Wednesday, August 7, 2013

RASHIDI PEMBE GWIJI LA SAXOPHONE.



RASHID PEMBE  GWIJI LA SAX TANZANIA


 RASHIDI PEMBE AKIPULIZA SAXOPHONE HUKO STOCKHOLM SWEDEN.

 RASHID PEMBE  KATIKATI AKIWA NA WANAMUZIKI WENZAKE KATIKA JIJI LA STOCKHOLM  NCHINI SWEDEN.




 RASHIDI PEMBE AKIWA NA WANAMUZIKI WENZAKE



 MELI KUBWA YA KITALII ALIYOKUWA AKIPIGIA MUZIKI RASHISI PEMBE HUKO SWEDEN.
 RASHIDI PEMBE(WAPILI KUSHOTO)AKIWA MELINI NA WANAMUZIKI WENZAKE,DEKULA KAHANGA(KATIKATI)STOCKHOLM NCHINI SWEDEN.
 RASHIDI PEMBE AKIWA NA MDOGO WAKE NA MWENYEJIWAO HUKO ULAYA

HISTORIA YA MAISHA YA RASHIDI PEMBE.


RASHID PEMBE NI MWANAMUZIKI MASHUHURI KWA UPULIZAJI WA SAXOPHONE HAPA NCHI NA NJE YA MIPAKA YETU. ALIZALIWA MWAKA 1957.
WAZAZI WAKE BI. FRIDA ABEL AMBAYE NI MAREHEMU, ALIKUWA MZALIWA WA KIJIJI CHA MIHUGWE, WILAYA YA KISARAWE MKOANI PWANI.
BABA YAKE MZEE PEMBE RASHID PIA MAREHEMU  ALIKUWA MZALIWA WA KIJIJI CHA KURUWI, TARAFA YA MZENGA, WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI.
RASHIDI PEMBE ANAIELEZEA HISTORIA YAKE AKISEMA...

"MWAKA 1963 NILIANZA ELIMU YA MSINGI CHANZIGE PRIMARY SCHOOL HAPO KISARAWE, ILA KWA KUWA MAMA ALIKUWA DAKTARI ALIHAMISHWA HUKU NA KULE
NASI NDIO TULIKUWA TUKIISHI NA MAMA KWANI WALISHAACHANA NA BABA
MAMA ALIPENDA SANA TU
SOME, ILA BABA HAKUWA NA MSISITIZO SANA WA SHULE, SIJUI KWA KUWA ALIKUWA MBALI NA SISI MAANA HUDUMA ILIKUWA KWA MBINDE KIDOGO.
1966 MAMA ALIHAMISHWA HOSPITALI YA KISARAWE NA KUPELEKWA VIKINDU HOSPITALI NASI TUKAHAMA SHULE KWENDA KUSOMA HAPO VIKINDU -WILAYA HIYO YA
KISARAWE NIKIWA DARASA LA 4.
1967 NILIINGIA MIDDLE SCHOOL HAPO VIKINDU DARASA LA 5 HAPO NDIO NILIKUTANA NA MWANAMUZIKI JOSEPH BENARD TUKIWA DARASA MOJA NA DAWATI MOJA AMBAE
NI MPIGA SAXAPHONE DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA.
JOSEPH AMBAE SASA ANAITWA YUSUPH BENARD ALIKUWA NI MPIGA FILIMBI BINGWA PALE SHULENI, KIASI AMBACHO NILIUMIA SANA, HADI NIKAMUOMBA ANIFUNDISHE NA ALINIFUNDISHA TUKAWA TUNAPIGA WOTE FILIMBI KTK BENDI YETU YA SHULE.
1968 NIKIWA DARASA LA 6 NILIUGUA MKONO ULIKUWA HAUKUNJUKI SIJUI ILIKUWA NI NINI MUHIMBILI HOSPT WALIAMUA WAUVUNJE NIKAKATAA, WAKANIFUKUZA HOSPT
KAMA SITAKI KUVUNJWA HALAFU UUNGWE TENA NA NITAKUWA KILEMA WA MKONO KUTOKUKUNJA TENA,
KWA MAPENZI YA MUNGU MKONO ULIKUNJUKA SIKU HIYOHIYO JIONI YAKE, WAKATI MWAKA MZIMA ULINIUMA , ULIVIMBA NA HAUKUWA UNAKUNJUKA.
KW HALI HIYO NILIACHA SHULE MWAKA MZIMA.
MWAKA HUO WA 1968 MAMA ALIHAMISHWA KUPELEKWA SOTELE HOSPT NA BAADAE KUHAMISHWA TENA KWENDA KISIJU HOSPT WILAYA HIYOHIYO YA KISARAWE NA NDIPO NILIPORUDI TOKA KWA BABA NILIPOKUWA NAUGUA, NA KURUDI TENA KWA MAMA.
MAMA AKANIAMBIA NIANZE DARASA LA 4 TENA KWA KUWA ILE SHULE ILKUWA MPYA HAIKUWA NA DARASA LA 5 WALA LA 6.
SIKUWA NAPENDA SHULE KABISA, KWENDA SHULE ILIKUWA HADI KWA VIBOKO KILA SIKU NILIPAMBANA NA MAMA NA NILIMSUMBUA SANA HADI KUMALIZA DARASA LA 7 MWAKA 1972 HAPO KISIJU PRIMARY SCHOOL.
MAMA ALINIPELEKA KWA MJOMBA DAR ILI ANITAFUTIE KAZI, NA KWELI MJOMBA ALINITAFUTIA KAZI KILIMANJARO TEXTILE KIWANDA KILICHOKUWA KINATENGENEZA
KHANGA NA VITENGE HAPO GONGOLAMBOTO .
1973 NILIANZA KAZI, NILIPOKUWA KAZINI TUKIWA NA MAVITAMBAA KUZIBA PUA NA WENGI KUUGUA TB KUTOKANA NA PAMBA TUNAZOSINDIKA KWENYE MASHINE
NIKAONA VIJANA WENZANGU VIJANA WADOGO, WAKIWA WAMESHIKA MAFAILI NA KUZUNGUKA HUKU NA KULE, WENGINE WAKIWA OFISINI ,NIKAWA NATAMANI KWA NINI NISIPATEKAZI KAMA WALE? IKABIDI NIULIZE MBONA WALE WANA KAZI NZURI? NDIO KUAMBIWA WALE WAMESOMA FORM 4 WALE, NDIO KUSHTUKA KUWA KUMBE NDIO MAANA MAMA ALINIAMBIA NISOME NIKAANZA KUJUA FAIDA YA KUSOMA NA KUMWAMBIA MAMA NATAKA KUACHA KAZI NIKASOME KITU AMBACHO KWANZA ALICHEKA
SANA HALAFU AKANIULIZA UMEONA ? ULINISUMBUA HUTAKI SHULE SASA UMEONA NINI? NIKAMUELEZA NDIPO ALIPOMUOMBA KAKA ANITAFUTIE SHULE NIKAPELEKWA SHULE YA BAGAMOYO TECHNICAL SECONDARY SCHOOL 1973 HADI 1978 SHULE ILIKUWA INAMILIKIWA NA UMOJA WA WAZAZI TAPA WAKATI HUO.
SASA NIKIWA MDOGO NILIPENDA SANA NGOMA ILIKUWA MDUNDIKO UKIPITA MAMA UPESI HUWAAMBIA DADA ZANGU WANITAFUTE WANIKAMATE BILA HIVYO NAWEZA KWENDA NAO NA NISIJUE MWISHO WAPI NILIKUWA NAPOTEA HADI WATAFUTE NGOMA HIYO ILIPOENDA NDIO WATANIKUTA HUKO? NA SIKUWA NA UJANJA WA KURUDI WATANIKUTA HAPOHAPO KWENYE MDUNDIKO.
WAKATI NIPO KAZINI, NILIPENDA SANA BENDI YA SAFARI TRIPERS YA MAREH MARIJANI RAJABU PALE PRINCES BAR MNAZI MMOJA. MI NILIKUWA NAJUA MUZIKI MTU ANAJUA TU KAMA KIPAJIN KAZALIWA NACHO MTU SIKUJUA KAMA HADI UJIFUNZE, SASA PALE NILIMKUTA ABDALLAH GAMA AKIWA ANAPIGA GUITAR NA ALIKUWA MDOGO SANA NDIPO NIKAJIULIZA KWA NINI HUYU MDOGO ANAJUA NA NI MDOGO HIVI? NDIPO NILIAMUA NIJIFUNZE GITA.
NIKAWA NA GUITAR SHULE KITU AMBACHO KAKA ANENISOMESHA ALIKASIRIKA AKNIAMBIA NILIUZE NIKAKATAA AKAAMUA KUNIFUKUZA KWAKE, NA NIKAAMUA KWENDA KWA DADA NAE SHEMEJI AKASEMA HAWEZI KUWA NA WATU LUKUKI PALE HOME KWAKE NIKAAMUA KUONDOKA, NA KUWA NALALA SOKONI KARIAKOO PALE NJE NDIPO SHIDA YA MAISHA ILIANZA NILITAMANI KUFA LAKINI SIKUUZA GUITAR. NILIKUBALI YOTE, NIKABEBA MIZIGO YA ABIRIA WANAOTOKA MBEYA NA MIKOA MBALIMBALI PALE
MANZESE HADI NIKATEUKA SHINGO JAMANI MAISHA NI KIBOKO LAKINI NILIMUAMINI SANA MUNGU NA KUMUOMBA KWA YALE MATESO NILIPATA HADI NILIMALIZA SHULE
BABA AKIWA ANALIPA ADA YA SHULE KAKA ALIKATAA KABISA KUNISOMESHA TENA.
BAADA YA MATOKEO NILICHAGULIWA KWENDA KUSOMEA UALIMU WA UFUNDI MRUTUNGURU -SIJUI NI MUSOMA AU WAPI NIKAKATAA, KWA NILISOMA KWA TAABU NAE BABA AKASEMA NDIO MAANA KAKA YAKO, KAKUFUKUZA WE HUTAKI KUSOMA UNATAKA KUPIGA MAGITAA KUANZIA LEO SITAKUSAIDIA KWA LOLOTE NIKAKUBALI NILAENDELE A JIONI  KULALA SOKONI KARIAKOO HADI RAFIKI YANGU MAREHEMU JOHN SEMLAMBA ALINIKUTA NAAMKA PALE AKAMUA KUNICHUKUA NA KUKAA KWAKE KWA KUWA NILIMUELEZA KILA KITU.
1979 NILIENDA JKT NILIJUA KUTOKANA NA CHETI CHANGU CHA UFUNDI MASON (UASHI) GRADE 1  KINGENIPA KAZI KUMBE KULE IKAWA KUJITOLEA NIKATOROKA KARIBU NAMBA ZA JESHI ZITOKE, WAKATI HUO JESHI LA POLISI WALIKUWA WANATAKA MAFUNDI TOKA SHULENI NA CHETI CHANGU NIKACHUKLIWA MOJA KWA MOJA NA POLISI. NIKAWA NAFANYA KAZI POLICE MAIN STORE PALE KILWA ROAD NA KUANZA MAISHA.
PALE NDIO NILIPOKUTANA NA  TX  MOSHI WILLIAM, MZEE KASSIM MAPILI AMBAE AKAAMUA KUNIENDELEZA KUPIGA GITA NA WALIAMUA WANICHUKUE ILI NIKAJIENDELEZE PALE POLICE BAND NA NILIKUBALI KUOMBA KUBADILISHA SECTION TOKA KIKOSI CHA UFUNDI NA KUINGIA BENDI YA POLISI.
KWA KUWA NILIKUWA KAMA MWANAFUNZI WA KUENDELEZWA MAREHEMU MZEE MAYAGILO ALIAMUA ANIPE  SAX NIACHE GITA KWA SABABU KUNA MPIGA SAX MZEE ABDUL MWALUGEMBE ALIKUWA ANASTAAFU HIVYO NILIINGIZWA SHULE YA PALE NA KUANZA KUSOMA NOTA NA KUANZA KUJIFUNZA SAXOPHONE MWAKA 1981.
MWAKA 1985 NILICHAGULIWA KWENDA COPLO  COARSE  ZANZIBAR NA NIKAFANIKIWA KUTUNIKIWA CHEO CHA  COPLO. SIKUWA NAPENDA SANA KUWA POLISI ILA NASHUKURU JESHI LA HILO  LIMENIFIKISHA HAPA NILIPO HASA KWA MASOMO YA MUZIKI AMBAYO YAMENIFANYA KUWA HAPA LEO"
MWEZI APRILI 1987  ALIAMUA KUJIUNGA NA BENDI YA VIJANA JAZZ AMBAKO ALIPIGA MUZIKI HADI MWAKA 2005 ALIPOAMUA KUACHA . AKAUNGA NA MWANAMUZIKI TOKA DRC SAMBA MAPANGALA KATIKA ZIARA ZAKE ZA AFRIKA HADI MWAKA 2006  ALIPOMUOMBA SAMBA MAPANGALA AMUACHE KWA KUWA WANAMUZIKI NDIO WALIOKUWA WAMEANZISHA BENDI HIYO MARK AMBAYO HADI HIVI SASA YUPO NAYO.
WALIIUNDA  KWA AJILI YA KUPIGA MUZIKI KATIKA   MAHOTELINI KWA KUWA ALIONA MIAKA TAKRIBANI  26 ALIYOITUMIA KUPIGA MUZIKI HAYAJAKUWA NA MAISHA BORA.
WAKAANZA KUPIGA KWENYE MAHOTEL YOTE HAPOYA JIJI LA DAR ES SALAAM  HADI WALIPOPATA MKATABA HUO AMBAO ULIWAPELEKA NCHI NYINGI ZA ULAYA ZIKIWEMO ZA UJERUMANI, MISRI,UFARANSA NA  WAKAENDA  NCHINI SWEDEN KUPIGA MUZIKI KATIKA MELI YA KITALII KATIKA JIJI LA STOCKHOLM KWA MKATABA.
ALIPOULIZWA JUU YA MAFANIKIA  ALIYOYAPATA PAMOJA NA CHANGAMOTO ZLIZOKUMBANA NAZO.  PEMBE ALISEMA …
“MAISHA YA MUZIKI NI MAGUMU SANA HASA KUTOKANA NA MPANGILIO WA HAKI ZA MUZIKI NA WANAMUZIKI WA AFRIKA NI TATIZO KUBWA AMBALO UDHIBITI HAKUNA KITU AMBACHO NI KIGUMU KWA MAISHA YETU”

MWISHO.


MAKOMA TROUPES



MAKOMA TROUPES

TUNAPOTAJA WAIMBAJI WA INJILI AMBAO WAMEWAHI KUTAMBA KATIKA KATIKA TASNIA HIYO NI PAMOJA NA KUNDI LA MAKOMA. 

KUNDI HILO LILILOKUWA LIKIWAKILISHWA NA NDUGU SITA KAKA WAKIWA WATATU NA DADA WATATU PAMOJA NA RAFIKI WA FAMILIA YAO LILIWEZA KUITIKISA DUNIA HASA KWA WAPENZI WA MUZIKI WA INJILI NA HATA WALE WANAOSIKILIZA NYIMBO ZA KIDUNIA KWA NYIMBO ZAO. 

HISTORIA YA KUNDI HILO LINALOVUTIA AMBALO LINAIMBA KWA KUTUMIA MTINDO WA RUMBA, POP NA R & B HUKU WAIMBAJI WAKE WAKITOKEA KINSHASA,JAMHURI YA DEMOKRASIA YA KONGO NA KUHAMIA UHOLANZI LIMESHAFANYA KAZI KARIBU NCHI NYINGI ZA AFRIKA.

WAIMBAJI WANALOUNDA KUNDI HILO NI NATHALIE MAKOMA ALIYEJITOA MWAKA 2004, ANNIE MAKOMA, PENGANI MAKOMA, TUTALA MAKOMA, DUMA MAKOMA, MARTIN MAKOMA NA RAFIKI YAO PATRICK BADINE. 

WAKIIMBA KWA KUTUMIA LUGHA YA LINGALA NA KIINGEREZA LAKINI PIA WANATUMIA KIFARANSA,KIRENO NA KIJERUMANI WAMEWEZA KUJIHAKIKISHIA KUENDELEA KUBAKI KATIKA TASNIA HIYO KILA WANAPOFYATUA ALBAMU. 

KUNDI HILO LILIPATA PIGO MWAKA 2004 BAADA YA MWIMBAJI WAO NYOTA WA KUNDI HILO LILILOJIPATIA UMAARUFU BARANI AFRIKA NA KWINGINEKO DUNIANI, NATHALIE MAKOMA AMBAYE AMEJIFUNGUA MTOTO WAKE WA KWANZA AITWAYE GIOVANNI CLAUDIO II, MWAKA HUU NA MUMEWE, JC ATAMBOTO, AMBAYE PIA ANAJIHUSISHA NA MAMBO YA MUZIKI KULIKACHA KUNDI HILO. 

NATHALIE BAADA YA KULIKACHA KUNDI HILO NA KUAMUA KUIMBA MUZIKI WA KIDUNIA AKIWA NJE YA KANISA KUTOKANA NA KILE ALICHODAI KUTAKA KUFANYA KAZI NYINGINE, HUKU WAJUZI WA MAMBO WAKIDAIWA KUWA NI UGOMVI BAINA YAKE NA KAKA YAKE MKUBWA AMBAO AMEKUWA AKIUZUNGUMZA SANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI HADI KUFIKIA MASHABIKI KUMTAKA BINTI HUYO AMBAYE ALIKUWA NI MWANZILISHAJI NA ANAYETEGEMEWA NA KUNDI HILO KWA TAKRIBANI NYIMBO ZOTE ZA KUNDI HILO, KUACHA KUFANYA HIVYO KWANI HATA IWEJE YULE NI KAKA YAKE PIA WANATAKIWA KUZUNGUMZA MASUALA YAO KIFAMILIA NA SIO KUANIKA KWA KILA MTU.

MWIMBAJI HUYO AMBAYE ALISHIKA NAFASI YA PILI KATIKA SHINDANO LA KUTAFUTA MWIMBAJI MAARUFU LILILOITWA NETHERLANDS IDOL MWAKA 2008 NA KUPEWA JINA LA TINA TURNER. 

NATHALIE MAKOMA ALIYEANZA KUIMBA MWAKA 1993 KATIKA BENDI YAO ILIJULIKANA KAMA "NOUVEAU TESTAMENT" KABLA KUJIUNGA NA MAKOMA. 

NATHALIE ALIPOFIKISHA MIAKA 14 ALIHAMIA UHOLANZI NA KUPATA ELIMU YA KULITAWALA JUKWAA KATIKA CHUO CHA ROCKACADEMIE HUKO TILBURG. 

BAADA YA KUNDI LA MAKOMA KUZUNGUKA DUNIANI NA KUPATA MAFANIKIO NATHALIE ALIACHA SHULE RASMI NA KUZUNGUKA AKITANGAZA NJILI KWA NJIA YA UIMBAJI. 

MASHABIKI WA KUNDI LA MAKOMA WAMEKUWA WAKIMUOMBEA MWIMBAJI HUYO ILI ARUDI KUMTUMIKIA MUNGU PIA KURUDISHA MAHUSIANO NA NDUGU ZAKE AMBAO PIA WALIKOSA HATA KUHUDHURIA SHEREHE ZA UVALISHWAJI PETE YA UCHUMBA AMBAYO ILIGUBIKWA NA UTATA BAADA YA KUONEKANA KWA VITUKO VINGI VILIVYOTOKEA HADI HARUSI NA KUSABABISHA MASWALI MENGI KAMA ILIKUWA NDOA YA KWELI ALIYOKUWA AKIIFANYA MWIMBAJI HUYO AMBAYE PIA AMESHIRIKISHWA NA PAPA WEMBA KATIKA MOJA YA NYIMBO ZAKE MKONGWE NCHINI CONGO. 

NATHALIE MAKOMA ALIZALIWA FEBRUARI 24, MWAKA 1982 HUKO LIBREVILLE ZAMANI GABON AKIWA KAMA MHOLANZI NA WAZAZI WAO WAKITOKEA DRC. 

NATHALIE MWIMBAJI MWENYE SAUTI NZITO, YENYE MVUTO MWENYE AIBU UKIZUNGUMZA NAE LAKINI AKIWA JUKWAANI NI MTU MWINGINE ASIYE NA AIBU WALA WOGA WA CHOCHOTE. 

WANAMUZIKI HAO AMBAO WALISHAWAHI KUPATA TUZO YA KORA WAKISHINDA KUNDI BORA LA MUZIKI LA AFRIKA MWAKA 2002 NA KUNDI BORA LA KUSINI MWA UKANDA WA PASIFIKI MWAKA 2005. 

KUNDI LA MAKOMA LINA ALBAMU SABA KIBINDONI JAPO ALBAMU YAO YA KWANZA ILIYOTOKA MWAKA 1999 YA NZAMBE NA BOMOYI (JESUS FOR LIFE) NDIYO ILIYOWAPA UMAARUFU NA KUKAMATA TASNIA YA MUZIKI WA INJILI IKITAMBA KWA NYIMBO KAMA NAPESI, BUTU NA MOYI, MWINDA, MOTO OYO, NATAMBOLI NA NZAMBE NA BOMOYI.
MWAKA 2000 KUNDI HILO LILIFYATUA ALBAMU NYINGINE ILIYOPEWA JINA LA KUNDI HILO AMBAYO ILIKUWA NA NYIMBO 14 IKIWEMO BABY COME,I'M SO EXCITED,MY LOVE IS TRUE ,SWEETER NA NYINGINEZO. 

HARAKATI ZA KUNDI HILO HAZIKUISHIA HAPO KWANI MWAKA 2002 WALITOA ALBAMU YAO NYINGINE MOKONZI NA BAKONZI IKIWA NA MAANA MFALME WA WAFALME IKIBEBA NYIMBO ZILIZOIMBWA KWA KILINGALA KAMA VILE MOKONZI NA BAKONZI, NASENGI,BANA, NALELI,NZAMBE NA NGAI NA TOLINGANA. 

MWAKA 2005 ALBAMU YA NA NZAMBE TE, BOMOYI TE IKIMAANISHA BILA YESU HAKUNA MAISHA WAKICHANGANYA LINGALA NA KIINGEREZA ILITAMBA NA KUWAFANYA KUENDELEA KUWA JUU KATIKA MUZIKI HUKO NCHINI UHOLANZI WAKIIMBA BILA NDUGU YAO NATHALIE. 

NA ALBAMU YAO YA TANO YA MY SWEET LORD WALIOFANYA KAMA KUNDI NA KUMSHIRIKISHA NATHALIE KAMA MWIMBAJI ANAYEJITEGEMEA. 

ALBAMU YA EVOLUTION WALIYOITOA MWAKA HUU IKIWA NA NYIMBO KUMI, ALBAMU HIYO INA NYIMBO KAMA VILE EVOLUTION, ALINGI BISO, YO OZALI, NDEKO, MOKONZI, SE YE, MABOKO LIKOLO, MOKILI, SOSOLA NA NGUYA NA YE. 

ALBAMU HIYO AMBAYO NI YA KWANZA TANGU WAUNGANE TENA MWAKA JANA NA KUAMUA KUITENGENEZA KUNA NYIMBO KAMA SOSOLA, YO OZALI NA NYIMBO NYINGINE ZIKIWA ZINAFANYA VIZURI KWENYE VITUO VYA RADIO NCHINI KWAO WALIKOZALIWA KONGO PAMOJA NA NCHINI NYINGINE DUNIANI BILA KUSAHAU AFRIKA YA MASHARIKI. 

KABEYA ‘NYOTA’ ILIYOZIMIKA GHAFLA.



KABEYA  ‘NYOTA’ ILIYOZIMIKA GHAFLA.

NA  MOSHY  KIYUNGI.

MARCH 2013.

KABEYA BADU ALIKUWA MWIMBAJI MAHIRI KATIKA BENDI YA LA CAPITALE, ALIYEWAACHA  WAPENZI NA MASHABIKI WA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI, WAKIWA BADO WANAMHITAJI.

ALIAGA DUNIA TAREHE 06 MARCH, 2013 AKIWA KATIKA HOSPITALI WA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA KWA MARADHI YA FIGO, AKIWA AMEFIKISHA UMRI WA MIAKA 68.

MPAKA ALIPOFIKWA NA UMAUTI, ALIKUWA NI MWANAMUZIKI MWENYE VIPAJI VYA KUTUNGA NA KUIMBA KATIKA BENDI YA LA CAPITALE ‘WAZEE SUGU’ INAYOONGOZWA NA MKONGWE KIKUMBI MWANZA MPANGO ‘KING KIKI’.


MSIMBA WA KABEYA ULIWATIA SIMANZI NA MAJONZI MAKUBWA WAOMBOLEZAJI WALIOFIKA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUUAGA MWILI WAKE NA KATIKA MAZISHI YALIYOFANYIKA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI MARCHI 07, 2013. UMATI WA WATU WALIBUBUJIKWA MACHOZI MARA WALIPOONA MWILI WAKE UKISHUSHWA KABURINI.

KABEYA BADU TOKA ALIPOANZA SAFARI YAKE KATIKA MUZIKI, KAMWE HAKUWA MTU MWENYE SONI. ALIKUWA TAYARI KUIACHA BENDI NA KWENDA NYINGINE WAKATI WOWOTE ULE, ILI MRADI MASLAHI YAWE MAZURI. BADU ALIPITIA BENDI NYINGI AKIWA HUKO KWAO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO, NA HAPA TANZANIA, AMBAPO  ALIPIGIA KATIKA BENDI SI CHINI YA TANO TOFAUTI.

SI VYEMA KUMSIFIA MTU BAADA YA KUFA, LAKINI KWA KABEYA NINALAZIMIKA KUFANYA HIVYO KWA KUWA MWISHONI MWA MWAKA JANA 2012, NILIBAHATIKA KUPATA FURSA YA KUFANYA MAHOJIANO NAYE ILI KUJUA WASIFU WAKE.

NILIZUNGUMZA NA KABEYA BADU  KWA TAKRIBANI SAA MBILI MFULULIZO, AKINISIMULIA HISTORIA YA MAISHA YAKE KWA UJUMLA.

KABEYA ALIAZA KWA KUTAJA  MAJINA YAKE  AKISEMA ANAITWA KABEYA CHIBANGU BADU. ALIZALIWA JANUARI 22, 1945 KATIKA MJI WA  LIKASI, HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.
ELIMU YA MSINGI ALIPATA KATIKA SHULE YA ECOLE  OFFICIALLE LAIQUE DE KOLWEZI NA KUMALIZA MWAKA 1959.

KABEYA ALISEMA MUZIKI ALIANZA TANGU AKIWA BADO MDOGO NA ALIPOPATA UMRI WA KWENDA KANISANI, ALIJIUNGA KATIKA KWAYA AKIIMBA NYIMBO INJILI.

AKIWA KANISANI HUMO, ALIJIFUNZA JINSI YA KUTENGENEZA ‘MELODY’ BAADAYE MWAKA 1963,  AKAJIAMINI KWAMBA ANAWEZA KUFANYA MUZIKI. ALIKWENDA KUJIUNGA NA BENDI YA MUZIKI WA DANSI YA  RICCO JAZZ, ILIYOKUWA KATIKA WILAYA YA KOLWEZI.

AKIWA KOLWEZI,  KABEYA ALIJIUNGA NA CHUO CHA UFUNDI AMBAKO ALICHUKUA MASOMO YA USEREMALA NA UASHI.
“TANGU  NIKIWA MDOGO, NILIPENDA SANA NYIMBO NA UIMBAJI WA TABU LEY ROCHEREAU NA KABASELE YAMPANYA ‘PEPE KALE’ NIKATAMANI SIKU MOJA NIFIKIE HADHI YAO…” ANASEMA KABEYA.

FAMILIYA YAKE ILIJITAHIDI KUMPA MOYO ILI AWEZE KUFANYA VIZURI KATIKA MUZIKI, HIVYO ILIMSHAURI KABEYA KUJIFUNZA LUGHA YA KIFARANSA AMBAYO INAZUNGUMZWA NCHINI MWAO.

KABEYA ALIKUBALIANA NA  USHAURI HUO NA ALINGIA KATIKA CHUO KILICHOKUWA KIKIMILIKIWA NA DHEHEBU LA DINI YA PROTESTANT HUKO KANANGA, JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.

KIU CHA KABEYA KILIPOZWA PALE ALIPOPOKEA CHETI BAADA YA KUFUZU SOMO HILO LA KIFARANSA.
HARAKATI ZA KABEYA BADU ZA KUTAFUTA MAISHA ZILIMFIKISHA KUFANYA KAZI KATIKA GAZETI MOJA LA LEALITY CONGOLESE LA  MJINI KANANGA, KWENYE KITENGO CHA USAMBAZAJI MWAKA 1967.

“BAADA YA MIAKA MIWILI KUPITA, MMILIKI WA GAZETI HILO ALIKAMATWA BAADA YA GAZETI HILO KUANDIKA HABARI ZILIZO MUUDHI RAIS WA WAKATI HUO MOBUTU SESESEKO, HATIMA YAKE GAZETI LIKAFUNGIWA, TUKAKOSA KAZI….” ANAELEZA KABEYA BADU.

‘KUVUNJIKA KWA KOLEO SI MWISHO WA UJENZI’ MSEMO HUU ALIUFANYIA KAZI KABEYA AMBAYE MWAKA HUO HUO ALIANZA SAFARI YAKE YA MUZIKI KIKAMILIFU. AKAJIUNGA KATIKA BENDI YA LUPE  JAZZ, BAADAYE AKAENDA KATIKA BENDI NYINGINE YA AMIDE SUCCESS.

KABEYA HAKUISHIA HAPO KWANI ALIONDOKA TENA NA KWENDA KUJIUNGA NA BENDI YA SANTA FEE BAADAYE AKAJIUNGA KATIKA BENDI YA LUPINA NATIONALE, AMBAKO ALIKUTANA NA KASONGO MPINDA ‘CLAYTON’ HUKO KANANGA.

UTULIVU KATIKA BENDI KWAKE HAUKUWEPO KABISA,  KWANI ALIONDOKA TENA NA KWENDA KUJIUNGA KATIKA BENDI YA LUPE REVOLUTION, ILIYOKUWA YA VIJANA KAMA YEYE.
JINA NA SIFA ZA UIMBAJI WAKE ZIKAZAGAA NDIPO ALIPOCHUKULIWA NA  OMER BABA GASTON KATIKA BENDI YAKE YA  BABA NATIONALE  MWEZI SEPTEMBA 1968.

BAADAYE MWAKA 1970, KABEYA ALISHAWISHIKA KWENDA KUTAFUTA AJIRA KATIKA MJI WA KINSHASA. ALIBAHATIKA KUPATA AJIRA KATIKA BENDI AMBAYO BAADAYE AKAGUNDUA KWAMBA  ILIMPA AHADI ZA UONGO ZA MASLAHI, NAYE AKAACHANA NAYO.
KATI YA  MWAKA 1971 NA 1972 KABEYA BADU ALIPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YA FESTIVAL DU ZAIRE KATIKA JIJI LA KINSHASA, JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.

KABEYA ALIRUDI LIKASI MWAKA HUOHUO WA 1972 NA KUJIUNGA NA BENDI YA SAFARI NKOI BAADA YA KUITWA NA MWANAMUZIKI KIKUMBI MWANZA MPANGO ‘KING KIKI’. KATIKA BENDI HIYO PIA  ILIKUWA NA WANAMUZIKI WENGINE MAGWIJI NDALA KASHEBA NA BAZIANO BWETII.
KABEYA BADU NASEMA KWAMBA ALISOMA  DARASA MOJA NA KIKUMBI MWANZA MPANGO ‘KING KIKI’ KATIKA SHULE YA MSINGI YA SHULE YA  ECOLE  OFFICIALLE LAIQUE DE KOLWEZI, AMBAKO WALIMALIZA MASOMO YAO MWAKA 1959.
“TANGU TUKIWA VIJANA TULIKUWA TUKIELEWANA SANA NA KIKI, NDIYO SABABU NIMEKUWA NAYE SAMBAMBA TUKIENDA SEHEMU MBALIMBALI HADI LEO NINAYE…” ANSEMA KABEYA.
WALIPOKUWA KOLWEZI WAKIPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YA SAFARI NKOI, WALIKUWA WAMEPANGA NYUMBA MOJA, WALICHANGIA BAJETI YA CHAKULA KWA PAMOJA KILA MWISHO WA MWEZI.

MWAKA 1973 UONGOZI WA  SAFARI NKOI ULIANZA KUWAFANYIA ‘MTIMANYONGO’ WANAMUZIKI WAKE AKIWEMO ‘KING KIKI’ LAKINI  KIKI  ALIGUNDUA MAPEMA HALI HIYO, AKAMSHAWISHI KABEYA MWAKA HUOHUO WA 1973, KUONDOKA NA KWENDA KUANZISHA BENDI YAO.

‘MWENYE BAHATI HABAHATISHI’ MSEMO HUO ULIJIONESHA DHAHIRI KWANI KABLA HAWAJAAZISHA BENDI YAO, AKAJITOKEZA  TAJIRI MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA PARADIZO, AKIMTAKA KIKI KWENDA LUBUMBASHI KUANZISHA BENDI YAKE.
“KIKI HAKUNIACHA MWAKA 1974 TUKAENDA LUBUMBASHI KUUNDA BENDI YA TAJIRI HUYO YA BUKA BUKA MABELE. NI UKIRITIMBA WA TAJIRI YETU, ULISABABISHA BENDI HIYO KUFA BAADA YA MIEZI SITA…” ANAELEZEA MWANAMUZIKI HUYO.

KABEYA AKAONGEZA AKISEMA BAADA YA KUFA KWA BENDI YA BUKA BUKA MABELE, KIKI MWAKA 1974 MWISHONI ALIAMUA KWENDA MJI MKUU WA CONGO DRC WA KINSHASA LAKINI KABLA HAJAONDOKA, ALIWASHAWISHI YEYE NA WANAMUZIKI WENZAKE WAREJEE SAFARI NKOI.

WALIKUBALI USHAURI HOU NAO WAKAREJEA NA WAKAPOKELEWA  NA UONGOZI WA SAFARI NKOI KWA MARA NYINGINE TENA. KWA KIPINDI HICHO AKIWA SAFARI NKOI, KABEYA AKAWA NA MAWASILIANO YA KARIBU NA KIKI AKIMSHAWISHI KURUDI SAFARI NKOI KWA HALI YA UTULIVU KATIKA BENDI ILIKUWA NI IMEIMARIKA.

KING KIKI ALIREJEA LUBUMBASHI MWAKA 1976, AKITOKEA KINSHASA PASIPO KUMAFAMAMISHA  MTU YEYOTE.
KABEYA ANASEMA “ TULIKUWA TUNAPIGA MUZIKI KATIKA UKUMBI MMOJA WA RELE NIGHT CLUB   MJINI LUBUMBASHI,  GHAFLA KIKI AKAPANDA JUKWAANI NA KUSHIKA ‘MIC’ AKAANZA KUIMBA. SOTE TUKABUTWAIKA  TUKAONA KAMA VILE ‘SHETANI’ ALIYETUA KIMIUJIZA JUKWAANI”


MWAKA 1977  KIKUMBI MWANZA MPANGO ALIFUATWA NA  CHIBANGU KATAYI ‘ MZEE PAUL’ ALIYETOKEA MAQUIS DU ZAIRE ILIYOKUWA HAPA NCHINI. KIKI ALIMUULIZA MZEE PAUL  IWAPO WANAMUZIKI WALIOPO MAQUIS DU ZAIRE WANAKIDHI  VIWANGO? MZEE  PAUL ALIJIBU KWA WASIWASI NA KUPENDEKEZA BORA KUCHUKUA  WANAMUZIKI HUKO DRC. KIKI ALIPENDEKEZA WANAMUZIKI WA KUONDOKA NAYE KUJA TANZANIA  AKIWEMO  KANKU KELLY, MUTOMBO SOZY, ILUNGA BANZA ‘MCHAFU’ WAKIWA SAFARINI KUJA NCHINI WALIPITIA  MJI WA KAMINA AMBAKO WALIMPATA MNENGUAJI  MWANADADA NGALULA TSHIANDANDA  ALIYEKUWA AKINENGUA KATIKA BENDI YA SAKAYONSA YA MJINI HUMO.

KABEYA BADU ALIKUWA AKIWASILIANA  NA KING KIKI NA AKAMUAHIDI KWAMBA ATAJITAHIDI AJE TANZANIA.


AHADI YA KIKI KWA KABEYA IKATIMIA BAADA YA KUFIKA MAQUIS DU ZAIRE. SAFU YA UIMBAJI IKAONEKANA KUPWAYA. ALIPENDEKEZA KUONGEZWA KWA WANAMUZIKI ZAIDI ILI KUIMARISHA BENDI HIYO YA MAQUIS  DU ZAIRE.  CHIBANGU KATAYI ‘ MZEE PAUL’ KWA MARA NYINGINE TENA AKATUMWA KWENDA CONGO  KUWALETA WANAMUZIKI WALIOPENDEKEZWA NA KIKI.
“ TULICHUKULIWA MIMI  KABEYA BADU NA KALALA  MBWEBWE  TUKIWA NI  WATUNZI NA WAIMBAJI,  MONGA KIYOMBO  ALIYEKUWA NA UWEZO WA KUPIGA  GITA LA RHYTHM NA  SAXOPHONE. WENGINE WALIOCHUKULIWA NI KINA  NGOI MUBENGA KWA UPANDE WA TARUMBETA NA KHATIBU ITEYI ITEYI ALIYEKUWA MPULIZJI WA SAXOPHONE  TUKALETWA TANZANIA MWAKA 1978…” NATAMKA KABEYA.

KABEYA ANASEMA MARA ALIPOTUA MAQUIS DU ZAIRE, ALITUNGA NA KUIMBA NYIMBO NYINGI, BAADHI YAKE NI ‘NDOA YA KWANGU NA MAMA KAZI’, ‘PONDAMALI’, ‘KIBWE MUTOMBO’ NA ZINGINE ZA MUNTANDA MULI, LWEMBE NA MANENO, AMBAZO  HAZIKUWAHI KUREKODIWA.

KABEYA BADU ALIPIGA NA MAQUIS DU ZAIRE KWA MIAKA MIWILI BAADAYE MWAKA 1980, ALICHOROPOKA NA KWENDA AKIJUNGA NA KING KIKI KATIKA BENDI YA ORCHESTRA SAFARI SOUND (OSS) ILIYOKUWA IKIMILIKIWA NA MFANYABIASHARA MAARUFU HUGO KISIMA.
AKIWA NA OSS KABEYA ALITUNGA NA KUIMBA NYIMBO ZA NANI ATASHIKA JEMBE NA POLE NDUGU. ANAELEZA KUWA WIMBO WA ‘YUYU’ ULIPIGWA NA KUREKODIWA KATIKA KIPINDI CHA KLABU RAHA LEO SHOW KILICHOKUWA KIKIRUSHWA NA RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM. (RTD)

BADU ALIKUWA AKIHITAJIKA SANA KATIKA BENDI HIZO MBILI PINZANI WAKATI HUO ZA MAQUIS NA OSS. HIVYO  AKAWA MITHIRI  YA ‘MUIGIZAJI’ KWA KUHAMAHAMA. ALIREJEA TENA MAQUIS  KWA KIPINDI KIFUPI KISHA MWAKA 1986 AKATAKIWA KUREJEA KWA MARA NYINGINE TENA KATIKA BENDI YA ORCHESTRA SAFARI SOUND.

ALIPOREJEA OSS TAYARI BENDI ILIKUWA CHINI YA UONGOZI WA NDALA KASHEBA NA HAICHUKUA MUDA MREFU AKATOKA NA WIMBO ULIOWAPAGAISHA WAPENZI WA OSS WA ZIADA. WIMBO HUO ALIUIMBA PEKE YAKE KWA HISIA KALI AKIMLILIA ZIADA, NA UKAMUONGEZEA SIFA KUBWA MIONGONI MWA WAIMBAJI WA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI.
ZINGINE ZILIKUWA ZA ‘ KURUTHUMU’, ‘SIMBA WALA WATU WAMEVAMIA MJI’ MAMA MWITA,  KAYANDA NA NYINGINE NYINGI.
KABEYA BADU ANAMWELEZEA KIKUMBI MWANZA MPANGO ‘KING KIKI’ KUWA NDIYE ANAYEJUA UMUHIMU WAKE NA HAPA ANASEMA… “ KIKI NDIYE ALIYEKUWA AKIJUA UMUHIMU WANGU KATIKA MUZIKI TOKA MWANZO HADI AKANIPACHIKA  JINA LA ‘ CHANGA CHA MKONYOYO’ IKIWA NA MAANA YA SIRI ILIYOFICHIKA…” ALIPEWA JINA HILO BAADA YA KUFYATUA WIMBO WA CHANGA CHA MKONYOYO’ ANAOULEZEA KUWA  NI UJUMBE MZITO JAPOKUWA WIMBO HUO  HAUKUWAHI KUREKODIWA.

ALIONDOKA OSS  NA KWENDA KUJIUNGA KWA MARA NYINGINE TENA NA MAQUIS DU ZAIRE  MWAKA 1988, HAPO NAPO HAKADUMU AKACHUKULIWA NA KWENDA KUJIUNGA NA BENDI YA TANCUT ALMASI ILIYOKUWA IKIPIGA MUZIKI WAKE MJINI IRINGA.

‘MSAHAU KWAO MTUMWA’ KABEYA ALITAMANI KUREJEA KWAO CONGO, NDIPO MWAKA 1990 AKAAMUA KURUDI KWAO LIKASI KATIKA JIMBO LA KATANGA.
KAMA NILIVYOKUJUZA MWANZONI KWAMBA KABEYA ALIKUWA MTAFUTAJI WA  MASLAHI MURUA, HIVYO ALIREJEA TENA TANZANIA  MWISHONI MWA MWAKA 1998.  MWAKA ULIOFUATIA WA 1999, AKAPEWA KAZI YA KUANZISHA BENDI YA MAGOMA SOUND YA JIJINI DAR ES SALAAM.

MWAKA 2001 ALIJIUNGA KATIKA BENDI YA LA CAPITALE INAYOONGOZWA NA KIKUMBI MWANZA MAPANGO ‘KING KIKI’ AU ‘BWANA MUKUBWA’ HADI MAUTI YAKE YALIPOMFIKA JUMATANO ILIYOPITA YA TAREHE 06 MACHI, 2013.


KABEYA ALISEMA KWAMBA ANA  MATARAJIO MAKUBWA ANAYOTAMANI KUFIKIA.   “NINA MPANGO WA KUNUNUA VYOMBO VYANGU VYA MUZIKI, PIA NATARAJIA KUREKODI NYIMBO ZAGU ZOTE NILIZOTUNGA NA KUZIIMBA, NZIUZE  MIMI MWENYEWE…” ANASEMA KABEYA AKIWA MWINGI WA TABASAMU USONI.

NINASIKITIKA KWA KUSEMA KUWA KUMBE KAULI HIYO IKIFUATIWA NA TABASAMU HILO,   ILIKUWA LA NDIYO  MWISHO,  TUKIAGANA NAYE!

KABEYA BADU ALINISISITIZA KWAMBA  MARA TU MAKALA HII IKITOKA,  NIMUALIFU ILI  AWAHI KUNUNUA GAZETI HILI, LAKINI MPANGAJI WA YOTE NI MUNGU.

KIONGOZI WA BENDI YA LA CAPITALE, KIKUMBI MWANZA MPANGO KING  KIKI’  ALIMUELEZEA KUWA PENGO LA KABEYA KAMWE HALITAZIBIKA.  “ KABEYA  PENGO LAKE HALITAZIBIKA KAMWE  AMETUACHIA UKIWA USIO NA  KIFANI. ALIKUWA NI MTUNZI  NA MWIMBAJI MZURI SI HIVYO TU PIA ALIKUWA MSIKIVU, MTU WA KAZI TULISHAURIANA KUTENGENEZA ‘MELODY’NA KWA KWA USHIRIKIANO HUO TULIKUWA TUKICHOKOZANA NA KUTOA VIBAO ‘MATATA’ SANA. TUMEMPOTEZA KABEYA…” KWA MASIKITIKO NA MAJONZI ANASEMA KIKI.
KABEYA CHIBANGU  BADU, AMEACHA MJANE NA WATOTO WANANE KATI YAO WATANO NI WA KIKE.

WAPENZI NA WADAU WA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI,  KAMWE HATAMSAHAU KABEYA BADU KWA JINSI ALIVYOKUWA  NA UWEZO WA KULISHAMBULIA JUKWA KWA KUCHEZA NA KUPAZA SUTI YAKE ILIYOKUWA NYORORO WAKATI AKIIMBA.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.

MWANDISHI WA MAKALA HII ANAPATIKANA KWA NAMBA HIZI: 0784331200,  0767331200 na 0713331200.