TABU LEY
ROCHEREAU ATIMIZA MIAKA 72.
Novemba 20, 2012
TABU LEY
ROCHEREAU ni mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki ambaye mwezi huu wa Novemba amesherehekea miaka 72 ya
kuzaliwa kwake.
Jina lake halisi ni Pascal Sinyamwe Tabu. Ni
kiongozi wa bendi ya Orchestra Afrisa
International aloyoiunda mwaka 1970 na ni mmoja kati ya waafrika maarufu kwa utunzi, uimbaji na kuandika nyimbo amabye amejijengea
umashuhuri Afrika.
Tabu Ley Rochereau ni
mwanamuziki mwenye historia ndefu katika tasnia hiyo aliyezaliwa Novemba 13,
1940 huko Bandundu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC)
Kwa kushirikiana na mpiga
gitaa Dr. Nico Kasanda waliasisi muziki wa Soukous ambao uliwafurahisha
waafrika kwa muda wa miongo minne, wakiutangaza muziki huo kimataifa kwa
kuunganisha muziki wa asili ya Kongo na Cuba, Caribbean na Rumba ya Latin
Amerika.
Mwaka 1954 akiwa na umri wa
miaka 14, Tabu Ley aliandika wimbo wake wa kwanza ulioitwa Bessama Muchacha
aliourekodi na Bendi ya African Jazz ya Joseph Kabasele (Grand Kale) na baada
ya kumaliza elimu ya juu alijiunga na bendi hiyo kama
mwanamuziki kamili.
Tabu Ley aliimba wimbo wa
kupigania uhuru wa watu weusi ulioitwa ‘cha cha’ ambao ulitungwa na Joseph
Kabasele ‘Grand Kale’ kipindi Kongo ilipopata uhuru mwaka 1960, wimbo ambao ulipelekea
yeye kupata umaarufu mkubwa.
Alibakia na bendi ya African Jazz
mpaka mwaka 1963 wakati yeye na
Dr. Nico Kasanda walipounda kundi lao lililoitwa
African Fiesta.
Miaka miwili baadaye Tabu Ley
na Dr.
Nico walitengana na Tabu Ley aliunda
kundi lake lililoitwa
African Fiesta Nationale pia bendi hiyo lilifahamika kama
African Fiesta Flash. Kundi hilo
lilikuwa na mafanikio kwa kuongoza mauzo katika historia ya Afrika.
Mwaka 1970 Alirekodi wimbo
uliokuwa umeshika chati za juu za
kiafrika uliojulikana kama Afrika
Mokili Mobimba na uliuza zaidi ya nakala milioni moja. Mzee huyo alifyatua
nyimbo zingine kali za Ibragimu, Sukaina, Ponce Pilate, Cadance Mudinda na Boya
Ye. Zingine zilikuwa Mbanda ya Ngai, Maze,Nzale, Sima Mambo Revens Itou,
Nalingi yo Linga, Nadina na nyingine
nyingi.
Papa Wemba na Sam Mangwana
walikuwa ni miongoni mwa wasanii maarufu wa muziki wa kiafrika ambao walikuwa
sehemu ya kundi hilo.
Sambamba na kundi la Franco
Luambo Lwanzo Makiadi lililoitwa T.P.OK. Jazz, kundi la Afrisa lilikuwa moja ya
kundi kubwa la kifrika. Walirekodi
nyimbo kama vile Sorozo, Kaful Mayay, Aon Aon
na Mose Konzo.
Katikati ya miaka ya 1980
Tabu ley alivumbua vipaji vya waimbaji na wachezaji, Mbilia bel aliyesaidia
kuipa bendi yake umaarufu zaidi. Mbilia Bel alikuwa muimbaji wa kwanza wa kike wa muziki wa
Soukous na kukaribishwa kwa shangwe Africa
nzima. Baadaye Tabu ley Na M’bilia Bel walioana harusi yao ilifungwa ndani ya ndege wakiwa hewani na
baadaye wakafanikiwa kupata mtoto mmoja aitwaye Melodie.
Mnamo mwaka 1988 Ley alimtambulisha mwimbaji
mwingine wa kike Faya Tess. Lakini baada ya ujio wa Tess katika bendi hiyo
kulimfanya M’bilia kuondoka kwa kile kilichoelezwa kuwa wivu wa
kimapenzi baina wana ndoa hao ulioingilliwa na Faya Tess.
Mara baada ya Mbilia Bell
kujitoa katia kundi la Afrisa Intrenationale
pamoja na upinzani wa mkubwa na kundi la T.P.OK. Jazz, Bell aliendelea kupoteza umaarufu.
Mwanzoni mwa miaka ya 1990 Tabu Ley aliishi Kusini mwa
Califonia na alianza kurekebisha muziki wake uendane na mashabiki wa kimataifa
kwa kuingiza lugha ya Kiingereza katika mashairi yake. Alifyatua Albamu za Muzina, Exil Ley,
Africa Worldwide na Babeti Soukous.
Alipata mafanikio kwa kutoa albamu kama vile Muzina,
Exile Ley, Africa worldwide na Babeti soukous.
Mwaka 1996 Tabu ley
alishiriki katika albamu ya Gombo Salsa iliyotengenezwa na Salsa Music Project
Africando. Wimbo uliojulikana kwa jina la ‘Paquita’ kutoka katika albamu hiyo ikiwa
ni toleo jipya alioimba mwishoni mwa miaka ya 1960 katika bendi ya African
Fiesta ulishika chati katika medani ya muziki.
Salsa akiwa na bendi ya Africando.
Salsa akiwa na bendi ya Africando.
Mwishoni mwa miaka ya 1990
Rais Mabutu Sese Seko Kuku Ng’endu Wazabanga alipoondolewa madarakani, Tabu ley
alirudi Kinshasa
na alipewa nafasi ya uwaziri katika Baraza la mawaziri katika Serikali mpya ya
Rais Laurent Kabila.
Kufuatia kifo cha Laurent Kabila Tabu Ley aliendelea na
Wadhifa huo chini ya Rais Joseph Kabila.
Tabu Ley hali yake ki-afya si nzuri
akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment