Sunday, May 24, 2015

FREDY MAYAULA MAYONI MCHEZA HADI MWANAMUZIKI




UKIPEKUA KUTAKA KUFAHAMU ORODHA YA WACHEZAJI WALIOWAHI KUCHEZA KATIKA KLABU YA DAR YOUNG AFRICANS YA TANZANIA, PASI SHAKA MWANAMUZIKI FRED MAYAULA MAYONI NI MIONGONI MWAO.

BABA YAKE ALIKUWA MFANYAKAZI KATIKA UBALOZI WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO (ZAIRE) NCHINI TANZANIA, MAYAULA ALIMFUATA BABA YAKE NA NDIPO ALIPOJIUNGA KLABU HIYO.


UGONJWA WA MOYO (BRAIN TRUMOUR) NDIO ULIOSABABISHA KUKATIZA UHAI WAKE MEI 27, 2010 HUKO JIJINI BRUSSELS, UBELIGIJI.

MAYONI ALIKUWA MWANAMUZIKI MKONGWE MWENYE KIPAJI CHA UTUNGA NA KUIMBA MUZIKI WA DANSI TOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.

FERDY MAYAULA ALIKUWA MWANAMZIKI ALIYEKULIA NA KUSOMEA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM, MNAMO  MIAKA YA 1960.


BABA YAKE ALIKUWA NI MWANADIPLOMASIA KATIKA UBALOZI WA KONGO (ZAIRE) NCHINI TANZANIA. 

VIJANA WA ZAMANI HUKO DRC, WATAMKUMBUKA MAYAULA PALE ALIPOJIUNGA NA BENDI YA T.P. OK. 


JAZZ, ILIYOKUWA INAONGOZWA NA GWIJI FRANCO LUAMBO MAKIADI, HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.

MAYONI ALIJIUNGA T.P. OK. JAZZ BAADA YA KURUDI KWAO KONGO (DRC) NA KUJIKITA KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI. ALIACHIA WIMBO MAARUFU ‘CHERIE BONDOWE’ AU ‘SHERRY BONDOWE’, WIMBO AMBAO ULIMPA UMAARUFU MNO.

MAYAULA PIA ALIWAHI KUFANYA KAZI NA MWANAMZIKI MWANAMAMA MPONGO LOVE.


FREDY MAYAULA MAYONI ALIZALIWA NOVEMBA 06, 1946,  KATIKA JIJI LA LÉOPOLDVILLE, AMBALO SASA LINAITWA KINSHASA. ALIMALIZA SHULE ZA AWALI BILA MATATIZO NA KUMALIZA ELIMU YA SEKONDARI MWAKA 1962 KATIKA CHUO CHA KISANTU.

ALIPENDA SANA MPIRA WA MIGUU NA KATI YA MWAKA 1968 NA 1971 ALICHEZA NAFASI YA WINGA WA KUSHOTO KATIKA TIMU YA ‘AS VITA CLUB’ YA KINSHASA.

ALIWEZA KUCHAGULIWA HATA TIMU YA TAIFA YA NCHI YAKE.

BABA YAKE ALIPOPATA NAFASI YA KUFANYA KAZI KATIKA UBALOZI WA JAMHURIYA KIDEMOKRASIA YA KONGO (ZAIRE) NCHINI TANZANIA, MAYAULA ALIMFUATA. 

ALIANZA KUONESHA CHECHE KWA KUJIUNGA NA TIMU YA DAR YOUNG AFRICANS.

BAADAE ALIONDOKA DAR ES SALAAM NA KUELEKEA JIJI LA CHARLEROI, NCHINI UBELGIJI ALIKOKWENDA KUJIENDELEZA KIMASOMO KATIKA KOZI YA DATA PROCESSING.

AKIWA HUKO ALIJIUNGA NA TIMU ZA MPIRA YA ‘RACING CLUB DE CHARLEROI’ BAADAE AKAJIUNGA NA ‘RACING CLUB DE JETTE’ YA BRUSSELS.
 
KWA MUDA MFUPI ALICHEZEA TIMU YA ‘FC YA FRIBOURG YA SWITZERLAND, NI KATIKA KIPINDI HICHO ALIPOANZA KUJIFUNZA KUPIGA GITAA.

MUDA SI MREFU AKAJIUNGA NA BENDI YA WANAFUNZI WA KIKONGO ILIYOITWA ORCHESTRA ‘AFRICANA’ AKIWA KAMA MPIGA RHYTHM GITAA.

ALIPORUDI KINSHASA, MAYAULA AKABADILI KAZI KUTOKA KWENYE MPIRA WA MIGUU NA KUWA MWANAMUZIKI MTUNZI.

HAIKUCHUKUA MUDA MREFU KUGUNDULIKA KIPAJI CHAKE NA FRANCO LUAMBO MAKIADI, ALIYEMTAKA MAYAULA KUJIUNGA NA T.P. OK. JAZZ.

AKIWA NA T.P.OK. JAZZ NDIPO WAKATI HUO MAYAULA AKATOA NA KIBAO CHA CHERIE BONDOWE. WIMBO HUU ULIPOKELEWA VIZURI SANA NA WAPENZI WA MUZIKI.

KWA BAHATI MBAYA NATIONAL CENSORSHIP COMMISSION YA ZAIRE WAKATI HUO, ILIUPIGA MARUFUKU WIMBO HUO KWA KUWA ULIKUWA NA HADITHI YAKE ILIYOMUELEZEA ‘CHANGUDOA’ MMOJA ALIYEKUWA AKIELEZEA SHUGHULI ZAKE ZILIVYO.

COMMISSION ILIONA WIMBO UNATETEA UCHANGUDOA NA HIVYO KUUPIGA MARUFUKU. T.P.OK. JAZZ ILILZAZIMIKA KUUSAMBAZA WIMBO HUO  KUTOKEA UBELGIJI NA HATIMAE UKAENEA KONGO NA SEHEMU NYINGINE ZA AFRIKA.

YASEMEKANA KUWA JAPO FRANCO ALIMKARIBISHA T.P. OK. JAZZ, HAKUWAHI KUWA MWANACHAMA HALISI WA KUNDI HILO KWANI ALIPENDELEA KUWA HURU KUTUNGA NYIMBO ZAKE, NA KUMPA MSANII ALIYEMTAKA. TUNGO ZAKE KADHAA ZILIFANYIWA KAZI NA T.P. OK. JAZZ KAMA VILE NABALI MISERE NA MONI.

MWAKA 1977 TUNGO YAKE ILIYOITWA NDAYA ILICHUKULIWA NA KUIMBWA NA MWANAMUZIKI MPONGO LOVE, WIMBO HUO ULIKUWA UNAONGELEA KUHUSU MWANAMKE ALIYE NA FURAHA KUTOKANA NA KUWA NA MUME BORA NA KUWEZA KUMBANA MUMEWE KUTOKA KWA WANAWAKE WENGINE.

MAYAULA ALIONDOKA  ZAIRE MWAKA 1981 AKIWA NA WANAMUZIKI KUTOKA BENDI YA ABETI MASIKINI NA KUHAMIA AFRIKA MAGHARIBI.

HADI KUFIKIA MWAKA 1984 TAYARI LIKUWA MEREKODI ALBUM KADHAA CHINI YA LABEL YA DISC-ORIENT YA MJINI LOME NCHINI TOGO.

MWAKA 1984 ALIRUDI ZAIRE NA MWAKA 1986 ALITOA ALBUM ILIYOITWA ‘FIONA FIONA’, NA MWAKA HUOHUO TSHALA MUANA ALIPATA UMAARUFU KUTOKANA NA WIMBO ‘NASI NABALI’, ULIOTUNGWA NA MAYAULA MAYONI.

BAADA YA HAPO AKAREKODI ALBUM YAKE MIZELE AKIWA NA T.P. OK. JAZZ WAKISINDIKIZWA NA WAIMBAJI CARLITO LASSA NA MALAGE DE LUGENDO.
ALBUM YA ‘L’AMOUR AU KILO’ ILIFYATULIWA MWAKA 1993 NA MIAKA SABA BAADAE AKATOA ALBUM NYINGINE ‘BIKINI’.

BAADA YA ALBUM HIYO MAYAULA ALIHAMIA DAR ES SALAAM NA KUANZA KUFANYA KAZI UBALOZI WA KONGO.

WAKAZI WENGI WA MAGOMENI JIJINI DAR ES SALAAM WATAMKUMBUKA MAYAULA, AMBAYE  KATIKA KIPINDI HICHO AKIFANYA KAZI UBALOZINI, ALIKUWA AKIISHI MAENO HAYO.

MUDA SI MREFU AKAANZA KUUGUA NA KUAMUA KURUDI KWAO ALIKOZALIWA KATIKA KIJIJI CHA MAKADI, JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.
HALI YA AFYA YAKE ILIZIDI KUWA MBAYA MWAKA 2005 AKAPELEKWA UBELGIJI KWA MATIBABU ZAIDI. 

HATA HIVYO JUHUDI HIZO HAZIKUZAA MATUNDA KWA MAYAULA AKAFARIKI DUNIA KATIKA JIJI LA BRUSSELS NCHINI UBELGIJI  MEI 26, 2010 AKIWA NA UMRI WA MIAKA 64.
KATIKA MAISHA YAKE ALIWAHI KUCHAGULIWA MTUNZI BORA WA ZAIRE 1978 KWA WIMBO BONDOWE 2, MWAKA 1979 KWA WIMBO NABALI MISERE NA MWAKA 1993 ‘OUSMANE BAKAYOKO’.

MWISHO.

MUNGU UILAZE ROHO YA MAYAULA PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.

Friday, May 22, 2015

'JEMBE' LA MSONDO NGOMA RIDHWANI PANGAMAWE



 RIDHWANI PANGAMAWE.



KILA MPENDA MUZIKI WA BENDI YA MSONDO NGOMA HUPATWA NA FARAJA KUBWA AKIMUONA MWANAMUZIKI RIDHWANI PANGAMAWE AKIWA KASHIKILIA GITA AKIPIGA.

WASIFU WA RIDHWANI UNAELEZA KUWA ALIANZA KUPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YA JUWATA AKIWA NA UMRI MDOGO WA MIAKA 15 MNAMO MWAKA 1979.

MUZIKI HAUKUMUIJIA KAMA MIUJIZA ILA YEYE ALIZALIWA KATIKA FAMILIA ILIYOKUWA YA WANAMUZIK. INAELEZWA KWAMBA BABA YAKE MZEE PANGAMAWE ALIKUWA MWANAMUZIKI KATIKA BENDI ILIYOKUWA MAARUFU PALE IRINGA MJINI, ILIYOITWA HIGHLAND STARS.
BENDI HIYO ILITIKISA MJINI HUMO HASA MWISHONI MWA  MIAKA YA 1960 NA 1970.

MAZOEZI YA WANAMUZIKI WA BENDI HIYO YALIKUWA YAKIFANYIKA NYUMBANI KWAO HATA MAMA YAKE PIA ALIKUWA ANAWEZA KUPIGA GITAA.
AMEKIRI KUUPENDA MUZIKI TANGIA AKIWA BADO KINDA. ALISEMA KUWA HATA KAKA YAKE, ZUBERI PANGAMAWE,  ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA RTC PALE IRINGA, ALIKUWA ANAJUA KUPIGA GITA.

RIDHWANI ALIAANZA KUONESHA KIPAJI CHA KUPIGA KINANDA AKIWA BADO MDOGO SANA WA UMRI KAMA MIAKA MITANO AMBAPO KAKA YAKE ZUBERI ALIMKUTA KWA MARA YA KWANZA AKIPIGA KINANDA.

ALISIMULIA KWAMBA KINANDA HICHO ALIKUWA AKIPENDA KUPIGA KILA ALIPORUDI SHULE HATA ULE WAKATI WA MCHANA ALIPOKUWA AKIRUDI KULA CHAKULA CHA MCHANA ALIKUWA LAZIMA AGUSE KINANDA. TABIA AMBAYO HADI LEO BADO ANAPENDA KUFANYA MAZOEZI SANA.

PANGAMAWE BAADA YA KUMALIZA SHULE YA MSINGI IRINGA ALIKUJA DAR ES SALAAM AKIWA NA NIA YA KUENDELEA NA MASOMO YA SEKONDARI. WAKATI AKIWA HAPO DAR ES SALAAM, KAKA YAKE ALIWAMTAARIFU KUWA WAJOMBA ZAKE AMBAO NDIO WALIKUWA WENYEJI WAKE KUWA RIDHWANI ANA UWEZO WA KUPIGA KINANDA.

KATIKA KIPINDI HICHO HICHO WAZIRI ALLY KISINGER, ALIKUWA AMEIACHA BENDI YA JUWATA  NA KURUDI KWENYE BENDI YAKE YA AWALI YA THE REVOLUTIONS SASA KILIMANJARO BAND ‘WANA NJENJE’.

HIVYO JUWATA IKAWA NA PENGO LA MPAPASAJI KINANDA KWANI WAKATI HUO BENDI ZOTE KUBWA ZILIKUWA NA MPIGA KINANDA.

WIMBO WA JUMA KAKERE ‘SOGEA KARIBU’ ULIKUWA UKIONGOZA KWA KINANDA NA UKATAMBA KATIKA ANGA ZA AFRIKA MASHARIKI KWA UTAMU WA KINANDA CHA WAZIRI ALLY.

MSONDO WALIANZA MKAKAKATI WA KUTAFUTA MPIGA KINANDA, AMBAPO WAPIGA VINANDA KADHAA MASHUHURI WA WAKATI HUO WALIJARIBU BAHATI ZAO KUJIUNGA NA BENDI HII WAKIWEMO KASSIM MAGATI NA HATA ALLY TAJRUNA AMBAYE ALIPIGIA BENDI HIYO KWA MWEZI MZIMA.

WAJOMBA ZAKE RIDHWANI, AMBAO WALIKUWA WAPENZI WAKUBWA WA MSONDO NA WALIKUWA WAKIISHI JIRANI NA MZEE JOSEPH LUSUNGU.  LUSUNGU WAKATI HUO ALIKUWA MMOJA WA VIONGOZI WA BENDI HIYO YA JUWATA NA PIA ALIKUWA MPULIZAJI HODARI WA TAREUMBETA.

WALIMFUATA MZEE HUYO NA KUMTAARIFU KUWA WANA MDOGO WAO AMBAE ANAWEZA KUPIGA KINANDA. MZEE LUSUNGU AKAWAELEZA KUWA APELEKWE KWA AJILI YA USAILI.

RIDHWANI AKAKARIBISHWA JUWATA ILI KUFANYIWA USAILI CHINI YA MSIMAMIZI WA USAILI WA MZEE KASSIM MPONDA.

KWA KUWA HAPO AWALI HAKUWAHI KUGUSA KINANDA KINACHO TUMIA  UMEME, HIVYO ALIBABAIKA KIDOGO. KABLA YA HAPO ALIKUWA AKITUMIA KINANDA CHA KUJAZA UPEPO.
LAKINI HEKIMA ZA MZEE MPONDA ZILITUMIKA KWA KUMUACHA PASIPO KUMTILIA MAANANI.

WAKATI HUO HUO BENDI ILIKUWA IKIFANYA MAZOEZI YA WIMBO DUNIA UWANJA WA FUJO,HIVYO MZEE LUSUNGU AKAMUACHA ANAENDELEA KWENYE CHUMBA KIMOJA ANAPIGAPIGA KINANDA PEKE YAKE.

UHURU MKUBWA ALIOUPATA ULIMFANYA AWE JASIRI AKAANZA KUPIGA NYIMBO ALIZOKUWA ANAFAHAMU. JAMBO LILILOWAVUTIA WANAMUZIKI WENZIWE WALIOMSIKIA KIASI CHA KUACHA MAZOEZI NA KUMFUATA NA KUMTUZA PESA.

WAKATI HUO HAIKUWA RAHISI KUTUZWA PESA KWA MWANAMUZIKI MGENI AMBAYE ALIKUWA HAJAWAHI HATA KUPIGIA BENDI YOYOTE KABLA YA PALE, NA TENA WAKIWA MAZOEZINI.

MARA MOJA WANAMUZIKI WALIKUBALIANA KUWA AJIUNGE NAO. ALIENDELEA KUPIGA NYIMBO ZILIZOACHWA NA WAZIRI, NA KUCHUKULIWA RASMI KAMA MWANAMUZIKI WA MSONDO.

JINA LA TOTOO ALIPACHIKWA KUFUATIA KWAMBA ALIKUWA BADO MDOGO KI UMRI NA UMBO. WIMBO WAKE WA KWANZA KUREKODI AKIPIGA KINANDA ULIKUWA WIMBO ‘ZHULEKA’ UTUNZI WA SHAABAN DEDE.

BAHATI MBAYA BAADA YA MUDA SI MREFU KINANDA KIKAHARIBIKA NA KWA MUDA WA ZAIDI YA MIAKA MIWILI AKAWA  HAPIGI TENA KINANDA.
AKAAMUA KUHAMIA KWENYE UPIGAJI WA GITA, ALIANZA NA KUPIGA SECOND SOLO. UJUZI WAKE MKUBWA UNASIKIKA KATIKA NYIMBO KAMA KAKA SELEMANI NA SIWEMA.

KISHA AKAWA PIA ANAPIGA ZITO LA BESI, KATIKA WIMBO ‘MSAFIRI KAFIRI’ PAMOJA NA KUPIGA GITA HILO LA BESI, ILITOKEA WAKATI KASSIM MPONDA AKAONDOKA KATIKA BENDI WIKI MOJA KABLA YA SIKU YA KUREKODI.
NAFASI YAKE AKAKABIDHIWA PANGAMAWE KUPIGA GITA LA SOLO. NAYE HAKUFANYA AJIZI, ALILIKUNG’UTA SOLO KWA UZURI KABISA KATIKA WIMBO HUO.

KATI YA NYIMBO AMBAZO ALIWAHI KUPIGA ANAZOZIPENDA ZAIDI MOJAWAPO NI WIMBO WA QUEEN KASSE.


HATIMAYE 1994 AKAANZA TENA KUPIGA KINANDA BAADA YA BENDI KUPATA VYOMBO VIPYA. AKAREKODI NYIMBO KADHAA UKIWEMO WIMBO WA ‘OLEE’.

KAMA ALIVYO KIONGOZI WA BENDI HIYO SAID MABERA, RIDHWANI PANGAMAWE NAYE HAJAWAHI KUHAMA KATIKA BENDI HIYO TANGU ALIPOJIUNGA NAYO.

ALISISITIZA KUWA HANA MPANGO WA KUHAMA KWA KUWA ANAONA HAKUNA SABABU KUBWA ZA MSINGI ZA KUMFANYA KUHAMA MSONDO.OFAUTI KUBWA KATIKA KUHAMA BENDI.


MWISHO.

Wednesday, May 20, 2015

ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' KIFO KIOLIKATIZA NDOTO ZAKE




 ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' KIFO KIOLIKATIZA NDOTO ZAKE.

KILA MWANADAMU HUJIPANGIA MAMBO YAKE AKITARAJI KUIKAMILISHA ANAYOYAFIKIRIA KUYAFANYA. LAKINI JUHUDI ZOTE HIZO HUWEZA KUPANGULIWA KWA UWEZO WAKE MUNGU, KWA NJIA MOJA AMA NYINGINE.
MWANAMUZIKI MAHIRI ABUU SEMHANDO NI MMOJA WAPO AMBAYE ALIWEKA FIKRA ZAKE ZOTE KATIKA KUYAENDESHA MAISHA YAKE NA FAMILIA KUPITIA MUZIKI.
FIKRA HIZO ZILIKATISHWA GHAFLA BAADA YA KUPATA AJALI ILIYOPELEKEA KUPOOTEZA MAISHA DESEMBA 18, 2010.
SEMHANDO KATIKA MAISHA YAKE ALICHANGIA MAFANIKIO MENGI KATIKA BENDI YA AFRICAN STAR ENTERTAINMENT TANZANIA (ASET), KWA ASILIMIA KUBWA KUTOKANA NA KUJITOA KWA KILA HALI.
ALIKUWA MMOJA KATI YA VIONGOZI WA ASET AKIWA ANA WADHIFA WA KATIBU WA BENDI. ALIDUMU KWA KIPINDI KIREFU KATIKA BENDI HIYO YA TWANGA PEPETA TOKA ALIPOJIUNGA MWAKA 1998, AKITOKEA BENDI YA DIAMOND SOUND WANA ‘KIBINDA NKOI’.
KWA MUJIBU WA MKURUGENZI WA ASET ASHA BARAKA ALIMUELEZEA ABUU KUWA ALIITUMIKIA TWANGA KAMA MALI YAKE BINAFSI. ALISEMA KUWA KIFO CHA SEMHANDO KILIMTIA SIMANZI YEYE BINAFSI, WANAMUZ\IKI WENZAKE PAMOJA NA WAPENZI WOTE WA TWANGA PEPETA NDANI NA NJE YA NCHI.

ALITAMKA KUWA ABUU ALIKUWA NI CHACHU YA MAFANIKIO YA ALBAMU ZOTE 10 AMBAZO WAMEZITOA KUTOKANA NA KUSHIRIKI KATIKA KUANDAA MUZIKI NA KUSIMAMIA NIDHAMU YA BENDI.
KIFO CHA ABUU SEMHANDO KATIKA FAMILIA YAKE KILIMGUSA SANA BINTI YAKE SHARIFA, AMBAYE SIKU AMBAYO ALIKUWA ANATAKIWA KUFUNGISHWA NDOA NA BABA YAKE NDIYO MAUTI YALIPOMKUTA NA KUFANYA SHEREHE HIZO KUGEUKA MSIBA.
WASIFU WA NGULI HUYO UNAELEZA KUWA JINA LAKE KAMILI LILILKUWA ABUU ALLY SEMHANDO MAARUFU ‘LOKASSA’ AU ‘BABA DIANA’
ALIKUWA MCHARAZAJI MAHIRI WA DRUM WAKATI HUOHUO ALIKUWA NDIYE MENEJA WA BENDI YA AFRICAN STARS ‘TWANGA PEPETA’.
ABUU ALLY SEMHANDO ‘LOKASSA’ ALIZALIWA MWAKA 1953 KIJIJI CHA KIBANDA WILAYA YA MUHEZA MKOANI TANGA.
ALIANZA SHUGHULI ZA MUZIKI MWANZONI MWA MIAKA 1970 AKIWA KATIKA BENDI YA TANGA INTERNATIONAL, BAADAE ALIKWENDA KUWA MMOJA KATI YA WAASISI WA BENDI ZA TANZA MUZIKA NA ORCHESTRA TOMATOMA KABLA YA KUTUA SAFARI SOUND ORCHESTRA (OSS)
SEMHANDO NA HAMZA KALALA NI MIONGONI MWA WANAMUZIKI WAANZILISHI WA BENDI YA SUPER MATIMILA NA NDIO WALIOWAKARIBISHA WANAMUZIKI RAIA WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO MOSESE FANFAN NA RAMADHA MTORO ONGALA ‘DK. REMMY’
BAADAE ALIJIUNGA NA BENDI YA VIJANA JAZZ ‘PAMBA MOTO’, INAYOMILIKIWA NA JUMUIA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM AMBAKOKWA UWEZO WAKE WA KUONGOZA ALIKABIDHIWA NAFASI YA KUWA KATIBU WA BENDI.
ABUU ALISHIRIKI KUPIGA DRUMS KWA KIWANGO KIKUBWA KATIKA NYIMBO NYINGI AMBAZO ZILIILETEA MAFANIKO YA BENDI HIYO.
AKIWA KATIKA BENDI HIYO MWIMBAJI MAARUFU TOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO KASALOO KYANGA, ALIMPACHIKA JINA BANDIA LA ‘LOKASSA’.
LICHA YA KUWA MPIGA DRUMS, SEMBANDO ALIKUWA NI MWANAMUZIKI MWENYE KIPAJI KIKUBWA CHA UONGOZI WA BENDI (MUSIC BAND MANAGEMENT). ALIKUWA AKISHIRIKI KATIKA KUANDAA MUZIKI ILI KUHAKIKISHA BENDI YOYOTE ALIYOPITIA INAPATA MAFANIKIO. JAMBO HILO LILIMJENGEA UMAARUFU KATIKA KILA BENDI ALIYOPIGIA.
HISTORIA INAONYESHA KUWA KILA BENDI ALIZOWAHI KUPITIA AKIWA KIONGOZI, MARA BAADA YEYE KUONDOKA, ZILIYUMBA NA ZINGINE KUTOKOMEA KABISA KATIKA MEDANI YA MUZIKI WA DANSI.
LAKINI SI MATIMILA PEKEE YAKE HATA ALIPOKUWA NA VIJANA JAZZ ‘SAGA RHUMBA’ AMBAKO ALIKUWA KATIBU CHINI YA UONGOZI WA HEMED MANETI, ALIKUWA MMOJA WANAMUZIKI WALIOSHIRIKI KATIKA KUILETEA MAFANIKIO KWA MIAKA YOTE HIYO KABLA YA KUJIONDOA. YAELEZWA KUWA ABUU PIA ALIKUWA MUASISI WA ‘VIJANA DAY’.
KATIKA BENDI HIYO YA VIJANA ALISHIRIKI KWA KIWANGO KIKUBWA KUTENGENEZA NYIMBO AKIWA NA WAIMBAJI KINA HEMED MANETI, SAIDI HAMIS ‘MISUKOSUKO’, FRED BENJAMIN, COSMAS TOBIAS CHIDUMULE NA KIDA WAZIRI.
AIDHA WAPIGA VYOMBO WAKATI HUO WALIKUWA AKINA KURWA WA MILONGE, HAMZA KALALA, HASSAN DALALI, AGGREY NDUMBALO NA DISFA SEMHANDO (MDOGO WAKE), ALIYEKUWA AKILIUNGURUMISHA GITAA ZITO LA BESI. ALIKUWEPO PIA MPIGA GITA LA SOLO SHABANI YOHANA ‘WANTED’ NA WENGINE WENGI.
AKIWA NA WANAMUZIKI HAO AMBAO NI BAADHI TU YA KUNDI ALILOKUWA NALO, WALISHIRIKI KUTENGENEZA NYIMBO KALI KAMA ‘BUJUMBURA’, ‘MARY MARIA’, ‘TAMBIKO LA PAMBAMOTO’, ‘MUNDINDE’, ‘ALI HASSAN MWINYI APEWE KURA ZA NDIYO’, ‘WIFI ZANGU WANANINYANYASA’, STELLA, ‘PENZI HALIGAWANYIKI’ NA NYINGINE NYINGI NZURI KUPINDUKIA.
NYIMBO HIZO ZILITIKISA ANGA YA MUZIKI CHINI YA UONGOZI SHUPAVU WA HEMED MANETI ALIYEKUWA KIONGOZI, HAMZA KALALA ALIKUWA NI KIONGOZI MSAIDIZI NA ABUU SEMHANDO MWENYEWE  ALIYEKUWA KATIBU.
KATIKA KUDHIHIRIKISHA UWEZO ALIOKUWA NAO ALIPOJING’ATUA VIJANA JAZZ, NDIPO JINAMIZI NA ANGUKO LA BENDI HIYO LILIPOANZA KUINYEMELEA. TANGU HAPO BENDI HIYO HAIJAFANYA VYEMA KATIKA MEDANI YA MUZIKI NCHINI.
BAADHI YA WANAMUZIKI ALIOFANYA NAO KAZI WALIMZUNGUMZIA MAREHEMU SEMHANDO AKIWEMO  JOHN KITIME AMBAYE ALISEMA KUWA ATAENDELEA KUMKUMBUKA ABUU SEMHANDO KWA UCHESHI WAKE, NA VILEVILE ALIMPOKEA NA KUMTAFUTIA MALAZI JIJINI MWAKA 1989, WAKATI ANAJIUNGA NA VIJANA JAZZ AKITOKEA TUNCUT ALMASI YA IRINGA.
KWA UPANDE WAKE MKUNG’UTAJI WA GITAA LA SOLO ALDOF MBINGA AMBAYE NAYE ALISEMA TASNIA YA MUZIKI WA DANSI IMEPOTEZA JEMEDARI AMBAYE ALIKUWA HAYUMBI KATIKA MISIMAMO YAKE JAMBO AMBALO LILIILETEA MAFANIKIO VIJANA JAZZ AKIWA KATIBU NA ASET.
MBINGA ALIFANYA KAZI NA SEMHANDO KWA KUTENGENEZA ALBAMU YA KWANZA YA TWANGA PEPETA YA ‘KISA MPEMBA’ NA ‘JIRANI’.
WENGINE WALIOMZUNGUMZIA MAREHEMU NI WAZIRI ALLY AMBAYE NI MWANAMUZIKI WA BENDI THE KILIMANJARO ‘WANA NJENJE’ AKIMTAJA SEMHANDO KAMA NGUZO ILIYOKATIKA GHAFLA WAKATI WATU WAKIHITAJI HUDUMA NA UKONGWE WAKE KATIKA MUZIKI.
USHUHUDA MWINGINE ULITOLEWA ISIHAKA KIBENE, AMBAYE ALISEMA, TWANGA PEPETA IMEPOTEZA MPIGANAJI NA MTAWALA MAHIRI KUTOKANA NA KUWA KIUNGO KATIKA KUFANYA MAJUKUMU YA KILA SIKU YA BENDI. “HUYU JAMAA NI RAFIKI YANGU SANA AMBAYE NILIWAHI KUFANYA NAYE KAZI KIWANDA CHA UCHAPAJI CHA PRINTPAK MIAKA YA 1970, NA HATA ALIPOANZA SHUGHULI ZA MUZIKI TULIENDELEA KUWA MARAFIKI..." ALISEMA KIBENE.
ABUU ALLY SEMHANDO AMEACHA MKE NA WATOTO 10 NA KABURI LAKE LIPO KIJIJI CHA KIBANDA WILAYA YA MUHEZA ALIPOZALIWA.

MUNGU AILAZE ROHOYO YAKE PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.

JOHN BOKELO MKONGWE WA MUZIKI KONGO.




JOHN BOKELO MKONGWE WA MUZIKI  KONGO.


JINA LA JEAN 'JOHNNY' BOKELO ISENGE LILIVUMA MNAMO MIAKA YA 1950 NA 1960.
ALIZALIWA MIAKA YA 1930 MWISHONI KATIKA KITONGOJI CHA KONGO BELGE, NJE KIDOGO NA MJI WA KINSAHASA HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.
JOHN ALIKUWA NI MDOGO WA MWANAMUZIKI MAARUFU NCHINI HUMO, PAUL 'DEWAYON' ISENGO.
DEWAYON ALIKUWA NA KUNDI LAKE LA WANAMUZIKI LILILOKUWA LIKIITWA WATAM.
BOKELO AKIWA NA UMRI WA MIAKA 12, ALIANZA KUPIGA GITA MNAMO MWAKA 1950.
BAADAE AKAPIGA MUZIKI KATIKA BENDI ZA KAKA YAKE ZA
CONGA JAZZ NA ORCHESTRA COBANTU. AKIWA KATIKA BENDI HIZO, BOKELO ALIWEZA KUCHOTA UJUZI MKUBWA KIASI KWAMBA MWAKA 1958, ALIAMUA KUUNDA KUNDI LAKE LIKAITWA  ORCHESTRA CONGA SUCCESS.
KAKA DEWAYON NAE PIA ALIJIUNGA KATIKA KUNDI HILO MWAKA 1960.

NYIMBO ZA BENDI HIYO ZILILENGA MAHSUSI KWENYE MAPENZI NA VIFO.

BOKELO NA KAKA YAKE DEWAYON WALIGAWANYIKA TENA MWAKA 1962, AMBAPO BOKELO ALIENDELEA KUIONGZA BENDI YAKE YA CONGA SUCCESS.

HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO MTINDO WA MUZIKI ULIOKUWA UKIPIGWA NA NGULI HAO BOKELO, DEWAYON NA FRANCO MAKIADI ZIMEBAKIA KAMA ALAMA YA MUZIKI NCHINI HUMU.

NYIMBO NYINGI ZA JOHN BOKELO ZILIKUWA NA MIRINDIMO INAYORANDANA NA ILE YA FRANCO.



MWAKA 1968 JOHNNY BOKELO ALIBADILISHA JINA LA BENDI YAKE YA CONGA SUCCESS, IKAIITWA “CONGA 68" VILE VILE AKABUNI NEMBO YAKE.

GARY STEWART ALIWAHI KUSIMULIA JINSI WANAMUZIKI WA BENDI HIYO WALIPOTISHIA KUIANCHA BENDI KWA KUTOLIPWA CHOCHOTE.

NYIMBO NYINGI WAKATI HUO ZILIREKODIWA LEBO ILIYOTOLEWA NCHINI UFARANSA IKIWA LEBO YA KIAFRIKA.

MNAMO MIAKA YA 1972 HADI 1974, BOKELO ISENGO ALIKUWA AKIFANYA KAZI YA KUREKODI MIZIKI KATIKA STUDI YAKE YA KUREKODI.

MNAMO MIAKA YA KATIKATI MWA MIKA YA 1970, VITENDEA KAZI KATIKA KUREKODI NYIMBO, ULIKUWA MBAYA.

BOKELO ISENGO ALIKUWA MMOJA WA WATAYARISHAJI WALIOATHIRIKA. ALIAMUA KUVUKA MIPAKA HADI KATIKA JIJ LA NAIROBI NCHINI KENYA AKIWA NA TAPE KWENDA KUREKODI.

JOHN BOKELO ISENGE ALIFARIKI DUNIA MWAKA 1995.
MUNGU ALAZE ROHO YAKE PAHALA PEPONI, AMINA.



MUNGU AIWEKE ROHO YAKE PAHALA PEMA PEPONO, AMINA.


   

KANDA BONGO MAN ALIVYOTESA AFRIKA MASHARIKI.






KANDA BONGO MAN ALIVYOTESA AFRIKA MASHARIKI.

KANDA BONGOMAN NI MWANAMUZIKI AMBAYE KAMWE HATASAHAULIKA NA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI HUSUSANI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM NCHINI TANZANIA.

WASIFU WA BONGOMAN UNAELEZA KUWA ALIZALIWA MWAKA WA 1955 KATIKA KIJIJI CHA INONGO, KILICHOPO NJE KIDOGO YA MJI WA KINSHASA HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.

ALIWEZA KUJIPATIA UMAARUFU MKUBWA KATIKA MUZIKI WA SOUKOUS AKITUNGA, KUIMBA NA KUCHEZA KATIKA MTINDO WA KWASA KWASA.

KANDA BONGOMAN ALIKUWA MWIMBAJI WA BENDI YA ORCHESTRA BELLE MAMBO MWAKA WA 1973.

KANDA ALIANZA MUZIKI RASMI BAADA YA KUHAMIA KATIKA JIJI LA PARIS NCHINI UFARANSA MWAKA 1979.

MUZIKI WAKE ULIANZA KUINGIZA VIPENGELE VYA MUZIKI WA ZOUK (ASILI YAKE NI KIFARANSA KATIKA WEST INDIES).

ALBAMU ZAKE ZA KWANZA  "IYOLE" ILIYOTOKA MWAKA 1981 NA "DJESSY" MWAKA 1982 ZILIVUMA VILIVYO KWA WAPENZI NA MASHABIKI WA MUZIKI WAKATI HUO.

BONGOMAN ALIWAHI KUSHIRIKI KATIKA MAONESHO YA WOMAD YALIYOFANYIKA NCHINI UINGEREZA MWAKA 1983, AMBAKO ALIFANIKIWA ‘KUWAKUNA’ MASHABIKI WALIOHUDHURIA.

MWAKA 1989, BONGO MAN ALIACHIA ALBUM YAKE YA KWANZA YA KWASA KWASA, ILIYOSAMBAZWA NA WAMAREKANI ILIYOUNGANISHA ZILE ALIZITOA ZA “LELA LELA" NA "SAI" 

ALIENDELEA KUTANUA WIGO WA MUZIKI KWA KUPIGA MUZIKI WA ZING ZONG, AKIWAKUMBUKA WANAMUZIKI WAWILI NDUGU AMBAO NI MAREHEMU SOKI VANGU NA SOKI DIAZENZA ALIOKUWA AKIPIGA NAO MUZIKI KATIKA BENDI YA ORCHESTRA BELLA BELLA MWAKA 1991.

BONGOMAN ALIFYATUA ALBUM YAKE YA TATU YA SOUKOUS CENTRAL PARK, ILIYOSAMBAZWA NCHINI MAREKANI MWAKA 1993. BAADAE AKAPATWA NA ARI YA KUCHEZA MUZIKI ‘LIVE ‘

AKIWA NA ALBUM YAKE HIYO MWAKA 1998, ALIALIKWA NCHINI AFRKA YA KUSINI AMBAKO ALIPATA UZOEFU MKUBWA TOKA MUZIKI WA NCHI HIYO. 

MIAKA HIYO YA 1990, KANDA ALIWEZA KUZIKONGA NYOYO ZA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI WA KENYA NA TANZANIA.

AKIWA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM MIAKA YA 1990, ALIWEZA KUJAZA WATU KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA KILIMANJARO.KIINGILIO KILIKUWA KIKUBWA CHA SHILINGI LAKI MOJA KWA MTU MMOJA.

TIKETI ZILIMALIZIKA HUKU WAPENZI NA MASHABIKI WAKIOMBA ZIKACHAPWE NYINGINE. LAKINI  HAIKUWEZEKANA KUTOKANA NA UWEZO MDOGO WA UKUMBI KUMUDU KUBEBA IDADI KUBWA YA WATU.

REKODI YA KIINGILIO KIKUBWA KAMA HICHO HADI LEO HAIJAVUNJWA NA BENDI NYINGINE YEYOTE YA MUZIKI WA DANSI  HAPA NCHINI.

BAADA YA KUONDOKA NCHINI, ‘ALIZALISHA’ BONGOMAN MWINGINE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM ALIJULIKANA KWA JINA LA SHAABAN KADET.

ALIPEWA JINA BANDIA LA ‘BONGOMAN WA TANZANIA’, KWA UWEZO WAKE MKUBWA WA  KUIGA MINDOKO YA KANDA BONGOMAN.

MSANII HUYU KUTOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO, NI MIONGONI MWA WASANII WALIOJITENGENEZEA UMAARUFU MKUBWA KATIKA MIONDOKO YA SOUKOUS BARANI AFRIKA.
LICHA YA UWEZO WAKE MKUBWA KATIKA UIMBAJI NA UTUNZI, UMAARUFU WAKE ULIJENGWA ZAIDI NA MUONEKANO WAKE WA KIMAVAZI SAMBAMBA NA UCHEZAJI.
KUPENDELEA KWAKE KUPENDA KOFIA ZA PAMA, KULICHANGIA KOFIA HIZO KUPACHIKWA JINA KANDA BONGOMAN.
BONGOMAN PAMOJA NA WANAMUZIKI WAKE, PIA YEYE NI MBUNIFU MAHUSUSI WA NGUO.YAELEZWA KUWA BAADHI YA NGUO ZAKE HUZIBUNI NA KUZISHONA MWENYEWE.
NI YEYE ALIYEREMBESHA SOUKOUS KWA KUHIMIZA UTUMIAJI WA GITA BAADA YA KILA MSTARI NA HATA WAKATI MWINGINE KATIKA MWANZO WA WIMBO.

KAMA WENGI WA WANAMUZIKI SOUKOUS NA RUMBA KUTOKA AFRIKA WALIOKUWA MBELE YAKE, KANDA BONGOMAN PIA ALIKUWA NA KUNDI LA WANAMUZIKI ALILOIMBA NALO.

WENGI WA WANAMUZIKI WA KUNDI HILO, BAADAE WALIHAMA NA KUANZA KUIMBA BINAFSI. 

MFANO WA KARIBU NI MPIGAJI MAARUFU WA GITAA LA SOLO DIBLO DIBALA ALIYEJULIKANA  KAMA "MACHINE GUN", ALIKUWA SEHEMU MUHIMU KATIKA KUNDI LA BONGOMAN KATIKA ALBAMU KADHAA ZIKIWEMO ZA "KWASA KWASA" NA "AMOUR FOU".

KANDA ALIWAHI KUZURU NCHI ZA ULAYA NA MAREKANI.  JULAI 2005 ALIIMBA KATIKA ONESHO LA AFRIKA KATIKA CORNWALL.

KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA KENYA, ALIWASHANGAZA WAKAZI WA WAISHIO KATIKA ENEO LA MUMIAS MAGHARIBI MWA NCHI YA KENYA, ALIPOFIKA KATIKA KITUO KIMOJAWAPO CHA KUJAZIA MAFUTA.

KANDA BONGOMAN KUANZA KUHUDUMIA WATEJA WALIOFIKA NA VYOMBO VYAO VYA USAFIRI, IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 TANGU NCHI YA KENYA ILIPOPATA UHURU WAKE KUTOKA MIKONONI MWA WAKOLONI.

MTANDAO MMOJA NCHINI KENYA ULIANDIKWA KWAMBA BONGOMAN ALIWASHANGAZA WATEJA WENGI WALIOFIKA KUJAZA MAFUTA KATIKA KITUO HICHO, KUTOKANA NA UMAARUFU MKUBWA ALIOJIZOLEWA NA KUPENDWA NA WATU WARIKA MBALIMBALI.

MSANII HUYO ALIPATA NAFASI YA KUFUNGUKA KUHUSIANA NA TUKIO HILO KWA KUSEMA KWAMBA ALIKUWA NCHINI KENYA KWA ZIARA YA KIMUZIKI KATIKA MIJI YA BUNGOMA, KISUMU NA MIJI MBALIMBALI NCHINI HUMO.

AKIWA NCHINI HUMO KANDA ALIAMUA KUINGIA MTAANI KUSIKILIZA CHANGAMOTO MBALIMBALI WANAZOPATA MASHABIKI WAKE.

NYIMBO NYINGI ZA MKALI HUYO ALIZOTAMBA NAZO ZILIKUWA ZA  IYOLE YA MWAKA1981, DJESSY YA1982,  AMOUR FOU 1984,  MALINGA YA 1986,   LELA LELA MWAKA 1987,   SAI NA  LIZA ZA 1988,  KWASSA KWASSA MWAKA 1989, NA   ISAMBE NA INDE  MONIE  ZA 1990.

ZINZIGINE ZILIKUWA  ZA  ZING ZONG YA 1991,  SANGO YA 1992,   SOUKOUS KATIKA CENTRAL PARK MWAKA 1993 NA  TAMU ALIYOFYATUA MWAKA 1995.

ALIACHIA VIBAO VINGINE VYA  KARIBU AFRIKA KUSINI YA MWAKA 1995,  FRANCOPHONIX YA1999,  BALOBI 2002 NA   SWALATI YA MWAKA 2003.

KANDA BONGOMAN ANA KIPAJI CHA KUWEZA KULITAWALA JUKWAA HUKU MASHABIKI WOTE HUFURAHIA BURUDANI KAMAMBE TOKA KWA NYOTA HUYO HASA KUPITIA MTINDO WAKE MAARUFU WA KWASAKWASA.
SAUTI YAKE NYORORO INAYOBEBA MASHAIRI MARIDHAWA KATIKA LUGHA YA KILINGALA NA KIFARANSA, ILIMFANYA KANDA BONGOMAN KUWA MIONGONI MWA WATUMBUIZAJI MACHACHARI BARANI AFRIKA.
KATIKA  KUUELEZEA WASIFU WAKE, YAELEZWA KWAMBA ALPOKUWA MWANAFUNZI ALIPANDWA  NA MZUKA KATIKA MUZIKI NA  KUMFANYA NYOTA HUYO ‘AKUKACHA SHULE’.
AKIWA NA UMRI WA MIAKA 18, TAYARI KANDA  ALISHAAMUA KUACHANA NA MASOMO NA KUJIUNGA NA BENDI ZA MTAANI ILI KUTIMIZA NDOTO YAKE YA KUWA MWANAMUZIKI.
 ALIFANYA HIVYO ILI KUINGIA KWENYE TASNIA HIYO YA MUZIKI AMBAYO ALIAMINI ILIKUWA IMO NDANI YA MOYO WAKE.
PAMOJA NA KUWA BONGOMAN ALIFAHAMIKA ZAIDI MWANZONI MWA MIAKA YA 1980, ALIVUTIWA ZAIDI NA UTUNZI NA UIMBAJI WA MWANAMUZIKI TABU LEY.
AKAJARIBU KILA NJIA ILI SIKU MOJA NAYE AWE NA JINA KUBWA KWENYE RAMANI YA MUZIKI JAMBO AMBALO LILIFANIKIWA.
ALIAMUA KUJITOA NA KUANZA KUFANYA KAZI ZAKE KAMA MWANAMUZIKI WA KUJITEGEMEA AKIAMINI KUWA IPO ANGELIFANIKIWA KUFIKIA MALENGO YAKE.
HAIKUMCHUKUA MUDA MREFU KWANI MWAKA 1981, ALIWEZA KUKAMILISHA ALBAMU YAKE YA KWANZA ILIYOITWA 'IYOLE' AMBAYO ALIREKODI KWA KUMSHIRIKISHA MCHARAZA GITAA MAHIRI DIBLO DIBALA.
HUO NDIYO UKAWA MWANZO WA MWANAMUZIKI HUYU KUJITENGENEZEA UMAARUFU MKUBWA HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO NA BARA ZIMA LA AFRIKA KWA UJUMLA.

KANDA BONGOMAN HIVI SASA YAELEZWA KUWA AMEACHANA NA MASWALA MAZIMA YA MUZIKI, ANAFANYA SHUGHULI ZAKE ZINGINE.

MWISHO.