakei Nairobi, Boya ye, Yamba ngay, Amour sans frantiere na Biu Mondo.
Mbilia aliimba nyimbo nyingine zaidi za Beyanga, Befosami, Faux Pas,Cadence Mudanda,
Motema na Napika. Nyimbo za Kuteleza si kuanguka, Faux Pas, Iyolela, Bafosami na Frontiere,. Zingine zilikuwa zaPhenomene,
Manzil manzil, Mbanda na Nga, Nadina, Mayaval, Eswii yo Wapi, Biu Mondo, Nelson
Mandela,Wende na Wende na nyingine zasizokuwa
na idadi zilimjengea heshima Mbilia Bell.
Karibia nyimbo zote alizoimba mwana mama huyo Bell akishirikiana na Rochereau hazichuji wala kukinai
kuziangalia runingani au kuzisikiliza redioni, hadi leo.
Mbilia Bell aliwahi kuja hapa Tanzania
akifuatana na mumewe Tabu Ley Rochereau
na
kundi zima la Afrisa Internationale Bell
alifanya kufuru katika maonyesho yao
yote waloyoandaliwa hapa nchini.
Akiwa katika jiji la Dar es Salaam Bell aliweza kulitawala
jukwaa mwanzo mwisho akitumia kuyachezesha maungo yake sanjari na uzuri wake, akawa
kivutio kikubwa.
Tabu Ley baadaye alimuongeza
mwimbaji mwingine wa kike ‘Faya Tess’ ambaye jina lake halisi
ni Kishila Ngoyi, akiwa na nia ya kuijenga vyema bendi yake. Lakini ujio wa Faya
Tess ulimfanya M’bilia kuamua kuiacha Afrisa Internationale na kuondoka kwenda
jiji la Paris
ambako alikutana na mwanamuziki wa sokous, mpiga gita Ringo ‘Star’ Bamundele
mwaka 1983.
Sababu kubwa za kuondoka
kwake ni kile kilichoelezwa kuwa wivu wa kimapenzi baina ya wana ndoa hao
ulioingilliwa na Faya Tess.
Mbilia Bell aliwahi kuishi nchini Gabon, ambayo inapakana na nchi yake ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alikataa kuolewa na Waziri mmoja katika serikali
ya nchi hiyo aliyempa sharti la kuacha muziki ili amuoe.
Anafurahia mafanikio yake na kujivunia kuwa yeye ni mmoja wa kati
ya wanafunzi wa Rochereau Tabu Ley ambaye alikuwa akimpa kipaumbele na
kuwa mwanafunzi bora katika shule yake.
Marikirala Mboyo M’bilia
anasema haikuwa kazi rahisi kukubalika kuwa mwanamuziki mwanamke wa kimataifa
katika maisha yake yote ya kazi za muziki. Watu wengi hawakuwa wakimuamini na kuichukulia kazi yake kwamba
haitakuwa endelevu.
Bell alikaririwa akisema kama
wao wanawake wanawaamini waume zao na wala hawawalazimishi kuacha kazi zao,
iweje wanaume wamfikirie yeye kila anapotikisa maungo yake kwamba huwa
anawavutia?
Alitoa wito kwa wanawake wenzake kuungana na kufanya wanaume
wawaone kwamba wao hawajirahisishi kama
wanavyofikiria.
Marikirala Mboyo ‘M’bilia’ akiwa na muda wa ziada huutumia kufanya
shghuli za kijamii zakiwa zile za kuwatembelea watoto wa mitaani, kurekebisha
vituo vya watoto hao na kugawa msaada wa vyakula na nguo.
Mwana mama huyo kwa kawaida huamka kila siku saa 12:00 asuhuhi na
kufanya maombi baadaye huenda kwenye
mazoenzi ya viungo. Anatoa siri ya kutochakaa mapema ni kuishi ukiwa na afya
njema, wala si kwa kula nyama na kunywa pombe.
Ratiba yake ya asubuhi ni glasi moja ya maziwa isiyokuwa na
mafuta, na glasi nyingine maji huwa ndiyo kifungua kinywa chake. Baada ya hapo
hutumia muda mwingi katika kuandika nyimbo zake na kuangalia sinema katika
televisheni.
Mbilia anasisitiza kwamba kazi ya muziki ni ya siku nzima na ni
gumu sana
hawezi kupata muda wa kutafuta kazi nyingine kwa kuwa hafikirii kuwa tajiri ila
ameridhika na hali aliyonayo.
Bell ana mpango wa
kuwahamsisha wanamuziki wa kike wa Afrika kuungana na wanamuziki wengine
kulilia amani.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment