Friday, October 14, 2011

Maoni ya mdau

The Legendary Safari Trippers, Marijani wa pili kulia kati ya waliosimama, wa kwanza ni Uvuruge mtunzi wa wimbo Georgina



Nyumbani tulikuwa na video cassette VHS aliyorekodiwa Marehemu Doza(Marijan Rajabu) na Orchestra Dar International kwenye show yao moja kule Buguruni Casanova Bar ( Kama sikosei) kwa Mwalimu Msuya. Ngoja nitawauliza waungwana nijue iko wapi.

Marehemu Doza si tu alikuwa muimbaji, mtunzi na mpiga guitar bali pia alikuwa anajua kuusoma muziki. Nadhani nadharia ya muziki alijifunza shuleni Olympio na Tambaza kwa sababu wakati ule muziki ulikuwa bado unafundishwa shuleni. Muziki lilikuwa somo linalofundishwa shule ya Tambaza hadi miaka ya '90 sijui kwa sasa.

Nikisikiliza tungo za Safari Trippers huwa nasikia muziki uliotungungwa kitaalam haswa kuanzia kwenye ghani/melody, midundo/rhythm, vikolombwezo/harmon hadi tenzi/lyrics. Safari Trippers iliundwa na na baaadhi ya wanamuziki waliokuwa "wataalam wa muziki" wakiwemo David Mussa, Mohamed Ibun, Musiba, Marehemu Doza na Marehemu Cris kazinduki. Nakumbuka Marehemu Cris alikuwa anafanyakazi Wizara ya Elimu na alikuwa wakati mwingine anajam na Mzee Kibira (Baba yao kina Onesmo Kibira) wakipiga muziki kwenye sherehe mbali mbali pale Wizarani. Mzee Kibira alikuwa anapiga Trombone. Naomba mnisahihishe kama nimekosea.

Kwa kumalizia: Moja ya Disadvantage ya kukosa televisheni Tanzania ni kukosa hifadhi ya mambo mengi katika mfumo wa filamu.

Mkuu, tafadhali wasiliana na Televisheni Zanzibar uone kama kuna uwezekano wa kupata clips za muziki. Nakumbuka kuna ile show ya Marquis du Zaire waliyokuwa wanaionyesha katika sherehe za kuzaliwa CCM mwaka 1977. Pia unaweza kuwasiliana na Audio-Visual Institute Kijitonyama walikuwa wana materials za muziki kibao. Chuo cha Sanaa Bagamoyo walikuwa wanarekodi sana matukio wakati wa Tamasha nina hakika kutakuwa na clips nyingi tu za bendi mbali mbali zilizokuwa zinatumbuiza katika ufunguzi na maonyesho mengine wakati wa Tamasha. Mtu mwingine ambaye anaweza kuwa na materials ni Mohamed Kissoky na ni Prof. Martin Mhando nina hakika haya majungu kuu hayakosi ukoko.

Nakutakia kila la heri na mafanikio katika jitihada zako.

Mdau Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.

No comments: