Monday, October 3, 2011

ISENGA TABORA.

Vijana wa zamani ambao kwa sasa ni wazee toka kushoto ni Mzee Bakari Kawego,Mzee Mashaka Mapalala Mankupu na Mzee Kiyungi wakiwa katika picha ya pamoja mjini Tabora mwaka 2008.Wazee hawa walizaliwa mwaka mmoja kwenye miaka ya 1950's lakini wakakutana na kukumbushana mengi hususan walivyokuwa wakuchezea magari ya mabua, kuogelea mabwawani, kuwinda ndege kwa manati na kuchuma na kupopoa matunda ya porini. Wallah ilikuwa siku ya furaha sana baada ya kupotezana toka mwaka 1968 katika kijiji chao walikozaliwa cha Isenga Tarafa ya Ilolanguru Wilaya ya Tabora Vijijini wakati huo(sasa ni Uyui) Mkoani Tabora.

No comments: