KOFFI OLOMIDE MCHUMI ALIYEBOBEA KATIKA MUZIKI
Machi
12, 2013.
KOFFI OLOMIDE
ni mwanamuziki msomi ambaye ni kiongozi wa bendi ya 'Quartier Latin', aliyezaliwa siku ya Ijumaa August 13 1956, Kaskazini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Alipachikwa
jina bandia la ‘Antoine Makila Mabe' likiwa na maana ya 'damu mbaya ya Antony'.
Koffi ni mwenye asili wa nchi mbili za
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sierra Leone.
Alipokuwa bado kinda, Antoine Koffi Olomide alikulia katika mazingira ya kuridhisha japo katika familiya yao hakuwepo mwanamuziki. Alianza kupenda muziki baada ya kujihusisha na familiya ambayo ni ya watu wenye vipaji vya muziki, ambao walimpa ufahamu wa kutengeneza muziki. Jirani yao ndiye aliyegundua kipaji cha Koffi na akamtia moyo zaidi na akaanza kumfundisha kupiga gita.
Olomide
alianza kupenda muziki tangu akiwa mtoto lakini ndoto zake kubwa zilikuwa awe
mchezaji wa mipra wa miguu.
Alipoanza kupevuka akiwa na
umri wa mika 18, wakati huo akiwa
mwanafunzi kijana, alivutiwa sana
na usanii pamoja na muziki, ndipo alipoanza kutunga na kuimba nyimbo.
Koffi alikuwa mwanafunzi
mwenye uwezo mkubwa shuleni. Alifaulu masomo ya Sayansi na kupata cheti cha Diploma mwaka 1980.
Baadaye baba yake alimpeleka nchini Ufaransa
kusomea masomo ya juu ya Utawala wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Bordeaux Business.
Mwaka 1978 alirudi Kinshasa akitokea Paris akiwa na Digrii ya
Uchumi. Pamoja na masomo mengine yaliyompeleka huko, pia alijifunza kupiga gita
na kurekodi album yake ya kwanza iliyopewa jina la Ngounda.
Aliporejea Congo akajuinga katika bendi ya
Viva la muzika iliyokuwa ikongozwa na Papa Wemba. Hapo akaanza taratibu kurudisha hadhi ya mtindo wa
Soukous ambayo ilikuwa tayari imeporomoka na kupitwa na wakati.
Olomide kwa juhudi
zake alianzaisha mtindo mwingine wa ‘Tcha Tcho’ uliomuongezea umaarufu zaidi
ndani na nje Congo wakati huo.
Kunako miaka hiyo ya 1970,
Koffi alianza kujijengea umaarufu
miongoni wa jamii Wacongo kama mtunzi
na mwimbaji bora.
Wimbo wake Onia ulikuwa ndiyo
wa kwanza kuonyesha mafanikio.
Akiwa likizo Koffi alirekodi
nyimbo za 'Asso' na 'Princesse Ya
Senza' katika studio za Veve
huko Kinshasha. Tokea hapo
akashirkiana na wasanii wengine nguli akiwemo
Papa Wemba na bendi ya Zaiko
Langa Langa. Koffi alitangazwa na
kuzawadiwa kama msanii bora wa Congo
mwaka 1978 kwa wimbo wake wa 'Aniba'
Rekodi yake ya kwanza ya 'Ngouda' alionesha juhudi zake na matarajio ya kupelekea nguvu zake katika kupiga muziki wa Kiafrika.
Rekodi yake ya kwanza ya 'Ngouda' alionesha juhudi zake na matarajio ya kupelekea nguvu zake katika kupiga muziki wa Kiafrika.
Alifanya kazi nyingine
akiwashirikisha wanamuziki wengine akina
Yakimi Kiesse na Fafa toka bendi ya
Molokai.
Mwaka 1986 Koffi Olomide alianzisha kundi la 'Quartier Latin', wakati huo huo alikuwa
akivutiwa sana
kundi la wanamuziki wa Kassav. Baada ya
miaka 10 ya mafaniko yake, akatamani
kuwa mwanamuziki wa Kimataifa.
Ilichukua kipindi kirefu akisubiri kuwa
mwanamuziki wa Kimataifa hadi ilipofika mwaka 1988, wimbo wa 'Henriquet'
ukatokea kuwa mkali uliopelekea kupachikwa jina bandia la ‘Golden Star'.Koffi Olomide aliyafurahia mafanikio zaidi baada ya kuandika wimbo akiwa na Binti yake pekee Minou, ukiitwa d 'Elle et Moi', Miaka 1990.
Koffi toka mwaka 1990 hadi 1994, alifurahia kukua kwa mafaniko yake ambayo kwa kipindi cha miaka chini ya minne, alifyatua zaidi ya album saba zikiwa chini ya jina lake na kundi lake la 'Quartier Latin'.
Mwaka 1992 Olomide alichaguliwa kuwa mwimbaji bora wa kiume na mshindi wa Video bora katika shindano la African Music Awards mjini Abidjan, Ivory Coast.
Koffi aliwahi kushiriki katika projekti ya muziki
wa Africando, pia aliwahi kushinda zawadi nne za Kora huko Afrika ya Kusini.
Vilevile alikuwa msanii bora katika nchi za Afrika ya kati.
Koffi Olomide alikwisha fyatua album nyingi
zilizojaa nyimbo za Attent, Adrada, Hero
National, Julia, Kisanola, Loin na Magie.
Alitoka na vibao vingine vya Micko, Motoromo, Number One, Oprphelina, Papa Bonheur,
Respect, Riziki, Rond Point na Ultimatum.
Koffi ni hodari wa kutunga na kuimba nyimbo kwani baadaye tena akafyatua nyimbo
za Stila, Sex pop, Shela Mbutu Solei Vanga, Zaiton, Esakola wimbo ambao alishirikiana na Papa
Wemba. Zingine ni za Titian Mbwiya, Nobles Oblige, Papa plus, Pharmacien, Force
de Frappe, Destination, Elle et moi , African King na nyingine nyingi.
Koffi Olomide kuna wakati alikimbiwa na wanamuziki
takribani wote, wakaenda kuunda bendi yao ya 'Quartier Latin Academia’ iliyokuwa ikiongozwa na
Suzuki 4 by 4.
Faida ya kufanya
muziki ukiwa msomi ilijionyesha kwa Koffi Olomide ambaye hakuteteleka kabisa.
Baada ya tukio hilo,
aliibua wanamuziki wengine vijana wenye vipaji toka sehemu mbalimbali nchini
humo, wanayo iimarisha bendi yake hadi
sasa.
Olomide ni
baba wa familiya ya mke na watoto watano.
Agosti 13, 2013,
Koffi Antonie Olomide atatimiza miaka 57
ya kuzaliwa kwake.
Mungu amuongezee maisha marefu, Amina.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment