Friday, May 22, 2015

'JEMBE' LA MSONDO NGOMA RIDHWANI PANGAMAWE



 RIDHWANI PANGAMAWE.



KILA MPENDA MUZIKI WA BENDI YA MSONDO NGOMA HUPATWA NA FARAJA KUBWA AKIMUONA MWANAMUZIKI RIDHWANI PANGAMAWE AKIWA KASHIKILIA GITA AKIPIGA.

WASIFU WA RIDHWANI UNAELEZA KUWA ALIANZA KUPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YA JUWATA AKIWA NA UMRI MDOGO WA MIAKA 15 MNAMO MWAKA 1979.

MUZIKI HAUKUMUIJIA KAMA MIUJIZA ILA YEYE ALIZALIWA KATIKA FAMILIA ILIYOKUWA YA WANAMUZIK. INAELEZWA KWAMBA BABA YAKE MZEE PANGAMAWE ALIKUWA MWANAMUZIKI KATIKA BENDI ILIYOKUWA MAARUFU PALE IRINGA MJINI, ILIYOITWA HIGHLAND STARS.
BENDI HIYO ILITIKISA MJINI HUMO HASA MWISHONI MWA  MIAKA YA 1960 NA 1970.

MAZOEZI YA WANAMUZIKI WA BENDI HIYO YALIKUWA YAKIFANYIKA NYUMBANI KWAO HATA MAMA YAKE PIA ALIKUWA ANAWEZA KUPIGA GITAA.
AMEKIRI KUUPENDA MUZIKI TANGIA AKIWA BADO KINDA. ALISEMA KUWA HATA KAKA YAKE, ZUBERI PANGAMAWE,  ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA RTC PALE IRINGA, ALIKUWA ANAJUA KUPIGA GITA.

RIDHWANI ALIAANZA KUONESHA KIPAJI CHA KUPIGA KINANDA AKIWA BADO MDOGO SANA WA UMRI KAMA MIAKA MITANO AMBAPO KAKA YAKE ZUBERI ALIMKUTA KWA MARA YA KWANZA AKIPIGA KINANDA.

ALISIMULIA KWAMBA KINANDA HICHO ALIKUWA AKIPENDA KUPIGA KILA ALIPORUDI SHULE HATA ULE WAKATI WA MCHANA ALIPOKUWA AKIRUDI KULA CHAKULA CHA MCHANA ALIKUWA LAZIMA AGUSE KINANDA. TABIA AMBAYO HADI LEO BADO ANAPENDA KUFANYA MAZOEZI SANA.

PANGAMAWE BAADA YA KUMALIZA SHULE YA MSINGI IRINGA ALIKUJA DAR ES SALAAM AKIWA NA NIA YA KUENDELEA NA MASOMO YA SEKONDARI. WAKATI AKIWA HAPO DAR ES SALAAM, KAKA YAKE ALIWAMTAARIFU KUWA WAJOMBA ZAKE AMBAO NDIO WALIKUWA WENYEJI WAKE KUWA RIDHWANI ANA UWEZO WA KUPIGA KINANDA.

KATIKA KIPINDI HICHO HICHO WAZIRI ALLY KISINGER, ALIKUWA AMEIACHA BENDI YA JUWATA  NA KURUDI KWENYE BENDI YAKE YA AWALI YA THE REVOLUTIONS SASA KILIMANJARO BAND ‘WANA NJENJE’.

HIVYO JUWATA IKAWA NA PENGO LA MPAPASAJI KINANDA KWANI WAKATI HUO BENDI ZOTE KUBWA ZILIKUWA NA MPIGA KINANDA.

WIMBO WA JUMA KAKERE ‘SOGEA KARIBU’ ULIKUWA UKIONGOZA KWA KINANDA NA UKATAMBA KATIKA ANGA ZA AFRIKA MASHARIKI KWA UTAMU WA KINANDA CHA WAZIRI ALLY.

MSONDO WALIANZA MKAKAKATI WA KUTAFUTA MPIGA KINANDA, AMBAPO WAPIGA VINANDA KADHAA MASHUHURI WA WAKATI HUO WALIJARIBU BAHATI ZAO KUJIUNGA NA BENDI HII WAKIWEMO KASSIM MAGATI NA HATA ALLY TAJRUNA AMBAYE ALIPIGIA BENDI HIYO KWA MWEZI MZIMA.

WAJOMBA ZAKE RIDHWANI, AMBAO WALIKUWA WAPENZI WAKUBWA WA MSONDO NA WALIKUWA WAKIISHI JIRANI NA MZEE JOSEPH LUSUNGU.  LUSUNGU WAKATI HUO ALIKUWA MMOJA WA VIONGOZI WA BENDI HIYO YA JUWATA NA PIA ALIKUWA MPULIZAJI HODARI WA TAREUMBETA.

WALIMFUATA MZEE HUYO NA KUMTAARIFU KUWA WANA MDOGO WAO AMBAE ANAWEZA KUPIGA KINANDA. MZEE LUSUNGU AKAWAELEZA KUWA APELEKWE KWA AJILI YA USAILI.

RIDHWANI AKAKARIBISHWA JUWATA ILI KUFANYIWA USAILI CHINI YA MSIMAMIZI WA USAILI WA MZEE KASSIM MPONDA.

KWA KUWA HAPO AWALI HAKUWAHI KUGUSA KINANDA KINACHO TUMIA  UMEME, HIVYO ALIBABAIKA KIDOGO. KABLA YA HAPO ALIKUWA AKITUMIA KINANDA CHA KUJAZA UPEPO.
LAKINI HEKIMA ZA MZEE MPONDA ZILITUMIKA KWA KUMUACHA PASIPO KUMTILIA MAANANI.

WAKATI HUO HUO BENDI ILIKUWA IKIFANYA MAZOEZI YA WIMBO DUNIA UWANJA WA FUJO,HIVYO MZEE LUSUNGU AKAMUACHA ANAENDELEA KWENYE CHUMBA KIMOJA ANAPIGAPIGA KINANDA PEKE YAKE.

UHURU MKUBWA ALIOUPATA ULIMFANYA AWE JASIRI AKAANZA KUPIGA NYIMBO ALIZOKUWA ANAFAHAMU. JAMBO LILILOWAVUTIA WANAMUZIKI WENZIWE WALIOMSIKIA KIASI CHA KUACHA MAZOEZI NA KUMFUATA NA KUMTUZA PESA.

WAKATI HUO HAIKUWA RAHISI KUTUZWA PESA KWA MWANAMUZIKI MGENI AMBAYE ALIKUWA HAJAWAHI HATA KUPIGIA BENDI YOYOTE KABLA YA PALE, NA TENA WAKIWA MAZOEZINI.

MARA MOJA WANAMUZIKI WALIKUBALIANA KUWA AJIUNGE NAO. ALIENDELEA KUPIGA NYIMBO ZILIZOACHWA NA WAZIRI, NA KUCHUKULIWA RASMI KAMA MWANAMUZIKI WA MSONDO.

JINA LA TOTOO ALIPACHIKWA KUFUATIA KWAMBA ALIKUWA BADO MDOGO KI UMRI NA UMBO. WIMBO WAKE WA KWANZA KUREKODI AKIPIGA KINANDA ULIKUWA WIMBO ‘ZHULEKA’ UTUNZI WA SHAABAN DEDE.

BAHATI MBAYA BAADA YA MUDA SI MREFU KINANDA KIKAHARIBIKA NA KWA MUDA WA ZAIDI YA MIAKA MIWILI AKAWA  HAPIGI TENA KINANDA.
AKAAMUA KUHAMIA KWENYE UPIGAJI WA GITA, ALIANZA NA KUPIGA SECOND SOLO. UJUZI WAKE MKUBWA UNASIKIKA KATIKA NYIMBO KAMA KAKA SELEMANI NA SIWEMA.

KISHA AKAWA PIA ANAPIGA ZITO LA BESI, KATIKA WIMBO ‘MSAFIRI KAFIRI’ PAMOJA NA KUPIGA GITA HILO LA BESI, ILITOKEA WAKATI KASSIM MPONDA AKAONDOKA KATIKA BENDI WIKI MOJA KABLA YA SIKU YA KUREKODI.
NAFASI YAKE AKAKABIDHIWA PANGAMAWE KUPIGA GITA LA SOLO. NAYE HAKUFANYA AJIZI, ALILIKUNG’UTA SOLO KWA UZURI KABISA KATIKA WIMBO HUO.

KATI YA NYIMBO AMBAZO ALIWAHI KUPIGA ANAZOZIPENDA ZAIDI MOJAWAPO NI WIMBO WA QUEEN KASSE.


HATIMAYE 1994 AKAANZA TENA KUPIGA KINANDA BAADA YA BENDI KUPATA VYOMBO VIPYA. AKAREKODI NYIMBO KADHAA UKIWEMO WIMBO WA ‘OLEE’.

KAMA ALIVYO KIONGOZI WA BENDI HIYO SAID MABERA, RIDHWANI PANGAMAWE NAYE HAJAWAHI KUHAMA KATIKA BENDI HIYO TANGU ALIPOJIUNGA NAYO.

ALISISITIZA KUWA HANA MPANGO WA KUHAMA KWA KUWA ANAONA HAKUNA SABABU KUBWA ZA MSINGI ZA KUMFANYA KUHAMA MSONDO.OFAUTI KUBWA KATIKA KUHAMA BENDI.


MWISHO.

No comments: