Wednesday, August 7, 2013

RASHIDI PEMBE GWIJI LA SAXOPHONE.



RASHID PEMBE  GWIJI LA SAX TANZANIA


 RASHIDI PEMBE AKIPULIZA SAXOPHONE HUKO STOCKHOLM SWEDEN.

 RASHID PEMBE  KATIKATI AKIWA NA WANAMUZIKI WENZAKE KATIKA JIJI LA STOCKHOLM  NCHINI SWEDEN.




 RASHIDI PEMBE AKIWA NA WANAMUZIKI WENZAKE



 MELI KUBWA YA KITALII ALIYOKUWA AKIPIGIA MUZIKI RASHISI PEMBE HUKO SWEDEN.
 RASHIDI PEMBE(WAPILI KUSHOTO)AKIWA MELINI NA WANAMUZIKI WENZAKE,DEKULA KAHANGA(KATIKATI)STOCKHOLM NCHINI SWEDEN.
 RASHIDI PEMBE AKIWA NA MDOGO WAKE NA MWENYEJIWAO HUKO ULAYA

HISTORIA YA MAISHA YA RASHIDI PEMBE.


RASHID PEMBE NI MWANAMUZIKI MASHUHURI KWA UPULIZAJI WA SAXOPHONE HAPA NCHI NA NJE YA MIPAKA YETU. ALIZALIWA MWAKA 1957.
WAZAZI WAKE BI. FRIDA ABEL AMBAYE NI MAREHEMU, ALIKUWA MZALIWA WA KIJIJI CHA MIHUGWE, WILAYA YA KISARAWE MKOANI PWANI.
BABA YAKE MZEE PEMBE RASHID PIA MAREHEMU  ALIKUWA MZALIWA WA KIJIJI CHA KURUWI, TARAFA YA MZENGA, WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI.
RASHIDI PEMBE ANAIELEZEA HISTORIA YAKE AKISEMA...

"MWAKA 1963 NILIANZA ELIMU YA MSINGI CHANZIGE PRIMARY SCHOOL HAPO KISARAWE, ILA KWA KUWA MAMA ALIKUWA DAKTARI ALIHAMISHWA HUKU NA KULE
NASI NDIO TULIKUWA TUKIISHI NA MAMA KWANI WALISHAACHANA NA BABA
MAMA ALIPENDA SANA TU
SOME, ILA BABA HAKUWA NA MSISITIZO SANA WA SHULE, SIJUI KWA KUWA ALIKUWA MBALI NA SISI MAANA HUDUMA ILIKUWA KWA MBINDE KIDOGO.
1966 MAMA ALIHAMISHWA HOSPITALI YA KISARAWE NA KUPELEKWA VIKINDU HOSPITALI NASI TUKAHAMA SHULE KWENDA KUSOMA HAPO VIKINDU -WILAYA HIYO YA
KISARAWE NIKIWA DARASA LA 4.
1967 NILIINGIA MIDDLE SCHOOL HAPO VIKINDU DARASA LA 5 HAPO NDIO NILIKUTANA NA MWANAMUZIKI JOSEPH BENARD TUKIWA DARASA MOJA NA DAWATI MOJA AMBAE
NI MPIGA SAXAPHONE DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA.
JOSEPH AMBAE SASA ANAITWA YUSUPH BENARD ALIKUWA NI MPIGA FILIMBI BINGWA PALE SHULENI, KIASI AMBACHO NILIUMIA SANA, HADI NIKAMUOMBA ANIFUNDISHE NA ALINIFUNDISHA TUKAWA TUNAPIGA WOTE FILIMBI KTK BENDI YETU YA SHULE.
1968 NIKIWA DARASA LA 6 NILIUGUA MKONO ULIKUWA HAUKUNJUKI SIJUI ILIKUWA NI NINI MUHIMBILI HOSPT WALIAMUA WAUVUNJE NIKAKATAA, WAKANIFUKUZA HOSPT
KAMA SITAKI KUVUNJWA HALAFU UUNGWE TENA NA NITAKUWA KILEMA WA MKONO KUTOKUKUNJA TENA,
KWA MAPENZI YA MUNGU MKONO ULIKUNJUKA SIKU HIYOHIYO JIONI YAKE, WAKATI MWAKA MZIMA ULINIUMA , ULIVIMBA NA HAUKUWA UNAKUNJUKA.
KW HALI HIYO NILIACHA SHULE MWAKA MZIMA.
MWAKA HUO WA 1968 MAMA ALIHAMISHWA KUPELEKWA SOTELE HOSPT NA BAADAE KUHAMISHWA TENA KWENDA KISIJU HOSPT WILAYA HIYOHIYO YA KISARAWE NA NDIPO NILIPORUDI TOKA KWA BABA NILIPOKUWA NAUGUA, NA KURUDI TENA KWA MAMA.
MAMA AKANIAMBIA NIANZE DARASA LA 4 TENA KWA KUWA ILE SHULE ILKUWA MPYA HAIKUWA NA DARASA LA 5 WALA LA 6.
SIKUWA NAPENDA SHULE KABISA, KWENDA SHULE ILIKUWA HADI KWA VIBOKO KILA SIKU NILIPAMBANA NA MAMA NA NILIMSUMBUA SANA HADI KUMALIZA DARASA LA 7 MWAKA 1972 HAPO KISIJU PRIMARY SCHOOL.
MAMA ALINIPELEKA KWA MJOMBA DAR ILI ANITAFUTIE KAZI, NA KWELI MJOMBA ALINITAFUTIA KAZI KILIMANJARO TEXTILE KIWANDA KILICHOKUWA KINATENGENEZA
KHANGA NA VITENGE HAPO GONGOLAMBOTO .
1973 NILIANZA KAZI, NILIPOKUWA KAZINI TUKIWA NA MAVITAMBAA KUZIBA PUA NA WENGI KUUGUA TB KUTOKANA NA PAMBA TUNAZOSINDIKA KWENYE MASHINE
NIKAONA VIJANA WENZANGU VIJANA WADOGO, WAKIWA WAMESHIKA MAFAILI NA KUZUNGUKA HUKU NA KULE, WENGINE WAKIWA OFISINI ,NIKAWA NATAMANI KWA NINI NISIPATEKAZI KAMA WALE? IKABIDI NIULIZE MBONA WALE WANA KAZI NZURI? NDIO KUAMBIWA WALE WAMESOMA FORM 4 WALE, NDIO KUSHTUKA KUWA KUMBE NDIO MAANA MAMA ALINIAMBIA NISOME NIKAANZA KUJUA FAIDA YA KUSOMA NA KUMWAMBIA MAMA NATAKA KUACHA KAZI NIKASOME KITU AMBACHO KWANZA ALICHEKA
SANA HALAFU AKANIULIZA UMEONA ? ULINISUMBUA HUTAKI SHULE SASA UMEONA NINI? NIKAMUELEZA NDIPO ALIPOMUOMBA KAKA ANITAFUTIE SHULE NIKAPELEKWA SHULE YA BAGAMOYO TECHNICAL SECONDARY SCHOOL 1973 HADI 1978 SHULE ILIKUWA INAMILIKIWA NA UMOJA WA WAZAZI TAPA WAKATI HUO.
SASA NIKIWA MDOGO NILIPENDA SANA NGOMA ILIKUWA MDUNDIKO UKIPITA MAMA UPESI HUWAAMBIA DADA ZANGU WANITAFUTE WANIKAMATE BILA HIVYO NAWEZA KWENDA NAO NA NISIJUE MWISHO WAPI NILIKUWA NAPOTEA HADI WATAFUTE NGOMA HIYO ILIPOENDA NDIO WATANIKUTA HUKO? NA SIKUWA NA UJANJA WA KURUDI WATANIKUTA HAPOHAPO KWENYE MDUNDIKO.
WAKATI NIPO KAZINI, NILIPENDA SANA BENDI YA SAFARI TRIPERS YA MAREH MARIJANI RAJABU PALE PRINCES BAR MNAZI MMOJA. MI NILIKUWA NAJUA MUZIKI MTU ANAJUA TU KAMA KIPAJIN KAZALIWA NACHO MTU SIKUJUA KAMA HADI UJIFUNZE, SASA PALE NILIMKUTA ABDALLAH GAMA AKIWA ANAPIGA GUITAR NA ALIKUWA MDOGO SANA NDIPO NIKAJIULIZA KWA NINI HUYU MDOGO ANAJUA NA NI MDOGO HIVI? NDIPO NILIAMUA NIJIFUNZE GITA.
NIKAWA NA GUITAR SHULE KITU AMBACHO KAKA ANENISOMESHA ALIKASIRIKA AKNIAMBIA NILIUZE NIKAKATAA AKAAMUA KUNIFUKUZA KWAKE, NA NIKAAMUA KWENDA KWA DADA NAE SHEMEJI AKASEMA HAWEZI KUWA NA WATU LUKUKI PALE HOME KWAKE NIKAAMUA KUONDOKA, NA KUWA NALALA SOKONI KARIAKOO PALE NJE NDIPO SHIDA YA MAISHA ILIANZA NILITAMANI KUFA LAKINI SIKUUZA GUITAR. NILIKUBALI YOTE, NIKABEBA MIZIGO YA ABIRIA WANAOTOKA MBEYA NA MIKOA MBALIMBALI PALE
MANZESE HADI NIKATEUKA SHINGO JAMANI MAISHA NI KIBOKO LAKINI NILIMUAMINI SANA MUNGU NA KUMUOMBA KWA YALE MATESO NILIPATA HADI NILIMALIZA SHULE
BABA AKIWA ANALIPA ADA YA SHULE KAKA ALIKATAA KABISA KUNISOMESHA TENA.
BAADA YA MATOKEO NILICHAGULIWA KWENDA KUSOMEA UALIMU WA UFUNDI MRUTUNGURU -SIJUI NI MUSOMA AU WAPI NIKAKATAA, KWA NILISOMA KWA TAABU NAE BABA AKASEMA NDIO MAANA KAKA YAKO, KAKUFUKUZA WE HUTAKI KUSOMA UNATAKA KUPIGA MAGITAA KUANZIA LEO SITAKUSAIDIA KWA LOLOTE NIKAKUBALI NILAENDELE A JIONI  KULALA SOKONI KARIAKOO HADI RAFIKI YANGU MAREHEMU JOHN SEMLAMBA ALINIKUTA NAAMKA PALE AKAMUA KUNICHUKUA NA KUKAA KWAKE KWA KUWA NILIMUELEZA KILA KITU.
1979 NILIENDA JKT NILIJUA KUTOKANA NA CHETI CHANGU CHA UFUNDI MASON (UASHI) GRADE 1  KINGENIPA KAZI KUMBE KULE IKAWA KUJITOLEA NIKATOROKA KARIBU NAMBA ZA JESHI ZITOKE, WAKATI HUO JESHI LA POLISI WALIKUWA WANATAKA MAFUNDI TOKA SHULENI NA CHETI CHANGU NIKACHUKLIWA MOJA KWA MOJA NA POLISI. NIKAWA NAFANYA KAZI POLICE MAIN STORE PALE KILWA ROAD NA KUANZA MAISHA.
PALE NDIO NILIPOKUTANA NA  TX  MOSHI WILLIAM, MZEE KASSIM MAPILI AMBAE AKAAMUA KUNIENDELEZA KUPIGA GITA NA WALIAMUA WANICHUKUE ILI NIKAJIENDELEZE PALE POLICE BAND NA NILIKUBALI KUOMBA KUBADILISHA SECTION TOKA KIKOSI CHA UFUNDI NA KUINGIA BENDI YA POLISI.
KWA KUWA NILIKUWA KAMA MWANAFUNZI WA KUENDELEZWA MAREHEMU MZEE MAYAGILO ALIAMUA ANIPE  SAX NIACHE GITA KWA SABABU KUNA MPIGA SAX MZEE ABDUL MWALUGEMBE ALIKUWA ANASTAAFU HIVYO NILIINGIZWA SHULE YA PALE NA KUANZA KUSOMA NOTA NA KUANZA KUJIFUNZA SAXOPHONE MWAKA 1981.
MWAKA 1985 NILICHAGULIWA KWENDA COPLO  COARSE  ZANZIBAR NA NIKAFANIKIWA KUTUNIKIWA CHEO CHA  COPLO. SIKUWA NAPENDA SANA KUWA POLISI ILA NASHUKURU JESHI LA HILO  LIMENIFIKISHA HAPA NILIPO HASA KWA MASOMO YA MUZIKI AMBAYO YAMENIFANYA KUWA HAPA LEO"
MWEZI APRILI 1987  ALIAMUA KUJIUNGA NA BENDI YA VIJANA JAZZ AMBAKO ALIPIGA MUZIKI HADI MWAKA 2005 ALIPOAMUA KUACHA . AKAUNGA NA MWANAMUZIKI TOKA DRC SAMBA MAPANGALA KATIKA ZIARA ZAKE ZA AFRIKA HADI MWAKA 2006  ALIPOMUOMBA SAMBA MAPANGALA AMUACHE KWA KUWA WANAMUZIKI NDIO WALIOKUWA WAMEANZISHA BENDI HIYO MARK AMBAYO HADI HIVI SASA YUPO NAYO.
WALIIUNDA  KWA AJILI YA KUPIGA MUZIKI KATIKA   MAHOTELINI KWA KUWA ALIONA MIAKA TAKRIBANI  26 ALIYOITUMIA KUPIGA MUZIKI HAYAJAKUWA NA MAISHA BORA.
WAKAANZA KUPIGA KWENYE MAHOTEL YOTE HAPOYA JIJI LA DAR ES SALAAM  HADI WALIPOPATA MKATABA HUO AMBAO ULIWAPELEKA NCHI NYINGI ZA ULAYA ZIKIWEMO ZA UJERUMANI, MISRI,UFARANSA NA  WAKAENDA  NCHINI SWEDEN KUPIGA MUZIKI KATIKA MELI YA KITALII KATIKA JIJI LA STOCKHOLM KWA MKATABA.
ALIPOULIZWA JUU YA MAFANIKIA  ALIYOYAPATA PAMOJA NA CHANGAMOTO ZLIZOKUMBANA NAZO.  PEMBE ALISEMA …
“MAISHA YA MUZIKI NI MAGUMU SANA HASA KUTOKANA NA MPANGILIO WA HAKI ZA MUZIKI NA WANAMUZIKI WA AFRIKA NI TATIZO KUBWA AMBALO UDHIBITI HAKUNA KITU AMBACHO NI KIGUMU KWA MAISHA YETU”

MWISHO.


No comments: