Wednesday, August 7, 2013

KOFI OLOMIDE



KOFFI OLOMIDE MCHUMI ALIYEBOBEA KATIKA MUZIKI.


Ni watu wachache mno ambao wanaweza kuamini kuwa unaweza kumkuta msomi mwenye digrii mbili akiamua kupanda jukwaani na kunengua kama mwanamuziki, lakini hali hii ipo tofauti kwa mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na mafanikio aliyonayo kimuziki pia ni msomi aliyebobea katika maswala ya hisabati

Koffi Olomide alizaliwa siku ya  ijumaa Julai 13, 1956  katika mji wa Kisangani uliopo kaskazini  mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Olomide ana asili wa  nchi mbili za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sierra Leone. Mama yake ni raia wa Congo akitokea katika kabila la Songye ambalo linapatikana katika mkoa wa kasai wakati baba yake ni mwenye asili ya Sierra Leone.

Kwa mujibu wa mila nautamaduni wa kabila la babu zake mama yake alimpa jina la ‘Koffi’ kutokana kuwa alizaliwa siku ya ijumaa alipokuwa bado ‘kinda’ koffi alipachikwa jina bandia la ‘Antoine Makila Mabe' likiwa na maana ya   'Damu mbaya ya  Antony'.

Antoine Koffi Olomide alikulia katika familia ya watu wenye uwezo wa kati na mahali ambapo elimu ilikuwa ikipewa kipaumbele

Olomide pamoja na kupenda muziki tangu akiwa mtoto, ndoto zake kubwa zilikuwa awe mchezaji wa mipra wa miguu.

Alipoanza kupevuka akiwa na umri wa miaka 18, wakati huo  akiwa mwanafunzi kijana, alivutiwa sana na usanii pamoja na muziki, ndipo alipoanza kutunga na kuimba nyimbo.

Kwa mujibu wa historia hiyo, Koffi alikuwa ana akili sana  darasani hali ambayo ilimfanya apate wadhamini wa kumlipia kwenda kusoma mjini Bordeaux, Ufaransa ambapo alipata Shahada yake ya kwanza ya Biashara na  Uchumi.
mbali na shahada hiyo inaeleza pia ana shahada ya pili katika masuala ya hisabati kutoka chuo kikuu cha paris

akiwa likizo Koffi alirekodi nyimbo za  'Asso' na 'Princesse ya Senza'  katika Studio za  Veve  huko  Kinshasha. Tokea hapo akashirkiana na wasanii wengine nguli akiwemo  Papa Wemba na  bendi ya Zaiko Langa Langa. Koffi  alitangazwa na kuzawadiwa  kama msanii bora wa Congo mwaka 1978
Akiwa Paris alianza kujifunza kupiga gitaa na kuandika nyimbo na aliporudi drc alijiunga na bendi ya muziki ya muziki ya viva la musica ambayo ilikuwa ikiongozwa na papa wemba, baada ya kujiunga na bendi hiyo Koffi aliimarisha mtindo wa polepole wa soukous uliokuwa umeisha umaarufu

aliuita mtindo huo Teha Tcho na ulipata umaarufu njee ya kongo, akiwa katika bendi hiyo mwanzo alikuwa ni mtunzi wa nyimbo, mwandishi na baadaye kama muimbaji, na hata baadaye aliamua kujitenga na kundi hilo na kuanza kuimba kama mwanamuziki wa peke yake na hadi mwaka 1986 alipounda bendi yake aliyoipa jina la Quartier latin mwaka wakati huo huo Olomide alikuwa akivutiwa sana kundi la wanamuziki wa  kassav. baada ya miaka  10 ya mafaniko yake, akatamani kuwa mwanamuziki wa kimataifa. ilichukua kipindi kirefu akisubiri kuwa mwanamuziki wa kimataifa hadi ilipofika mwaka 1988, wimbo wa 'henriquet' ukatokea kuwa mkali uliopelekea kupachikwa jina bandia la ‘Golden Star'.




Koffi olomide aliyafurahia mafanikio zaidi baada ya  kuandika wimbo akiwa na  binti yake pekee minou, ukiitwa D'elle et Moi', miaka ya 1990.
koffi toka mwaka 1990 hadi 1994, alifurahia kukua kwa mafaniko yake  ambayo kwa kipindi cha miaka chini ya minne, alifyatua zaidi ya album saba zikiwa chini ya jina lake na kundi lake la 'quartier latin'.
mwaka 1992 olomide alichaguliwa kuwa mwimbaji bora  wa kiume na  mshindi wa video bora katika shindano la african music awards mjini abidjan, ivory coast.
muziki wa koffi olomide unapendwa na mashabiki wengi afrika hata ulaya,  kufuatia tungo zake kuwa ni zenye ujumbe mzito kwa jamii. yaelezwa kwamba ujuzi wa aina yake, mpangilio mzuri wa muziki,  ukichangiwa na kuusomea muziki,  kumempa umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi yake ya jamhuri ya kidemokrasia ya congo(drc).
antoine koffi olomide  amefyatua  albam yake kali inayotamba hivi saaa ya abracadabra, iliyonguliwa na albam za  ngounda, efrakata, tcha tcho, haute de gamme – koweit na rive gauche.
katika kile kuonyesha umahiri wake katika muziki, koffi   alitoka na albam zingine nyingi za   pas de faux pas, live a bercy, attentant, le rambo du zaire, ultimutum, golden star na noblesse  oblige.
kama hizo hazitoshi,  msomi huyo aliwapagaisha wapenzi wake wa  muziki kwa kutoa albam zaidi za  v12,loimore, monde arabic, riziki, papa plus, zaiton na  phamacien. wimbo huo wa phamacien, sehemu kubwa ya uimbaji alitamba mwimbaji wake fally ipupa.
zingine zilikuwa  loi, Magie, Stila, Sexy pop, Rounge  A Levre, Etant Civil,  Round Poit, San suit, Respect 2,l Autre la, Miss Dess, Nolesse Oblige na  Escola. wimbo wa Escola alimshirikisha mwimbaji nguli papa wemba.
Mwaka 1998, Koffi akiwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa, alikimbiwa na wanamuziki takribani wote, baada ya onesho kubwa lilofanyika katika ukumbi wa Olympia.
Bendi hiyo ilisambaratika na baadhi ya wanamuziki wake wakaenda kuunda bendi yao ya Orchestra ‘Quartier Latin Academia.
Faida ya kufanya muziki ukiwa msomi ilijionyesha kwa Koffi Olomide ambaye ni mithiri ya chuo. hakuteteleka kabisa baada ya tukio hilo kwani haikuchukuwa kipindi kirefu akaibua tena vijana wengine wenye  vipaji toka sehemu mbalimbali nchini humo. Olomide ana sifa kubwa ya kutokuchukuwa wanamuziki toka bendi kubwa.  yeye huibua vipaji vya vijana wadogo hadi wanafikia kuwa wanamuziki wa kukubalika.
Amewafundisha wanamuziki wengi chipukizi ambapo wengine wameamua kujitegemea na kusimama wenyewe katika kazi za muziki na wengine bado wapo na bendi hiyo hiyo

Baadhi ya wanamuziki ambao ameshawatoa ni Fele Mudogo, Motana Kamenga, ambaye alitimka kwenda kujiunga bendi ya big star ya general defao. Wengine ni pamoja na Bruno Mpela, Soleil Wanga, Sam Tshintu, Suzuki 4 by4, Ferre Gola  na Fally Ipupa. Ipupa hivi sasa ni kati  ya wanamuziki mwenye jina kubwa na kuheshimika duniani anakula ‘maisha’ murua nchini marekani, akiwa ubavuni mwa kundi la g unit na lile la mwanamuziki 50 cent.
Hata hivyo katika siku za hivi karibuni suzuki amekuwa akionekana mara kwa mara katika maonyesho ya quartier latin sambamba na mwanamuziki wa kike mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Cindy le Coeur

Koffi aliwahi kushiriki katika projekti ya muziki wa africando, pia aliwahi kushinda zawadi nne za kora huko afrika ya kusini. vilevile alikuwa msanii bora katika nchi za afrika ya kati mwaka 2002.
Olomide aliwahi kufika hapa nchini mwezi Desemba 2012 aambapo  alimwaga burudani kamambe zilizokonga nyoyo za watanzania walihudhuria onyesho lake lililofanyika katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini  Dar es salaam, Desemba 14, 2012. 
Koffi Olomide  ni baba wa familiya ya mke na watoto saba. 
Mungu mwingi wa rehma iwapo atamfikisha Julai 13, 2013   Koffi Antonie Olomide atatimiza miaka 57 ya kuzaliwa kwake.
 Mwisho.


No comments: