MIAKA 14 BAADA YA KIFO CHA PEPE KALLE.
Novemba 26, 2012
Kesho
kutwa Jumatano Novemba 28, 2012, ndugu, jamaa na wapenzi wa muziki wa dansi Afrika
Mashariki, Kati, Magharibi na Ulimwenguni kwa ujumla, itakuwa ni siku ya majonzi
tukiomboleza miaka 14 toka kifo cha mwanamuziki Pepe Kalle aliyefariki Novemba
28, 1998 kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 47.
Jitu la
miraba minne Pepe Kalle baada ya
kuzaliwa Novemba 30, 1951 katika Jiji la Kinshasa
huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo alipewa
jina Kabasele Yampanya.
Alikuwa
mtunzi, mwimbaji wa muziki wa soukous na kiongozi wa bendi ya Empire Bakuba. Umbo
lake kubwa lilikuwa limebeba uzito wa Kilo
136 na urefu wake ulikuwa Sentimeta 190
ambazo ni sawa na Futi Sita na Inchi tatu.
Pepe Kale
alikuwa bingwa wa miondoko ya soukous na kiongozi wa bendi ya Empire Bakuba, ambayo
ilikuwa maarufu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Sauti yake nyembamba iliyokuwa na uwezo mkubwa
wa kughani, alikuwa anauwezo mkuwa wa kucheza jukwaani akitikisa umbo lake licha
ya kuwa na uzito mkubwa.
Watanzania
wengi tutaendelea kumkumbuka mwanamuziki huyu hasa wakati alipokuja nchini
mwetu na kutikisa majiji ya Arusha, Dar es Salam na Mbeya.
Wakati wa
ujio wake hapa Tanzania, Pepe Kalle ambaye sauti yake ilikuwa nyembemba na
nyororo, alifuatana na wanamuziki akiwemo
mipiga wa gita la besi Lofombo na waimbaji akina Papy Tax, Dilu Dilumona na Djo
Djo Ikomo.
Rapa wake
mahiri na kiongozi wa wacheza Shoo
Bileku Mpasi na mbilikimo wawili Emoro
na Jolly Bebbe walitoa burudani tosha kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam mwaka 1991. Mwaka
uliofuatia wa 1992, Emoro alifariki
dunia akiwa na bendi yake nje ya nchi kwa safari za kikazi ya muziki.
‘Kizuri
huigwa’ usemi huo ulijionyesha dhahiri baada ya msanii mmoja aliyejulikana kwa
jina la Kokoriko, kuweza kuiga miondoko ya uchezaji wa Bileku Mpasi. Msanii
huyo alipachikwa jina la Bileku Mpasi wa Tanzania.
Pepe
wakati wa uhai wake alirekodi nyimbo zaidi wa 300 na kufyautua album 20 katika
miongo miwili ya muziki wake na alijulikana kama
‘Tembo wa Afrika’.
Historia
yake katika muziki inaeleza kwamba alianza muziki rasmi katika bendi ya Afrikan Jazz ya Baba yake mzazi Joseph Kabasele ‘Grand Kalle’ aliyemtengeneza mwanaye huyo.
Baada ya
kukomaa kimuziki akatimka na kwenda kujiunga na bendi ya Lipua Lipua iliyokuwa
ikimilikiwa na Kiamunagana Mateta Wanzo
la Mbonga ‘Verkeis’
Akipotua
Lipua Lipua, haikuchukua kipindi kirefu akafanywa kuwa mwimbaji kiongozi akishirikiana na mwimbaji wengine Nyboma
Mwandido.
Safari
yake katika muziki haikuishia hapo kwani mwaka 1973 Pepe kale akiwa na Dilu Dilumona na Papy Tax
waliondoka katika bendi hiyo ya na
kuunda bendi yao
iliyopewa jina la Empire Bakuba.
Jina la Empire
Bakuba lilitokana na mashujaa wapiganaji wa makabila ya Kongo.
Katika miaka
hiyo ya 1970 Empire Bakuba na Zaiko Langa Langa ndizo zilikuwa zakitikisa jiji
la Kinshasa
vilivyo na kujizolea umaarufu mkubwa kwa wapenzi wa muziki wa dansi.
Vibao vya
Dadou cha Pepe Kalle na Sango ya Mwa ya Papy Tex, iliiweka Empire Bakuba kwenye chati na
ikaanzisha mtindo wa Kwasakwasa.
Mwaka
1982 yalipofanyika maadhimisho ya miaka kumi ya bendi hiyo, Empire Bakuba
ilipigiwa kura na ikashinda kuwa bendi bora huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo zamani Zaire.
Miaka ya
1980 Bakuba ilijizolea wapenzi na mashabiki lukuki
ikishirikiana na Nyboma Mwandido kurekodi
wimbo wa Moyibi mwaka 1988 wimbo ambao uliiongeza bendi hiyo
umaarufu katika
nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa huko Afrika ya Kati na Magharibi.
Album ya Roger
Milla iliyokuwa ikimuenzi na kumsifia mchezaji wa mpira wa miguu Roger Milla
ambaye alichezea timu yake ya taifa ya Cameroon akiwa na umri mkubwa
kuliko wote mwaka 1990.
Miaka ya
1990 Pepe Kale alitoa album zingine za Gigant Afrique Lager than Life na
Cocktail. Nyimbo zingine zilikuwa za Hidaya, Sintia, Reovisie, Guy guy na Yanga Afrika. Nyimbo
zingine zilizotikisa masikio ya wapenzi zilikuwa La- rhumba,Don’t Cry Yaja, Zouke Zouke Nakutuna na Pon moun Paka
Buoge.
Empire Bakuba ilifanya
ziara sehemu mbalimbali za nchi hiyo ya Kongo (DRC) na hata nje ya nchi hiyo.
Kama wanamuziki wengine Pepe Kalle ailiwashirikisha wanamuziki
wengine wakongwe katika tasnia ya muziki akina Simaro Lutumba na Nyoka Longo.
Bendi ya
hiyo ya Empire Bakuba ilitoweka katika sura muziki baada ya kifo cha kiongozi
wake Pepe Kalle.
Watanzania
tutaendelea kumukumbuka Pepe Kalle ambaye alipotua Tanzania, ilitunga nyimbo
kupitia lugha ya Kiswahili, za Yanga Afrika, akisifia Klabu ya Yanga iliyokuwa ikitajwa mfadhili wa klabu hiyo Abbas
Gulamali, Hidaya, wimbo alioimba akilalamika kupoteza mkanda wake wa kiuno na mpenzi Bupe, aliutunga alipotoka jijini la
Mbeya kufanya onyesho.
Mwisho.
Mungu aiweke roho yake pahala pema peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment