Sunday, May 24, 2015

FREDY MAYAULA MAYONI MCHEZA HADI MWANAMUZIKI




UKIPEKUA KUTAKA KUFAHAMU ORODHA YA WACHEZAJI WALIOWAHI KUCHEZA KATIKA KLABU YA DAR YOUNG AFRICANS YA TANZANIA, PASI SHAKA MWANAMUZIKI FRED MAYAULA MAYONI NI MIONGONI MWAO.

BABA YAKE ALIKUWA MFANYAKAZI KATIKA UBALOZI WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO (ZAIRE) NCHINI TANZANIA, MAYAULA ALIMFUATA BABA YAKE NA NDIPO ALIPOJIUNGA KLABU HIYO.


UGONJWA WA MOYO (BRAIN TRUMOUR) NDIO ULIOSABABISHA KUKATIZA UHAI WAKE MEI 27, 2010 HUKO JIJINI BRUSSELS, UBELIGIJI.

MAYONI ALIKUWA MWANAMUZIKI MKONGWE MWENYE KIPAJI CHA UTUNGA NA KUIMBA MUZIKI WA DANSI TOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.

FERDY MAYAULA ALIKUWA MWANAMZIKI ALIYEKULIA NA KUSOMEA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM, MNAMO  MIAKA YA 1960.


BABA YAKE ALIKUWA NI MWANADIPLOMASIA KATIKA UBALOZI WA KONGO (ZAIRE) NCHINI TANZANIA. 

VIJANA WA ZAMANI HUKO DRC, WATAMKUMBUKA MAYAULA PALE ALIPOJIUNGA NA BENDI YA T.P. OK. 


JAZZ, ILIYOKUWA INAONGOZWA NA GWIJI FRANCO LUAMBO MAKIADI, HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.

MAYONI ALIJIUNGA T.P. OK. JAZZ BAADA YA KURUDI KWAO KONGO (DRC) NA KUJIKITA KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI. ALIACHIA WIMBO MAARUFU ‘CHERIE BONDOWE’ AU ‘SHERRY BONDOWE’, WIMBO AMBAO ULIMPA UMAARUFU MNO.

MAYAULA PIA ALIWAHI KUFANYA KAZI NA MWANAMZIKI MWANAMAMA MPONGO LOVE.


FREDY MAYAULA MAYONI ALIZALIWA NOVEMBA 06, 1946,  KATIKA JIJI LA LÉOPOLDVILLE, AMBALO SASA LINAITWA KINSHASA. ALIMALIZA SHULE ZA AWALI BILA MATATIZO NA KUMALIZA ELIMU YA SEKONDARI MWAKA 1962 KATIKA CHUO CHA KISANTU.

ALIPENDA SANA MPIRA WA MIGUU NA KATI YA MWAKA 1968 NA 1971 ALICHEZA NAFASI YA WINGA WA KUSHOTO KATIKA TIMU YA ‘AS VITA CLUB’ YA KINSHASA.

ALIWEZA KUCHAGULIWA HATA TIMU YA TAIFA YA NCHI YAKE.

BABA YAKE ALIPOPATA NAFASI YA KUFANYA KAZI KATIKA UBALOZI WA JAMHURIYA KIDEMOKRASIA YA KONGO (ZAIRE) NCHINI TANZANIA, MAYAULA ALIMFUATA. 

ALIANZA KUONESHA CHECHE KWA KUJIUNGA NA TIMU YA DAR YOUNG AFRICANS.

BAADAE ALIONDOKA DAR ES SALAAM NA KUELEKEA JIJI LA CHARLEROI, NCHINI UBELGIJI ALIKOKWENDA KUJIENDELEZA KIMASOMO KATIKA KOZI YA DATA PROCESSING.

AKIWA HUKO ALIJIUNGA NA TIMU ZA MPIRA YA ‘RACING CLUB DE CHARLEROI’ BAADAE AKAJIUNGA NA ‘RACING CLUB DE JETTE’ YA BRUSSELS.
 
KWA MUDA MFUPI ALICHEZEA TIMU YA ‘FC YA FRIBOURG YA SWITZERLAND, NI KATIKA KIPINDI HICHO ALIPOANZA KUJIFUNZA KUPIGA GITAA.

MUDA SI MREFU AKAJIUNGA NA BENDI YA WANAFUNZI WA KIKONGO ILIYOITWA ORCHESTRA ‘AFRICANA’ AKIWA KAMA MPIGA RHYTHM GITAA.

ALIPORUDI KINSHASA, MAYAULA AKABADILI KAZI KUTOKA KWENYE MPIRA WA MIGUU NA KUWA MWANAMUZIKI MTUNZI.

HAIKUCHUKUA MUDA MREFU KUGUNDULIKA KIPAJI CHAKE NA FRANCO LUAMBO MAKIADI, ALIYEMTAKA MAYAULA KUJIUNGA NA T.P. OK. JAZZ.

AKIWA NA T.P.OK. JAZZ NDIPO WAKATI HUO MAYAULA AKATOA NA KIBAO CHA CHERIE BONDOWE. WIMBO HUU ULIPOKELEWA VIZURI SANA NA WAPENZI WA MUZIKI.

KWA BAHATI MBAYA NATIONAL CENSORSHIP COMMISSION YA ZAIRE WAKATI HUO, ILIUPIGA MARUFUKU WIMBO HUO KWA KUWA ULIKUWA NA HADITHI YAKE ILIYOMUELEZEA ‘CHANGUDOA’ MMOJA ALIYEKUWA AKIELEZEA SHUGHULI ZAKE ZILIVYO.

COMMISSION ILIONA WIMBO UNATETEA UCHANGUDOA NA HIVYO KUUPIGA MARUFUKU. T.P.OK. JAZZ ILILZAZIMIKA KUUSAMBAZA WIMBO HUO  KUTOKEA UBELGIJI NA HATIMAE UKAENEA KONGO NA SEHEMU NYINGINE ZA AFRIKA.

YASEMEKANA KUWA JAPO FRANCO ALIMKARIBISHA T.P. OK. JAZZ, HAKUWAHI KUWA MWANACHAMA HALISI WA KUNDI HILO KWANI ALIPENDELEA KUWA HURU KUTUNGA NYIMBO ZAKE, NA KUMPA MSANII ALIYEMTAKA. TUNGO ZAKE KADHAA ZILIFANYIWA KAZI NA T.P. OK. JAZZ KAMA VILE NABALI MISERE NA MONI.

MWAKA 1977 TUNGO YAKE ILIYOITWA NDAYA ILICHUKULIWA NA KUIMBWA NA MWANAMUZIKI MPONGO LOVE, WIMBO HUO ULIKUWA UNAONGELEA KUHUSU MWANAMKE ALIYE NA FURAHA KUTOKANA NA KUWA NA MUME BORA NA KUWEZA KUMBANA MUMEWE KUTOKA KWA WANAWAKE WENGINE.

MAYAULA ALIONDOKA  ZAIRE MWAKA 1981 AKIWA NA WANAMUZIKI KUTOKA BENDI YA ABETI MASIKINI NA KUHAMIA AFRIKA MAGHARIBI.

HADI KUFIKIA MWAKA 1984 TAYARI LIKUWA MEREKODI ALBUM KADHAA CHINI YA LABEL YA DISC-ORIENT YA MJINI LOME NCHINI TOGO.

MWAKA 1984 ALIRUDI ZAIRE NA MWAKA 1986 ALITOA ALBUM ILIYOITWA ‘FIONA FIONA’, NA MWAKA HUOHUO TSHALA MUANA ALIPATA UMAARUFU KUTOKANA NA WIMBO ‘NASI NABALI’, ULIOTUNGWA NA MAYAULA MAYONI.

BAADA YA HAPO AKAREKODI ALBUM YAKE MIZELE AKIWA NA T.P. OK. JAZZ WAKISINDIKIZWA NA WAIMBAJI CARLITO LASSA NA MALAGE DE LUGENDO.
ALBUM YA ‘L’AMOUR AU KILO’ ILIFYATULIWA MWAKA 1993 NA MIAKA SABA BAADAE AKATOA ALBUM NYINGINE ‘BIKINI’.

BAADA YA ALBUM HIYO MAYAULA ALIHAMIA DAR ES SALAAM NA KUANZA KUFANYA KAZI UBALOZI WA KONGO.

WAKAZI WENGI WA MAGOMENI JIJINI DAR ES SALAAM WATAMKUMBUKA MAYAULA, AMBAYE  KATIKA KIPINDI HICHO AKIFANYA KAZI UBALOZINI, ALIKUWA AKIISHI MAENO HAYO.

MUDA SI MREFU AKAANZA KUUGUA NA KUAMUA KURUDI KWAO ALIKOZALIWA KATIKA KIJIJI CHA MAKADI, JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.
HALI YA AFYA YAKE ILIZIDI KUWA MBAYA MWAKA 2005 AKAPELEKWA UBELGIJI KWA MATIBABU ZAIDI. 

HATA HIVYO JUHUDI HIZO HAZIKUZAA MATUNDA KWA MAYAULA AKAFARIKI DUNIA KATIKA JIJI LA BRUSSELS NCHINI UBELGIJI  MEI 26, 2010 AKIWA NA UMRI WA MIAKA 64.
KATIKA MAISHA YAKE ALIWAHI KUCHAGULIWA MTUNZI BORA WA ZAIRE 1978 KWA WIMBO BONDOWE 2, MWAKA 1979 KWA WIMBO NABALI MISERE NA MWAKA 1993 ‘OUSMANE BAKAYOKO’.

MWISHO.

MUNGU UILAZE ROHO YA MAYAULA PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.

No comments: