Thursday, January 9, 2014

KOMANDOO HAMZA KALALA ''Mzee wa madongo'



HAMZA KALALA ‘KOMANDO’

HAMZA KALALA NI MWANAMUZIKI MKONGWE KATIKA TASNIA YA MUZIKI HAPA NCHI. SIFA ZAKE ZILIANZA KUZAGAA WAKATI ALIPOANZA KULICHARAZA GITA LA SOLO KWA UMAHIRI MKUBWA.

ALIZALIWA MKOANI TANGA NA KUSOMA SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI HUMO. MARA BAADA YA KUZAILIWA ALIPEWA JINA LA NYUMBANI LA ‘KAPESULA’  BABA YAKE ALIKUWA MFANYAKAZI WA KATIKA SHIRIKA LA RELI KATIKA STESHENI YA MPANDA. BAADAE ALIHAMISHIWA MKOANI TANGA AMBAKO ALIBAHATIKA KUOA MKE WA KABILA LA KIZIGUA AMBAYE NDIYE MAMA WA KOMANDO KALALA. KWA MATIKI HIYO HAMZA KALALA NI CHOTARA WA KINYAMWEZI NA KIZIGUA.

KOMANDO HAMZA KALALA ALIANZA KUHAMASIKA KATIKA MAMBO YA MUZIKI MWAKA 1966 AKIWA SHULE YA MSINGI DARASA LA NNE WAKATI ALIPOKUWA AKIMSHUDIA BABA YAKE AKIIMBA NA KUCHEZA NGOMA YA KINYAMWEZI YA MANYANGA HUKO HUKO TANGA.
WAKATI HUO WAKATA MIKONGE WALIKUWA WAKIFANYA MASHINDANO YA NGOMA KATI YA WANYAMWEZI NA NGOMA ZA MAKABILA MENGINE WALIOKUWA KATIKA MASHAMBA TOFAUTI YA  MKONGE YA KIBARANGA YA AMBONI NA MENGINE MENGI LAKINI NGOMA  YA MANYANGA YA WANYAMWEZI NA ILE YA WAMAKONDE NDIZO ZILIZOKUWA ZIKITIA FORA  KATIKA MASHINDANO HAYO KILA MARA.

KALALA ANELEZA KWAMBA MJOMBA WAKE ALIKUWA NA GITA NYUMBANI HIVYO ALIKUWA AKIJARIBU KUSHIKA GITA KAMA ANAVYOSHIKA YEYE MJOMBA WAKE. KIPAJI CHAKE KILIANZA KIJITOKEZA BAADA YA KUONA KWAMBA HAIKUMSUMBUA SANA KUJUA KUCHANGANYA NYUZI ZA GITA.

KOMANDO ‘MZEE WA MADONGO’ MWAKA 1968 ALIANZA KUPIGA MUZIKI KATIKA BENDI NDOGO SANA HAPO TANGA IITWAYO KWANDURU JAZZ BAND. BENDI HIYO  ILIKUWA KATIKA MASHAMBA YA MKONGE NA BAADAYE AKAJIUNGA NA BENDI YA  AMBONI JAZZ.

HUKO HAKUKAA SANA NA ALIRUDI MJINI TANGA AMBAKO AKIWA NYUMBANI AKIFANYA MAZOEZI YA KUPIGA GITA,  AKAPITA MKONGOMAN  MMOJA ALIYEMTAJA KWA JINA MOJA LA CHIVOSHA AMBAYE ALIKUWA MWIMBAJI MZURI SANA  ALIMCHUKUA  NA KUANZA KUPIGA MUZIKI KATIKA BENDI YAOM YA VILLA NEGRO SUCCSSES. MWAKA 1969 ALIACHANA NA BENDI HIYO NA KUELEKEA MKOA  WA MOROGORO AKIWA NA NIA YA KUJIU KATIKA BENDI YA MOROGORO JAZZ AU CUBAN MARIMBA. LAKINI ALIAMUA KWENDA KATIKA WA KILOSA AMBAKO ALIKUWA AKIJUWA KUWA ABELL BARATAZAR YUKO HUKO. LAKINI ALIPOFIKA ALIAMBIWA KUWA ALISHAREJEA DAR ES SALAAM. ALIPIGA MUZIKI HAPO MKILOSA  LAIKINI HAKUPAPENDA KWA KUWA HAPAKUWA NA USHINDANI WA BENDI. KOMANDOO AKAAMUA KURUDI KWAO TANGA NA KUKUTANA MWANAMUZIKI MWENZAKE AMBAPO WAKAPANGA SAFARI YA KWENDA MOROGORO. WALIFIKA KATIKA MJI HUO WAKIWA NA HALI MBAYA SANA KIFEDHA KALALA WAKATI HUO ALIKUWA AKIVUTA SIGARA HIVYO ALIJIKUTA AMEFIKA MJINI MOROGORO AKIWA NA SENTI KUMI NA TANO PEKEE MFUKONI MWAKE AMBAZO HAZITOSHI KULA  WALA CHOCHOTE KILA LAKINI MWENZAKE  HAUKWA MVUTAJI SIGARA ALIKUWA NA AKIBA YA SENTI HAMSINI ZILIZOWAZWEZESHA KUPATA CHAI NA WAKALALA STENDI YA BASI HADI ASUBUHI WAKAANZA KUZITAFUTA HIZO KLABU ZA BENDI ZA MOROGORO JAZZ NA CUBAN MARIMBA
BAHATI HAIKUWA UPANDE WAO KWANI WALIKUTA BENDI HIZO ZIKIWA SAFARI  MOROGORO JAZZ ALIKUWA IMEENDA ZANZIBAR WAKATI CUBAN MARIMBA ALIKUWA SONGEA.
HAMZA KALALA ANAMTAJA MPIGA GITA LA SOLO WA CUBAN MARIMBA WAZIRI NYANGE ALIYEWAPOKEA WAKATI WAKISUBIRI BENDI HIZO ZIREJEE. MSEMO WA KUFA KUFAANA ULIJITOKEZA BAADA YA WANAMUZIKI WA MOROGORO JAZZ KUPATWA NA MATATIZO HIVYO ALIPOFANYIWA USAILI ILIKUWA KWAKE NI RAHISI KUCHUKULIWA KATIKA BENDI HIYO BAADA YA KUFANYIWA USAILI WAM KUPIGA GITA KATIKA WIMBO WA ‘ SINA PESA MIYE’
CUBAN MARIMBA ALIPOREJEA IKIONGOZWA NA JUMA KILAZA AMBAYE ALIKUWA MSHIRIKA MWASISI MWENZA  PIA NDIYE ALIYEKUWA  MWENYEJI WAO WAZIRI NYANGE, HIVYO ALICHUKULIWA NA CUBAN MARIMBA  NA ALIPOFIKA HAPO ALIKUTA  BENDI IKIPIGA KATIKA MTINDO WA SUBI SUBI.  AKIWA NA CUBAN ALIPATA SAFARI YA KWANZA YA KWENDA TANGA KUPIGA MUZIKI.
SIKU MOJA USIKU ALIKUJA KATIBU WA CHAMA WA WILAYA YA BAGAMOYO  MZEE MWITA ALIYETUMWA NA MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO WAKTI HUO
MOSSES NNAYE KWENDA BAGAMOYO KUENDESHA BENDI YA VIJANA YA TYL.
WAZIRI NYANGE ALIKUWA NA FAMILIYA YAKE PALE MOROGORO HIVYOM IKIMUWIA VIGUMU KWENDA BAGAMOYO LAKINI AKAMPA PANDE HAMZA KALALA KWENDA BAGAMOYO. KAZI KUBWA YA BENDI HIYO KILA JUMAMOSI WALIKUWA WAKIENDA RUVU KUWABURUDISHA WAPIGANIA UHURU WA FRELIMO NA ZAMBIA.
MWAKA 1970 AKASIKIA BENDI YA VIJANA JAZZ ANAANZISHWA. ALIFUATWA NA WANAMUZIKI ANAOWATAJA KWA MAJINA YA NDALA FASUTINE AMBAYE BAADAYE ALIONDOKA NCHINI KWA MATATIZO YA KUCHANGANYA KAZI NA UASHERATI.
NDALA ALIKANYWA NA WAZEE WA BAGAMOYO KUACHA UASHERATI LAKINI HAKUSIKIA. HAMZA ANAELEZEA KISA CHA KUKUTA PAKA ZAIDI YA 30 KWENYE MAKAZI YAO YALIYOKUWA GHOROFANI,WALIKUWA WAKILIA KWA SAUTI KAMA MAGITA.NDALA FAUSTINE AKAINGIA NDANI AKACHUKUA MKIA WA TAA , KALALA AKAMKANYA ASIWACHAPE PAKA HAO LAKINI YEYE ALIENDELEA KUWACHAPA LAKINI HAWAKUONDOKA HADI SA 11 ALFAJIRI NDIPO WALIPOONDOKA TARATIBU. SAUTI ZA PAKA HAO ZILIPOTOWEKA NDALA NAYE AKAANZA KUIMBA NYIMBO  AKIMTAJA MPENZI WAKE ALIYEKUWA AKIKANYWA ASIMCHUKUE. WAZEE WA BENDI HIYO AKIWEMO MASUDI NA MZEE DOLA ALIYEKUWA AKIKUSANYA USHURU SOKONI BAGAMOYO AMABO WALKUWA WAZEE BENDI WAKAMSAIDIA NA ALIPOPONA AKAONDOKA BAGAMOYO.
MWAKA HUO WA 1970 ALIPOKWENDA VIJANA JAZZ ALIKUTA KUNA VYOMBO VYA MUZIKI LAKINI HAPAKUWA NA MPANGO WA KUANZISHA BENDI.
HAMZA KALALA AKAFIKIRIA JINSI YA KUISHI MJINI DAR ES SALAAM NDIPO AKAMFUATA JOHN ONDOLO CHAHA ALIYEKUWA AFISA UHUSIANO WAKATI HUO. MZEE ONDOLO AKAMUELEAZA KWAMBA VYOMBO HIVYO VIMEFUNGIWA BAADA YA KUVUNJWA KWA BENDI YA GREEN JAZZ BAND NA  BARAZA KUU LA UMOJA WA VIJANA  NA KWAMBA HIVI SASA HAPANA MPANGO WA KUANZISHA BENDI.TENA. ONDORO AKAMUULIZA ANAPIGA CHOMBO GANI AKAMWELEZA KUWA ANAOIGA GITA. MZEE JOHN ONDORO AKAMWAMBIA AENDE AKAMSIKILIZA NIKAPIGA NYIMBO ZAKE KAMA USAILI BAADAYE AKARIDHIKA NA KUWAPA PESA YA CHAKULA. ALIPELEKWA KWENDA KINONDONI MAGO GARDEN NA KUANZA KUFANYA MAZOEZI YA KUPIGA MUZIKI.
WALONGEZEKA WANAMUZIKI WENGINE WAKIWA  KATIKA KAMBI KAMA YA JESHI.
RAMADHAN MTORO  DRUMS, ABDALLAH KWESA HASSAN HOKORORO NA IKATOKEZEA BAHATI YA MTENDE KUOTA JANGWANI BAADA YA BENDI HIYO KUJIPATIA UMAARUFU BILA KUJALI KKIPATO.
KATIBU MKUU WA CHAMA MICHAEL BARUTI KUPITA NA KUWAKUTA WAKIPIGA MUZIKI AKAWAPENDA SANA. MIAKA KUMI YA UHURU MZEE  JOHN ONDORO ALIENDA KWENYE SHIRIKA LA MAZAO WAKATI HUO AMBAKO ALIWAAMBIA KWAMBA WANA BENDI AMBAYO ITAKUWA IKIBURUDISHA KWENYE BANDA LAO. WALIKUBALIANA NA AKALIPWA SHILINGI ELFU KUMI NA MOJA. WALIFANAYA KAZI NA SHIRIKA HILO HADI MAADHIMISHP YA MIAKA KUMI YA UHURU  YALIPOKWISHA  NDIPO WAKAAMBIWA KUWA WATAKUWA WAKILIPWA POSHO YA SHILINGI HAMSINI KWA MWEZI. TUKAENDELEA  KUPIGA MUZIKI HADIM KILIPOFIKIA KIFO CHA RAIS WA KWANZA WA  ZANZIBAR  BENDI AMANI KARUME MWAKA 1972 WAKATENGENEZA WIMBO AMBAO ULIPENDWA NA WAZEE. AKAJA MZEE ANDREW SHIJA AKASHANGAA KUWAONA WAKIZAGAA NJE YA OFISI AKAAMRISHA WAPELEKWE JKT WAKAFUNZWE NIDHAMU. TUKAPELKWA KAMBI YA JKT RUVU WAKIWA NA HASSAN DALALI NA DK. CHARLES KIMEI. BAADAYE WALIPELEKWA MPAKANI MWA TANZANIA NA UGANDA VITANI AMBAVYO HATA HIVYO HAVIKUPUGANWA. WALIPOREJEA WAKATUNGA WIMBO UNAHUSU KIFO CHA MAREHEMU ABEID AMANI KARUME NA MGENI WA HESHIMA SIKU HIYO ALIKUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS NA WAZIRI MKUU RASHID MFAUME KAWAWA NA MAKAMU WA RAIS WA KENYA DANIEL ARAP MOI. MZEE KAWAWA AKAFURAHISHWA NA MUZIKI WALIUPOROMOSHA SIKU HIYO NA NDIPO ALIPOWAULIZA HAWA VIJANA WANATOKA WAPI. AKATOA MAELEKEZO YA KUANZISHWA BENDI YA VIJANA JAZZ.
BAADA YA KUANZISHWA MWISHO WA MWEZI ULIPOFIKA WALIANZA KULIPWA POSHO ZAO KATIKA OFOSI YA LUMUMBA ZA SHILINGI 150 TOKA SHILINGI 50 ZA AWALI.  KWA WAKATI HUO SHILINGI 150 ZILIKUWA NI NYINGI SANA  KWA MATUMIZI YA KAWAIDA. MWAKA 1974/75 WAKATOKA NA WIMBO HEMEDI MANETI AKIWA AMEKWISHA INGIA AKITOKEA MOROGORO  AKATUNGA WIMBO KURUKA UKUTA UTUNZI WA MANETI.
KALALA AKATUNGA WIMBO WA MAGDALENA NIPENI POLE.
WAKENYA WALIUSIKIA WIMBO HUO NA KUUPENDA SANA WIMBO HUO. AKAJA MKENYA ALIYEJULKANA KAMA OLUOCHI KANINDO AKAWAOMBA KWENDA KENYA KUREKONDI NYIMBO ZAO KWENYE KAMPUNI YAKE HUKO NAIROBI. WAKAPATA OFA YA KUREKODI KILA MWAKA ZAIDI YA MARA MBILI.
1977 KALALA AKAJIUNGA NA UDA JAZZ IKARUS KUMBAKUMBA. AKIWA NA UDA JAZZ KUNA SIKU ALIKUTANA NA MZEE MMOJA AMBROS MBURA ALIYEKUWA MMILIKI WA BENDI YA SUPER MATIMILA AKAMWAMBIA AENDE KILIMANAJARO HOTEL AKIWA NA HEMEDI MANETI  AJILI YA MAZUNGUMZO.
WALIPATANA KUONDOKA KWENDA SONGEA KWA NDEGE KUFUATIA BARABARA YA HUKO KUWA MBAYA. ALIWAKODIA NDEGE LAKINI MANETI HAKUWEZA KWENDA KWANI  HADI NDEGE INAPAA  ALIKUWA HAJAFIKA UWANJA WA NDEGE.
MKATABA WAKE NA MZEE AMBROSE ULIKUWA MZURI LAKINI AKACHUKUA MKATABA WA MIAKA MIWILI HADI 1979 AKAMALIZA MKATABA WAKE.
1979 WAKATI WAAJESHI WA JWTZ WANAREJEA TOKA VITANI UGANDA AKATENGENEZA WIMBO UITWAO MCHAKAMCHAKA. BAADAYE AKARUDI DAR NA AKAHITAJIKA TENA NA BENDI YA UDA NDIPO AKAJIUNGA NAO KWA MARA NYINGINE TENA NA KUBUNI MTINDO WA BAYAKANTA.
MWAKA 1981 MATIMILA AKAHAMIA DAR NA MZEE AMBROSE AKAMAKA ARUDI KWENYE BENDI YAKE.
MASLAHI YAKAMSHAWISHI KUONDOKA UDA NA KUJIUNGA NA MATIMILA HADI MWKA 1981.AKISHIRIKIANA NA DK. REMMY ONGALA. MWISHONI MWA MWAKA HUOHUO ALIFUATWA NA KAPTENI MCHUNGA AKIFUATANA NA HEMEDI MANETI WAKIMTAKA AFIKE OFISI YA UMOJA WA VIJANA.
AKAAMBIWA MPIGA SOLO WA BENDI HIYO HASSAN DAALALI KAONDOKA HIVYO WAKAMTAKA ASHIKE NAFASI YAKE NA KUWA KIONGOZI WA BENDI YA VIJANA.  MWAKA 1982 AKAIUNGA RASMI VIJANA AKATOKA NA WIMBO WA MAISHA YA AMBA. MIAKA YA 1985 HADI 1988  VIJANA JAZZ WAKATOKA NA MITINDO YA TAKATUKA, HEKAHEKA  NA PAMBAMOTO
 WIMBO WA SIFA ZA STELLA ALIUTUNGA WIMBO  HUO IKIWA NI NJIA YA KUMSHAWISHI BINTI HUYO AMBAYE WAKATI HUOA LIKUWA MWANAFUNZI WA CHUO MJINI MOROGORO NA NYUMBANI KWAO AMBAKO NI KWA MBUNGE WA BARIADI MASHARIKI, MHESHIMIWA JOHN CHEYO ‘ MZEE MAPESA’ AMBAYE NYUMBA YAKE ILIKUWA NA GETI KALI. STELLA ALIVUTIKA NA KUWA MPENZI WAKE HADI KUFUNGANAYE NDOA NA KUPATA WATOTO WAWILI AMBAO NAO WAMEFUATA NYAYO ZA BABA YAO AKIWEMO TOTO KALALA NA KALALA JOURNIOR. KOMANDO KALALA ANA WATOTO WENGINE WAWILI WA KIKE FATUMA AMBAYE NI MKE WA MTU NA FATUMA NI MWANFUNZI WA CHUO.




1988 AKAJIUNGA NA BENDI YA WASHIRIKA JAZZ ‘ WATUNJATANJATA’ KWA MWAKA MMOJA TU IKIWA NI NJIA YA KUTAFUTA JINSI YA KUJITEGEMEA MWENYEWE.MANDELA MWANA WA AFRIKA, NIMEKUSAMEHE  LAKINI SITOKUSHAU, JULLIE WIMBO ULIOTUNGWANA MADARAKA MORRIS NA NYINGINE NYINGI.
BAADAYE AKAANZISHA BENDI YA BANTU GROUP AMBAKO ALIWASHIRIKISHA WAPIGA MAGITA WAKIWEMO AKINA MANGELE SANGE UPANDE WA SOLO, ALLI ADINANI, RASHID KALALA BESI/SOLO. WENGINE NI BATI PETER NA MICHAEL LILOKO UPANDE WA DRUMS ALLI CHOKI NA MUUMIN MWINJUMA WAKIWA NI WAIMBAJI.MUSEMBOWA MINYUNGU NA ALLA MASHOOM KWA UPANDE WA TUMBA.
 BABA JENI NA SUVUYA WA NIMBA, NALILA MASUMANDA NA KASIMBAGU, NGOZI YA KITI MOTO.
 BABA YAKE MZEE KALALA ALIINGIA NCHINI AKIWA NA DADA ZAKE WAWILI WAKITOKEA DRC NA KUFIKIA KATIKA KIJIJI CHA IPWAGA HUKO INYONGA  AMBAKO ALIISHI NA KUWA MAARUFU NA KISHA KUFANYWA KUWA MTEMI. UFIKAPO INYONGWA FAMILIYA YA KALALA NI MAARUFU SANA HADI LEO.,
BANTU GROUP BADO IPO NAYE YUPO KWENYE MICHAKATO YAKINIFU YA KUANDAA VIBAO VIKALI VITAVYOTIKISA MASIKIO YA WAPENZI WA MUZIKI HAPA NCHINI.
KUHAKIKISHA WELEDI WAKE UIFAIDISHE FAMILIYA YAKE NA JAMII KWA UJUMLA.
USHAURI KWA WANAMUZIKI WA KIZAI KIPYA WAPIGE MUZIKI  LIVE. KISA KWA NINI BENDI HUFA BAADA YA KIONGOZI MKUBWA KUFARIKI
UOGOZI NI KIPAJI ANACHOKITOA MUNGU PEKEE SI KILA MTU ANAWEZA KUONGOZA.

MWISHO.



                         

No comments: