GWIJI LA SAXOPHONE DIBANGO LATIMIZA MIAKA 79
January 09, 2013
GWIJI LA KUPULIZA SAXOPHONE MANU DIBANGO
jana Februari 10, 2013
alitimiza miaka 79 ya kuzalikwa kwake. Dibango ni mwanamuziki aliyejizolea sifa kubwa barani Afrika na
ulimwenguni kwa ujumla.
Jina lake halisi
ni Emmanuel Dibango ambaye pamoja na kupuliza chombo hicho cha Saxophone, pia
ni mtunzi na mwimbaji mahiri mwenye sauti nzito.
Manu Dibango ni kiongozi wa
bendi ya Makossa, aliyezaliwa February 10, 1934, katika mji wa Douala
nchini Cameroon
nchini Afrika ya Magharibi.
Baba yake alikuwa mfanyakazi
serikalini na vilevile alikuwa mtayaarishaji maarufu wa nguo.
Dibango alikuwa mmoja kati ya
waanzilishi muziki wa kidunia katika miaka ya 1970. Kwa mantiki hii ninafahamu vijana wa kizazi cha sasa
hawamfahamu ama hawakuwahi kusikia muziki wa nguli huyu. Yawezekana wengi wao
walikuwa bado kuzaliwa au walikuwa wadogo nyakati hizo akitamba Manu Dibango.
Kama kawaida ya wanamuziki
walio makini kwa kazi yao,
Manu ni miongoni mwao kwani alipiga ‘kitabu’ na kupata elimu yake katika shule
ya Baccalaureate nchini Ufaransa.Mwaka 1956.
Manu Dibango ni kiongozi wa
bendi ya Makossa, yaelezwa kwamba kati ya mwaka 1949 -1954 Dibango alichukua
masomo ya kupiga ala ya Piano na akanza kupiga muziki wa jazz. Alianza kupiga
muziki rasmi mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 20.
Emmanuel Dibango aligundulika kuwa ni mtu mwenye kipaji baada
ya kuonekana alivyokuwa akipenda muziki, toka alipokuwa bado mdogo akiwa
nyumbani na husan Kanisani ambako mama yake alikuwa kiongozi wa kwaya. Manu alifahamika sana katika nchi zote ambazo
zilitawaliwa na wafaransa huko Afrika ya Magharibi.
Ni mwanamuziki analiyejiwekea
kumbukumbu kwa wapenzi wa muziki kwa wimbo wake uliotamba wa ‘Supa Kumba’ ambao
alipipuliza saxophone huku akiimba kwa
kutumia sauti yake nzito iloyeleta mvuto wa aina yake miaka ya 1970.
Manu
alikuwa mmoja kati ya waanzilishi muziki wa kidunia katika miaka 1970, na
ameendelea kuhodhi hadhi ya kimataifa akiwa mwanamuziki wa kutegemewa katika
muziki wa kiafrika miaka ya 1990.
Mwaka
1994, Boston Globe ilimpendekeza kuwa mwanamuziki bora kwa kibao chake cha
‘Wakafrika’ alipokea tuzo hizo akiwa na Nyota wa wanamuziki toka Afrika na Ulaya akina, King Sunny Ade,
Ladysmith Black Mambazo, Peter Gabriel, and Sinead O'Connor.
Ingawa Manu Dibango amekuwa
akipingwa sana
kwa kutumia sauti za kigeni za Waafrika,Wazungu na Wamerekani lakini alikuwa na
msimamo madhubuti la kutetea alama yake katika muziki ‘Identity’
Muziki katika bendi yake ya Makossa
ulipanda chati ambapo ulionekana ni wa kisasa zaidi kwa watu wa Cameroon
huko Afrika ya Magharibi mwaka 1973,
baada ya kutoa album ya muziki wa Soul iitwayo Makossa.
Kama nilivyokujuza awali Dibango alipokuwa na umri wa
miaka 15 akiwa na familia yake walikwenda nchini Ufaransa na yeye akaingia
shule akisomea cheti cha Diploma.
Akiwa huko alisikia muziki wa
Jazz wa ki-marekani na alitamka furaha yake kumsikia kwa mara ya kwanza radioni
mwanamuziki Louis Armstrong.
Miaka ya 1940 Manu
Dibango ilielekeza nguvu zake katika upigaji wa chombo cha Saxophone
akikabwaga chombo ‘kilichomtoa’ cha Piano ambacho ndicho alikuwa akikitumia.
Mwishoni mwa miaka ya
1950 Dibango alihamia nchini katika jiji
la Brussels
nchini Ubelgiji.
Akiwa huko miaka ya 1960
makubaliano ya kupatikana kwa Uhuru wa nchi ya Kongo yalikuwa yamefikiwa.
Manu Dibango pia alipiga
muziki na wanamuziki wakongwe wa muziki katika Afrika waliokuwa wakiishi Ulaya
akiwemo Joseph Kabasele ‘Grand Kale’ ambaye alikuwa mwimbaji nyota toka nchi
ya Kongo.
Baada ya Kongo kupata uhuru
wake mwaka 1960 ikabadilishwa jina na kuwa Zaire.
Album yake ya
Independence Cha-Cha, ikaja kuwa moto kwa wapenzi wa muziki Afrika na
Ubelgiji hususan mji wa Brussels.
Mwaka 1961 Dibango alicheza
na kurekodi nyimbo zaidi ya 100 nchini
humo, akishirikiana na Joseph Kabasele
‘Grand Kalle’ katika bendi ya African Jazz hadi ilipofika mwaka 1963, ambapo
Dibango aliamua kurejea nyumbani kwao Cameroon baada ya kuiacha kwa
miaka 12.
Hata hivyo mwaka 1965
alilazimika kwenda Paris nchini Ufaransa ambako
wapenzi wa muziki wake wa Soul katika
jiji hilo
walimuhitaji. Huko Paris, akaanza kupiga muziki wa kimataifa akitumia Saxophone
yake.
Baada ya kupata mafanikio
makubwa Dibango alitoa album nyingi za muziki wa kiafrika akichanganya na wa
ule wa Jazz na Bleus.
Mwaka 1979 alijaribu kupiga
muziki wa reggae, na alirekodi na baadhi ya wanamuziki
wa kikundi cha The Wailers huko Jamaica. The Wailers ilikuwa ikimilikiwa na hayati Bob Marley.
Manu Dibango mwaka 1984 alifanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka 30
ya kupiga muziki, iliyowakutanisha wanamzuki wengine toka sehemu mbalimbali.
Mwanamuziki wa Ulaya Sinead O'Connor na Peter Gabriel waliungana
na wanamuziki nyota toka Afrika Youssou
N'Dour, King Sunny Ade, na Ladysmith Black Mambazo kurekodi na Manu Dibango katika album yake ya mwaka 1994
iliyojulikana kama ‘Wakafrika’
Nyimbo zingine zilizompa umaarufu zilikuwa Supa
Kumba aliyoitoa mwaka 1974 na
Africadelic ya 1975.
Zingine ni pamoja na Gone Clear, Island, ya mwaka
1979, Ambassador, Island ya mwaka 1981, Waka Juju na Sonodisc, 1982, O Boso, ya
mwaka 1971, Soma Loba, 1972, Soul Makossa, Atlantic,
1973, Super Kumba, 1974 na Africadelic ya
1975. Film scores L'herbe sauvage, Cote
d'Ivoire, 1976, Ceddo, Senegal na Le
prix de la liberte, Cameroon
za mwaka 1976.
Dibango alifytua vibao vingine vya With Sly (Dunbar and Robbie Shakespeare) Gone Clear, Island ya mwaka 1979, With Dunbar and Shakespeare Ambassador, Island ya 1981, Waka Juju, Sonodisc iliyotoka mwaka 1982, Soft and Sweet ya mwaka 1983 na Melodies Africans, Volumes 1 & 2, 1983. Manu Dibango ni mwenye kipaji ambacho kimefanya muziki wake kukubalika kimataifa kufuataia nimbo zake alizotunga na kuzipiga katika mataifa mbalimbali duniani. Mwaka 1984 aliachia nyimbo zingine za Abele Dance, RCA na mwaka uliofuatia 1985, Dibango akatoka na wimbo wa Electric Africa, Celluloid.
Kama vile hazitoshi Mzee mzima akaachia vibao vya Afrijazzy, Soul Paris ya mwaka 1986, Polysonic, iliyorekodiwa na Bird Productions mwaka
1990, na Live '91, FNAC Music, 1991. Mwaka 1994 akaja
na album ya Wakafrika ikiwa na nyimbo
nyingi zikiwemo za ‘ Soul Makossa,’ ‘Ca
Va Chouia,’ na ‘Biko’. Mzee mzima Manu Dibango akamalizi kazi kwa kutengeneza
wimbo wa Giant mwaka 1994.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment