Sunday, March 10, 2013

KOFFI OLOMIDE MCHUMI ALIYEBOBEA KATIKA MUZIKI


KOFFI OLOMIDE MCHUMI ALIYEBOBEA KATIKA MUZIKI


Machi 12,  2013.

KOFFI OLOMIDE ni mwanamuziki msomi ambaye ni kiongozi wa bendi ya  'Quartier Latin', aliyezaliwa siku ya  Ijumaa August 13 1956, Kaskazini  wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Alipachikwa jina bandia la ‘Antoine Makila Mabe' likiwa na maana ya   'damu mbaya ya  Antony'. Koffi ni mwenye asili wa  nchi mbili za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sierra Leone.



Alipokuwa bado kinda,  Antoine Koffi Olomide alikulia katika mazingira ya kuridhisha japo katika familiya yao hakuwepo mwanamuziki. Alianza kupenda muziki baada ya kujihusisha na familiya ambayo ni ya watu wenye vipaji vya muziki, ambao walimpa ufahamu wa kutengeneza muziki. Jirani yao ndiye aliyegundua kipaji cha Koffi na akamtia moyo zaidi na akaanza kumfundisha kupiga gita.

Olomide alianza kupenda muziki tangu akiwa mtoto lakini ndoto zake kubwa zilikuwa awe mchezaji wa mipra wa miguu.
Alipoanza kupevuka akiwa na umri wa mika 18, wakati huo  akiwa mwanafunzi kijana, alivutiwa sana na usanii pamoja na muziki, ndipo alipoanza kutunga na kuimba nyimbo.


Koffi alikuwa mwanafunzi mwenye uwezo mkubwa shuleni. Alifaulu masomo ya Sayansi  na kupata cheti cha Diploma mwaka 1980. Baadaye baba yake alimpeleka nchini Ufaransa  kusomea masomo ya juu ya Utawala wa Biashara  katika Chuo Kikuu cha Bordeaux Business. Mwaka 1978 alirudi Kinshasa akitokea Paris akiwa na Digrii ya Uchumi. Pamoja na masomo mengine yaliyompeleka huko, pia alijifunza kupiga gita na kurekodi album yake ya kwanza iliyopewa jina la Ngounda.
Aliporejea Congo akajuinga katika bendi ya Viva la muzika iliyokuwa ikongozwa na Papa Wemba. Hapo  akaanza taratibu kurudisha hadhi ya mtindo wa Soukous ambayo ilikuwa tayari imeporomoka na kupitwa na wakati.
Olomide kwa juhudi zake alianzaisha mtindo mwingine wa ‘Tcha Tcho’ uliomuongezea umaarufu zaidi ndani na  nje Congo wakati huo.

Kunako miaka hiyo ya 1970, Koffi alianza kujijengea umaarufu  miongoni wa jamii Wacongo kama mtunzi na mwimbaji bora.
Wimbo wake Onia ulikuwa ndiyo wa kwanza kuonyesha mafanikio.

Akiwa likizo Koffi alirekodi nyimbo za  'Asso' na 'Princesse Ya Senza'  katika studio za  Veve  huko  Kinshasha. Tokea hapo akashirkiana na wasanii wengine nguli akiwemo  Papa Wemba na  bendi ya Zaiko Langa Langa. Koffi  alitangazwa na kuzawadiwa  kama msanii bora wa Congo mwaka 1978 kwa wimbo wake wa  'Aniba'

Rekodi yake ya kwanza ya  'Ngouda' alionesha juhudi zake  na matarajio ya kupelekea nguvu zake katika kupiga muziki wa Kiafrika.
Alifanya kazi nyingine akiwashirikisha wanamuziki wengine akina  Yakimi Kiesse na Fafa toka bendi ya  Molokai.

Mwaka 1986 Koffi Olomide   alianzisha kundi la  'Quartier Latin', wakati huo huo alikuwa akivutiwa sana kundi la wanamuziki wa  Kassav. Baada ya miaka  10 ya mafaniko yake, akatamani kuwa mwanamuziki wa Kimataifa.
Ilichukua kipindi kirefu akisubiri kuwa mwanamuziki wa Kimataifa hadi ilipofika mwaka 1988, wimbo wa 'Henriquet' ukatokea kuwa mkali uliopelekea kupachikwa jina bandia la ‘Golden Star'.
Koffi Olomide aliyafurahia mafanikio zaidi baada ya  kuandika wimbo akiwa na  Binti yake pekee Minou, ukiitwa d 'Elle et Moi', Miaka 1990.
Koffi toka mwaka 1990 hadi 1994, alifurahia kukua kwa mafaniko yake  ambayo kwa kipindi cha miaka chini ya minne, alifyatua zaidi ya album saba zikiwa chini ya jina lake na kundi lake la 'Quartier Latin'.
Mwaka 1992  Olomide alichaguliwa kuwa mwimbaji bora  wa kiume na  mshindi wa Video bora katika shindano la African Music Awards mjini Abidjan, Ivory Coast.
Koffi aliwahi kushiriki katika projekti ya muziki wa Africando, pia aliwahi kushinda zawadi nne za Kora huko Afrika ya Kusini. Vilevile alikuwa msanii bora katika nchi za Afrika ya kati.
Koffi Olomide alikwisha fyatua album nyingi zilizojaa nyimbo za  Attent, Adrada, Hero National, Julia, Kisanola, Loin na  Magie.
Alitoka na vibao vingine vya Micko, Motoromo,  Number One, Oprphelina, Papa Bonheur, Respect, Riziki, Rond Point  na Ultimatum. Koffi ni hodari wa kutunga na kuimba nyimbo kwani baadaye tena akafyatua nyimbo za Stila, Sex pop, Shela Mbutu Solei Vanga, Zaiton,  Esakola wimbo ambao alishirikiana na Papa Wemba. Zingine ni za Titian Mbwiya, Nobles Oblige, Papa plus, Pharmacien, Force de Frappe, Destination, Elle et moi , African King na nyingine nyingi.
Koffi Olomide kuna wakati alikimbiwa na wanamuziki takribani wote,  wakaenda kuunda bendi yao ya 'Quartier Latin Academia’ iliyokuwa ikiongozwa na Suzuki 4 by 4.
Faida ya kufanya muziki ukiwa msomi ilijionyesha kwa Koffi Olomide ambaye hakuteteleka kabisa. Baada ya tukio hilo, aliibua wanamuziki wengine vijana wenye vipaji toka sehemu mbalimbali nchini humo,  wanayo iimarisha bendi yake hadi sasa.
Olomide  ni baba wa familiya ya mke na watoto watano.

Agosti 13,  2013,  Koffi Antonie Olomide atatimiza miaka 57 ya kuzaliwa kwake.
Mungu amuongezee maisha marefu,  Amina.

Mwisho.




No comments: