Wednesday, May 20, 2015

ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' KIFO KIOLIKATIZA NDOTO ZAKE




 ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' KIFO KIOLIKATIZA NDOTO ZAKE.

KILA MWANADAMU HUJIPANGIA MAMBO YAKE AKITARAJI KUIKAMILISHA ANAYOYAFIKIRIA KUYAFANYA. LAKINI JUHUDI ZOTE HIZO HUWEZA KUPANGULIWA KWA UWEZO WAKE MUNGU, KWA NJIA MOJA AMA NYINGINE.
MWANAMUZIKI MAHIRI ABUU SEMHANDO NI MMOJA WAPO AMBAYE ALIWEKA FIKRA ZAKE ZOTE KATIKA KUYAENDESHA MAISHA YAKE NA FAMILIA KUPITIA MUZIKI.
FIKRA HIZO ZILIKATISHWA GHAFLA BAADA YA KUPATA AJALI ILIYOPELEKEA KUPOOTEZA MAISHA DESEMBA 18, 2010.
SEMHANDO KATIKA MAISHA YAKE ALICHANGIA MAFANIKIO MENGI KATIKA BENDI YA AFRICAN STAR ENTERTAINMENT TANZANIA (ASET), KWA ASILIMIA KUBWA KUTOKANA NA KUJITOA KWA KILA HALI.
ALIKUWA MMOJA KATI YA VIONGOZI WA ASET AKIWA ANA WADHIFA WA KATIBU WA BENDI. ALIDUMU KWA KIPINDI KIREFU KATIKA BENDI HIYO YA TWANGA PEPETA TOKA ALIPOJIUNGA MWAKA 1998, AKITOKEA BENDI YA DIAMOND SOUND WANA ‘KIBINDA NKOI’.
KWA MUJIBU WA MKURUGENZI WA ASET ASHA BARAKA ALIMUELEZEA ABUU KUWA ALIITUMIKIA TWANGA KAMA MALI YAKE BINAFSI. ALISEMA KUWA KIFO CHA SEMHANDO KILIMTIA SIMANZI YEYE BINAFSI, WANAMUZ\IKI WENZAKE PAMOJA NA WAPENZI WOTE WA TWANGA PEPETA NDANI NA NJE YA NCHI.

ALITAMKA KUWA ABUU ALIKUWA NI CHACHU YA MAFANIKIO YA ALBAMU ZOTE 10 AMBAZO WAMEZITOA KUTOKANA NA KUSHIRIKI KATIKA KUANDAA MUZIKI NA KUSIMAMIA NIDHAMU YA BENDI.
KIFO CHA ABUU SEMHANDO KATIKA FAMILIA YAKE KILIMGUSA SANA BINTI YAKE SHARIFA, AMBAYE SIKU AMBAYO ALIKUWA ANATAKIWA KUFUNGISHWA NDOA NA BABA YAKE NDIYO MAUTI YALIPOMKUTA NA KUFANYA SHEREHE HIZO KUGEUKA MSIBA.
WASIFU WA NGULI HUYO UNAELEZA KUWA JINA LAKE KAMILI LILILKUWA ABUU ALLY SEMHANDO MAARUFU ‘LOKASSA’ AU ‘BABA DIANA’
ALIKUWA MCHARAZAJI MAHIRI WA DRUM WAKATI HUOHUO ALIKUWA NDIYE MENEJA WA BENDI YA AFRICAN STARS ‘TWANGA PEPETA’.
ABUU ALLY SEMHANDO ‘LOKASSA’ ALIZALIWA MWAKA 1953 KIJIJI CHA KIBANDA WILAYA YA MUHEZA MKOANI TANGA.
ALIANZA SHUGHULI ZA MUZIKI MWANZONI MWA MIAKA 1970 AKIWA KATIKA BENDI YA TANGA INTERNATIONAL, BAADAE ALIKWENDA KUWA MMOJA KATI YA WAASISI WA BENDI ZA TANZA MUZIKA NA ORCHESTRA TOMATOMA KABLA YA KUTUA SAFARI SOUND ORCHESTRA (OSS)
SEMHANDO NA HAMZA KALALA NI MIONGONI MWA WANAMUZIKI WAANZILISHI WA BENDI YA SUPER MATIMILA NA NDIO WALIOWAKARIBISHA WANAMUZIKI RAIA WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO MOSESE FANFAN NA RAMADHA MTORO ONGALA ‘DK. REMMY’
BAADAE ALIJIUNGA NA BENDI YA VIJANA JAZZ ‘PAMBA MOTO’, INAYOMILIKIWA NA JUMUIA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM AMBAKOKWA UWEZO WAKE WA KUONGOZA ALIKABIDHIWA NAFASI YA KUWA KATIBU WA BENDI.
ABUU ALISHIRIKI KUPIGA DRUMS KWA KIWANGO KIKUBWA KATIKA NYIMBO NYINGI AMBAZO ZILIILETEA MAFANIKO YA BENDI HIYO.
AKIWA KATIKA BENDI HIYO MWIMBAJI MAARUFU TOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO KASALOO KYANGA, ALIMPACHIKA JINA BANDIA LA ‘LOKASSA’.
LICHA YA KUWA MPIGA DRUMS, SEMBANDO ALIKUWA NI MWANAMUZIKI MWENYE KIPAJI KIKUBWA CHA UONGOZI WA BENDI (MUSIC BAND MANAGEMENT). ALIKUWA AKISHIRIKI KATIKA KUANDAA MUZIKI ILI KUHAKIKISHA BENDI YOYOTE ALIYOPITIA INAPATA MAFANIKIO. JAMBO HILO LILIMJENGEA UMAARUFU KATIKA KILA BENDI ALIYOPIGIA.
HISTORIA INAONYESHA KUWA KILA BENDI ALIZOWAHI KUPITIA AKIWA KIONGOZI, MARA BAADA YEYE KUONDOKA, ZILIYUMBA NA ZINGINE KUTOKOMEA KABISA KATIKA MEDANI YA MUZIKI WA DANSI.
LAKINI SI MATIMILA PEKEE YAKE HATA ALIPOKUWA NA VIJANA JAZZ ‘SAGA RHUMBA’ AMBAKO ALIKUWA KATIBU CHINI YA UONGOZI WA HEMED MANETI, ALIKUWA MMOJA WANAMUZIKI WALIOSHIRIKI KATIKA KUILETEA MAFANIKIO KWA MIAKA YOTE HIYO KABLA YA KUJIONDOA. YAELEZWA KUWA ABUU PIA ALIKUWA MUASISI WA ‘VIJANA DAY’.
KATIKA BENDI HIYO YA VIJANA ALISHIRIKI KWA KIWANGO KIKUBWA KUTENGENEZA NYIMBO AKIWA NA WAIMBAJI KINA HEMED MANETI, SAIDI HAMIS ‘MISUKOSUKO’, FRED BENJAMIN, COSMAS TOBIAS CHIDUMULE NA KIDA WAZIRI.
AIDHA WAPIGA VYOMBO WAKATI HUO WALIKUWA AKINA KURWA WA MILONGE, HAMZA KALALA, HASSAN DALALI, AGGREY NDUMBALO NA DISFA SEMHANDO (MDOGO WAKE), ALIYEKUWA AKILIUNGURUMISHA GITAA ZITO LA BESI. ALIKUWEPO PIA MPIGA GITA LA SOLO SHABANI YOHANA ‘WANTED’ NA WENGINE WENGI.
AKIWA NA WANAMUZIKI HAO AMBAO NI BAADHI TU YA KUNDI ALILOKUWA NALO, WALISHIRIKI KUTENGENEZA NYIMBO KALI KAMA ‘BUJUMBURA’, ‘MARY MARIA’, ‘TAMBIKO LA PAMBAMOTO’, ‘MUNDINDE’, ‘ALI HASSAN MWINYI APEWE KURA ZA NDIYO’, ‘WIFI ZANGU WANANINYANYASA’, STELLA, ‘PENZI HALIGAWANYIKI’ NA NYINGINE NYINGI NZURI KUPINDUKIA.
NYIMBO HIZO ZILITIKISA ANGA YA MUZIKI CHINI YA UONGOZI SHUPAVU WA HEMED MANETI ALIYEKUWA KIONGOZI, HAMZA KALALA ALIKUWA NI KIONGOZI MSAIDIZI NA ABUU SEMHANDO MWENYEWE  ALIYEKUWA KATIBU.
KATIKA KUDHIHIRIKISHA UWEZO ALIOKUWA NAO ALIPOJING’ATUA VIJANA JAZZ, NDIPO JINAMIZI NA ANGUKO LA BENDI HIYO LILIPOANZA KUINYEMELEA. TANGU HAPO BENDI HIYO HAIJAFANYA VYEMA KATIKA MEDANI YA MUZIKI NCHINI.
BAADHI YA WANAMUZIKI ALIOFANYA NAO KAZI WALIMZUNGUMZIA MAREHEMU SEMHANDO AKIWEMO  JOHN KITIME AMBAYE ALISEMA KUWA ATAENDELEA KUMKUMBUKA ABUU SEMHANDO KWA UCHESHI WAKE, NA VILEVILE ALIMPOKEA NA KUMTAFUTIA MALAZI JIJINI MWAKA 1989, WAKATI ANAJIUNGA NA VIJANA JAZZ AKITOKEA TUNCUT ALMASI YA IRINGA.
KWA UPANDE WAKE MKUNG’UTAJI WA GITAA LA SOLO ALDOF MBINGA AMBAYE NAYE ALISEMA TASNIA YA MUZIKI WA DANSI IMEPOTEZA JEMEDARI AMBAYE ALIKUWA HAYUMBI KATIKA MISIMAMO YAKE JAMBO AMBALO LILIILETEA MAFANIKIO VIJANA JAZZ AKIWA KATIBU NA ASET.
MBINGA ALIFANYA KAZI NA SEMHANDO KWA KUTENGENEZA ALBAMU YA KWANZA YA TWANGA PEPETA YA ‘KISA MPEMBA’ NA ‘JIRANI’.
WENGINE WALIOMZUNGUMZIA MAREHEMU NI WAZIRI ALLY AMBAYE NI MWANAMUZIKI WA BENDI THE KILIMANJARO ‘WANA NJENJE’ AKIMTAJA SEMHANDO KAMA NGUZO ILIYOKATIKA GHAFLA WAKATI WATU WAKIHITAJI HUDUMA NA UKONGWE WAKE KATIKA MUZIKI.
USHUHUDA MWINGINE ULITOLEWA ISIHAKA KIBENE, AMBAYE ALISEMA, TWANGA PEPETA IMEPOTEZA MPIGANAJI NA MTAWALA MAHIRI KUTOKANA NA KUWA KIUNGO KATIKA KUFANYA MAJUKUMU YA KILA SIKU YA BENDI. “HUYU JAMAA NI RAFIKI YANGU SANA AMBAYE NILIWAHI KUFANYA NAYE KAZI KIWANDA CHA UCHAPAJI CHA PRINTPAK MIAKA YA 1970, NA HATA ALIPOANZA SHUGHULI ZA MUZIKI TULIENDELEA KUWA MARAFIKI..." ALISEMA KIBENE.
ABUU ALLY SEMHANDO AMEACHA MKE NA WATOTO 10 NA KABURI LAKE LIPO KIJIJI CHA KIBANDA WILAYA YA MUHEZA ALIPOZALIWA.

MUNGU AILAZE ROHOYO YAKE PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.

No comments: