Saturday, October 10, 2015

BENDI YA MLIMANI PARK ILIVYOLITEKA JIJI LA DAR ES SALAAM



BENDI YA MLIMANI PARK ILIVYOLITEKA JIJI LA DAR ES SALAAM

KWA KAWAIDA HISTORIA YA JAMBO LOLOTE HUWA HAIFUTIKI. HISTORIA YA BENDI YA MLIMANI PARK ORCHESTRA INAELEZA KUWA MWANAMUZIKI MWANZILISHI WA BENDI HIYO ALIKUWA ABEL BARTAZAR ALIYEUNGANA NA WANAMUZIKI WANANE WALIOIHAMA BENDI YA DAR INTERNATIONAL WAKAENDA KUIJENGA VILIVYO MLIMANI PARK ORCHESTRA  MWAKA 1978.

WANAMUZIKI HAO NI PAMOJA NA ALIYEKUWA MTAALAMU WA KUPIGA ALA ZOTE ZA MUZIKI, MICHAEL ENOCK ‘KING’, JOSEPH BENARD, JOSEPH MULENGA, ABDALAH GAMA, COSMAS CHIDUMULE, MACHAKU SALUM NA HABIB JEFF. 

BENDI YA MLIMANI PARK ORCHESTRA ILIKUWA CHINI YA UONGOZI WA TANZANIA TRANSPORT AND TAX SERVICES (TTTS), IKIWA NA MASKANI YAKE PALE MLIMANI CLUB MITAA YA MWENGE JIJINI DAR ES SALAAM.

MLIMANI BAADAE MWAKA 1983, ILICHUKULIWA KUWA CHINI YA SHIRIKA LA MAENDELEO YA DAR ES SALAAM (DDC), BAADA YA  WALIOKUWA WAMILIKI TTTS  KUFILISIKA.

BENDI HIYO IKAANZA KUITWA KWA JINA LA DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA IKIWA CHINI YA WANAMUZIKI WAASISI, MUHIDIN MAALIM GURUMO, ABEL BALTAZAR, HASSAN REHANI BITCHUKA, AMBAO WALITOKEA JUWATA JAZZ BAND HUKU COSMAS THOBIAS CHIDUMULE, MICHAEL ENOCH ‘KING MICHAEL’ NA MPIGA GITAA LA SOLO MAHIRI, JOSEPH BATHOLEMEO MULENGA.

WANAMUZIKI HAO WALICHUKULIWA KATIKA BENDI YA DAR INTERNATIONAL.

ALIKUWA GWIJI MUHIDIN GURUMO ALIYEBUNI MTINDO WA SIKINDE NGOMA YA UKAE, ALIOUELEZEA KUWA NI MTINDO WA NGOMA ZA UTAMADUNI WA KABILA LAKE LA KIZARAMO.

MTINDO HUO HADI SASA NDIO UNAOTAMBA NA WAKATI MWINGINE HUTUMIWA NA WAPENZI KUITA SIKINDE KAMA JINA LA BENDI.

BENDI HIYO ‘ILIACHIA’ VIBAO VINGI VILIVYOTAMBA NA HADI LEO VINASIKIKA VIKIPIGWA NA BAADI YA VITUO VYA REDIO HAPA NCHINI.

BAADHI YA VIBAO HIVYO NI PAMOJA NA SAUDA, MV MAPENZI, NEEMA, USITUMIE PESA KAMA FIMBO, MUME WANGU JERRY, CLARA, HIBA NA MATATIZO YA NYUMBANI.

NYIMBO ZIGINE ZILIKUWA ZA MAJIRANI HUZIMA REDIO, NIDHAMU YA KAZI, KASSIM AMEFILISIKA,TALAKA YA HASIRA, HADIJA, BARUA TOKA KWA MAMA, CELINA, EDITHA NA FIKIRI NISAMEHE.

BENDI HIYO ILIKUWA NA WATUNZI WENGI MNO KIASI KWAMBA WALIWEZA KUTUNGA NA KUIMBA NYIMBO ZINGINE ZAIDI ZIKIQWEMO ZA POLE MKUU MWENZANGU, DIANA, PESA, HATA KAMA , BUBU ATAKA SEMA, MNANIONESHA NJIA YA KWETU, TANGAZIA MATAIFA YOTE, MTOTO AKILILIA WEMBE, NALALA KWA TABU NA DUNIANI KUNA MAMBO. 

ZINGINE ZAIDI NI KIU YA JIBU, DUA LA KUKU, NAWASHUKURU WAZAZI, PATA POTEA, NELSON MANDELA, UZURI WA MTU, MDOMO HUPONZA KICHWA, TAXI DRIVER, TUCHEZE SIKINDE, CONJESTA NA NYIMBO NIYNGINE NYINGI.


DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA ILIKUWA NA WANAMUZIKI WENGI WENYE VIPAJI TOFAUTI AKINA MICHAEL ENOCK, JOSEPH BENARD, JOSEPH MULENGA, ABDALAH GAMA, COSMAS CHIDUMULE, MACHAKU SALUM, HABIB JEFF NA MUHIDIN MAALIM GURUMO.

WENGINE WALIKUWA HASSAN REHANI BITCHUKA, ABEL BARTHAZAR, HENRY MKANYIA, FRESH JUMBE, HUSSEIN JUMBE, BENNO VILLA ANTHONY, TINO MASINGE 'ARAWA', HASSAN KUNYATA, FRANCIS (NASSIR) LUBUA, MAALIM HASSAN ‘KINYASI’, NA ABDALLAH GAMA.

SAFU HIYO ILIKUWA PIA NA MAX BUSHOKE, MUHARAMI SAID, KASSIM MPONDA, JULIUS MZERU, SAID CHIPELEMBE, ALLY JAMWAKA, MACHAKU SALUMNA  ALLY YAHAYA.

WENGINE WALIOENEZA SAFU HIYO NI PAMOJA NA SHABAN LENDI, JOSEPH BERNARD, JUMA HASSAN TOWN NA WENGINE WENGI. SHIRIKA LA MAENDELEO DAR ES SALAAM BAADE LIKAJITOA KUIFADILI BENDI HIYO JAPO ILIWAACHIA VYOMBO VYOTE VYA MUZIKI ILI WAWEZE KUJITEGEMEA. WAKABADILISHA JINA LA BENDI NA KUWA MLIMANI PARK ORCHESTRA. BENDI HIYO BADO INALITIKISA JIJI LA DAR ES SALAAM WAKIWA NA MAKAO YAO MAKUU KWENYE UKUMBI WA DDC KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM.

B

No comments: