Saturday, April 16, 2016

MORENO BATAMBA ALIVYOTAMBA



MORENO BATAMBA ALIVYOTAMBA   
      
WIMBO WA ‘PILI MUSWAHILI’ ULIGONGA VICHWA VYA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI AFRIKA MASHARIKI NA KATI MIAKA YA 1980 HADI 1990.

SAUTI NZITO YENYE MVUTO WA AINA YAKE KATIKA NYIMBO HIZO ILIKUWA YA INAYOTAMBA KATIKA WIMBO HUO NI YA MORENO BATAMBA.

MAKALA YA LEO INAMZUNGUMZIA MWANAMUZIKI HUYU ALIYEJIZOLEA SIFA KEMKEM KWA UTUNZI NA UIMBAJI WAKE USIOIGIKA. 

WASIFU WA MORENO UNAELEZA KUWA ALIZALIWA MWAKA 1955, KATIKA MJI WA KISANGANI, HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO (DRC).

KAMA HISTORIA YA WANAMUZIKI WENGI KUACHA MASOMO NA KUKIMBILA MUZIKI, HALI KADHALIKA MWANAMUZIKI HUYO NAE ALIINGIA KATIKA MKUMBO HUO.

WAKANEMA NI MIONGONI MWA HAO YEYE ALIAMUA KUACHA SHULE MWAKA 1971, AKAENDA KUJIUNGA KATIKA BENDI YA ORCHESTRA MAQUIS SASA BATA.

BAADA YA KUJIAMINI KWAMBA AMEKOMAA KIMUZIKI, ALIONDOKA NCHINI MWAO NA AKAINGIA NCHINI UGANDA MWAKA 1974, AKAJIUNGA KATIKA BENDI YA ORCHESTRA BANA NGENGE, ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA MWIMBAJI  JOJO IKOMO. 

AKIWA NCHINI HUMO ALIWAHI KUFANYA MAZUNGUMZO NA MMOJA WA WANAMUZIKI WA BENDI YA ORCHESTRA VEVE, SAMBA MAPANGALA. 

BENDI HIYO YA VEVE ALIKUWA NA ANAMUZIKI TOKA DRC WALIOCHUKULIWA HUKO KWA AJILI YA KUFANYA MAONESHO KATIKA JIJI LA KAMPALA.

ORCHESTRA VEVE ILIKUWA TAYARI NI MAARUFU NCHINI HUMO, WAKAIBEBA BENDI YA BANA NGENGE.

WAKIWA KATIKA JIJI LA KAMPALA BENDI YA BANA NGENGE WALITOKA NA ALBAMU NYINGI. 

BADHI YAKE NI KAMA MAYATU, ILIKUJA REKODIWA TENA KWA JINA LA ‘MAYA TU’,
AZONGA, KOYOKA KOYOKA, OKEI KOLAKATE NIKA, NA BANGI MAKAMBO NA MABAKU.

BANA NGENGE AU KWA JINA JINGINE ILIKUWA IKITWA BANA MOJA,  KATIKA MIAKA YA 1970 ILIONDOKA KAMPALA WAKAENDA KATIKA JIJI LA NAIROBI NCHINI KENYA.

BAADHI YA WANAMUZIKI WALOIUNDA BENDI HIYO ILIKUWA NI PAMOJA NA WATUNZI NA WAIMBAJI JOJO IKOMO, N'DALA MOBANGI, BEYA MADUMA, ROXY TSHIMPAKA, FATAKI LOKASSA LOSI LOSI ‘MASUMBUKO YA DUNIYA’, MAKWANZI DUKI, KUKA MWANA BITALA NA HASSAN OMARI. 

WENGINE WALIKUWA AKIA NSILU BANSILU MANITCHO ALIYEKUWA AKILIUNGURUMISHA GITAA LA BESI, MORO MAURICE NA LAWISON SOMANA  WALIKUWA AKUPULIZA SAXOPHONE.

WALIKUWAPO OCHUDIS, MANDALI OTIS MUSA, ZENGELE SAIDA ALIYEKUWA MPIGA GITAA. KWA UPANDE SAXOPHONE ALIKUWEPO N'TALU NKATU NA TUMBA ZILIKUWA ZIKIDUNDWA NA MUKAPUTU KALEMBI.

MWAKA 1972 BENDI HIYO ILKIINGIA KATIKA MAPARAGANYIKO ULIOSABABISHA WANAMUZIKI WENGI WAKAONDOKA.

IKUMBUKWE KWAMBA MTUNZI NA MWANAMUZIKI JOJO IKOMO, ALIKUWA MMOJA WA WAANZILISHI WA BENDI YA ORCHESTRA BANA MOJA, AMBAPO AKIWA NA BENDI HIYO MWAKA 1974.

MWANAMUZIKI FATAKI LOKASSA ALISAFIRI AKIWA NA BENDI YA BANA NGENGE WAKAINGIA TANZANIA AMBAKO KWA BAHATI MBAYA MWAKA 1975, WANAMUZIKI WA BENDI HIYO WAKAGAWANYIKA.

MGAWANYIKO HUO  ULIPELEKEA BENDI HIYO KUFA NA KUWAFANYA WANAMUZIKI MORENO BATAMBA NA JOJO IKOMO WAKAENDA KUJIUNGA KATIKA BENDI YA LES NOIRS MWAKA 1976.

MWAKA 1978 FATAKI ALIREJEA TENA KATIKA JIJI LA NAIROBI AMBAKO AKAJIUNGA KATIKA BENDI YA LES KINOIS, ILIYOJULIKANA BAADAE KWA JINA  LA ORCHESTRA VIRUNGA.

WAKIWA KATIKA BENDI HIYO WALITOKA NA KIBAO CHA
"TSHIKU", AMBACHO HADI SASA HUSIKIKA KATIKA BAADHI YA REDIO HAPA NCHINI.

WANAMUZIKI WENGINE WA BENDI HIYO WALIKUWA NI PAMOJA NA MUKAPUTU KALEMBY KAJOS, WILLIAM TAMBWE LOKASSA, ALIYEKUWA AKILIUNGURUMISHA GITAA ZITO LA BESI, MANKWAZI DUKI DIEUDOS NA  CHUZA KABASELLEH. 

MWANAMUZIKI DIEUDOS MAKWANZI ALIONDOKA NCHI KENYA AKAREJEA KWAO KONGO MAPEMA MIAKA YA 1980.
BENDI YA LES NOIRS ALIACHIA VIBAO VYA "MUNGU IKO HELENA", “CHUZA NA LES NOIRS NA "SIKIYA SAUCE" KILICHOTUNGWA NA DIEUDOS MAKWANZI.

WALIWAHI KUPIGA WIMBO WAKAIMBA KWA WAKIWASIFIA VIONGOZI JOMMO KENYETTA WA KENYA NA MOBUTU SESESEKO WA KONGO (ZAIRE) WAKATI HUO.

BAADA YA KUACHIA WIMBO HUO, BENDI HIYO IKAONEKANA NI BENDI YA KWANZA TOKA KONGO, KUNG’AA NCHINI KENYA KATIKATI MWA MIAKA YA 1970.

MORENO BATAMBA ALIWAHI KUISHI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM KATI YA MIAKA YA 1978 HADI 1980, AKITUNGA NA KUIMBA KATIKA BENDI YA ORCHESTRA SAFARI SOUND (OSS), KABLA YA KURUDI TENA NAIROBI.

BENDI YA OSS ILIKUWA IKIMILIKIWA NA MFANYABIASHARA MAARUFU WAKATI HUO HUGO KISIMA.  

MWAKA WA 1980 MORENO ALIANZISHA BENDI YA ORCHESTRA MOJA ONE, AKIWA SAFU YA WANAMUZIKI AKINA  COCO ZIGO MIKE, MPIGA GITAA SIAMA MATUZUNGIDI, MCHARANGA DRUM LAVA MACHINE NA WENGINE WENGI WALIOTOKA KATIKA BENDI YA SHIKA SHIKA. 

ORCHESTRA MOJA ONE ILFYATUA NYIMBO KALI ZILIZOWASHIKA  WAPENZI NA MASHABIKI WA MUZIKI WA DANSI AFRIKA YA MASHARIKI. 

NYIMBO HIZO ZILIKUWA ZA "PILI MSWAHILI", "DUNIA NI DUARA”, " "MAPENZI YA SHINDA", "MWANAMKE HATOSHEKI", UREMBO SI HOJA”  NA "ANGELA " ZILIZOREKODIWA MWAKA 1981 NA "UREMBO SI HOJA.
KIBAO CHA "PILI MUSWAHILI" KILIKUWA MAHSUSI KWA AJILI YA RAFIKI YAKE WA KIKE ALIYEJULIKANA KWA MAJINA YA  PILI MIKENDO KASSIM. 

PILI ALIKUWA MTANZANIA WALIYEKUTANA NAYE ALIPOKUWA KATIKA BENDI YA ORCHESTRA LES NOIRS KATIKA MJI WA MOMBASA MWAKA 1976.

MORENO KWA KIPINDI KIFUPI ALIJIUNGA KATIKA BENDI YA ORCHESTRA VIRUNGA YA SAMBA MAPANGALA MWAKA 1983.

BENDI YA ORCHESTRA VIRUNGA, YAELEZWA KUWA ILIKUWA NI BENDI ‘NYOTA’ ILIYOWEZA KUPIGA MUZIKI ‘LIVE’ KATIKA BAADHI YA KUMBI ZA JIJI HILO.

ILIWASHIRIKISHA WANAMUZIKI WENGINE WAKIWEMO AKINA  COCO ZIGO, FATAKI LOKASSA, DAGO MAYOMBE NA BAADAE MORENO BATAMBA,  OTTIS NA SAMBA MAPANGALA.

WENGINE WALIKUWA NI MANITCHO NSILU, SAMMY MANSITA, DJANGO NKULU MWILAMBWE, BEJOS, SIAMA MATUZUNGIDI KWA UPANDE WA UIMBAJI.

MPENZI MSOMAJI WA MAKALA HAYA UNAWEZA KUONA MAJINA YA WANAMUZIKI HAO KUJIRUDIA KWA TAKRIBANI KILA BENDI. 

HII NI KUTOKANA NA KUHANGAIKA KWA WANAMUZIKI HAO AMBAPO KILA BENDI MPYA ILIPOANZISHWA WALIKUWA WAKICHUKULIWA.

MORENO BATAMBA ALIKUWA AKIPENDELEA ZAIDI KUTUNGA NA KUIMBA NYIMBO ZAKE KWA LUGHA YA KISWAHILI. NYIMBO ZAKE ZILIKUWA ZIKIGUSA HISIA ZA JAMII ZOTE.

AIDHA ALIIMBA WIMBO WENYE MAHADHI YA TAARABU BAADA YA KUIMBA WIMBO WA “VIDONGE SITAKI” AKIWA KATIKA KIKUNDI CH GOLDEN STAR MWAKA 1993.

KWA MAPENZI YA MUNGU NGULI HUYO  MORENO BATAMBA ALIFARIKI MWAKA HUOHUO 1993, AKIWA NA UMRI MDOGO WA MIAKA 38.

MUNGU AIWEKE ROHO YAKE PAHALA PEMA PEPONI, AMINA.

MWISHO.



No comments: